Warioba, kafara EPA kushitakiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba, kafara EPA kushitakiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 16, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Warioba, kafara EPA kushitakiwa

  Mwandishi Wetu Oktoba 15, 2008
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  Jeetu Patel na matajiri wenzake kupeta

  Ni funika kombe mwanaharamu apite

  KUNA uwezekano mkubwa kwamba Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba akaingizwa matatani kutokana na uchunguzi unaofanyika ndani ya kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Mwananchi Gold, Raia Mwema imeambiwa.

  Hayo yakiendelea, kuna habari pia kwamba karibuni Serikali itapeleka mahakamani kesi ya kuwashitaki wahusika ‘dhaifu' wa tuhuma za wizi wa Fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania hatua zote hizo zikilenga kufunika kombe mwanaharamu apite.

  Vyanzo kadha vya habari vimeiambia Raia Mwema kwamba kesi hizo zimekuwa zikiandaliwa ili pamoja na mambo mengine, zikianza ziweze kushusha joto la kisiasa lililopanda kutokana na kuonekana kana kwamba watawala hawachukui hatua thabiti juu ya tuhuma za ufisadi zinazowakabili wanasiasa na matajiri kadhaa walio karibu na chama tawala wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


  Kwa mujibu wa habari hizo, kesi hizo, zinatakiwa ziendelee hadi hata baada ya 2010 ili kutoa picha kwamba utawala umedhamiria kupambana na ufisadi hata kama kesi hizo zitakuwa zikitajwa tu na watuhumiwa, hasa wale wa EPA wakiwa ndani chini ya tuhuma kama za hujuma ya uchumi, kughushi na kula njama kuiba.

  Kama hatimaye zitafunguliwa katika kiasi cha wiki chache sasa kabla ya Oktoba 31 siku ambayo imetangazwa kuwa ya mwisho ya watuhumiwa kurejesha fedha za EPA, kesi hizo zitakuwa zikiendelea tu mahakamani kama ambavyo imekuwa ikiendelea nyingine ya aina hiyo ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania Italia, Profesa Costa Mahalu.


  Kwa upande wake Jaji Warioba, mmoja wa wakosoaji wakubwa wa jinsi vitendo vya kifisadi vinavyoshaniri nchini, anahusishwa na kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Mwananchi Gold ambamo yeye ni Mwenyekiti wa Bodi na ambako chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM) kinahusishwa.

  Taarifa za wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) zinaonyesha kuwa, Mwananchi Gold Company Limited ni kampuni binafsi ambayo wamiliki wake ni Benki Kuu ya Tanzania (hisa 500), Shirika la Maendeleo la Taifa ( NDC hisa 375), Mwananchi Trust Company Ltd (hisa 1,123) na Chimera Company Limited (hisa 500).

  Alipoulizwa wiki hii juu ya habari hizo za kushitakiwa, Jaji Warioba alisema kwamba hakuwa amesikia juu ya habari hizo lakini akasema pia kwamba alisoma tu magazetini siku kadhaa zilizopita kwamba maandalizi ya kesi hiyo yalikuwa mbioni.

  " Kweli sijasikia kuhusu kuwapo kwa kesi hiyo. Nilisoma tu wiki chache zilizopita katika gazeti moja kuwa kesi hiyo ipo," alisema Jaji Warioba.

  Mmoja wa maofisa waandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) yenye dhamana na uchunguzi wa kesi za aina hiyo ameiambia Raia Mwema kwamba kati ya kesi kadhaa inazoandaa TAKUKURU kesi ya Mwananchi Gold imo.

  Habari zaidi zimesema kwamba baadhi ya wakurugenzi wa Mwananchi Gold kama Yusuf Mushi wamepata kutafutwa wahojiwe lakini ikashindikana kwa ugonjwa na kwamba Mkurugenzi mwingine, Vulfrida Mahalu katika siku za karibuni amehojiwa mara mbili na TAKUKURU. Raia Mwema haikufanikiwa kuwapata kueleza undani wa mahojiano hayo.

  Kwa upande wa EPA wanaotajwa kufikishwa mahakamani ni wamiliki wa kampuni za Changanyikeni Residential Complex Limited, Malegesi Law Chambers, G&T International Limited na Karnel Meals Holdings Ltd.

  Nyaraka zinaonyesha kwamba Changanyikeni Residential Complex inamilikiwa na Jose Van de Merwe, Samson Mapunda na Charles Mabina wakati Maregesi Law Chambers inamilikiwa na Beredy Maregesi, ambaye pia anatajwa kumiliki kampuni ya G&T International Limited akiwa na mwenzake Octavio Timoth.

