Warioba, the last credible PM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba, the last credible PM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crucifix, Sep 3, 2012.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nampa Saluti Warioba

  Nyerere alimuachia Mwinyi urithi wa waziri mkuu Warioba. Mwinyi akampiga chini, akam-demote na kumpa kauwaziri fulani (kazi kama sikosei). Tangu hapo maadili katika uongozi yakaporomoka kwa kasi sana kwani ajenda ya warithi wa Warioba ilikuwa kama ifuatavyo


  1. Malecela - urais wa Tanganyika kwa nguvu ya wabunge 55 (G55) kabla Nyerere hajashtuka
  2. Sumaye - ni marufuku kumwagilia mchicha au kuosha magari, kuna uhaba wa maji ruvu chini/juu
  3. Lowassa - urais mwenza na JK (yaani kama mke mwenza vile ikulu - na wote mnajua matatizo ya ukewenza)
  4. Pinda - "sijui ni kwa nini Tanzania ni maskini, ngoja nimpigie simu mwenye nchi" (JK)

  Nawapa saluti pia Salim na Msuya, ambao u-PM wao umewafanya kuwa watu wa kuheshimiwa katika nchi hii. Saluti ya mikono miwili kwa 'jembe' marehemu Sokoine.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Hujamtaja kabisa Kawawa....i wonder why?

  Kabla hatujawa jamhuri alikuwa PM tena bila Rais.......

  angeweza 'kumuingiza Nyerere mjini' but hakufanya hivyo...
   
 3. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Usishangae, sijamtaja Kawawa kwa makusudi. U-PM wa Kawawa ni tofauti na hawa wengine. Yeye alikuwa PM mkuu wa nchi, kama alivyokuwa Zenawi wa Ethiopia. Cheo cha marehemu Kawawa ilikuwa sawa na Nyerere, Mwinyi, Mkapa na JK. Ni vile tu historia huwa inapindishwa pindishwa, na pia Nyerere alimpa nchi lakini akaendelea kuongoza chama kiutawala na chama ndio kilikuwa kinaamua, serikali inatekeleza. Hapo utaona ukuu wa Kawawa ulikuwa na mushkeli kidogo na ndio maana hatajwi saaaaaaaana.
   
 4. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  safiii!huyu wa sasa ni mbwa asiye na meno poor mizengo!
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,778
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..mimi namuona kama muoga-muoga hivi.

  ..namuona kama vile hataki kuonekana mbaya kwa CCM ktk kukemea uovu.

  ..pia nasikitishwa na vitendo vyake vya kurusha vijembe vya chini-chini dhidi ya CDM.

  NB:

  ..kwa wale wenye hamu ya kuiona CCM inaondolewa madarakani, msitegemee msaada wowote ule toka kwa Mzee Joseph Warioba.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Kuna Mshua mmoja MNigeria, alipojua mimi Mtanzania, akacheka sana. Akasema Watanzania watu waaminifu sana.

  Nikamuuliza kwa nini anasema hivyo? Akasema Prime Minister wenu Nyerere ashawahi kumuachia mtu nchi, akaenda kwenye shughuli za chama, akarudi kwenye kuongoza nchi kama kamuachia zuzu.

  Akasema hiyo isingeweza kutokea Nigeria kabisa.

  Nikamwambia hizo ni habari za historia na leo hii tofauti ni ndogo zaidi.

  Kawawa kashawahi kukataa kulipa madeni ya CCM na kutaka Bima i write off kama "bad debts". hawa ndo wamefanya ufisadi kabla ya vyama vingi na uhuru wa vyombo vya habari.

  Kwenye swala la credibility, Mzee Warioba namuheshimu sana lakini ameonyesha kutatizwa na too much reverence for the presidency. Amesema mara kadhaa kwamba urais upewe heshima, hata pale alipotegemewa kuonyesha muelekeo. Mbona hata Nyerere alishamblast Mwinyi akiwa rais?

  Lakini all in all angalau kwa mtu kama Warioba hata nikisema ninaona matatizo yanakuja kwenye a deep philosophical question, sio kwenye fluff kama wengine.

  Salim anaheshimika wakati kashindwa hata ku field a spirited campaign against the unfair smear campaign on him by Kikwete?

  Msuya yupi? Huyu huyu wa "kila mtu atatuchukua mzigo wake mwenyewe" au mwingine?
   
 7. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuna thread moja inayohusu mpaka wa Malawi ambayo nimeshauri watanzania wanaokurupuka kama wewe waache umbumbumbu wajikite kusoma vitabu vinavyoozea makatba bila msomaji (Bionyeza hapa).

