Warioba, Salim, Zitto na Slaa washirikiana kufanikisha mazungumzo ya Ikulu

Najua wapo watu hii hawatapenda kuisikia zitto alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha hili....lakini ndio hali halisi,lazima tuiseme .

Wadau mi nadhani baadhi yetu wakati umefika sasa tubadili mitazamo yetu kuhusu ZITTO KABWE;kiukweli kijana anaonyesha ukomavu wa kisiasa kila kukicha tofauti na vijana wengi ambao wanakimbilia posho tu;zitto kumbe anafanya mambo mengi bila kupiga mayowe wala kuita wapiga picha...hili nalisema kufuatia kugundua kuwa Mh. zitto kabwe kuwa chanzo cha mazungumzo maarufu yanayoendelea ikulu kati ya chadema na Rais kikwete,mambo yako hivi.....

Safari ilianza hivi; baada ya kuona mwenendo wa mijadala na mwelekeo wa baadhi ya viongozi wenzake, hasa katika siku ambazo CHADEMA kilikuwa kinatangaza kwamba kingeitisha maandamano nchi nzima kupinga mchakato wa katiba mpya uliokuwa umewasilishwa na Serikali bungeni, baadhi ya wanaCHADEMA na wengine miongoni mwa umma, walihisi kuwako kwa hatari ya kweli ya vurugu kuibuka nchini, ambayo isingekisaidia chama hicho au kundi jingine lolote, hivyo Zitto alifunga safari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ili kuteta na Dk. Slaa.

Katika mazungumzo yao, vyanzo kadhaa vya habari vimesema, hoja ilikuwa ni umuhimu wa kuchukua njia ya mazungumzo katika suala la mchakato wa katiba mpya, kuliko njia ya maandamano. Lakini Dk. Slaa amekaririwa akiashiria kwamba ilikuwa vigumu zaidi kuanzisha njia ya mazungumzo kwake kuliko njia ya shinikizo kupitia maandamano.

Raia Mwema limeambiwa kwamba kutokana na ugumu huo, Dk. Slaa amekaririwa kumueleza Zitto kuwa wanaweza, katika kufikia kupata muda wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete, kuwatumia wazee wenye utulivu na busara, wasio na misimamo mikali ya kisiasa, wenye kutanguliza mbele maslahi ya nchi na wanaosimamia zaidi nguvu ya hoja, ambao miongoni mwao ni Dk. Salim na Jaji Warioba.

Habari zinasema, tatizo kubwa alilokuwanalo Dk. Slaa katika kuwafikia wazee hao ni kwamba hakuwa na ukaribu wa kiasi hicho nao na Raia Mwema limeelezwa kwamba katika mazingira hayo ndipo Zitto alipoahidi kuwatafuta wahusika na kuwaeleza mtazamo huo na kisha kusikiliza mawazo yao.

"Zitto alikwenda kuwaona Jaji Warioba na Dk. Salim na wakati huo, vikao vya Bunge vilikuwa vikiendelea Dodoma. Kule wale wazee walimsikiliza Zitto na kuona mapendekezo yao yana mantiki na kwa hiyo, Zitto akarudi kumweleza Dk. Slaa na baadaye wakapanga kukutana na Warioba na Salim.
"Walizungumza sana, wakafanya uchambuzi wa kina na njia bora zaidi ya kuweza kufikisha suala hilo kwa Rais Kikwete. Jaji Warioba aliombwa afanye kazi hiyo kuwa kiunganishi na taarifa zinasema baada ya kujiridhisha na hali ya mambo naye aliwasiliana na Ikulu na mchakato ukaanza.

Ndani ya Kamati Kuu CHADEMA

Habari za uhakika zinasema baada ya Dk. Slaa na Zitto kukubaliana na akina Warioba, kibarua kigumu kwao kilikuwa kuwasilisha mawazo yao mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA.
Taarifa hizo zinaelezwa kuwa Zitto hakuwa amehudhuria kikao hicho cha Kamati Kuu na hivyo, mzigo ulibaki kwa Dk. Slaa. Wakati huo, Zitto alikuwa amerejea kutoka India alikokuwa akitibiwa na hivyo hakuweza kushiriki kikao cha Kamati Kuu kwa sababu ya hali yake kiafya kutoimarika.

"Zitto aliitwa na Dk. Slaa kwenye Kamati Kuu amsaidie kueleza suala hilo, tulimwona alikuwa ametoka kuumwa alijitahidi sana kujieleza. Lakini kabla ya hapo, uchokozi wa wazo hilo uliibuliwa na Regia Mtema, ambaye alisema tukamwone Rais Kikwete ili tuzungumze naye....wajumbe karibu wote wakaguna wakimpinga na kumwona msaliti, wengine wakisema eti katumwa.

