Warioba: Msikurupuke kupitisha Katiba Mpya

Warioba: Msikurupuke kupitisha Katiba Mpya

5525

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
5,487
Reaction score
6,517
Bunda. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka Watanzania kutokurupuka kuipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa kuwa imeyaacha kando maoni yao mengi na akawataka waisome kwa makini kabla ya kuikubali au kuikataa.

Akiwa katika likizo ya wiki moja nyumbani kwake Bunda, Mkoa wa Mara, Jaji Warioba alialikwa na vijana wa mji huo kupitia Jukwaa lao la Uwazi na Fikra Yakinifu, wakiomba azungumze nao kuhusu masuala mbalimbali hasa mchakato wa Katiba Mpya.

Katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Harrieth, Jaji Warioba aliulizwa na kujibu maswali; anaionaje Katiba Inayopendekezwa na iwapo CCM imemgeuka kwa nini asihame chama?

Akijibu maswali hayo, Jaji Warioba alisema Katiba hiyo haina maoni yote ya wananchi kama Bunge Maalumu lilivyojinadi, bali yamewekwa machache ambayo hata hivyo yamo hata katika Katiba ya sasa.

Mathalan, alisema wananchi wengi walipendekeza kiwepo kipengele cha maadili ya viongozi ili kuwadhibiti dhidi ya vitendo viovu wanavyovifanya kwa sasa kama ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, lakini wajumbe wa Bunge walikirekebishana hadi kikapoteza maana.

Kwa kufanya hivyo, alisema wajumbe hao walionyesha wanafurahishwa na hali iliyopo ya viongozi kukosa uzalendo, uadilifu na kukosa uwajibikaji hata kuwasababishia Watanzania maisha magumu ambayo kupitia maoni yao, walikuwa wameyatafutia dawa kwa kupendekeza maadili yatambulike kikatiba.

Alisema wananchi walipendekeza muundo wa muungano wa serikali tatu ili kuondoa matatizo yaliyopo, kupatiwa madaraka ya kuwawajibisha wabunge wao pamoja na rais kupunguziwa madaraka, mambo ambayo yameondolewa na Bunge hilo Maalumu.

"Kazi yetu kama Tume ya kuandaa Katiba ya Watanzania tuliimaliza. Bunge nalo limemaliza kazi yake japo ina upungufu. Sasa kazi imebaki kwenu wenye Katiba; kuisoma iliyopendekezwa kwa makini kabla ya kuipigia kura," alisema Warioba.

Jaji Warioba alieleza kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge la Katiba, Samuel Sitta siku ya kukabidhi Katiba Inayopendekezwa kwa Rais, kwamba Bunge hilo limeweka ndani ya katiba hiyo asilimia 81 ya maoni ya Tume, akisema huo ni uongo mkubwa.

"Ukweli ni kwamba wamechukua asilimia 20 tu na kutupa nje asilimia iliyobaki na kubandika yaliyomo katika Katiba ya sasa ambayo hayawezi kuleta mabadiliko yoyote," alisema Jaji Warioba.

Hivyo, Jaji Warioba aliwataka Watanzania kwa umoja wao bila kujali tofauti zao za kisiasa, dini, rangi, kabila kuhakikisha kuwa wanapata Katiba Inayopendekezwa na kutumia muda mwingi kuisoma kabla ya kuipigia kura na kuwa wakikurupuka watajuta siku za usoni.

Akizungumzia hatima ya Muungano wa serikali mbili uliopo kwa sasa, Warioba alisema hachelei kusema kwamba huenda ukakumbana na changamoto nyingi siku za usoni iwapo wananchi watauridhia kupitia kura yao kwa vile asilimia kubwa ya Wazanzibari hawaukubali.

"Hapa napo kuna tatizo, Mpaka mgogoro uliopo miongoni mwa Wazanzibari umalizwe. Wao wenyewe wanataka kuendeleza tamaduni zao ndani ya Zanzibar wanayoitambua kama nchi huru. Sidhani kama watakubaliana," alisema Warioba.

Kuhusu kujitoa CCM, Jaji Warioba alisema hawezi kufanya hivyo, bali ataendelea kuwa mwanaCCM daima kwani anaamini katika chama hicho lakini akawaponda wanachama wenzake aliosema wanaweka masilahi binafsi mbele badala yale ya wananchi.

"Mimi ni mwanaCCM na nitadumu hivyo daima kwani ndicho chama ninachokiamini. Mimi siyo mwanachama masilahi ambaye akikosa kitu fulani au akiguswa kidogo tu anahamia chama kingine," alisema Jaji Warioba.

Chanzo: Mwananchi
 
HAhahaa Mzee Warioba tupo wote..hata wezangu ninawaambiaga kuwa miye ni MwanaCCM Radical sio Masalia au Maslahi. Wallah biashara imetubadilishia CCM we know..waumini wa kufuata miiko ya MwanaCCM kama inavyoonyeshwa kwenye katiba yetu ya Chama ni wachache mnoo..na hapa Jukwaani nadhani niko mwenyewe..Viva Warioba once an Angel you will always remain the one!!
 