  Sijui kwa nini nisikuite mbumbumbu mkurupukaji. Kwa sababu hapo kwenye RED unaropoka kwamba Rais Mwinyi alimpiga chini Warioba yaani akam-demote kwa kumpa Uwaziri mwingine mbali na Uwaziri Mkuu.Ni mbumbumbu tu anayweze kukurupuka kama wewe kwa sababu Warioba hakuwa demoted kama unavyosema.

  Kilichotokea ni kwamba Rais Julius Nyerere ali-resign na kustaafu November 04, 1985 yaani siku Rais Ali Hassan Mwinyi alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzani. hadi siku ya kuapishwa Waziri Mkuu alikuwa Salim Ahmed Salim.

  Kesho yake Joseph Sinde Warioba akateuliwa kuwa Waziri Mkuu. Kumbuka serikali ya Mwinyi na cabineta yake ilikuwa na uhalali wa miaka mitano na si milele. Hivyo, ilitakiwa kutawala kwa miaka mitano na uje uchaguzi mwingine ili ije serikali nyingine.

  Serikali ikafanya kazi yake hadi uchaguzi wa mwaka 1990 uliofanyika October 28, 1990. Mwinyi akashinda uchaguzi huo na akaapishwa upya kuwa Rais wa Tanzania November 08, 1990. Kesho yake yaani siku moja baada ya kuapishwa akamteua John Malecela kuwa Waziri Mkuu wa serikali mpya. Warioba akapewa Wizara ya TAMISEMI kweny ehii serikali mpya iliyoanza November 1990.

  Hivyo, kama kichwa chako kinafanya kazi yake badala ya kufunga nywele, huwezi kamwe kusema Warioba alipata demotion au hata kuhamishwa. Serikalini au kwenye taasisi yoyote unapohamishwa toka post moja kwenda nyingine lazima kuna barua inayoonyesha hivyo. Kama Warioba angekuwa amehamishwa toka Uwaziri Mkuu na akapewa Uwaziri mwingine ndani ya kipindi cha miaka mitano ya uchaguzi basi ningekubali kwamba ni demotion.

  Lakini hakuna barua ya uhamisho aliyowahi kupewa Warioba. Kama ni barua basi ni ya kumaliza kutumikia Uwaziri katika Serikali ya 1985 hadi Nov. 1990. Kwa kifupi anatakiwa kusifiwa kumaliza kipndi hiki salama.

  Nadhani maelezo haya yanakutosha kwa ufafanuzi. Sasa tuje kwa msimamo wa Warioba kama humfahamu.

  Kama ni suala la kumpiga chini mwenzake basi Warioba ndiye alimpiga chini Rais wake Ali Hassan Mwinyi mwaka huo 1990. Kwa sababu hujui unatakiwa ufundishwe kwamba NEC-CCM ilikaa chini ya Mwenyekiti Julius Nyerera kuanzia February 07 hadi 12, 1990.

  Kwenye hiyo NEC ililetwa report ya jinsi rushwa ilivyoenea serikalini. Mwenyekiti yaani Julius Nyerere akakemea vibaya rushwa ile na kama unakumbuka speech yake kwenye mkutano wa kumchagua Mkapa kuwa mgombea wa CCM, Nyerere alikumbusha wajumbe hili kwamba kemeo lake mle NEC lilifanya Waziri Mkuu aandike barua ya kujiuzuru.

  Ingawa kujiuzuru kwa Warioba haukutangaziwa bali tulitangaziwa tu kwamba Rais Mwinyi kavunja baraza la mawaziri (click here). Hata ukisoma habari hiyo utaona kwamba Mwinyi alivunja cabinet March 12, 1990. Ilileta utata hadi ikadhaniwa labda ziara ya Mandela iliyomkuza sana Nyerere badala ya Mwinyi Rais wa nchi ilichangia maana ilikuwa ni siku mbili tu baada ya Mandela kumaliza ziara yake hapa nchini.

  Baada ya kuvunja cabinet yake Mwinyi akamtangaza tena Warioba kuwa Waziri Mkuu wake. Ingekuwa ni kumpiga chini basi Mwinyi angetumia nafasi hii kumpiga chini Warioba kama alivyotumia nafasi hii kumuingiza serikalini kwa mara ya kwanza waziri kijana yaani Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Nishati, Maji na Madini.

  Hivyo, aliyekuwa ameonyesha nia ya kuondoka serikalini ni Warioba mwenyewe lakini Mwinyi akamrudisha. Na kama nilvyofafanua hapo juu, serikali hii ilipomaliza muda wake, alitakiwa kuja Waziri Mkuu mpya na akaja John Malecela.