"Baada ya Zitto kuitwa na Dk. Slaa, ndipo alianza kutoa maelezo na hatimaye wajumbe wakaridhia. Na baadaye Mbowe akaandika barua kwenda kwa Rais kuomba kukutana naye ili kuwasilisha mapendekezo ya chama," kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Warioba ‘messanger' mtiifu

Habari zinasema baada ya Mbowe kuandika barua ya kuomba kukutana na Rais Kikwete, Jaji Warioba ndiye aliyekuwa ‘wakala' wa mawasiliano kati ya pande hizo mbili, yaani CHADEMA na Rais Kikwete.
"Barua ile alipewa Jaji Warioba naye binafsi kwa mkono wake aliifikisha Ikulu moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye baadaye alifanya mazungumzo na Kikwete pamoja na Dk. Salim na kisha kukubali ombi hilo la CHADEMA.
"Warioba akarejea tena kwa viongozi wa CHADEMA kwa ajili ya kutoa majibu kama ‘mjumbe' na akaeleza kuwa Rais hana tatizo kukutana na ujumbe wa CHADEMA kwa sababu hili ni suala la kitaifa, si la kwake pekee," anaeleza mtoa taarifa huyo.

Waziri Mkuu Pinda arudi Dar

Kutokana na kuanza kwa mchakato huo wa ‘kimya kimya' vyanzo vyetu vya habari kutoka bungeni vinaeleza kuwa mjadala wa sheria hiyo ulikuwa ukisogezwa mbele kwa maelezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kutoa nafasi kwa mchakato huo wa CHADEMA, Dk. Salim, Jaji Warioba na Rais Kikwete, ambao mpaka wakati huo haukuwa rasmi, ushike kasi.
Vyanzo vingine vya habari vimesema kuna wakati Waziri Mkuu Pinda alikwenda Dar es Salaam kutoka Dodoma kwa ajili ya mazungumzo kuhusu suala hilo na baada ya mjadala wa sheria hiyo kusogezwa mbele kujadiliwa bungeni kwa mara kadhaa, ilibidi mjadala uruhusiwe.

Milango ya Ikulu yafunguliwa

Baada ya kazi hiyo ya ‘kimya kimya' na baada ya Bunge kujadili, kurekebisha na hatimaye kupitisha muswada huo, ujumbe wa CHADEMA ulikaribishwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo.
Makaribisho hayo yaliwekwa bayana na Ikulu kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano na kuanza rasmi Novemba 27, mwaka jana, na kurejewa tena siku iliyofuata, Novemba 28, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo ya CHADEMA kuhusu sheria hiyo.
"Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa," inaeleza taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa baada ya duru la kwanza la mazungumzo hayo.

Kamati Kuu CCM yatia neno

Hata hivyo, wakati CHADEMA wakiwa wameomba kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilikuwa inaendelea na kikao chake mjini Dodoma, ambako ilimshauri Rais Kikwete kutanua wigo kwa kukutana na wadau wengine, ambao ni pamoja na vyama vingine vya siasa, ambavyo hata hivyo, tayari vimeonana na kuzungumza na Kikwete. Vyama hivyo ni Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.
Kwa upande mwingine, ushauri huo wa Kamati Kuu ya CCM ulizua mjadala mpya katika jamii, wengine wakiupinga na kuukosoa, wengine wakiuunga mkono lakini mwishowe, Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini, aliuzingatia.

Viongozi wanne waibuka vinara

Kama suala hili litafikia hatua nyingine katika hali isiyokuwa na malumbano tofauti na dalili za awali zilivyokuwa zikiashiria, basi, vinara wa kutuliza hali hiyo ni pamoja na Rais Kikwete binafsi ambaye aliridhia kukutana na wawakilishi wa makundi tofauti licha ya muswada kupitishwa na Bunge naye mwenyewe kuutia saini kuwa sheria.
"Angeweza kugoma na kutumia ubabe wa dola kulazimisha mambo, lakini hakufanya hivyo," kinaeleza chanzo chetu cha habari na kuongeza kuwa; "Shukurani za kipekee ziwaendee Dk. Slaa, Zitto, Dk. Salim na Jaji Warioba, wameonyesha upeo mkubwa wa kiuongozi."

Muswada kufanyiwa marekebisho

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa mazungumzo hayo pamoja na ya vyama vingine yamezingatiwa na Rais Jakaya Kikwete na kwa hiyo, katika mkutano ujao wa Bunge unaonza wiki ijayo mjini Dodoma, sheria hiyo ya mchakato wa Katiba mpya nchini itafanyiwa marekebisho.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kurejesha uwezekano wa viongozi wanasiasa, wakiwamo wabunge kuweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Katiba ambao watateuliwa na Rais, kinyume cha ilivyokuwa awali, wanasiasa wakizuiwa kuteuliwa wajumbe.

