Warioba ataka wazee waondoke madarakani

Warioba ataka wazee waondoke madarakani

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,695
Reaction score
9,580
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba amewashauri viongozi wazee na
waliokaa madarakani muda mrefu kuacha
kung’ang’ania madaraka.
Amesema kuwa ni vyema kwa viongozi
hao kung’atuka ili kutoa nafasi kwa vijana
wenye nguvu na akili kulitumikia taifa
katika uongozi.

Warioba aliyasema hayo juzi jijini Dar es
Salaam katika mahojiano maalumu na
gazeti hili, pamoja na mambo mengine
alizungumzia uongozi wa nchi hii.
“Mwalimu Julius Nyerere aling’atuka akiwa
na nguvu zake kabisa. Kiasili kung’atuka ni
dhana ya kuwapisha vijana kuwa mbele
katika kutekeleza majukumu na ninyi
wazee siyo kuondoka, bali kuendelea
kuwapa ushauri na mwongozo,”alisema
Jaji Warioba.

Alieleza kuwa kung’atuka kunamfanya
aliyechukua hatua hiyo kuishi maisha ya
raha yenye furaha na amani jambo
ambalo yeye sasa analifurahia.
Aliongeza: “Haiwezekani mzee ukakaa
kundi moja na kijana wako aliyetahiriwa
juzi, kwani kwa kawaida, kijana akitahiriwa
hupandishwa daraja na kukaa kundi la
wakubwa, hapo wewe baba yake hata
kama una miaka 40, unahamishwa na
kuingia kundi la wazee.”

Alifafanua kuwa hata katika uongozi ni
muhimu kung’atuka na kuwapisha vijana
ili waweze kutumia akili na nguvu zao
kuendeleza taifa huku wakipata
maelekezo na mwongozo kutoka kwa
wazee.

“Maisha yangu sasa baada ya kuacha
uongozi ni ya furaha na amani bila woga
kuliko wakati wowote, tofauti na
nilipokuwa bado kiongozi katika Serikali,”
alisema.

“Ukiwa kiongozi unaweza kuishi kwa hofu
na shaka huku ukituhumiwa,” alibainisha
Jaji Warioba aliyewahi kuwa Waziri Mkuu
na Makamu wa Kwanza wa Rais mwaka
1985 - 1990.

Kauli ya Warioba imekuja huku kukiwa na
kundi kubwa la viongozi wenye umri
mkubwa katika nafasi mbalimbali
madarakani muda mrefu, huku
wakiendelea kutamani nafasi za juu zaidi.

Miongoni mwa viongozi hao, wapo
wanaotajwa kuunda makundi ya kusaka
urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu
ujao mwaka 2015.

Hii siyo mara ya kwanza viongozi wenye
umri mkubwa kutakiwa kung’atuka
madarakani.

Januari 14, 2010, Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, aliwashauri wazee watumie busara
kupima uamuzi wa kugombea tena nafasi
za ubunge kwenye uchaguzi mkuu. Pinda
alitoa rai hiyo alipokuwa akijibu maswali
ya wahariri katika mkutano alioitisha
kujibu maswali yao jijini Dar es Salaam.

Source: Mwananchi
 
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba amewashauri viongozi wazee na
waliokaa madarakani muda mrefu kuacha
kung’ang’ania madaraka.
Amesema kuwa ni vyema kwa viongozi
hao kung’atuka ili kutoa nafasi kwa vijana
wenye nguvu na akili kulitumikia taifa
katika uongozi.
Warioba aliyasema hayo juzi jijini Dar es
Salaam katika mahojiano maalumu na
gazeti hili, pamoja na mambo mengine
alizungumzia uongozi wa nchi hii.
“Mwalimu Julius Nyerere aling’atuka akiwa
na nguvu zake kabisa. Kiasili kung’atuka ni
dhana ya kuwapisha vijana kuwa mbele
katika kutekeleza majukumu na ninyi
wazee siyo kuondoka, bali kuendelea
kuwapa ushauri na mwongozo,”alisema
Jaji Warioba.
Alieleza kuwa kung’atuka kunamfanya
aliyechukua hatua hiyo kuishi maisha ya
raha yenye furaha na amani jambo
ambalo yeye sasa analifurahia.
Aliongeza: “Haiwezekani mzee ukakaa
kundi moja na kijana wako aliyetahiriwa
juzi, kwani kwa kawaida, kijana akitahiriwa
hupandishwa daraja na kukaa kundi la
wakubwa, hapo wewe baba yake hata
kama una miaka 40, unahamishwa na
kuingia kundi la wazee.”
Alifafanua kuwa hata katika uongozi ni
muhimu kung’atuka na kuwapisha vijana
ili waweze kutumia akili na nguvu zao
kuendeleza taifa huku wakipata
maelekezo na mwongozo kutoka kwa
wazee.
“Maisha yangu sasa baada ya kuacha
uongozi ni ya furaha na amani bila woga
kuliko wakati wowote, tofauti na
nilipokuwa bado kiongozi katika Serikali,”
alisema.
“Ukiwa kiongozi unaweza kuishi kwa hofu
na shaka huku ukituhumiwa,” alibainisha
Jaji Warioba aliyewahi kuwa Waziri Mkuu
na Makamu wa Kwanza wa Rais mwaka
1985 - 1990.
Kauli ya Warioba imekuja huku kukiwa na
kundi kubwa la viongozi wenye umri
mkubwa katika nafasi mbalimbali
madarakani muda mrefu, huku
wakiendelea kutamani nafasi za juu zaidi.
Miongoni mwa viongozi hao, wapo
wanaotajwa kuunda makundi ya kusaka
urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu
ujao mwaka 2015.
Hii siyo mara ya kwanza viongozi wenye
umri mkubwa kutakiwa kung’atuka
madarakani.
Januari 14, 2010, Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, aliwashauri wazee watumie busara
kupima uamuzi wa kugombea tena nafasi
za ubunge kwenye uchaguzi mkuu. Pinda
alitoa rai hiyo alipokuwa akijibu maswali
ya wahariri katika mkutano alioitisha
kujibu maswali yao jijini Dar es Salaam Source Mwananchi
Ujumbe mahususi kwa Mzee Samweli Sitta
 