  Kusoma ni kazi rahisi sana kuliko kukurupuka, kuropoka na kupayuka.
   
 8. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  wewe ndiye unatumia kichwa kufugia nywele na kumejaa kamasi tu humo kichwani mwako. Kutoka uwaziri mkuu hadi TAMISEMI ni promo? acha kutukana kama zuzu...........Mwinyi alimpiga chini Warioo na kuanzia hapo maadili katika uongozi O%
   
 9. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo mawaziri wakuu wote wa nchi hii kasoro Pinda walipigwa chini. Najua Tanzania imejaa mambumbumbu lakini si umbumbumbu wa kiwango hiki.
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nikupateje nimeisoma hiyo post yako ya hapo juu nimeona iko sahihi. Umesahau kitu kimoja tu kwamba Rais Mwinyi aliposema mawaziri wote wajiuzulu, Warioba aliuliza hata mimi. Pili kama Warioba alikuwa hataki kuitumikia Serikali basi alipomaliza Uwaziri Mkuu wakatu wa kipindi cha kwanza cha awamu ya pili angepumzika badala ya kukubali uwaziri wa TAMISEMI. Mimi naona kwamba Warioba alipigwa chini. Pia ukumbuke kwamba Warioba aliingia kwenye Uwaziri Mkuu kwa pendekezo na shinikizo la Nyerere na baada ya Mwinyi ku consolidate powers akaona amuache Warioba.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Jiulize kama Nyerere then angemuachia Kambona au Chief Fundikira
  how hii nchi ingekuja ku shape now?
  siku hizi tunafanana na Nigeria pamoja na 'Ujamaa wa Nyerere wa zaidi ya miaka 20'
  Je tungeanza na kina Kambona au Chief????????
   
 12. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kimbunga,

  Umeanza tena. Leo tu umetoka kuniomba radhi kwenye ile thread ya Malawi (click here) kwamba ulipotoka. Sasa unarudia tena mchezo uleule.


  Hivi na wewe kweli unaamini porojo za mtaani kwamba Warioba alitamka hayo uliyoweka hapo kwenye RED?


  Kimbunga, usiwe kama asilimia kubwa ya watu hapa nchini wanaodhani siku hizi ni kama zamani ambako kuumbuliwa uongo ilikuwa ni kazi. Siku hizi unachemka unapewa ushahidi ndani ya dakika kumi tu na wewe unanywea.

  Nimeeleza kwamba ile March 12, 1990, Joseph Warioba si kwamba aliomba ku-resign bali aliandika mwenyewe barua ya ku-resign kuachana na Serikali ya Mwinyi iliyojaa rushwa iliyokemewa na Nyerere kwenye NEC wiki chache kabla.


  NImeeleza, na sirudii, ila kama huamini msikilize Nyerere mwenyewe akilieleza vizuri. (Click here). Sikiliza hiyo video kwa walau dakika tatu za mwanzo halafu rudi hapa jamvini tuone kama hutarudi kuomba msamaha wa pili ndani y asiku moja baada ya kushushiwa data za uhakika!


  Ningekuwa mimi ndiye ninauliza swali kama lako hili, ningeli-frame kwenye muda ule Warioba alipo-resign halafu angekataa kurudi kwenye cabinet.

  Lakini hata hivyo hili swali linapaswa kuulizwa na mtu asiyeelewa nini maana ya dissolution of cabinet or any corporate body.

  Cabinet inapokuwa disolved that is the end of it na tunatarajia kije kitu kipya. Hivyo Mwinyi alipotaja cabinet mpya, ile March 13, 1990, Warioba hakuwa na sababu za kukataa kurudi kuwa Prime Minister.

  Alikataa kuwa Prime Minister kwa sababu ya cabinet iliyopita. Dissolution (not reshuffle) ilileta cabinet mpya. Sasa hakukuwa na sababu za kwa nini asirudi serikalini. Na kitaalamu si kurudi, bali ni kuanza upya maana ni cabinet mpya, ajirani mpya, kiapo ni kipya na ikibidi stratergies ni mpya.

  Na upya nimeuthibitisha kwamba ndipo zikaonekana sura mpya kama ya Jakaya Kikwete ambaye hadi leo ni Rais wako.

  Concept hiyohiyo ndiyo ilitumika November mwaka huo kwani cabinet mpya ilianza na John Malecela. Hakuna mahala Rais anapolazimishwa kisheria au kimaadili eti kumchukua Waziri Mkuu yuleyule tena kwenye succeedding goverment kama alivyofanya Mkapa kwa Sumaye au Kikwete kwa Pinda.