Marekebisho hayo yatawasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kabla ya mkutano huo kwisha na zipo taarifa nyingine kuwa huenda Rais Jakaya Kikwete akakutana na wabunge wa Chama cha Mapinduzi au kile alichopaswa kuzungumza nao kikafikishwa kwao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Inatarajiwa kuwa wabunge hao wataelezwa hatua kwa hatua kuhusu kilichojiri kati ya mkutano wa Rais Kikwete na vyama vya upinzani kuhusu muswada walioupitisha ambao hatimaye naye aliutia saini kuwa sheria.
Una habari nzuri sana lakini imeghoshiwa na kampeni zako kwa Zitto nimehesabu umemtaja Zitto mara 20 katika habari ndogo kama hii.
 
HABARI IMEPIKWA hiii!!!!!!!!!!!!!! Kama ZITTO ndiyo alikuwa source wa yote kwanini kwenye timu ya kwenda IKULU hakuwemo!!!! Na kipindi kile Zitto alikuwa India kwa matibabu!!!! hapa kuna dalili za kutaka kumfanya MBOWE yupoyupo tu, hakuwa na la mchango!!!!!!!

Kwa ulivyoandika hapa juu hakika uchaguzi ndani ya chadema umekaribia na ndio lengo kuu la mleta mada.Lakini akumbuke maneno ya Sumaye aliposema-Wanaotumia kalamu kuingia Ikulu baadaye watatumia risasi.Na tusubiri tuone yanayoendelea Chadema.
 
HABARI IMEPIKWA hiii!!!!!!!!!!!!!! Kama ZITTO ndiyo alikuwa source wa yote kwanini kwenye timu ya kwenda IKULU hakuwemo!!!! Na kipindi kile Zitto alikuwa India kwa matibabu!!!! hapa kuna dalili za kutaka kumfanya MBOWE yupoyupo tu, hakuwa na la mchango!!!!!!!

Umesoma kilichoandkiwa kwenye thread lakini?au umekimbilia kusoma post na kuanza kujibu post,mi nadhani ungesoma vizuri kwanza acha uvivu majibu ya mashaka yako yote yapo kwenye thread,issue imeanza siku nyingi mpaka zitto akaanza kuumwa mambo yalikua yameshaiva anarudi kutoka india ndio wakawa wanapakua kabisa na slaa umeona akamuomba licha kuwa mgonjwa ajikongoje aje kwenye kikao cha kamati kuu kuwasaidia kuweka sawa mambo,na akatii wito wa bosi wake huyo,sasa unataka nini zaidi,yeye kazi yake imekwisha,ikulu kawaacha waende wenye chama!yeye alikua anasadia kuepusha maandamano na amefanikiwa kuwarejesha wakubwa zake mezani basi inatosha,ndio maana hata warioba na salim huwaoni kwenye zile juice za ikulu,kazi yao walishaimaliza.
 
Una habari nzuri sana lakini imeghoshiwa na kampeni zako kwa Zitto nimehesabu umemtaja Zitto mara 20 katika habari ndogo kama hii.

Nenda hapo barabarani kwa muuza magazeti mwambie akupe gazeti la raia mwema ndio uanze kubishana nalo kutwa nzima leo,mimi nilikua nawapa kwa ufupi,lakini huko ndio kuna full mziki,mbowe yuko busy na posho na malupulupu ya kiongozi wa upinzani bungeni,ndio anapitwa an mambo mengi
 
mi naijua chadema kushinda wewe mzee,sisi ndio vijana wanzilishi enzi wa chadema,tulikua na wazee wetu kina mtei,bob na wengine,tulifanya siasa safi mpaka nyerere alitupenda na kutusifia sana,wewe enzi hizi ukiwa unakimbiza mwenge wa ccm pengine enzi hizo.

