BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,329
*Akerwa pesa kutumika kununua umaarufu
Friday, 25 June 2010
Na Kitiko Mpacha, Tanga
Majira
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuamua kura za maoni zishirikishe wanachama wote kuanzia ngazi ya kijiji kwa imani kwamba mgombea hawezi kuhonga wanachama wote bado sio dawa ya ufumbuzi.
Akifungua Mkutano Mkuu wa Baraza la Habari nchini (MCT), Jaji Warioba alisema hivi sasa wapo wagombea wanapita majimboni wakigawa pikipiki, baiskeli na kanga kwenye majimbo ya uchaguzi.
"Hivi sasa kuna watu wanatamba kwamba watatumia zaidi ya sh. milioni 200 kwenye jimbo la uchaguzi na uwezo wa kuhonga kila mwanachama wanao ili kutimiza matakwa yao ya kuongoza nchi kwa kutumia fedha," alisema na kuongeza:
"Wana uwezo pia wa kununua mamluki, tayari kadi za vyama vya siasa hasa CCM zinauzwa kwa madhumuni hayo, baadhi ya matajiri wanapanga kuwanunua wanachama ili siku ya uchaguzi wapotee na wasipige kura ili kupunguza kura za wapinzani wao," alisema.
Alisema watu wanafanya kampeni za ovyo kwa kivuli cha kutangaza nia ya kugombea na fedha zinatumika hata kununua umaarufu, na kwamba hivi sasa imezuka mbinu ya kuchangia wagombea ili ionekane wanapendwa kumbe ni rushwa.
Alisema inashangaza kuona wananchi maskini wanawachangia matajiri fedha ili wagombee, lakini nia ni kuonesha kuwa hao wagombea wanapendwa lakini ukweli ni kwamba wengi wa wagombea hao au wapambe wao ndio wanatoa fedha hizo ili kuleta hadaa kwamba wanakubalika.
"Kwa kifupi fedha imeingiza sumu mbaya sana kwenye uchaguzi, zamani mgombea kupita bila kupingwa ilitokana na kukubalika katika jamii, lakini siku hizi ukisikia mtu amepita bila kupingwa utasikia watu wakisema huyo amenunua uteuzi kwenye chama chake na amenunua wapinzani, viongozi na wananchi kwa ujumla wanajua ni nani amenunua uongozi.
"Vitendo vya rushwa vinaonekana wazi wazi, watu wanahonga waziwazi lakini wananchi wanaambiwa ni kusaidia maendeleo, matamshi ya viongozi ni kwamba bado wakati wa kampeni, lakini zawadi za ajabu ajabu zinatolewa kwenye wilaya na majimbo.
"Kwa bahati mbaya sheria haina taasisi nzito ya kusimamia, msajili wa vyama vya siasa ndiyo msimamizi mkuu wa sheria na kama akiridhika kwamba mgombea au chama chake kimetenda kinyume na matakwa ya sheria, basi msajili anaweza kutoa pingamizi kwa mkurugenzi wa uchaguzi na baada ya hapo tume ya uchaguzi inaweza kumzuia mgombea au chama chake." alisema, Jaji Warioba.
"Msajili ana ofisi ndogo mjini Dar es Salaam, uchaguzi uko nchi nzima na idadi ya wagombea ni maelfu, kuanzia kata, jimbo hadi taifa, msajili hana wafanyakazi wa kutosha na hana fedha za kutosha. Kama hawezi kupata nauli ya kusafiri na kuhakiki wanachama wa chama cha siasa, atapata wapi fedha za kuwapata wafanyakazi hadi ngazi ya kata?" alihoji.
Aidha alisema msajili pia hana uzito wa kutoa maamuzi chini ya sheria, yeye ni mtumishi wa serikali na katika hali halisi hili ni jambo la kumwonea msajili kwani hatakuwa na ubavu wa kumzuia mgombea urais au ubunge, achilia mbali kuzuia chama cha siasa kisiteue mgombea.
Alisema wananchi kwa ujumla wanaamini yanayosemwa na vyombo vya habari, kwa hiyo ni vyombo vya habari vimechangia katika matatizo tuliyonayo na wakati mwingine vimepotosha mambo na kuweka uzito kwenye mambo ambayo yanaleta uhasama.
Alisema katika siasa vyombo vya habari vimejali zaidi watu kuliko sera, vimetumika kwa kujua au bila kujua katika kuleta uhasama kati ya viongozi au makundi na kwamba vimekuwa mstari wa mbele kufuatilia malumbano ya viongozi kwa kiwango kikubwa.