  Kampuni Karnel Meals Holdings Ltd inamilikiwa na Johnson Lukaza na Mwesigwa Rutakyamilwa Lukaza ikiwa imepata usajili Agosti 4, 1998.

  Habari zinasema ni Maregesi, Mapunda na Lukaza tu ambao ndio watakaofikishwa mahakani katika hatua inayozua minong'ono ya kuwa watuhumiwa wakubwa wa fedha za EPA wanakingiwa kifua kwa kuwa wana uhusiano wa karibu na chama tawala.

  " Ni kama sasa wanataka kutolewa kafara. Hata muda uliotolewa wa Oktoba 31 ni kama uliwalenga wao. Wamekuwa wakikataa kurudisha fedha wakidai kwamba wao walifanya kazi, walioiba ni hao ambao sasa wanaelezwa kwamba wamerudisha. Kwamba wao sasa wanataka kushitakiwa huku wakubwa wakiachwa maana yake kubwa ni kwamba watawala wanafunika kombe," alisema mmoja wa watu walio karibu na watuhumiwa hao.

  Kampuni zilizokwiba fedha nyingi zaidi kutoka akaunti ya EPA na ambazo sasa kwa utaratibu huu wamiliki wake hawataguswa ni pamoja na ya Kagoda Agricultural Limited na nyingi za mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia, Jeetu Patel.


  Kwa mujibu wa wakaguzi Kagoda ilighushi nyaraka zilizotumika kuchota zaidi ya shilingi bilioni 40 wakati Jeetu Patel, naye amechota zaidi ya nusu ya fedha zilizoibwa akitumia kampuni nane.

  Maofisa wa Serikali hususan wale wa vyombo vya dola wakiwamo wajumbe wa kikosi kazi (task force) kilichokabidhiwa kazi ya kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya wahusika waliochota fedha hizo, walipoulizwa kuhusu kushitakiwa kwa wachache tu katika wizi wa EPA wote walidai kwamba muda aliotoa Rais Jakaya Kikwete kukamilika kwa suala hilo haujakwisha.

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI), Robert Manumba, ambaye alitajwa na vyanzo vya habari kwamba ofisi yake ndiyo inakamilisha taratibu za kuwashitaki wahusika aliiambia Raia Mwema jana Jumanne kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa msemaji wa kikosi kazi (task force) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

  Kauli kama hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hosea naye hakuwa tayari kuzungumzia hatua ambayo wamefikia katika kuwashitaki wahusika, huku Ofisa Mwandamizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, akisema kwamba kila kitu kitajulikana siku chache zijazo.

  Mapema Jumatatu wiki hii, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, Peter Kivuyo, aliliambia Raia Mwema kwamba mtu anayeweza kuzungumzia masuala ya EPA ni ofisa mwenzake aliyemtaja kwa jina la Kasara, ambaye hata hivyo alipotafutwa kwa simu alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi naye hakuwa tayari kuzungumzia kuhusu mashitaka dhidi ya watuhumiwa wa EPA, kwa maelezo kwamba jana Jumanne ilikuwa ni siku ya mapumziko na alikuwa katika shughuli za kifamilia.

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye ndiye anayeelezwa na wenzake kuwa anapaswa kuzungumzia suala hilo hakuweza kupatikana jana Jumanne huku msemaji wake, Omega Ngole akisema kwa sasa hawako katika nafasi ya kuzungumzia suala hilo.

  Hata hivyo, Raia Mwema limethibitishiwa kwamba Maregesi, Mapunda na Lukaza, wanatajwa kuwa watu watakaotolewa kafara kutokana na kile kilichoelezwa kwamba wamekuwa na "jeuri ya Kiafrika" kwa kukataa kulipa fedha wanazotuhumiwa kuzichota.

  Imeelezwa kwamba tokea awali watuhumiwa hao wamekuwa wakigoma ‘kutoa ushirikiano' jambo ambalo limeelezwa kuwakera baadhi ya wanasiasa na watendaji wa Serikali walioamua sasa kuwaburuza mahakamani.

  Raia Mwema imethibitisha kwamba bado akaunti za watuhumiwa hao zinaendelea kushikiliwa hata baada ya muda wa miezi sita kisheria kupita kwa maelekezo ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

  Habari zinaeleza kwamba awali watuhumiwa hao walikuwa wafikishwe mahakamani sambamba na maofisa wa BoT waliohusika katika mchakato wa EPA, lakini uamuzi huo ulibadilishwa baada ya tishio kutoka kwa watumishi hao kwamba ‘wataanika' kila kitu hadharani wakitolewa kafara.

