WARNING: Kariakoo na iPhone Date bug

Nyasiro

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
1,200
551
Ni Kama wiki 2 zinakaribia tangu igundulike kuwepo kwa "bug" katika iOS ambayo hupelekea iPhone kushindwa kuwaka iwapo tarehe katika simu itasetiwa kuwa Mei 1970 kurudi nyuma. Unaweza kusoma zaidi kwenye mtandao kuhusu hii bug.

Jana katika pitapita zangu maduka ya kariakoo niliingia kwenye uchochoro mmoja nikitafuta USB cable ya simu yangu, katika lile duka pembeni alikua amekaa dada mmoja akiwa na iPhone 5 halafu jamaa mmoja aliyekua pamoja na yule dada aliniomba nimsaidie kuseti muda wakati huohuo yule dada akinipatia simu yake basi mimi nikaangalia muda nikaiseti ile simu katia muda sahihi lakini nikagundua kuwa kwenye tarehe ilikua inasoma mwaka 1970 ndipo nikastuka kidogo nikamwambia yule dada mbona mwaka ni 1970 nikamwachia simu yake na kumpa tahadhari kuhusu hiyo bug.

Nilichokifikiria mimi ni kwamba yule dada alitaka niseti muda halafu simu yake isipowaka wanibambikizie ile kesi. Kama ukikutana mchezo wa namna hii kuwa makini usiingie mkenge.
 
Back
Top Bottom