Hakuna anaemchafua free tunaeleza ukweli ambao na wewe unaujua,zitto ndio kachangia kwa kiasi kikubwa kuwaleta chadema mezani na kuachana na strategy ya kuandamana alioiamini mbowe wako,zitto kwa kuwa ana akili nyingi alitazama mbali,akawaonea huruma nyie mnaotumiwa na wanasiasa kuandamana,zitto hakua na cha kupoteza kwa kuwa katika hali ya kawaida ambao mngeenda kupambana na guvu za dola ni nyie kama ilivyokuwa arusha,viongozi wangebaki nyumbani na familia zao wakishiriki maandamano kwa njia ya simu,zote akaona kwa nini iwe hivyo na yeye yupo,kajitolea kuacha posho za vikao kusafiri kati ya dar na dom usiku na mchana kushawishi mazungumzo,huo ndio ukweli lazima credit yake aipate,nikuulize toka jamaa awe kiongozi wa upinzani bungeni amefanya nini cha kukumbukwa ukiacha kuwaongoza wabunge "wake" siku ile kutoka bungeni na kwenda kujifungia kwenye kichumba kimoja wapo kidogo kwenye majengo ya bunge kumsikiliza rais?mtihani wa kwanza ni posho za wabunge,vipi amejihangaisha vipi na hiyo issue?au kamuachia naibu wake ashughulike na suala la kugomea posho?
Ndio unaijua CDM na lengo lako ni kuharibu hali ya hewa kama ulivyotumwa na magamba!! unapopiga kampeni ukiwa ndani ya Chama ukipendacho huwezi kuwa hivi hata punguani ataelewa lengo lako OVU. Nimeona hata Farida Foxy amekuunga mkono hongera!!!!!
 
Nenda hapo barabarani kwa muuza magazeti mwambie akupe gazeti la raia mwema ndio uanze kubishana nalo kutwa nzima leo,mimi nilikua nawapa kwa ufupi,lakini huko ndio kuna full mziki,mbowe yuko busy na posho na malupulupu ya kiongozi wa upinzani bungeni,ndio anapitwa an mambo mengi
Malupulupu ni nini? una maana ya marupurupu!!??
 
Najua wapo watu hii hawatapenda kuisikia zitto alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha hili....lakini ndio hali halisi,lazima tuiseme .

Wadau mi nadhani baadhi yetu wakati umefika sasa tubadili mitazamo yetu kuhusu ZITTO KABWE;kiukweli kijana anaonyesha ukomavu wa kisiasa kila kukicha tofauti na vijana wengi ambao wanakimbilia posho tu;zitto kumbe anafanya mambo mengi bila kupiga mayowe wala kuita wapiga picha...hili nalisema kufuatia kugundua kuwa Mh. zitto kabwe kuwa chanzo cha mazungumzo maarufu yanayoendelea ikulu kati ya chadema na Rais kikwete,mambo yako hivi.....

Safari ilianza hivi; baada ya kuona mwenendo wa mijadala na mwelekeo wa baadhi ya viongozi wenzake, hasa katika siku ambazo CHADEMA kilikuwa kinatangaza kwamba kingeitisha maandamano nchi nzima kupinga mchakato wa katiba mpya uliokuwa umewasilishwa na Serikali bungeni, baadhi ya wanaCHADEMA na wengine miongoni mwa umma, walihisi kuwako kwa hatari ya kweli ya vurugu kuibuka nchini, ambayo isingekisaidia chama hicho au kundi jingine lolote, hivyo Zitto alifunga safari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ili kuteta na Dk. Slaa.

Katika mazungumzo yao, vyanzo kadhaa vya habari vimesema, hoja ilikuwa ni umuhimu wa kuchukua njia ya mazungumzo katika suala la mchakato wa katiba mpya, kuliko njia ya maandamano. Lakini Dk. Slaa amekaririwa akiashiria kwamba ilikuwa vigumu zaidi kuanzisha njia ya mazungumzo kwake kuliko njia ya shinikizo kupitia maandamano.

Raia Mwema limeambiwa kwamba kutokana na ugumu huo, Dk. Slaa amekaririwa kumueleza Zitto kuwa wanaweza, katika kufikia kupata muda wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete, kuwatumia wazee wenye utulivu na busara, wasio na misimamo mikali ya kisiasa, wenye kutanguliza mbele maslahi ya nchi na wanaosimamia zaidi nguvu ya hoja, ambao miongoni mwao ni Dk. Salim na Jaji Warioba.

Habari zinasema, tatizo kubwa alilokuwanalo Dk. Slaa katika kuwafikia wazee hao ni kwamba hakuwa na ukaribu wa kiasi hicho nao na Raia Mwema limeelezwa kwamba katika mazingira hayo ndipo Zitto alipoahidi kuwatafuta wahusika na kuwaeleza mtazamo huo na kisha kusikiliza mawazo yao.

“Zitto alikwenda kuwaona Jaji Warioba na Dk. Salim na wakati huo, vikao vya Bunge vilikuwa vikiendelea Dodoma. Kule wale wazee walimsikiliza Zitto na kuona mapendekezo yao yana mantiki na kwa hiyo, Zitto akarudi kumweleza Dk. Slaa na baadaye wakapanga kukutana na Warioba na Salim.
“Walizungumza sana, wakafanya uchambuzi wa kina na njia bora zaidi ya kuweza kufikisha suala hilo kwa Rais Kikwete. Jaji Warioba aliombwa afanye kazi hiyo kuwa kiunganishi na taarifa zinasema baada ya kujiridhisha na hali ya mambo naye aliwasiliana na Ikulu na mchakato ukaanza.