  "Baada ya watumishi hao wa BoT kutishia kumwaga kila kitu hadharani, mwelekeo umebadilika na sasa wataitwa kama mashahidi wa upande wa serikali kesi hizo zitakapofikishwa mahakamani, lakini bado wanaweza kuiharibia serikali watakapoamua kutaja watu ambao wamefichwa," anasema mtoa habari wetu aliye karibu na vyombo vya dola.


  Raia Mwema imefahamishwa kwamba kesi hizo zinatarajiwa kutumika kama mwavuli wa kuivusha serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kukwepa wimbi la manung'uniko ya wazi kwamba serikali ya CCM imekuwa ikiwalea watuhumiwa wa ufisadi, wengi wakiwa ni wafadhili wa chama hicho.

  Wakaguzi wa ndani na wale wa nje, walibaini kuwapo kwa wizi mkubwa wa fedha katika akaunti ya EPA katika kipindi cha mwaka mmoja pekee wa 2005/2006 ambako zilipotea zaidi ya Shilingi bilioni 133.

  Wakaguzi hao walibaini kwamba kati ya fedha hizo shilingi bilioni 90 ni zile ambazo zimethibitika kuchotwa kwa kutumia nyaraka za kughushi, sehemu kubwa zikiwa zimekwenda kwa wafanyabiashara wawili, wamiliki halisi wa Kagoda Agricultural Limited na Jeetu Patel kupitia kampuni zake nane.

  Ripoti ya Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young waliofanya kazi kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilionyesha kwamba kiasi cha Shilingi 90,359,078,804.00 zililipwa kwa kampuni 13 ambazo zilitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi na kwamba kampuni hizo hazikustahili kulipwa chochote.

  Wakaguzi hao na Ikulu kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wake, Philemon Luhanjo, Januari 9, 2008, walipendekeza moja kwa moja bila kuuma maneno kwamba wahusika wa kampuni hizo 13 wachukuliwe hatua za kisheria mara moja, kauli ambayo Rais Kikwete aliirejea katika hotuba yake bungeni, lakini bila ukali tena.

  Makampuni ambayo Jeetu Patel anahusika nayo na ambayo yamethibitika kughushi nyaraka na kuchota fedha BoT ni Navycut Tobacco (T) Limited, Ndovu Soaps Limited, Bina Resorts Limited, Bencon International Limited, Maltan Mining Company Limited, Bora Hotels & Apartments Limited, Venus Hotels Limited, and B.V. Holdings Limited.

  Pamoja na kampuni hizo za Jeetu Patel, kampuni nyingine zilizohusika na jinai ya kughushi nyaraka ni pamoja na Kagoda Agriculture Limited ambayo wanaoonekana katika nyaraka ni John Kyomuhendo mwenye hisa 40 na Francis William anayemiliki hisa 60 katika kampuni hiyo.

  Kampuni nyingine ni V.B & Associeties Company inazomilikiwa na Devendra Patel na Jantkumar Chandubhai Patel na Changanyikeni Residential Complex Limited inayomilikiwa na Jose Van de Merwe, Samson Mapunda na Charles Mabina ikiwa na makao yake, Sinza, Kumekucha, Dar es Salaam.

  Pia katika orodha hiyo ya kampuni 13 zilizoghushi nyarakaambazo wahusika wake wamependekezwa kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja ni Money Planners & Consultants inayomilikiwa na Paul Nyingo na Fundi Kitungi na kampuni ya Njake Hotel & Tours Limited inayomilikiwa Japhet Lema, Anna Lema, Abel Lema, Derick Lema na Benard Lema wa Arusha.

  Jeetu Patel katika baadhi ya kampuni anashirikiana na wafanyabiashara wengine wa Dar es Salaam ambao wanatajwa kushiriana naye katika kuhamisha fedha hizo kwenda nje kwa kuzibadili kutoka shilingi za Kitanzania kwenda Dola za Merakani ama Euro bila kufuata mkondo halali wa fedha kinyume cha Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu.

  Miongoni mwa wanaotajwa kushirikiana na Jeetu Patel ni Sidik Yacoubu kupitia kampuni yao ya Ndovu Soap Limited ambayo kwa mujibu wa nyaraka za Wakala wa Leseni na Usajili wa Kampuni (BRELA), kampuni hiyo yenye namba ya usajili 20536 ya Februari 3, 1992, wamiliki wake ni Jayantulal Chandubhai Patel na Sidik Yacoubu.

