Warioba amshangaa Kikwete kusema mpasuko ndani ya CCM ni kidogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba amshangaa Kikwete kusema mpasuko ndani ya CCM ni kidogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 30, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,790
  Likes Received: 83,163
  Trophy Points: 280
  • Amshangaa Kikwete kusema ni mpasuko kidogo
  • Yeye asisitiza uliopo ni mkubwa unaoligawa taifa
  • Asema tatizo ni tofauti ya kipato cha tajiri, maskini
  Na Nyakasagani Masenza
  Majira
  29 September 2009

  WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amevunja ukimya na kusema kuwa upo mpasuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao unaweza kuwagawa Watanzania katika matabaka ya udini na ukabila.

  Jaji Warioba alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na baadhi ya vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam ili kutoa ujumbe wa miaka 10 ya Tanzania bila Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

  Alisema Watanzania wanafahamu kuwa upo mpasuko ndani ya chama, ambao pia ulithibitishwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipozungumza na wananchi kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) kuwa upo mpasuko kidogo.

  Hata hivyo, Jaji Warioba aliyeshika maraka ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais kati ya mwaka 1985-90, alisema kauli hiyo ya Rais Kikwete ilimshangaza kwa mwenyekiti wa chama kusema kuwa upo mpasuko mdogo, wakati uliopo ni mkubwa.

  Alisisitiza kuwa ndani ya CCM kuna mpasuko mkubwa, akitolea mfano kauli ya Rais Kikwete kuwa wabunge wa CCM sasa hawaaminiani hata kuachiana glasi zao za maji kwa kuhofia kuwekeana sumu, jambo ambalo Jaji Wariona alisema linathibitisha kuwa kuna mpasuko mkubwa ndania ya chama.

  Kiongozi huyo alisema wakati taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, yameibuka makundi na matabaka kiasi kwamba mtu akitangaza adhima ya kugombea uongozi ndani ya vyama vya siasa anaonekana kuwa adui kiasi cha kutafutiwa sababu, tofauti na zamani ambapo wagombea uongozi walitaniana kabla ya kushindana.

  Kwa mujibu wa Jaji Warioba, msingi umeanza kusambaratika tofauti na enzi za Mwalimu Nyerere, ambapo wananchi walikuwa na mshikamano bila ubaguzi, wakiitana ndugu, tofauti na sasa ambapo wamegawanyika katika makundi na matabaka.

  Akizungumzia sababu ya mgawanyiko huo, Jaji Warioba alisema unatokana na tofauti kubwa kati ya matajiri na masikini, jambo ambalo halikuwapo wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere ambaye alijitahidi kuleta usawa kwa wananchi.

  "Wananchi walikuwa na sauti katika kuongoza nchi, leo matajiri ndio wenye sauti. Viongozi wako karibu na matajiri, zamani ukiwa serikalini lazima utunze siri za serikali, leo siri zinavuja sana, watu wanaona yanayotendeka, wengine wanalipwa milioni tano na marupurupu, wengine wanaambulia laki moja, ndio maana sasa kuna migomo ya walimu, wanafunzi na wananchi," alisema.

  Jaji Warioba alisema imani ya
  wananchi kwa serikali imepungua, matokeo yake yameibuka matabaka, huku wengine wakiwaunga mkono wabunge wanaohubiri mapambano dhidi ya ufisadi na wengine wakiwakatisha tamaa kwa kuwaona wasaliti ndani ya chama.

  “Jamii itaamini nini kuhusu mgawanyiko ulioibuka ndani ya CCM na kusababisha Spika Bw. Samuel Sitta kukumbwa na wakati mgumu na baadaye tuhuma zake kumalizwa kimya kimya. NEC ilitoa msimamo kuwa Spika anafanya mambo peke yake, baadaye wakakanusha, mgogoro huu ukiisha kimya kimya utazua maswali mengi kwa wananchi," alisema Jaji Warioba na kufafanua kuwa CCM ina ushawishi mkubwa, mgawanyiko unapotokea ndani yake unaweza kuigawa Tanzania nzima.