Ndani ya Kamati Kuu CHADEMA

Habari za uhakika zinasema baada ya Dk. Slaa na Zitto kukubaliana na akina Warioba, kibarua kigumu kwao kilikuwa kuwasilisha mawazo yao mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA.
Taarifa hizo zinaelezwa kuwa Zitto hakuwa amehudhuria kikao hicho cha Kamati Kuu na hivyo, mzigo ulibaki kwa Dk. Slaa. Wakati huo, Zitto alikuwa amerejea kutoka India alikokuwa akitibiwa na hivyo hakuweza kushiriki kikao cha Kamati Kuu kwa sababu ya hali yake kiafya kutoimarika.

“Zitto aliitwa na Dk. Slaa kwenye Kamati Kuu amsaidie kueleza suala hilo, tulimwona alikuwa ametoka kuumwa alijitahidi sana kujieleza. Lakini kabla ya hapo, uchokozi wa wazo hilo uliibuliwa na Regia Mtema, ambaye alisema tukamwone Rais Kikwete ili tuzungumze naye....wajumbe karibu wote wakaguna wakimpinga na kumwona msaliti, wengine wakisema eti katumwa.

“Baada ya Zitto kuitwa na Dk. Slaa, ndipo alianza kutoa maelezo na hatimaye wajumbe wakaridhia. Na baadaye Mbowe akaandika barua kwenda kwa Rais kuomba kukutana naye ili kuwasilisha mapendekezo ya chama,” kinaeleza chanzo chetu cha habari.

Warioba ‘messanger’ mtiifu

Habari zinasema baada ya Mbowe kuandika barua ya kuomba kukutana na Rais Kikwete, Jaji Warioba ndiye aliyekuwa ‘wakala’ wa mawasiliano kati ya pande hizo mbili, yaani CHADEMA na Rais Kikwete.
“Barua ile alipewa Jaji Warioba naye binafsi kwa mkono wake aliifikisha Ikulu moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye baadaye alifanya mazungumzo na Kikwete pamoja na Dk. Salim na kisha kukubali ombi hilo la CHADEMA.
“Warioba akarejea tena kwa viongozi wa CHADEMA kwa ajili ya kutoa majibu kama ‘mjumbe’ na akaeleza kuwa Rais hana tatizo kukutana na ujumbe wa CHADEMA kwa sababu hili ni suala la kitaifa, si la kwake pekee,” anaeleza mtoa taarifa huyo.

Waziri Mkuu Pinda arudi Dar

Kutokana na kuanza kwa mchakato huo wa ‘kimya kimya’ vyanzo vyetu vya habari kutoka bungeni vinaeleza kuwa mjadala wa sheria hiyo ulikuwa ukisogezwa mbele kwa maelezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kutoa nafasi kwa mchakato huo wa CHADEMA, Dk. Salim, Jaji Warioba na Rais Kikwete, ambao mpaka wakati huo haukuwa rasmi, ushike kasi.
Vyanzo vingine vya habari vimesema kuna wakati Waziri Mkuu Pinda alikwenda Dar es Salaam kutoka Dodoma kwa ajili ya mazungumzo kuhusu suala hilo na baada ya mjadala wa sheria hiyo kusogezwa mbele kujadiliwa bungeni kwa mara kadhaa, ilibidi mjadala uruhusiwe.

Milango ya Ikulu yafunguliwa

Baada ya kazi hiyo ya ‘kimya kimya’ na baada ya Bunge kujadili, kurekebisha na hatimaye kupitisha muswada huo, ujumbe wa CHADEMA ulikaribishwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo.
Makaribisho hayo yaliwekwa bayana na Ikulu kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano na kuanza rasmi Novemba 27, mwaka jana, na kurejewa tena siku iliyofuata, Novemba 28, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo ya CHADEMA kuhusu sheria hiyo.
“Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa,” inaeleza taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa baada ya duru la kwanza la mazungumzo hayo.

Kamati Kuu CCM yatia neno

Hata hivyo, wakati CHADEMA wakiwa wameomba kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilikuwa inaendelea na kikao chake mjini Dodoma, ambako ilimshauri Rais Kikwete kutanua wigo kwa kukutana na wadau wengine, ambao ni pamoja na vyama vingine vya siasa, ambavyo hata hivyo, tayari vimeonana na kuzungumza na Kikwete. Vyama hivyo ni Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.
Kwa upande mwingine, ushauri huo wa Kamati Kuu ya CCM ulizua mjadala mpya katika jamii, wengine wakiupinga na kuukosoa, wengine wakiuunga mkono lakini mwishowe, Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini, aliuzingatia.