Pia slaa,sharif hamad,makaidi, mangula,nk

Sharrif hamad bado ni kijana hajawahi kushika madaraka makubwa, Warioba ameongelea watu waliokubuhu akina Lowasa, sitta na Wasira
 
Hapa Mzee Warioba alikuwa anamlenga Mh. Dr. Slaa, kwa kuwa katika Tanzania kwa sasa wanasiasa wenye umri mkubwa ni Kingunge (86) na Dr. Slaa (82), Kingunge yeye ameshang'atuka toka 2010, lakini Dr. Slaa bado hataki kuwaachia madaraka vijana wa Tanzania wenye damu na uwezo mpya wa kufikiri.
 
Hapa Mzee Warioba alikuwa anamlenga Mh. Dr. Slaa, kwa kuwa katika Tanzania kwa sasa wanasiasa wenye umri mkubwa ni Kingunge (86) na Dr. Slaa (82), Kingunge yeye ameshang'atuka toka 2010, lakini Dr. Slaa bado hataki kuwaachia madaraka vijana wa Tanzania wenye damu na uwezo mpya wa kufikiri.

Mhe mbona Slaa amezaliwa 29/10/1948,miaka 82 inatoka wapi?au kumbukumbu za bunge hazikuwa sahihi!!!?
 
Mhe mbona Slaa amezaliwa 29/10/1948,miaka 82 inatoka wapi?au kumbukumbu za bunge hazikuwa sahihi!!!?

Wanahila tu na Dr.Slaa hawa Interahamwe,hata vasco dagama ni kizee kwa slaa.
 
Ingekuwa busara zinauzwa hadi nje ya nchi hii tungempostia Mugabe.
 
Mhe mbona Slaa amezaliwa 29/10/1948,miaka 82 inatoka wapi?au kumbukumbu za bunge hazikuwa sahihi!!!?

Mkuu Kiche,

Itakuwa ni typing error Slaa ana miaka 82 na siyo 66 kama unavyotaka kuaminisha watu

Amezaliwa 29/10/1932
 
Mhe sina sababu hata kidogo ya kuaminisha watu,typing error gani inaendana na muda wa masomo!!!?au maelezo binafsi hata wakati anagombea urais yalikuwa typing error!?na kingunge alifikisha miaka 82 may 30 2014,naye hana miaka 86!!na hii miaka aliitamka mwenyewe mwezi april 2014.
 
Aache porojo zake na yeye. Ameacha lini uongozi wakati wote bado Ni kiongozi wa CCM. Kustaafu maana yake unakuwa huru. Si CCM or kwingine. Unakuwa ni mzee wa wote. Unasimama kwa miguu yako na kwenda Kilimanjaro hotel na kusema na kutoa maoni yako ukiwa huru. Pamoja na kuendelea kulipwa maruprupu kutoka kodi zetu bado Ni waumini wa CCM. Hawawezi kusimama na kuwaambia kuwa wanatuharibia nchi yetu. Leo anataka kusema nini. Akae kimya. It is too late.
 
Sharrif hamad bado ni kijana hajawahi kushika madaraka makubwa, Warioba ameongelea watu waliokubuhu akina Lowasa, sitta na Wasira
Kweli Wassira , Lowasa Sitta, hamad ondokeni bwana mkalee wajukuu bila kumsahau Prof. Tibaijuka
 
Back
Top Bottom