Warioba Jaji anayejipambanua kama msomi asiyefungamana na upande wowote isipokuwa ule wenye masilahi mapana ya Taifa na wananchi
 
Rasimu ya Jaji Warioba ilikuwa ni ya kibaguzi inapingana haki za raia ya kuchagua na kuchaguliwa kwamba mbunge lazima na elimu ya kidato cha 4 na zaidi? Huu ni ubaguzi na siyo maoni ya wananchi.
 
Rasimu ya Warioba, Mbunge asiponekana miezi 6 awe amejifuta mwenyewe Ubunge je Warioba alitaka wabunge waende na madripu bungeni?
 
Rasimu ya Jaji Warioba ilikuwa ni ya kibaguzi inapingana haki za raia ya kuchagua na kuchaguliwa kwamba mbunge lazima na elimu ya kidato cha 4 na zaidi? Huu ni ubaguzi na siyo maoni ya wananchi.

nadhani maana yake ni kwamba mbunge akiwa na elimu angalau ya kidato cha nne anaweza kufafanua makabrasha yanayoletwa na serikali na kuweza kuisimamia serikali ipasavyo. Kama atakuwa hana uelewa wowote atawezaje kufanya kazi zake za kuwakilisha wananchi
 
Eti Rasimu ya Warioba inataka pawepo na benki kuu mbili kwenye nchi moja uliona wapi duniani?
[FONT=Times

Unataka kunambia mapinduzi ya zanzibar kumuondoa sultan nchi yao ikawa huru ni batili? Katiba ipi iliyoandika zanxibar na Tanganyika ni nchi1?
 
Eti Rasimu ya Warioba inataka pawepo na benki kuu mbili kwenye nchi moja uliona wapi duniani?

jinga hil tena apa warioba ni mtu makin.usituletee akil za kiunoni kwa baba yko p.u.m.b.u kabisa
 
Rasimu ya Jaji Warioba ilikuwa ni ya kibaguzi inapingana haki za raia ya kuchagua na kuchaguliwa kwamba mbunge lazima na elimu ya kidato cha 4 na zaidi? Huu ni ubaguzi na siyo maoni ya wananchi.

hahahahaa kwa hiyo ulieishia std.3 leo unautaka ubunge ndo uone ujabaguliwa acha kufuga tumbo ndo linakuongezea virus vya use*ng
 
Rasimu ya Jaji Warioba ilikuwa ni ya kibaguzi inapingana haki za raia ya kuchagua na kuchaguliwa kwamba mbunge lazima na elimu ya kidato cha 4 na zaidi? Huu ni ubaguzi na siyo maoni ya wananchi.
Kwa hiyo wewe unataka bunge letu liongozwe na watu waioishia darasa la saba, lakini wanajinadi kuwa maprofesa, kama yule mganga wa kienyeji, wa jimbo la Korogwe?!

Na CCM wamefanya hivyo makusudi, ili wabunge hao 'Vihiyo' washindwe kuisoma mikataba ya kifisadi, iliyoandikwa kwa lugha ya kimombo, ili watawala wetu waifanye nchi hii la kupora rasilimali za Taifa, katika design ya shamba la bibi, hadi mwisho wa Dunia!
 
nadhani maana yake ni kwamba mbunge akiwa na elimu angalau ya kidato cha nne anaweza kufafanua makabrasha yanayoletwa na serikali na kuweza kuisimamia serikali ipasavyo. Kama atakuwa hana uelewa wowote atawezaje kufanya kazi zake za kuwakilisha wananchi
kwa hiyo unataka kusema yule mgombea mwenza wa babu slaa 2010, angekuwa makamu mbumbumbu kupata kutokea karne ya 21 kama babu angetinga ikulu? maana kaishia primary.
 
bunda. Mwenyekiti wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba, jaji joseph warioba amewataka watanzania kutokurupuka kuipitisha katiba inayopendekezwa kwa kuwa imeyaacha kando maoni yao mengi na akawataka waisome kwa makini kabla ya kuikubali au kuikataa.

Akiwa katika likizo ya wiki moja nyumbani kwake bunda, mkoa wa mara, jaji warioba alialikwa na vijana wa mji huo kupitia jukwaa lao la uwazi na fikra yakinifu, wakiomba azungumze nao kuhusu masuala mbalimbali hasa mchakato wa katiba mpya.

Katika mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya harrieth, jaji warioba aliulizwa na kujibu maswali; anaionaje katiba inayopendekezwa na iwapo ccm imemgeuka kwa nini asihame chama?

Akijibu maswali hayo, jaji warioba alisema katiba hiyo haina maoni yote ya wananchi kama bunge maalumu lilivyojinadi, bali yamewekwa machache ambayo hata hivyo yamo hata katika katiba ya sasa.