Viongozi wanne waibuka vinara

Kama suala hili litafikia hatua nyingine katika hali isiyokuwa na malumbano tofauti na dalili za awali zilivyokuwa zikiashiria, basi, vinara wa kutuliza hali hiyo ni pamoja na Rais Kikwete binafsi ambaye aliridhia kukutana na wawakilishi wa makundi tofauti licha ya muswada kupitishwa na Bunge naye mwenyewe kuutia saini kuwa sheria.
“Angeweza kugoma na kutumia ubabe wa dola kulazimisha mambo, lakini hakufanya hivyo,” kinaeleza chanzo chetu cha habari na kuongeza kuwa; “Shukurani za kipekee ziwaendee Dk. Slaa, Zitto, Dk. Salim na Jaji Warioba, wameonyesha upeo mkubwa wa kiuongozi.”

Muswada kufanyiwa marekebisho

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa mazungumzo hayo pamoja na ya vyama vingine yamezingatiwa na Rais Jakaya Kikwete na kwa hiyo, katika mkutano ujao wa Bunge unaonza wiki ijayo mjini Dodoma, sheria hiyo ya mchakato wa Katiba mpya nchini itafanyiwa marekebisho.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kurejesha uwezekano wa viongozi wanasiasa, wakiwamo wabunge kuweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Katiba ambao watateuliwa na Rais, kinyume cha ilivyokuwa awali, wanasiasa wakizuiwa kuteuliwa wajumbe.

Marekebisho hayo yatawasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kabla ya mkutano huo kwisha na zipo taarifa nyingine kuwa huenda Rais Jakaya Kikwete akakutana na wabunge wa Chama cha Mapinduzi au kile alichopaswa kuzungumza nao kikafikishwa kwao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Inatarajiwa kuwa wabunge hao wataelezwa hatua kwa hatua kuhusu kilichojiri kati ya mkutano wa Rais Kikwete na vyama vya upinzani kuhusu muswada walioupitisha ambao hatimaye naye aliutia saini kuwa sheria.

Makala yako ni ya kigombanishi!!!!!! kwani Zitto akitoa wazo ndani chama si anatimiza wajibu wake? Usitake kuwagombanisha watu!!! Kama kiongozi wa CHADEMA ZITTO ana haki ya kutoa maoni na mawazo na kisha kukubaliwa kwa pamoja. Mbona suala la posho, yeye ndiye aliyelianzisha na kutaka posho zake ziende Kigoma, hilo hukusema na kwa kuwa ni suala la fedha,,, MBOWE alivyoanza kulisemea akaonekana yeye ana hela za kutosha hataki wenzake wapate na mwanzilishi wa hoja akaachwa!!!!!!

Nadhani habari yako haina dalili ya kujenga!!! nilitegemea basi utuonyeshe zaidi jitihada za Salim na Warioba kushirikiana na kukubaliana na CHADEMA kuliko chama chao cha CCM, lakini ulivyoiandika ni dhahiri unataka kuonyesha utendaji na uongozi wa CHADEMA unafanya kazi kwa kuviziana!!! CHAMA ni vikao, na wazo lolote linaamuliwa kwenye vikao na linakuwa wazo la Chama!!!!

Acha uchonganishi!!!!!!!! tuna waamini viongozi wa CHADEMA ni watu wenye kutumia busara na kuangalia maslahi ya taifa. Badala ya kuupongeza uongozi mzima kwa kuafikiana kwenda kumwona Kikwete wewe unaanza kuangalia nani alifanya nini kwenye kikao. Sasa unaandika hii makala kwa faida ya nani?

Ndiyo maana MKAPA aliwaita waandishi wa Tanzania ni waandishi uchwara!! maana wanapelekwa pelekwa tu!!!!

Nafikiti tuwapongeze wote!!! kuanzia Rais kwa kuangalia uzalendo na kukubali kuongea na watu aliotofautina nao lakini kwa CHADEMA Kususa Bungeni ndiyo msukumo mkubwa uliofanya JK aliwaite Ikulu. Wasingetoka wakashiriki mchakato, angewaita wanini kama walichangia na kupitisha Muswada. Halafu mwandishi wa Makala hii alipinga sana CHADEMA kutoka, leo anakuja na story nyinyine
. I hate this kind of Journalist.
 
