Warioba, Salim, Zitto na Slaa washirikiana kufanikisha mazungumzo ya Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba, Salim, Zitto na Slaa washirikiana kufanikisha mazungumzo ya Ikulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Jan 26, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Najua wapo watu hii hawatapenda kuisikia zitto alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha hili....lakini ndio hali halisi,lazima tuiseme .

  Wadau mi nadhani baadhi yetu wakati umefika sasa tubadili mitazamo yetu kuhusu ZITTO KABWE;kiukweli kijana anaonyesha ukomavu wa kisiasa kila kukicha tofauti na vijana wengi ambao wanakimbilia posho tu; Zitto kumbe anafanya mambo mengi bila kupiga mayowe wala kuita wapiga picha...hili nalisema kufuatia kugundua kuwa Mh. zitto kabwe kuwa chanzo cha mazungumzo maarufu yanayoendelea ikulu kati ya chadema na Rais kikwete,mambo yako hivi.....

  Safari ilianza hivi; baada ya kuona mwenendo wa mijadala na mwelekeo wa baadhi ya viongozi wenzake, hasa katika siku ambazo CHADEMA kilikuwa kinatangaza kwamba kingeitisha maandamano nchi nzima kupinga mchakato wa katiba mpya uliokuwa umewasilishwa na Serikali bungeni, baadhi ya wanaCHADEMA na wengine miongoni mwa umma, walihisi kuwako kwa hatari ya kweli ya vurugu kuibuka nchini, ambayo isingekisaidia chama hicho au kundi jingine lolote, hivyo Zitto alifunga safari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ili kuteta na Dk. Slaa.


  Katika mazungumzo yao, vyanzo kadhaa vya habari vimesema, hoja ilikuwa ni umuhimu wa kuchukua njia ya mazungumzo katika suala la mchakato wa katiba mpya, kuliko njia ya maandamano. Lakini Dk. Slaa amekaririwa akiashiria kwamba ilikuwa vigumu zaidi kuanzisha njia ya mazungumzo kwake kuliko njia ya shinikizo kupitia maandamano.

  Raia Mwema limeambiwa kwamba kutokana na ugumu huo, Dk. Slaa amekaririwa kumueleza Zitto kuwa wanaweza, katika kufikia kupata muda wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete, kuwatumia wazee wenye utulivu na busara, wasio na misimamo mikali ya kisiasa, wenye kutanguliza mbele maslahi ya nchi na wanaosimamia zaidi nguvu ya hoja, ambao miongoni mwao ni Dk. Salim na Jaji Warioba.

  Habari zinasema, tatizo kubwa alilokuwanalo Dk. Slaa katika kuwafikia wazee hao ni kwamba hakuwa na ukaribu wa kiasi hicho nao na Raia Mwema limeelezwa kwamba katika mazingira hayo ndipo Zitto alipoahidi kuwatafuta wahusika na kuwaeleza mtazamo huo na kisha kusikiliza mawazo yao.

  "Zitto alikwenda kuwaona Jaji Warioba na Dk. Salim na wakati huo, vikao vya Bunge vilikuwa vikiendelea Dodoma. Kule wale wazee walimsikiliza Zitto na kuona mapendekezo yao yana mantiki na kwa hiyo, Zitto akarudi kumweleza Dk. Slaa na baadaye wakapanga kukutana na Warioba na Salim.
  "Walizungumza sana, wakafanya uchambuzi wa kina na njia bora zaidi ya kuweza kufikisha suala hilo kwa Rais Kikwete. Jaji Warioba aliombwa afanye kazi hiyo kuwa kiunganishi na taarifa zinasema baada ya kujiridhisha na hali ya mambo naye aliwasiliana na Ikulu na mchakato ukaanza.

  Ndani ya Kamati Kuu CHADEMA

  Habari za uhakika zinasema baada ya Dk. Slaa na Zitto kukubaliana na akina Warioba, kibarua kigumu kwao kilikuwa kuwasilisha mawazo yao mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA.
  Taarifa hizo zinaelezwa kuwa Zitto hakuwa amehudhuria kikao hicho cha Kamati Kuu na hivyo, mzigo ulibaki kwa Dk. Slaa. Wakati huo, Zitto alikuwa amerejea kutoka India alikokuwa akitibiwa na hivyo hakuweza kushiriki kikao cha Kamati Kuu kwa sababu ya hali yake kiafya kutoimarika.

  "Zitto aliitwa na Dk. Slaa kwenye Kamati Kuu amsaidie kueleza suala hilo, tulimwona alikuwa ametoka kuumwa alijitahidi sana kujieleza. Lakini kabla ya hapo, uchokozi wa wazo hilo uliibuliwa na Regia Mtema, ambaye alisema tukamwone Rais Kikwete ili tuzungumze naye....wajumbe karibu wote wakaguna wakimpinga na kumwona msaliti, wengine wakisema eti katumwa.