  Alizungumzia pia Tanzania kujiunga OIC na Waraka wa Maaskofu, Jaji Warioba: "Niliangalia majadiliano ndani ya bunge, akisimama mbunge mkiristo anapinga hoja, akisimama mwislamu anaunga mkono, baada ya hapo umekuja waraka na mwongozo, sijui msingi wake, kila tunapoelekea Uchaguzi Mkuu mambo haya hujitokeza, ilianza 1994, ikaibuka tena 1999 na 2004," alisema.

  Jaji Warioba amesema Watanzania wameanza kuchanganya dini na siasa, wakati wa Pasaka mtu anakaribisha watu sikukuu kwa msingi wa siasa, hivyo hivyo wakati wa Mwezi wa Ramadhani kiongozi wa siasa anaandaa futari wakati hakufunga, jambo ambalo amesema lisipewe nafasi na Watanzania

  Jaji Warioba amesema Hayati Mwalimu Nyerere alifanya kazi kwa uadilifu, hakuchanganya dini na siasa kama ilivyo kwa baadhi ya wanasiasa sasa, alikuwa msikivu sana pamoja na wananchi kusema kuwa Mwalimu alikuwa mtu mbishi asiyeambilika, jambo ambalo si kweli.

  Kuhusu vita dhidi ya Ufisadi, Jaji Warioba amesema inatia matumaini baada ya watu wazito kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, huku akitoa tahadhali kuwa kesi za aina hii zinatokana na msukumo wa kisiasa, na kwamba kuna hatari zake, akitoa mfano kesi za uhujumu uchumi mwaka 1983, ambapo serikali ililipa fidia.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Namheshimu warioba but i find it funny kwamba amegusia deep green,na meremeta bila kuitaja mwananchi gold ambayo yeye ametajwa

  i dont know what to say..............
   
 3. Makalangilo

  Makalangilo Senior Member

  #3
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa habari za Warioba mtafute Mike Tyson wa Bunda.Hana lolote bora anyamaze.
   
 4. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Warioba asitake kujifanya anajua sana kukosowa wenzake, yeye kashfa ya mwananchi gold zinamsubiri.

  Vile vile mbona hakuifanyia lolote nchi hii alipokuwa waziri mkuu!!! Yeye ni mwanachama hai wa CCM, je amekishauri nini chama chake ili kutatua matatizo ya sasa?
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mkuu hii sijaelewa ulikuwa unataka kumaanisha nini?unaposema hakuifanyia lolote ni too general
   
 6. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  lakini Warioba ni part of the problem
  sioni kwanini anakosoa wenzie wa CCM au anaogopa kivuli chake?
  naona wengi wanafikiria kutoka kwa kuonekana kwenye magazeti, lakini hayo wanayoyasema wanawatoka rohoni? au walikosa mwanya mzuri wa kula? (aliyoongea kadinali Pengo) au anataka tu publicity?
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  CCM ni kapu la wajanja ila sasa ujanja wao ndiyo unaishia ishia na mwisho watalazimisha kutumia nguvu kupata madaraka na inakuwa CIVIL WAR . Warioba mie nilisha mtosa zamani sana .
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,790
  Likes Received: 83,163
  Trophy Points: 280
  Msekwa: Sina cha kuongeza kwenye maoni ya Warioba
  Na Waandishi Wetu
  Mwananchi
  9/30/2009

  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa, amesema hana cha kuongeza kwenye maoni ya Jaji Joseph Warioba kwa kuwa alitumia uhuru wake kuzungumza na kwamba wananchi ndio watakaopima ukweli.

  Juzi, Jaji Warioba ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili alisema nchi inaelekea pabaya anapoangalia jinsi mambo yanavyoendeshwa na kwamba, serikali haitaweza kushinda vita ya rushwa iwapo haitaelekeza nguvu zake katika mfumo unaoleta tatizo hilo.

