Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

Mleta mada umepatia sana. Mungu akubariki. Jaji warioba nampenda, lakini kwa serikali tatu kaweka utashi wake. Njelu kasaka, muumini wa serikali tatu hakubaliani naye. Stay tune! Tanzania yangu maskini inakufa
. Tutaipigania hadi mwisho.

Kweli kabisa 'Mpiganaji Wangu'!
 
Muungano ni wa kupigiwa kura kama ni:
A) Serikali mbili,
B) Serikali tatu, au
C) Serikali moja
Halafu utafutwe wastani wa asilimia za kura za bara na zile za visiwani ili kuamua ni muungano gani wananchi wanataka! NJE YA HAPO NI KUEDELEA KULEA TATIZO! HONGERA KWA KULIONA HILO BABA YETU WARIOBA!
 
Bwana Mashakaa, wacha klalamika hovyo,
kama yamekushinda...
 
Tanzania for tanzanians.sikuzaliwa tanganyika. Siijui tanganyika. Nchi yangu ni tanzania!!!
 

Nyerere alijenga viwanda ccm mkauza, Nyere alihifadhi maliasili zetu ccm mnagawa, alitunza tembo ,faru. ccm mnauwa kwakasi, ni ktk awamu hii tunashudia biashara ya madawa ya kulevya ikishamiri, kati yenu na warioba nani anamsaliti nyerere?
 

Okay, lakini wasiibuke watu kwa kuwa Nyerere amefariki dunia, kudai kuwa Nyerere hakuwa na mawazo mgando, kwa maana ya kutaka kuhalalisha kuwa eti labda Nyerere angeliunga mkono wazo la serikali tatu! Hilo nalipinga hadi kaburini--msimamo wa Nyerere katika muungano hakuwa na mswalie mtume! Angeweza kukubali jambo lolote jingine libadilishwe kama alivyorelax katika suala la kubehuliwa kwa Ujamaa na mengine kadhaa (hata Azimio la Arusha) lakini sio katika muungano huu uliopo--hakutaka mchezo nalo kabisa akiamini kuwa ni suala la Msingi wa Taifa. Ninaposema hivyo sina maana kwamba ni dhambi kumkosoa Nyerere (coz hakuwa malaika), lakini ni dhambi kumpachika msimamo ambao aliupinga hadi mwisho wa maisha yake!! Baadhi yetu tulipata bahati ya kumfahamu vyema Mwalimu, tusidanganyane mchana kweupe!!
 
Binafsi Tanzania haijanisaidia lolote, zaidi ya kuishi miaka yote nikiwa nimesahaulika na kukandamizwa kama Tanganyika.
Acha uvunjike tuu huo muungano, kwanza kwetu wengine umelete gundu tu.
 

Uko right kabisa mkuu,kikwete kapigana na mawazo mengi sana ya wanaccm wenzake,tutamkumbuka kwa machache yake.
Navyojua mimi tanganyika inajitosheleza kwa kila kitu na sababu kubwa za kuing'ang'ania zanzibar ni sababu za kiusalama tu plus uwepo wa gesi na mafuta ila tofauti na hapo hatuna tunachokipata wala kufaidika na zenji,labda wakuu wa nchi wanasababu zao za msingi ambazo wananchi wa kawaida hatuzijui.
 
Binafsi Tanzania haijanisaidia lolote, zaidi ya kuishi miaka yote nikiwa nimesahaulika na kukandamizwa kama Tanganyika.
Muungano wenyewe gundu kibao.
 
Nyerere alijenga viwanda ccm mkauza, Nyere alihifadhi maliasili zetu ccm mnagawa, alitunza tembo ,faru. ccm mnauwa kwakasi, ni ktk awamu hii tunashudia biashara ya madawa ya kulevya ikishamiri, kati yenu na warioba nani anamsaliti nyerere?

Lete ushahidi usio na mashaka kuwa tiba ya madhambi hayo ni serikali tatu!
 
Binafsi Tanzania haijanisaidia lolote, zaidi ya kuishi miaka yote nikiwa nimesahaulika na kukandamizwa kama Tanganyika.
Muungano webyewe gundu kibao.

Wanakudanganya kuwa Tanganyika ndio itakupa kula ukishinda kijiweni?
 
Someni kitabu cha mwalimu "uongozi wetu na hatima ya tanzania". Mwalimu hakuacha kitu. Nawaomba sana msome hicho kitabu. Hata jaji warioba na kina butiku hawakipendi maana kinawaumbua. Haki ya MUngu hicho kitabu kimemaliza yote. Warioba team watajuta kusaliti hekima za mwalimu. Wameanza kuwa wakali, why? Nafsi zinawasuta. Wanajua dhambi yao. Eeh mwalimu, lala salama ukijua tanzania inakata roho. Umepuuzwa, lakini ukweli haupo mbali.
 
Wanakudanganya kuwa Tanganyika ndio itakupa kula ukishinda kijiweni?

Potelea mbali nikidanganywa sasa, maana tulipo toka nimeshadanganywa sana kuhusu faida za muungano wa serikali mbili.
Uongo huo ndiyo umenifikisha hapa kijiweni nilipo sasa.
 

Ndugu, hata kama una hoja lakini kwa kuwa umetumia lugha ya mitaani wakati hii ni mada nyeti, nakuacha!
 

Hivi kumbe hata azimio la arusha nalo lilikuwa ni kero kwako? Haya basi, muungano nao ni kero ya mwisho kwako; serikali 3 ni ubinafsi tu uliokomaa, kama bado tunautaka muungano ni bora tume ingelijikita kuhoji wananchi ni kwa nini sasa tusiende kwenye serikali moja. Ujinga wa sasa wa serikali tatu ni kurudi nyuma tu na kuendekeza utengano na ubinafsi!
 

Ufumbuzi siyo kuendelea na serekali 2 ufumbuzi ni serekali 1.
 

Nadhani umejichanganya mno kiasi kwamba nashindwa kukupata sawasawa, sorry sana!
 
Ufumbuzi siyo kuendelea na serekali 2 ufumbuzi ni serekali 1.

Ukweli ni kwamba huo ndio msimamo wa Watanzania wengi, mimi nikiwemo. Ila sote twajua kuwa hilo halikuwepo tangu day one ya kuundwa kwa muungano na limeendelea kupingwa, hasa na Wazanzibar kwa kuogopa kumezwa. Muungano wa serikali mbili tumekuwa nao kwa miaka 50 na wengi wetu tumezaliwa Watanzania na tumeishi ndani ya Tanzania kwa miaka yote hiyo 50--waswahili wanasema heri zimwi likujualo! hatupingi kubadili au kuandika katiba mpya, lakini tunapinga mabadiliko for the sake of mabadiliko--tunataka mabadiliko yenye tija sio yatakayovunja nchi tuliyozaliwa na kuipigania kwa miaka 50!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…