Ndio unaijua CDM na lengo lako ni kuharibu hali ya hewa kama ulivyotumwa na magamba!! unapopiga kampeni ukiwa ndani ya Chama ukipendacho huwezi kuwa hivi hata punguani ataelewa lengo lako OVU. Nimeona hata Farida Foxy amekuunga mkono hongera!!!!!

wewe bado unafikiri jamii forum ni mali ya chadema na unadhani kila anaeingia ni chadema!!!ur very wrong mzee,ila habri ndio,watu wote makao makuu marehemu Regia angekuwepo angetusaidia hapa,watu wote cdm makao makuu sio siri wanajua part aliyoplay zitto kufanikisha vile vikao vya ilkulu mabavyo kina mbowe,mnyika,tundu lisa na wengine tunawaona wanavichekelea kwenye makochi ya ikulu,raha mustarehe,watu wamehangaika havikuja hivi hivi tu kazi imefanyika mzee,sema zitto sio mtu wa misifa na kupiga mayowe,ndio maana unaona kimya.
 
Hivi kuna kuna watu wanampenda mnafiki zitto kabwe makubwa(watakuwa ni ccm na cuf hawa ili chama kife).muwekeni basi agombee urais muone kama hatapata kura hata laki tano.na mmlinganishe na slaa.watu tunajua kutofautisha kati ya kondoo na mbuzi.
 
Umesoma kilichoandkiwa kwenye thread lakini?au umekimbilia kusoma post na kuanza kujibu post,mi nadhani ungesoma vizuri kwanza acha uvivu majibu ya mashaka yako yote yapo kwenye thread,issue imeanza siku nyingi mpaka zitto akaanza kuumwa mambo yalikua yameshaiva anarudi kutoka india ndio wakawa wanapakua kabisa na slaa umeona akamuomba licha kuwa mgonjwa ajikongoje aje kwenye kikao cha kamati kuu kuwasaidia kuweka sawa mambo,na akatii wito wa bosi wake huyo,sasa unataka nini zaidi,yeye kazi yake imekwisha,ikulu kawaacha waende wenye chama!yeye alikua anasadia kuepusha maandamano na amefanikiwa kuwarejesha wakubwa zake mezani basi inatosha,ndio maana hata warioba na salim huwaoni kwenye zile juice za ikulu,kazi yao walishaimaliza.

Mkuu unataka kila mtu aelewe kama ulivyoelewa wewe?
 
wewe bado unafikiri jamii forum ni mali ya chadema na unadhani kila anaeingia ni chadema!!!ur very wrong mzee,ila habri ndio,watu wote makao makuu marehemu Regia angekuwepo angetusaidia hapa,watu wote cdm makao makuu sio siri wanajua part aliyoplay zitto kufanikisha vile vikao vya ilkulu mabavyo kina mbowe,mnyika,tundu lisa na wengine tunawaona wanavichekelea kwenye makochi ya ikulu,raha mustarehe,watu wamehangaika havikuja hivi hivi tu kazi imefanyika mzee,sema zitto sio mtu wa misifa na kupiga mayowe,ndio maana unaona kimya.

Kwa nini unatoka povu hivi? Kuna lingine au?
 
Makala yako ni ya kigombanishi!!!!!! kwani Zitto akitoa wazo ndani chama si anatimiza wajibu wake? Usitake kuwagombanisha watu!!! Kama kiongozi wa CHADEMA ZITTO ana haki ya kutoa maoni na mawazo na kisha kukubaliwa kwa pamoja. Mbona suala la posho, yeye ndiye aliyelianzisha na kutaka posho zake ziende Kigoma, hilo hukusema na kwa kuwa ni suala la fedha,,, MBOWE alivyoanza kulisemea akaonekana yeye ana hela za kutosha hataki wenzake wapate na mwanzilishi wa hoja akaachwa!!!!!!

Nadhani habari yako haina dalili ya kujenga!!! nilitegemea basi utuonyeshe zaidi jitihada za Salim na Warioba kushirikiana na kukubaliana na CHADEMA kuliko chama chao cha CCM, lakini ulivyoiandika ni dhahiri unataka kuonyesha utendaji na uongozi wa CHADEMA unafanya kazi kwa kuviziana!!! CHAMA ni vikao, na wazo lolote linaamuliwa kwenye vikao na linakuwa wazo la Chama!!!!

Acha uchonganishi!!!!!!!! tuna waamini viongozi wa CHADEMA ni watu wenye kutumia busara na kuangalia maslahi ya taifa. Badala ya kuupongeza uongozi mzima kwa kuafikiana kwenda kumwona Kikwete wewe unaanza kuangalia nani alifanya nini kwenye kikao. Sasa unaandika hii makala kwa faida ya nani?

Ndiyo maana MKAPA aliwaita waandishi wa Tanzania ni waandishi uchwara!! maana wanapelekwa pelekwa tu!!!!

Nafikiti tuwapongeze wote!!! kuanzia Rais kwa kuangalia uzalendo na kukubali kuongea na watu aliotofautina nao lakini kwa CHADEMA Kususa Bungeni ndiyo msukumo mkubwa uliofanya JK aliwaite Ikulu. Wasingetoka wakashiriki mchakato, angewaita wanini kama walichangia na kupitisha Muswada. Halafu mwandishi wa Makala hii alipinga sana CHADEMA kutoka, leo anakuja na story nyinyine
. I hate this kind of Journalist.