  "Nimeanza kuwa na wasiwasi, tunakokwenda sina hakika kama umoja wetu utadumu," alisema Warioba katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

  Alipotakiwa jana kuzungumzia maoni ya mwanasiasa huyo mkongwe nchini, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa alisema kutolea maoni hoja za Jaji Warioba ni sawa na kumfumba mdomo jambo ambalo sio sahihi.

  Alisema kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake juu ya suala lolote na kwamba yeye anawaachia wananchi wapime ukweli wa maoni ya Jaji Warioba kutokana na kwamba wananchi wana akili kupambanua ukweli.

  “Ukiniuliza unazungumziaje kauli hiyo, mimi siwezi kukueleza chochote kwa sababu, mimi nikizungumza na kumpinga, nitakuwa nimemfumba hata siku nyingine akitaka kutoa maoni yake kwa suala lingine atashindwa akihofia kwamba atapingwa,” alisema Msekwa na kuongeza:

  “Kikubwa ninachopenda kukueleza ni kuwa, Jaji Warioba ana uhuru wa kutoa maoni yake kama watu wengine, lakini pia wananchi wenyewe wanayo akili ya kupima ukweli wa anachokizungumza.”

  Alipoulizwa anazungumziaje hoja ya Jaji Warioba kuwa, uongozi hivi sasa uko karibu sana na matajiri kuliko wananchi, na kwamba kwa sasa matajiri ndio wenye sauti, hivyo kuchangia kwa wananchi kutumia nguvu ya umma kwa kutoiamini serikali, Msekwa alihoji:

  “Aha! Ina maana hata wanafunzi kufunga barabara ili kudai kuwekewa matuta na taa za kuongozea magari barabarani, hii pia ni kwa sababu serikali imekumbatia matajiri?”

  Aliongeza kuwa, “Kama hivyo ndivyo, unataka mimi niseme nini, kama hayo ndio maoni yake siwezi kumpinga, sasa mimi niseme ili siku nyingine ashindwe kueleza anachofikiria kwa sababu tu amewasema viongozi.”

  Hata hivyo wakati Msekwa akisema hivyo, Profesa Mwesiga Baregu alionya kuwa, maoni yaliyotolewa juzi na Warioba yanapaswa kutekelezwa vinginevyo amani ya nchi itakuwa hatarini.

  Alisema maoni hayo ambayo pia yalitolewa na Waziri Mkuu mstaafu Dk Salim Ahmed Salim ni ya kizalendo na kwamba yasipotekelezwa, nchi itaenda kubaya.

  “Dk Salim na Warioba wote wawili kwa pamoja ni watu wakubwa, kauli zao zinaonyesha wasiwasi mkubwa kuwa wananchi wamepoteza imani na serikali, tukiendelea hivi, bila kuzingatia maoni yaliyotolewa na watu hawa, imani ya nchi itatoweka kwa sababu vitatokea vikundi vingi na kila mtu ataanza kufanya anachotaka,” alisema Profesa Baregu na kuongeza:

  “Wananchi wakifikia hatua ya kutumia nguvu ya umma, serikali nayo itaanza kutumia nguvu kutawala, matokeo yake ni umwagaji wa damu kama katika baadhi ya nchi za kiafrika zenye machafuko kwa sasa.”

  Profesa Baregu pia alisema, sababu kubwa iliyowafanya watendaji hao wakuu wastaafu wa serikali kutoa kauli hizo nzito, ni kutopata nafasi ya kufanya hivyo ndani ya chama chao.

  Akizungumzia kauli aliyoitoa Jaji Warioba kuwa “Uongozi hivi sasa uko karibu sana na matajiri kuliko wananchi; kwa sasa matajiri ndio wenye sauti."

  Profesa Baregu alisema, matajiri kwa sasa wana sauti kuliko watu wanyonge kwa sababu ndio walioiweka serikali madarakani.