  Vinginevyo basi hata bunge lisingekuwa linawapigia kura kuwathibitisha kwa sababu si ni yuleyule wa outgone cabinet, sasa kwa nini apigiwe tena kwenye incoming government.

  Kuwaza hivyo, ni jambo la ujinga. Kila cabinet mpya ni mpya inayohusisha appointment of prime minister lazima huyo prime Minister aapishwe kwa sababu ni mpya.

  Si suala la kupigwa chini hapo. Ndiyo maana kuna mpuuzi mmoja humu nimemjibu kwamba kama hiyo ndiyo conept ya kupigwa chini, basi ambaye hajawahi kupigwa chini ni Pinda tu na yeye kama hatafia kwenye uwaziri mkuu basi kwa hizi concept zenu ni kwamba ataondoka kwenye premier kwa kupigwa chini!

  Watu wa ajabu sana nyinyi wenye uelewa huu!

  Porojo ambazo huwezi kuzithibitisha.
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Umesahau Mawaziri Wakuu Wawili

  1. JK Nyerere

  2. Rashid Mfaume Kawawa
   
 14. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Napendaga michango yenye mashiko kama hii post. KWamba hata kama hukubaliani na hoja si lazima kutukana kama hili ***** Nikupateje

  Nashangaa pia kwa nini jamaa anakataa kuwa Warioba hakupigwa chini!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ndugu, hawa wawili walikuwa wakuu wa nchi, si ma-PM watendaji chini ya rais. Waache bana, wapumzike kwa amani. Amina.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Sep 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa hiyo kukuomba radhi tu basi unataka kunifanya mateka wako. hakuna kitu kama hicho. Ukitoa hoja nzuri nitakuunga mkono ila naona unataka kupitiliza na kuanza kutukana watu. Si vizuri kutukana kama unajua kitu kielezee kwa uzuri bila matusi utaeleweka tu. Kila mtu anasoma vitabu na kuijua historia.

  Suala la porojo linatoka wapi? Kama huamnini kuwa Warioba aliingia kwa mgongo wa Nyerere basi kaa hivyo hivyo. Kama huamini kwamba baba wa Taifa alikuwa akitawala kwa kuwatumia akina Butiku, Warioba na gen. Musuguri basi subiri habari hizo ziandikwe kwenye vitabu.

  Kama huamini kwamba Mwinyi alivyojitoa kwenye umateka wa Baba wa Taifa na baba wa Taifa ikabidi aje public basi subiri historia itaandika na wewe uende maktaba na kusoma. Kama huamini kwamba Mwinyi alivunja baraza la Mawaziri na kumshutumu Warioba kwa kushindwa kuisimamia serikali (Baraza la Mawaziri) na rushwa kushamiri lakini akapata shinikizo toka kwa Mzee wetu wa Butiama basi subiri wanhistoria wataandika nas tutaenda kuazima vitabu na kusoma.
   
 17. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  (hapo italics na msitari) K ASINGEWEZA, uwezo wake ulikuwa wa chini mno: alichoweza pekee ni kutekeleza maagizo ya MZEE JK bila kuhoji, kwa njia hiyo alifanikiwa na kudumu ktk siasa.KWW ALIKUWA anatumia kichwa cha JK kufanyakazi, kama MED na PUTIN kule URUSI, a protege, yeye mwenyewe anajua na ndiyo maana hakujaribu, siyo kweli kwamba alikuwa hataki kuwa PRES bali alijua asingeweza kupambana na mwl JK
   
 18. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kawawa alikuwa hana akili ya kuweza kumuingiza Nyerere mjini ingekuwa Kambona ndio!!!
   
 19. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Na wewe ukitumaini kwamba itabidi tuamini hayo ya jikoni unayotuletea basi wataleta wengi kama walivyoleta zile porojo kwamba kifimbo cha Nyerere kilisahauliwa mahala wakashindwa kukibeba.

  Tutaamini hadi zile porojo kwamba Kawawa hakuwa anajua English akawa anaongezewa chai hadi Nyerere akamwambia "Kawawa funika Kikombe".

  Na wote wanaoelta porojo hizo base yao ni hiihii kama wewe kwamba tusubiri yaandikwe vitabuni kama wataandika.

  Porojo tupu.
   
 20. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Hizo sifa mnazompa huyo mzee mtashangaa atakapotoka na katiba ya HOVYOOO ndiyo mtajua hafai.Nitawakumbusha rasimu ikitoka
   
Loading...