Mimi nilikusa najaribu kuweka kumbukumbu sawa na kusema kile ambacho watu hawapendi kukisikia lakini kipo,hiyo ndio principle yangu,nasema yale ambayo watu hawapendi kusikia,mi nasema tu sijali;slaa anajua kitu alichofanaya zitto na part aliyoplay,tatizo kuna watu huko chadema kwenu hampendi kusikia wakipata credit kwa hofu ya urais 2015 japo zitto kaweka wazi hajafikiria kugombea so far lakini bado mna weweseka tu,hii haina uhusiano na urais wadau,iko kizalendo zaidi na inaonyesha ukomavu na busara za zkiuongozi alizonazo kijana,tumpe credit yake hapa, kafanya na matokeo yanaonekana,kishaacha alama,huo ndio uongozi,kuacha alama!
 
Mkuu Asante sana.Huyu mwandishi Godifrey Dilunga tumeshamjadili sana hapa.Ni mtu ambaye siku zote anaamini Chadema ni mbaya na haina viongozi makini.Alichokiandika ni kujaribu kuleta mgogoro kati ya Mbowe na viongozi wenzake.Si ajabu huyu mwandishi ndiye aliyeleta hii mada kwa jina bandia.Nawashauri wana Chadema puuzeni hii makala na haina jema lolote kwa chama
 
...busara za dk. Slaa siku zote zimeipeleka nchi hii mahali salama na pa amani...namheshimu dokta kuliko kikwete...mtu anayefanya mambo yake kwa kuogopa eti wenzake kwenye chama hawatamwelewa...siku atafanya kitu cha ajabu ili mradi tu awaridhishe wenzake kwenye chama...conglatulation to dokta slaa...
 
Mkuu unataka kila mtu aelewe kama ulivyoelewa wewe?

mzee hii sio bible kusema kila anatafsiri yake,kitu kiko wazi kabisa usichoelewa kipi ambacho mimi na mwingine tumekielewa,make it easy man why u wanna complicate kitu easy kama hiki,tatizo hapa ni zitto,ndio mana mmehamaki,angekua yeyote hata mabere marando au shibuda kusingekua na tatizo.
 
Haya mapovu yanakudondoka kwa sababu sijauona ushujaa wa Zitto kwenye ishu hii? Unataka watanzania wote wamtazame Zitto kwa jicho hilo hilo unalomtazamia wewe? Ikiwa hivyo Zitto hamalizi mwaka atakuwa ameporomoka kisiasa kwa kasi ya ajabu. Unamwona Zitto hivyo leo kwa sababu hajawahi kuziba masikio kusikiliza hoja za wanaompinga
Mzito! Achana na KIM ni GAMBA lililotumwa kuharibu hali ya hewa CDM! huoni anavyoshupalia jambo! Achana naye kabisa mtambue tu kama Gamba!!!
 
...busara za dk. Slaa siku zote zimeipeleka nchi hii mahali salama na pa amani...namheshimu dokta kuliko kikwete...mtu anayefanya mambo yake kwa kuogopa eti wenzake kwenye chama hawatamwelewa...siku atafanya kitu cha ajabu ili mradi tu awaridhishe wenzake kwenye chama...conglatulation to dokta slaa...

mi nampongeza zitto zaidi kwa kumlainisha dokta na kumfanya aache kuamini katika maandamano,kwa kuwa yangetuumiza sisi kuliko wao viongozi mwisho wa siku,ila slaa nae nampongeza kwa kukubali kulainika na kupunguza kile kisirani chake toka akose urais!
 
Mimi nilikusa najaribu kuweka kumbukumbu sawa na kusema kile ambacho watu hawapendi kukisikia lakini kipo,hiyo ndio principle yangu,nasema yale ambayo watu hawapendi kusikia,mi nasema tu sijali;slaa anajua kitu alichofanaya zitto na part aliyoplay,tatizo kuna watu huko chadema kwenu hampendi kusikia wakipata credit kwa hofu ya urais 2015 japo zitto kaweka wazi hajafikiria kugombea so far lakini bado mna weweseka tu,hii haina uhusiano na urais wadau,iko kizalendo zaidi na inaonyesha ukomavu na busara za zkiuongozi alizonazo kijana,tumpe credit yake hapa, kafanya na matokeo yanaonekana,kishaacha alama,huo ndio uongozi,kuacha alama!

Shusha mori mzee mwenye kustahili sifa zinakuja tu wala usiwe na wasiwasi
 
Back
Top Bottom