  "Baada ya Zitto kuitwa na Dk. Slaa, ndipo alianza kutoa maelezo na hatimaye wajumbe wakaridhia. Na baadaye Mbowe akaandika barua kwenda kwa Rais kuomba kukutana naye ili kuwasilisha mapendekezo ya chama," kinaeleza chanzo chetu cha habari.

  Warioba ‘messanger' mtiifu

  Habari zinasema baada ya Mbowe kuandika barua ya kuomba kukutana na Rais Kikwete, Jaji Warioba ndiye aliyekuwa ‘wakala' wa mawasiliano kati ya pande hizo mbili, yaani CHADEMA na Rais Kikwete.
  "Barua ile alipewa Jaji Warioba naye binafsi kwa mkono wake aliifikisha Ikulu moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye baadaye alifanya mazungumzo na Kikwete pamoja na Dk. Salim na kisha kukubali ombi hilo la CHADEMA.
  "Warioba akarejea tena kwa viongozi wa CHADEMA kwa ajili ya kutoa majibu kama ‘mjumbe' na akaeleza kuwa Rais hana tatizo kukutana na ujumbe wa CHADEMA kwa sababu hili ni suala la kitaifa, si la kwake pekee," anaeleza mtoa taarifa huyo.

  Waziri Mkuu Pinda arudi Dar

  Kutokana na kuanza kwa mchakato huo wa ‘kimya kimya' vyanzo vyetu vya habari kutoka bungeni vinaeleza kuwa mjadala wa sheria hiyo ulikuwa ukisogezwa mbele kwa maelezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kutoa nafasi kwa mchakato huo wa CHADEMA, Dk. Salim, Jaji Warioba na Rais Kikwete, ambao mpaka wakati huo haukuwa rasmi, ushike kasi.
  Vyanzo vingine vya habari vimesema kuna wakati Waziri Mkuu Pinda alikwenda Dar es Salaam kutoka Dodoma kwa ajili ya mazungumzo kuhusu suala hilo na baada ya mjadala wa sheria hiyo kusogezwa mbele kujadiliwa bungeni kwa mara kadhaa, ilibidi mjadala uruhusiwe.

  Milango ya Ikulu yafunguliwa

  Baada ya kazi hiyo ya ‘kimya kimya' na baada ya Bunge kujadili, kurekebisha na hatimaye kupitisha muswada huo, ujumbe wa CHADEMA ulikaribishwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo.
  Makaribisho hayo yaliwekwa bayana na Ikulu kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano na kuanza rasmi Novemba 27, mwaka jana, na kurejewa tena siku iliyofuata, Novemba 28, kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo ya CHADEMA kuhusu sheria hiyo.
  "Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa," inaeleza taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa baada ya duru la kwanza la mazungumzo hayo.

  Kamati Kuu CCM yatia neno

  Hata hivyo, wakati CHADEMA wakiwa wameomba kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya mazungumzo, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilikuwa inaendelea na kikao chake mjini Dodoma, ambako ilimshauri Rais Kikwete kutanua wigo kwa kukutana na wadau wengine, ambao ni pamoja na vyama vingine vya siasa, ambavyo hata hivyo, tayari vimeonana na kuzungumza na Kikwete. Vyama hivyo ni Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.
  Kwa upande mwingine, ushauri huo wa Kamati Kuu ya CCM ulizua mjadala mpya katika jamii, wengine wakiupinga na kuukosoa, wengine wakiuunga mkono lakini mwishowe, Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho kikongwe nchini, aliuzingatia.

  Viongozi wanne waibuka vinara

  Kama suala hili litafikia hatua nyingine katika hali isiyokuwa na malumbano tofauti na dalili za awali zilivyokuwa zikiashiria, basi, vinara wa kutuliza hali hiyo ni pamoja na Rais Kikwete binafsi ambaye aliridhia kukutana na wawakilishi wa makundi tofauti licha ya muswada kupitishwa na Bunge naye mwenyewe kuutia saini kuwa sheria.
  "Angeweza kugoma na kutumia ubabe wa dola kulazimisha mambo, lakini hakufanya hivyo," kinaeleza chanzo chetu cha habari na kuongeza kuwa; "Shukurani za kipekee ziwaendee Dk. Slaa, Zitto, Dk. Salim na Jaji Warioba, wameonyesha upeo mkubwa wa kiuongozi."

