Warning: Credit card/ATM users

Pape

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2008
Posts
5,487
Reaction score
86
Kuna jamaa yangu ameingizwa mjini $2000 za kimarekani kupitia credit card yake nchini Japan.

Huyu jamaa yuko bongo na credit card yake ni ya benki fulani kubwa hapa bongo, na yeye hajawahi kusafiri kwenda Japan hata siku moja lakini credit card yake imetumika kutolea kiasi hicho huko Japan!!!!!

Onyo: Kuna watu ambao kazi zao ni ku-hack ATMs, credit cards, etc kwahiyo kuweni makini na vitu kama hivi!

Mara unapohisi kwamba ATM au credit card yako imetumika bila wewe kujua basi wasiliana na benki yako mara moja ili uweze kuzuia wahalifu hao wasiendelee kuchota bingo zako!
 
Mara unapohisi kwamba ATM au credit card yako imetumika bila wewe kujua basi wasiliana na benki yako mara moja ili uweze kuzuia waharifu hao wasiendelee kuchota bingo zako!

Waharifu unamaanisha WAHALIFU?
 
hivi wakishakuibia ukiripoti benki husika wanaweza kuwakamata kweli na kurudishiwa pesa zako zilizoibwa msaada pls
 
Tunashukuru kwa taarifa. Tunaomba jina la benki maana mabenki makubwa hapa nchini ni mengi.
 
Tunashukuru kwa taarifa. Tunaomba jina la benki maana mabenki makubwa hapa nchini ni mengi.
karibu ila nyoosha mkono huo ndugu....gonga kitufe basi!
 
hivi wakishakuibia ukiripoti benki husika wanaweza kuwakamata kweli na kurudishiwa pesa zako zilizoibwa msaada pls

Ni ngumu kaka, kwani hao watu wanaiba si kwenye bank tu, hata madukani, hotels nk. Wanakuwa wanalipa kwa credit cards. Kumbe yako ndio inatumika.. Asante Mkubwa.
 
Ni ngumu kaka, kwani hao watu wanaiba si kwenye bank tu, hata madukani, hotels nk. Wanakuwa wanalipa kwa credit cards. Kumbe yako ndio inatumika.. Asante Mkubwa.
Ni ngumu sana ila siku moja litawatokea puani...za mwizi 40...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…