  Katika kampuni ya Bora Hotels and Apartments iliyosajiliwa Septemba 8, 2005 inaonyeshwa katika orodha ya BRELA kwamba wamiliki wake wamo Jayantkumar Chandubhai Patel na Devandra Patel wakati Bina Resort Limited iliyosajiliwa Machi 31, 2005, wamo Jayantikumar Chandubhai Patel na Devendra Patel.

  Kampuni ya Maltan Mining Company iliyosajiliwa Machi 8, 1993 inamilikiwa na Jantkumar Chandubhai Patel na Hariharier Radhakrishna wakati Navy Cut Tobacco iliyosajiliwa Oktoba 12, mwaka 1995 inamilikiwa na Jantkumar Chandubhai Patel na Radakrishna.

  Kampuni nyingine ni Bencon Limited, B.V Holdings, Venus Hotels na V.B & Associeties Company zinazomilikiwa na Devendra Patel na Jantkumar Chandubhai Patel, ambazo zote zilisajiliwa Aprili 4, 2005.

  Katika orodha ya BRELA imo pia kampuni ya Excellent Service Limited inayomilikiwa na Emil Samanya, Peter Sabas na Elisifa Ngowi ambaye anatajwa kuwa ni Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambaye yumo katika task force inayochunguza wizi huo. Kampuni hiyo ilisajiliwa Mei 13, 1992 na kupewa namba 26959.

  Ngowi anahusishwa pia katika kampuni nyingine ya Clyton Marketing iliyosajiliwa Juni 6, 2005 akiwa na mwenzake Edwin Mtoi, ambaye haikuweza kufahamika mara moja anafanya shughuli gani zaidi ya kuwa katika kampuni hiyo.

  Wamiliki wengine waliofahamika ni Rajabu Maranda na Thabit Katunda ambao wanatajwa kumiliki kampuni ya Liqiud Service Limited ambayo usajili wake ulifanyika Desemba 12, 2004 na kupewa namba 15007. Maranda anatajwa kuwa mmoja wa wana CCM mashuhuri mkoani Kigoma na alidaiwa kutaka kuiingiza familia ya viongozi wa juu serikalini katika biashara zake bila mafanikio hususan baada ya Rais Kikwete kuwa makini zaidi.

  Wamiliki wengine waliofahamika ni Johnson Lukaza na Mwesigwa Rutakyamilwa Lukaza ambao wao wanamiliki kampuni ya Karnel Meals Holdings Ltd ambayo usajili wake ulipatikana Agosti 4, 1998, Mibale Farm iliyosajiliwa Septemba 2, 2005 na kupewa namba 154039 ambayo inamilikiwa na Kizza Selemani na Farijala Hussein, Malegesi Law Chambers inayomilikiwa na Beredy Malegesi ambayo ilisajiliwa Septemba 24, 2001.

  Wamiliki wengine ni Paul Nyingo na Fundi Kitungi, wanaomiliki Kampuni ya Money Planners & Consultants iliyosajiliwa Machi 22, 2005 na Kiloloma & Bros Enterprises inayomilikiwa na Charies Kissa, ambayo ilisajiliwa Aprili 8, 2005.

  Katika ukusanyaji wa fedha hizo, task force ya serikali inaelezwa kukusanya shilingi 53,738,835,392/= fedha ambazo Rais Kikwete ameagiza ziingizwe katika mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo zikichanganywa na nyingine zinazotarajiwa kufikia shilingi 64,844,770,688/=
   
 2. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ...never ending story
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  yetu macho na masikio...

  I bet there is a day when we will be told the whole truth... nothing but the truth... AND that is when we will have a "RECONCILLIATION COMMISSION" institued in order to get these thieves to confess and ask for forgiveness...

  We have been taken for the ride for so oooo long....
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Wanatuzungusha akili zetu maana wanajipanga kisawasawa na kutoana kafara..ili wengine waweze kusafishwa.......mahakamani ukweli wote utajulikanaa..soon.
   
 5. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #5
  Oct 17, 2008
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kazi mnayo Watazamaji ... oups! ... Kazi mnayo Watanzania.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi badow anaendelea kutishiana kupelekana mahakamani!!!!!
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nimeipenda hiyo, "wanatishiana" maana hakuna kinachofanyika ni porojo na kuzugana tu. Wacha waendelee kutuzuga maana mawe na kuzomea hakutoshi, wanataka makubwa zaidi
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kama ni kupelekwa mahakamani basi wapelekwe. Nina hakika mwanasheria Maregesi atakuwa na mengi ya kueleza. Sidhani atakubali kutolewa kafara.
   
