Kijana hii ni tuhuma ninayoisikia kw amara ya kwanza kuhusu huyu Mzee.................."Naomba niseme tena namheshimu sana Mzee Warioba, na si kweli kama mimi nimemtukana ila Mzee Warioba ni miongoni mwa wazee wasiopenda kupingwa wala kukosolea na anapenda hoja yake ichukuliwe ni fikra sahihi ambayo kila Mtanzania anapaswa kuiheshimu.
"Ninamwomba kama kweli yeye ni mwana CCM thabiti tena Waziri Mkuu mstaafu, anashindwaje kutumia uzoefu wake kutoa ushauri kwa viongozi wa chama na Serikali katika vikao vyao, au kuwaona moja kwa moja maofisini, awe Rais , Waziri Mkuu na viongozi wa juu katika chama?
" Je fursa hizo kwake yeye anaona zimeshindikana na anaona ni vema ashauri kupitia vyombo vya habari? Au ni busasra gani ya kushauri Serikali kwa kuita waandishi wa habari? Kwanini yeye anapenda kukosoa kupitia vyombo vya habari? " Alihoji Bw. Makalla.
"Mimi sijajipendekeza kwa Kikwete kama anavyodai yeye mimi ni wajibu wangu kama mwana CCM na kiongozi kutetea chama changu na Serikali ya CCM . Yeye mwenzangu ameamua kutafuta umaarufu wa kuikosoa Serikali ya chama chake hadharani kwa maslahi binafsi, "
" Namshukuru amekiri kwa mara ya kwanza wazi wazi kuwa alikuwa kwa Salim 2005. Hivi kama inajulikana hivyo, sasa tutegemee nini unapolaumu Serikali hata jambo moja la kusifia hana kwanini nisiamini kuwa anaendekeza makundi.?
"Hivi anataka nimkumbushe kuwa siku ya mkutano wa kupata mgombea urais 2005 yeye tayari alishavaa shati lake safi la CCM lenye nembo ya Bendera ya Taifa huku akiiamini kuwa Salim akishinda anakuwa mgombea mwenza! Kwanini nisiamini kuwa Salim alishakubali kushindwa lakini yeye akikumbuka umakamu basi hasira zake ndiyo kushambulia Serikali, tukimkosoa anasema ametukanwa!..............
" Nachelea kuamini kama uzee ni dawa, lakini si kila mzizi ni dawa ipo mizizi mingine ni sumu.
"Nimemlaumu kwa kulaamu pasipo kutoa majawabu. Namtaka Mzee Warioba na Watanzania wote tushirikiane na Serikali kujenga nchi yetu, tuache siasa zitakazobomoa umoja wetu na amani tuliyonayo," alisema Bw. Makalla .
Warioba is also part of the problem (mnafiki)...anaendeleza makundi vilevile jino kwa jino wacha walumbane tunawaita walewale (agenda zao zinafanana) wamejificha kwenye nyasi fupi.
Angakuwa huwa anapita hapa JF nimemshauri apunguze safari za nje ambazo binafsi naziona hazina tija kwa Watanzania zaidi ya yeye kufanya utalii zaidi,kwa dunia ya sasa huwezi kujisifu kwa jinsi unavyoweza kupata misaada toka nje ila unaweza ukajisifu kwa mikakati bora ya kuzalisha na kukuza uchumi bila kutegemea nchi wahisani.
Warioba asitake kujifanya anajua sana kukosowa wenzake, yeye kashfa ya mwananchi gold zinamsubiri.
Vile vile mbona hakuifanyia lolote nchi hii alipokuwa waziri mkuu!!! Yeye ni mwanachama hai wa CCM, je amekishauri nini chama chake ili kutatua matatizo ya sasa?
Hayo mambo ya Salim kuwa Hizbullah ni scaremongering za CCM Zanzibar wasiomtaka Salim kwa sababu ni Mpemba.Serikali nayo ijirekebishe kwani watu wamechoka jamani.
And so the race begins for 2010! Mi naona ni dalili nzuri, we need honest dialogue, inabidi tuache unafiki na tuwe wawazi. The only problem is that the powers that be will try to clamp down harder on free speech and right to express ourselves.
How much time before they will start vicious attacks on Salim, Warioba and Butiku? Even jamiiforums will be again targeted. We have to ensure that we keep the conversation going.
Sasa natumaini wapambe hawaji kui-hijack topic hii with trivialities....