Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Na wewe ukitumaini kwamba itabidi tuamini hayo ya jikoni unayotuletea basi wataleta wengi kama walivyoleta zile porojo kwamba kifimbo cha Nyerere kilisahauliwa mahala wakashindwa kukibeba.
Tutaamini hadi zile porojo kwamba Kawawa hakuwa anajua English akawa anaongezewa chai hadi Nyerere akamwambia "Kawawa funika Kikombe".
Na wote wanaoelta porojo hizo base yao ni hiihii kama wewe kwamba tusubiri yaandikwe vitabuni kama wataandika.
Porojo tupu.
Mkuu hizo nyekundu ni porojo za shule ya vidudu! Kama ulisoma shule ya vidudu utakuwa ulizisikia lakini kama umesoma kindergarten utakuwa hujazisikia.
Nilichosema si porojo wala ni hali halisi na mambo ndivyo yalivyo. Wewe unategemea hotuba ya Nyerere na bahati mbaya humjui ama hukupata kumjua vizuri Mwalimu Nyerere. Pia nadhani hukujua jinsi Nyerere alivyomwachia madaraka Mwinyi na yeye kubaki kwenye Chama ambacho kilikuwa kinashika hatamu!
Nakuambia tena kwa nia nzuru kwamba kama una hoja zitoe bila matusi utapata tunu. Suala la Nyerere kumweka pale Warioba linajulikana hata kwa watoto waliokuwa chekechea enzi hizo.