 9. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  I'll be making PopCorn read for this movie, ila kama itakuwepo. Kwa sababu wafanyakazi wa BOT walivyowageuka ndio wanawaweka mashahidi, The drama continues. lakini mpaka tutafika.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Oct 17, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa hawapelekani mahakamani, na hata wakipelekana si kwa sababu ya kushinda kesi bali kwa ajili ya kufanya mazingaombwe ya sheria. Hakuna Jaji mwenye akili timamu atakayeweza kusema watuhumiwa wametendewa haki.
   
 11. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2008
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  This is not fair. Kwa nini watanzania wazawa tu ndio wanapelekwa mahakamani wakati Rostam amechota 40billion na Jeetu Patel amechukuwa more than 60 billion which is almost 80% of the funds wao wanapeta? I don't like this.

  I say wapelekwa mahakamani wakiongozwa na Jeetu au watu wote especially wazawa wapewe same immunity.
   
 12. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #12
  Oct 18, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebwanaeee.............wakitengeneza series (movie) ya hili zimwi FISADI ........walahi watauza sana.........na pengine kupata tuzo!
   
 13. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2008
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Binafsi Raia Mwema napenda kuliita Gazeti la Waliondotoni. La wale wasiochoka kusoma ngeli za nita...., wata..., tuta....., ita......, Hadithi zao zote huwa ni speculations. Bahati mbaya hizo Future Tense zao mara zote hazikamiliki kwa matukio.

  Hapo Juzi tulisoma Balali kurejea nchini na kukutana na waandishi, HAKURUDI kisha TuKasoma Waraka wa Balali kuwekwa wazi na wakili maarufu, HALIKUTOKEA baadaye tukasoma JK kuwafilisi wezi wa EPA, tena wakazuga ANNA Muganda kuweka mambo wazi....etc.

  Nafikiri Jenerali na Mbwambo wanatumia goodwill yao vibaya kabisa kuamsha hisia za wananchi kwa jinsi ya kumtetea JK na Serikali ilihali wakijua ni UZUSHI MTUPU. Nauona uwepo sa Salva katika bodi ya wahariri wa Raia Mwema kwa wingi wa tungo za namna hii.

  Nitajipa Homework ya kukusanya habari hewa na mfu za hili gazeti ili mukubaliane nami.
   
 14. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2008
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri Jenerali na Mbwambo wanatumia goodwill yao vibaya kabisa kuamsha hisia za wananchi kwa jinsi ya kumtetea JK na Serikali ilihali wakijua ni UZUSHI MTUPU. Nauona uwepo sa Salva katika bodi ya wahariri wa Raia Mwema kwa wingi wa tungo za namna hii. [/QUOTE]

  Yaani hata mimi nimekuwa nikifikiria hivyo hivyo kila siku ninapolisoma Raia Mwema.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  JK labda atawafungulia kesi makapuku waliohusika na ufisadi huu, lakini wale vingunge kama Jeetu Patel, Mramba, Mgonja na wengineo kamwe hatawagusa maana wanajua mafisadi mbali mbali waliomsaidia JK kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa CCM. Akiamua kuwagusa basi nao watamtosa hadharani na hapo ndipo kutakuwa na kizaazaa cha patashika nguo kuchanika.
   
 16. A

  Abura Member

  #16
  Oct 19, 2008
  Joined: Nov 12, 2007
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Subject: Why Mbeki’s fall is a timely lesson to Kikwete

  In South Africa: Election will be held in 2009. Recent fail in Mbeki’s political charisma and local popularity caused people to argue that he lacked leadership skills and was branded a lame duck. When Mbeki launched corruption crack down in South Africa he started in his own backyard with a major ANC party fundraiser and sponsor Mr. XYZ sent to prison by a competent court of law. Although this gave Mbeki a credit at least internationally, his influential party-men and sponsors were not amused. Next, he courageously went after his own vice president, and a darling of the ANC youth and labour wings, a fellow comrade, Mr Zuma. Firstly, he fired him from the lucrative vice president position and he then sent law enforcers after him. While some doubted whether Mbeki knew the repercussion of his actions firstly on top ANC sponsor and secondly on Zuma others believed that being a true comrade he is, he just wanted to make the record straight no matter the consequences.