  “Matajiri ndio walioiweka serikali madarakani, matajiri hawa wenye sauti serikalini kwa sasa, walitumia kampuni za Kagoda na Dip green kuchota pesa BoT ambazo zilitumika katika uchaguzi wa mwaka 2005, uchaguzi ambao ndio umeiweka serikali ya sasa madarakani,” alisema Profesa Baregu.

  Profesa Baregu alitolea mfano malalamiko ya walimu kuwa ni kielelezo cha serikali kutojali vilio vya watu maskini.

  Baregu alisema kwa sasa kinachotakiwa kufanyika ili kuiokoa nchi na janga linaloikabili ni kufanyika kwa mdahalo kitaifa wa kujadili mustakabali wa nchi.

  “Kwa sasa inatakiwa tufanye ‘national debate’ (mdahalo wa kitaifa) kujadili mustakabali wa nchi, bila kufanya hivyo serikali itatupeleka pabaya,” alisema Profesa Baregu.

  Aidha, imeelezwa kuwa maoni yaliyotolewa na Mawaziri Wakuu wastafu Jaji Joseph Warioba na Dk Salim Ahmed Salim yasipotekelezwa, amani ya nchi itakuwa hatarini.

  Kwa nyakati tofauti mawaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Warioba na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk Salim Ahmed Salim jana walitoa kauli tofauti kuhusu mustakabali wa taifa, ambapo walisema mwenendo na mfumo wa Serikali ya Tanzania umezidiwa na rushwa na hivyo hauwezi kumsaidia Rais Kikwete kuikabili rushwa.

  Akitoa maoni yake juu ya kauli za viongozi hao, Mwenyekiti wa Chama Cha National League for Democracy (NLD), Dk Emmanuel Makaidi alisema kauli za viongozi hao ni dalili ya CCM kukosa uungwaji mkono na viongozi wake.

  Akizungumza katika ofisi za gazeti hili Dk Makaidi alisema pia kwamba, hiyo ni ishara kuwa viongozi hao, wanashinikiza mabadiliko ambayo pia wananchi wanayataka.

  “Hii ni dalili ya CCM kukosa ‘support’ ya viongozi wake pia ni ishara kwamba watu wamebadilika na wanataka mabadiliko, viongozi hao wanahimiza mabadiliko. Ni jambo zuri kuwa waliokuwa wapishi ndani ya CCM wamebadilika na kuhimiza mabadiliko,” alisema Makaidi.

  Aliongeza kuwa CCM haiwezi kuwachukulia hatua yoyote viongozi hao hata kuwahoji na kwamba, anawapongeza kwa ujasiri na kuwataka wengine kuiga mfano huo wa kusema wazi uozo ndani ya serikali kwa maslahi ya taifa. Imeandaliwa na Hussein Kauli, Fred Azzah na Exuper Kachenje
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ama kweli tutasikia mengi.
   
 10. L

  Lampart Senior Member

  #10
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I say, huyu mzee namuonea huruma? Is he trying to help CCM or destroy Tanzania?
  Kukosa ukubwa ni mbaya kweli! Mzee wa watu huyu anaadhirika ovyo!
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  no kusema maoni yake mtu kusichukuliwe kama usaliti au ni uasi au asiseme kwa kuwa yeye anayo yake

  ktk nchi ya kidemokrasia kaama tz tuijengayo kuna haki na wajiabu kwa serikali kutoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni yao na serikali kuyapim a na kuyafanyaia kazi na nnnaamini serikali inajua ikaifanyacho na pale wanapoona mjadala unaelekea kuligawa taifa inajua ni vipi wauzime mie nna imani sana na serikali yetu
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Warioba, Dk Salimu wote ni viporo ndani ya CCM wanaosutwa na nafsi zao kwa wakati usio wao.