  Muswada kufanyiwa marekebisho

  Taarifa zaidi zinabainisha kuwa mazungumzo hayo pamoja na ya vyama vingine yamezingatiwa na Rais Jakaya Kikwete na kwa hiyo, katika mkutano ujao wa Bunge unaonza wiki ijayo mjini Dodoma, sheria hiyo ya mchakato wa Katiba mpya nchini itafanyiwa marekebisho.

  Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kurejesha uwezekano wa viongozi wanasiasa, wakiwamo wabunge kuweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Katiba ambao watateuliwa na Rais, kinyume cha ilivyokuwa awali, wanasiasa wakizuiwa kuteuliwa wajumbe.

  Marekebisho hayo yatawasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kabla ya mkutano huo kwisha na zipo taarifa nyingine kuwa huenda Rais Jakaya Kikwete akakutana na wabunge wa Chama cha Mapinduzi au kile alichopaswa kuzungumza nao kikafikishwa kwao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Inatarajiwa kuwa wabunge hao wataelezwa hatua kwa hatua kuhusu kilichojiri kati ya mkutano wa Rais Kikwete na vyama vya upinzani kuhusu muswada walioupitisha ambao hatimaye naye aliutia saini kuwa sheria.
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nilijua tu marekebisho ni kwa ajili ya wajumbe wa kamati na si vinginevyo, yaani ni ulaji tu
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Sijauona ushujaa wa Zitto bado
   
 4. T

  THE WHITE ELEPHANT Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani mboe wakati mambo yote yakiendelea nasikia alikua amelala usingizi akisubiri posho bungeni,huku dogo akipiga kazi kwa kushirikiana na wazee warioba na salim,na akafanikiwa kumuingiza king DR wa "phd"! dogo agombee tu urais,slaa atakua waziri mkuu,hakuna ubishi hapo,slaa bonge la mtendaji!
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Huwezi kuuona kwa kuwa umesha ji 'tune" hivyo katika kila jambo linalomuhususu zitto umejiapiza kutokuliunga mkono mpaka uchaguzi wa kumpata mgombea urais wa chadema 2015 uishe,ndio utapona ugonjwa unaokusumbua!lakini wenye macho na wanaotumia akili zao wanaona kila kitu1
   
 6. K

  KIFILI Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mh.Zitto ndiye aliyezua wazo hilo ambalo hata hivyo, lilipofikishwa kwenye Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu, marehemu Regia Mtema, lilipata wakati mgumu kiasi cha zitto licha ya kuwa mgonjwa akiwa ndio kwanza karejea toka india kupata matibabu kuitwa na Dk. Slaa kwenda kusaidia kutoa ufafanuzi zaidi.
   
 7. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr.slaa bwana kwa maandamano!anapeeenda.....yani yeye bado alikua anaamini njia bora ya kufikia suluhu ni maandamano tu,ona kijana mdogo masikini alijua athari za maandamano kwamba wanaoumiaga siku zote ni wapiga kura, viongozi wanajifungia vyumbani mara nyingi na kushiriki maandamano kwa njia ya simu za mkononi,kuulizia mmefikia wapi sasa?polisi hawajawavamia?...n.k.
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Uongozi ni pamoja na kufanya kazi na wenzako na kusikiliza maoni ya wenzako pia. Zitto sio kiongozi pekee kwenye chama na ndio maana hoja yake alimpelekea Slaa naye baada ya kusita sana aliikubali na ikawa agenda kwenye kamati kuu ambapo mwishowe ikaridhiwa.

  Shujaa hapa ni KAMATI KUU YA CDM sio Zitto. Hayo ya kukutana ma Salim na Warioba yalikuwa ni maamuzi ya viongozi(msije mkadhani hayo yalifanyika bila ya Mwenyekiti, Makamu wake, wakurugenzi na wazee wa chama walikuwa hawajui)
  hamumjengi Zitto mnambomoa kwa kumpa sifa za kijinga.

  Natambua Zitto anafanya kazi kubwa na inayoonekana hasa kwenye kamati yake ya Mashirika ya Umma. Nilikuwa Kigoma hivi karibuni ikiwa ni safari yangu ya 3 ndani ya miaka minne, kiukweli kijana amedhamiria kuwasaidia ndugu zake, lakini kwa hili; hakuna cha ushujaa hapa.
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Haya mapovu yanakudondoka kwa sababu sijauona ushujaa wa Zitto kwenye ishu hii? Unataka watanzania wote wamtazame Zitto kwa jicho hilo hilo unalomtazamia wewe? Ikiwa hivyo Zitto hamalizi mwaka atakuwa ameporomoka kisiasa kwa kasi ya ajabu. Unamwona Zitto hivyo leo kwa sababu hajawahi kuziba masikio kusikiliza hoja za wanaompinga
   
 10. T

  THE WHITE ELEPHANT Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana mzito Mbowe na Lissu ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia, Mbowe ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni wakati Lissu ni Mnadhimu wa kambi hiyo na wakati ‘mchoro' wa mazungumzo unaibuliwa, wao walikuwa bungeni wakiendelea na vikao vya Bunge, Novemba, mwaka jana!