  It is a shame that he failed to indict Zuma and as a consequence was kicked out chairmanship of ANC and presidency due to his internal opponents making his case too political and due to his failure to cover-up his personal ambition to ensure a reputable ANC person (other than Zuma) emerges as the next president of South Africa. His several attempts to woe prominent ANC personalities into presidency proved futile, as none could take an obvious risk. This turn of events seems to confirm those who argued that Mbeki really underestimated Zuma’s x-factor i.e. the game of charisma, local popularity and hence the number.

  Some would imagine that the majority of intellectual South Africans - black, white and coloured are horrified by the fact that the most unwanted person as a president of SA, will infact become their president in a matter of few months whether they like it or not!

  Others argue that the say that goes what goes around comes around is manifesting itself in the present turn of events. The previous white regimes never wanted to black SAs to be educated and this makes the majority of them who have the power of number incomprehensible of what makes a good president.

  In Tanzania elections will be held in next two years i.e. 2010. President J. Kikwete is facing somewhat similar dilemma. He has been facing corruption scandals after scandals since he took over presidency in 2000.

  Need not mention key of these are the BAE/Radar, Mwananchi-Meremeta Gold, Richmond, Kiwira privatisation and EPA.

  Similarity to Mbeki’s case is that all these ill deals are allegedly to have been perpetrated by prominent CCM leaders and sponsors. Other alleges that some of these ill deals were orchestrated by CCM big wigs.

  CCM is alleged to lack legitimate investment vehicle to funds its party operations. For that reasons it continues to use prominent scrupulous business people mainly of Asian community to help them fund-raise. Cash for favour or typical partners in corruption.

  Bad to J Kikwete as he is presently spending his entire first presidential term cleaning up and covering up the messy left by his predecessors. Ofcourse he was part of and is a prodigy from that regime too.

  Local papers have written a lot some too appealing. J Kikwete has could only be persuaded because he has left some traces into some of the ill deals. He has tainted hand himself so he can not really act. He will just dilly-dally and play hide and seek game.

  Too bad he is alleged that Rostam, Jeetu Patel and Yusuf Manji are the Key fellow holding JK by the balls. Why by the balls, if JK think he is smart to betray these guys, they will press the balls more until they burst. JK knows about this.

  Others opportunistic thieves such as the Lowassas, Yona, Chenge, Enos Bukuku, etc are also helping pulling on JK’s balls.

  Too bad is what J. Kikwete doesn’t know, or pretend not to know as to what the majority of intellectual Tanzanians both residing locally and internationally and the donor community in Tanzania knows of his precarious situations. Junajua mheshimiwa hali ilivyo mbaya.

  Kikwete is being held hostage by four Asians and the country is his collateral. Other Asians are not happy at all, and they feel sorry for Tanzania for having really stupid leaders. Asian community are tainted by these few individuals who are helped by the Government. Shame. Other argues that may be J. Kikwete is not the one who has held the country hostage because he doesn’t have the final say, may be CCM-NEC has, or rather a few powerful CCM king pins have?

  Too bad for these few so called intellectual Tanzanian, who have no numbers, never vote, cowards as they never speak their minds. Good that Nyerere’s strategy of not empowering Tanzanian intellectually is paying out. Forget about civil rights and education, majority of Tanzania are ignorant peasants they do what they are told to do. The Governmental organ in most villages is the local party cadres and they can track you down if you vote against the party wishes.

  I can imagine Rostan, Jeetu Pater, Manji, Mkapa warning JK, - dare you betray us little boy, we assure you we will fix you, remember you are our partner in crime, we are in this game together, if you want to fail us be assured it is you who will fail alone – we will make you sacrificial lamb, we will not fail. Remember, you have left traces which we will be happy to disclose to the public if you ever betray us. Don’t even think about it. We are ahead of you in this game. Moreover, we will Mbeki you. We will vote you out of Chairmanship of CCM and your office term will be only one term.

  So what is left of J.Kikwete?

  Can easily take his people for a bad ride, majority of them are ignorant peasants, they don’t understand a things, you can easily fool them, MPs are even worse, all they want is allowances, make them too worried of the upcoming elections and they will obey you.
  The so called intellectual don’t bother, they are too smart to line up for vote, practically they never come out to vote.
   
 17. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Nyerere kasema sheria na haki si vitu sawa, hivyo hata wakienda mahakamani sheria itawaaaachia kwani si haki kutendewa haki ndani ya sheria za haki tuliyoamua kuifuata
   
Loading...