  Wasijaribu kutupumbaza kuwa CCM ni safi ila WATU WACHACHE ndio waovu! si KWELI!! CCM NI ZAO LA UFISADI NA UHAI WAKE UNATEGEMEA UFISADI.Period!
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Oct 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  JK alifanya tu juhudi za kuingia ikulu, baada ya kuingia safari za nje, period! Kama nchi inasambaratika au la si jukumu lake! Namuunga mkono yule mbunge wa Tanga, CUF, aliyefunguliwa mashtaka kwa kusema JK anachekacheka tu hana lolote!
   
 14. R

  Ronaldinho Member

  #14
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inchi yetu iko katika mapito,na ndani ya haya mengi yatatokea ila twahitaji Muomba Mungu tuweze pita kipindi hiki kwa amani
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  aaaah lakini ni vitu gani hivi vinavyoendelea katika nchi hii ?
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  You guys are not serious.
  Warioba na Salim ni wazee wanaoheshimika nchini mwetu. Wana uchungu wa dhati kabisa wa nchi yao. Kuanza kuwakandia namna hii ni kukosa nidhamu na kufanya tuweke question marks juu ya uzalendo wenu. Hawa Wazee wanao wajibu wa kutoa mawazo yao ili wenye akili nzuri wayafanyie kazi na kusaidia kuinusuru nchi yetu kutokana na leadership vacuum iliyopo hivi sasa nchini. Najua mtanirukia na kutaka kunirarua lakini ukweli ndio huo. Lazima tuwe serious na mustakabali wa nchi yetu la sivyo tutaiangamiza nchi hii. It is high time na wazee wengine wakajitokeza kusema ili kulinusuru taifa letu na janga linalotunyemelea la nchi kusambaratika.

  Warioba na Salim ni patriots wa nchi hii, na hawana chembe ya ufisadi. Anayesema hawa wanahusika kwa hujuma yoyote nchini ni WAZUSHI na hawastahili kuitwa Watanzania! Tumechoka kusikia watu makini wakidhalilishwa kwa sababu ya kusema ukweli kujaribu kuinusuru nchi yetu.

  Nawafahamu vyema sana wazee hawa kwa kufanya nao kazi kwa kipindi kirefu so I know what I am talking about.

  Tuache mchezo mchafu wa kuchafua watu wazalendo bila sababu za msingi.
   
 17. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi JK anasikia kelele za wananchi ama yeye anaona ni sawa kabisa???NIlishawahi kusema,once watanzania wakionja utamu wa kubeba bunduki,machettes na mawe hiinchi itakuwa ndogo.
  Tuombe Mungu yasifike huko!
   
 18. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Lampart,

  Ukikanywa na kukumbushwa yaote ni kuambiwa kuwa jitizame kuna kasoro sasa unaposema ana Jaribu kusaidia au ku destroy TZ sijakuelewa hapo,

  Tatizo letu na viongozi wetu tukiambiwa kitu au kukoselewa kwanza huanza niambie wewe hujioni jamani tuwe na kasumba ya kuangalia jambo uambiwalio au ukosolewalo na ulipime pia na ulitendee kazi ila sisi tu wabishi sana as if tuta ishi milele dunia hii
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kevo,

  Napenda wambia Ikulu is an institution ambayo ina watu waano wajibika kwa kumshauri Rais na kama hawafuatilia mambo ya wananchi wao kiunda na kumpa report mbovo basi hapo rais wetu ana kazi ya ziada ya kuwa na kitengo chake cha siri cha kumhabarisha direct maana kuna mijitu mingine humo sijui kama kweli yana uchungu na nchi yetu hii au wako tu basi siku iwe imepita
   
 20. M

  Mchili JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Walichosema mzee Warioba na Salimu ni kweli, suala la kuwa ni wanaccm au walishindwa kufanya chochote wakati wa uongozi wao halifuti ukweli huo.

  Warioba was very effective as PM kwenye awamu ya kwanza ya Mzee Ruksa na ndio maana serikali ile ilifanya vizuri ukilinganisha na awamu ya pili ambapo warioba aliondolewa.
   
Loading...