  Kwanini hii hamtaki kuikubali, M boe na kina Lissu wamekuja kufahamu baadae mwaka huu tena,wakati harkati zilianza novemba last year,ni kawaida ya mamba haya kwanza kuanza na wachache ndio hufanikiwa lakini wangeanza wooote wasingefika popote,kwa hili Zitto tunampa credit, japo yeye hataki kusema amekaa kimya kama hajui kinachoendelea hata vikao vya ikulu yeye na Slaa hawakuwemo.

  Ni hivi juzi tu ndio mwenzake Slaa tumemuona akiingia ikulu, lakini yeye hatujamuona, kazi yake ilishaisha, sasa ni zamu ya wauza sura!
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,177
  Trophy Points: 280
  Kuna baadhi ya taarifa unamisi wewe!, au umeamua kuziacha kimakusudi?
   
 12. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sasa ndo nimemjua Zito ni mtu wa namna gani kwa kazi hi aliyofanya na kutojionyesha naweza kusema ni hazina kubwa iliyopo ndani ya chadema ambayo haijapata wahi onekana.Pole kwa wasiomkubali pole kwa mzito kabwela mnaweza kumtafakari upya kwenye vichwa vyenu.Hongera mpambanaji Zito ndo mambo tunayotaka kutoka kwako.
   
 13. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Mh.Zitto ndo aina ya vijana tunaowahitaji,hana nongwa za kisiasa, creative wa aina yake,mwenye confidence ya aina yake,bobezi la uchumi anaetumia muda mwingi kufanya tafiti za kiuchumi badala ya kushinda Idara ya habari kuuza 'fuvu'.viva zitto zubeir kabwe,taratibu maadui zako kisiasa wataanza kuumbuka hasa Saed Kubenea na kipeperushi chake cha mwanahalisi.
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Binafsi naamini mashujaa ni Mbowe, Dr Slaa na kamati kuu yote kwa kukubali kuridhia mazungumzo na JK. Nasema hivyo kwa sababu walikuwa na uwezo wa kuyakataa haya mapendekezo ya Regia na Zitto lakini kutokana na kuwa visionary wakayakubali.
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo unataka kusema nini labda mzee,zitto hastahili credit hapa au?haya basi tumtaje mnyika pengine ndio utaona raha..au vipi,maana unaambiwa kabisa kwamba idea ilikua ni ya zitto lakini kwa makusudi tu umeamua kukataa..
   
 16. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wakati huo huo tumeambiwa Zitto na JK wako karibu nikimaanisha uhusiano wao siyo mbaya sana!!
   
 17. T

  THE WHITE ELEPHANT Member

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  zipi hizo kamanda?au unataka uwekewe gazeti zima nini?
   
 18. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wabongo bwana,yani umejitahidi kutumia kila ujanja wa kuandika mradi ili zitto tu asionekana,chuki zingine bwana yani unamchukuia mtu mpaka unashindwa kuficha hisia zako hata kwa muda tu,hii hatari,unamtaja slaa unamruka zitta aliempelekea slaa idea na kumlainisha abadili mawazo aache kuamini maandano ndio suluhu ya kila jambo..

  Unamuona mbowe kwa kuwa ndio anaoneka kwenye zile juice za ikulu mara kwa mara,unafikiri zile juice zimekuja hivi hivi tu kuna kazi ilifanyika nyuma ya pazia watu wakisamehe posho na kusafiri kutwa kati ya dar na dodoma kuwaandalia watu zile juice unazoziona kwenye mabilauli katika meza za ikulu!
   
 19. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ndio uliozaa unachokiona kinaendelea watu kupishana kwenye mageti ya ikulu..

  [​IMG]

  .............BORN TO BE A LEADER
   
 20. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe zitto ndie aliyewezesha hii kitu! Nimemvulia kofia kama ndio hivyo,maana kile kisirani cha slaa hakikua kidogo, sasa kuona kalainika kirahisi namna tulianza kupata mashaka tukajua kuna nguvu flani kutoka nje labda kwa mafisadi, kumbe Zitto ndio alimshika masikio hili ni jambo la kutia moyo sana hasa kutokana na umri wake hii inatufanya vijana tutembee kifua mbele kwamba na sisi tunaweza sio kila kitu wazee tu.

  Huyo dogo asingeyumbishwa na rostam pale katikati saa hizi angekua mbali sana kisiasa,lakini bado anayo nafasi hasa baada ya hili.
   
Loading...