Mathalan, alisema wananchi wengi walipendekeza kiwepo kipengele cha maadili ya viongozi ili kuwadhibiti dhidi ya vitendo viovu wanavyovifanya kwa sasa kama ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, lakini wajumbe wa bunge walikirekebishana hadi kikapoteza maana.

Kwa kufanya hivyo, alisema wajumbe hao walionyesha wanafurahishwa na hali iliyopo ya viongozi kukosa uzalendo, uadilifu na kukosa uwajibikaji hata kuwasababishia watanzania maisha magumu ambayo kupitia maoni yao, walikuwa wameyatafutia dawa kwa kupendekeza maadili yatambulike kikatiba.

Alisema wananchi walipendekeza muundo wa muungano wa serikali tatu ili kuondoa matatizo yaliyopo, kupatiwa madaraka ya kuwawajibisha wabunge wao pamoja na rais kupunguziwa madaraka, mambo ambayo yameondolewa na bunge hilo maalumu.

“kazi yetu kama tume ya kuandaa katiba ya watanzania tuliimaliza. Bunge nalo limemaliza kazi yake japo ina upungufu. Sasa kazi imebaki kwenu wenye katiba; kuisoma iliyopendekezwa kwa makini kabla ya kuipigia kura,” alisema warioba.

Jaji warioba alieleza kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa lililokuwa bunge la katiba, samuel sitta siku ya kukabidhi katiba inayopendekezwa kwa rais, kwamba bunge hilo limeweka ndani ya katiba hiyo asilimia 81 ya maoni ya tume, akisema huo ni uongo mkubwa.

“ukweli ni kwamba wamechukua asilimia 20 tu na kutupa nje asilimia iliyobaki na kubandika yaliyomo katika katiba ya sasa ambayo hayawezi kuleta mabadiliko yoyote,” alisema jaji warioba.

Hivyo, jaji warioba aliwataka watanzania kwa umoja wao bila kujali tofauti zao za kisiasa, dini, rangi, kabila kuhakikisha kuwa wanapata katiba inayopendekezwa na kutumia muda mwingi kuisoma kabla ya kuipigia kura na kuwa wakikurupuka watajuta siku za usoni.

Akizungumzia hatima ya muungano wa serikali mbili uliopo kwa sasa, warioba alisema hachelei kusema kwamba huenda ukakumbana na changamoto nyingi siku za usoni iwapo wananchi watauridhia kupitia kura yao kwa vile asilimia kubwa ya wazanzibari hawaukubali.

“hapa napo kuna tatizo, mpaka mgogoro uliopo miongoni mwa wazanzibari umalizwe. Wao wenyewe wanataka kuendeleza tamaduni zao ndani ya zanzibar wanayoitambua kama nchi huru. Sidhani kama watakubaliana,” alisema warioba.

Kuhusu kujitoa ccm, jaji warioba alisema hawezi kufanya hivyo, bali ataendelea kuwa mwanaccm daima kwani anaamini katika chama hicho lakini akawaponda wanachama wenzake aliosema wanaweka masilahi binafsi mbele badala yale ya wananchi.

“mimi ni mwanaccm na nitadumu hivyo daima kwani ndicho chama ninachokiamini. Mimi siyo mwanachama masilahi ambaye akikosa kitu fulani au akiguswa kidogo tu anahamia chama kingine,” alisema jaji warioba.

chanzo: Mwananchi

warioba ni jembe.ccm maslahi ndio kero.komaa mzee wetu tutafika haya mafisadi ya chama chako ndio kikwazo kwenye katiba
 
Duchi acha uongo na vinginevyo usichangie kama huna hoja.

Ukisema ni ubaguzi kuweka kiwango cha elimu mgombea ubjnge...je na je si ubaguzi kusema b18yrs ruksa jupiga kura lakini kugkmbea ubunge lazima ufikishe 21??? Na na vile vike katiba yenu ya sasa kusema mtu heyite mwenye 18yrs old ruksa kupiga kura lakini kugombea lazima uwe mwanachama cha siasa na ufikishe sijui 20+ yrs.

Duchi acha kudanganywa namwana ccm maslahi bali jaribu kuwa objective. Ni kawaida mambo mengi kuwekewa minimum requirements wala siyo kugombea ubunge tu.
 
Rasimu ya Warioba, Mbunge asiponekana miezi 6 awe amejifuta mwenyewe Ubunge je Warioba alitaka wabunge waende na madripu bungeni?

Wewe usipo onekana kazini kwako miezi sita unastahili kua mfanya kazi? Mbona kama hufikrii kabisa na ndo kutowajibika huko sasa utakaaje na mbunge akimaliza vikao miezi mitatu Dodoma anapitiliza dar anasubir kikao kingine haonekan mwaka mzima jimboni anamuwakilisha nani nahajui chochote kuhu jimbo lake
 
Back
Top Bottom