GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Waraka wangu kwa Wabunge CHADEMAIkiwa leo ni Ijumaa ya 17 Juni 2011 tayari siku 9 za bunge la Bajeti zimekwishaondoka huku dhahiri kambi ya wabunge wa CDM haijakaa imara katika kutetea hoja zao ambazo zinaipa changamoto serikali kwa kuondokana na vitendo dhalimu na ufisadi unaonyong'onyeza ustawi wa Taifa.
Nimefuatilia kwa ukaribu mijadala yote tangu kuanza kwa Mkutano wa Nne wa Bunge na mijadala ya Bajeti kwa kuanzia na ule wa kupitisha rasimu ya mpango wa Maendeleo 2011/12 – 2015/16, hoja nyingi za kambi ya CDM zimekumbana na mgogoro wa kanuni za Bunge na nyingi kupuuzwa na waendeshaji wa Vikao vya Bunge na Nyingine kupewa maelekezo kuwa zipitie kwa katibu wa Bunge kwanza ajiridhishe kabla ya kupewa Baraka za kujadiliwa Bungeni.
Sikujua ni fungu gani alilolitumia Mh.George Simbachawene hapo jana kukataa kusikiliza hoja binafsi ya Mh. John Mnyika, kwani hata alipotajiwa fungu la kanuni za Bunge kuwa kuna hoja ambazo zinaweza kuwasilishwa bila hata taarifa ya Maandishi alikataa hoja hiyo na kumwambia Mh Myika, '' kama kiti kimekosea kuna utaratibu unaopaswa kuutumia kuwasilisha malalamiko yako na si kwa kubishana na kiti na kwa mantiki hii naendelea kusisitiza kuwa sikubaliani na kuwasilishwa hoja yako kabla katibu wa Bunge hajajiridhisha''.
Ukweli ni kwamba hoja hii iliwasilishwa na kupangwa katika kazi za Bunge za jana na ndio maana ilitambulishwa hata aliposimama Mnyika ni kwa ridhaa na kuitwa na Mwenyekiti, licha ya kuwa ghafla alimtaka kukaa kwa madai kuwa hajajiridhisha na uamuzi huo wa kuwasilishwa hoja jambo ambalo lilimchukua muda kutafakari na kisha kutoa uamuzi huo ambao sina shaka utakuwa uliharibu siku nzima ya Mnyika na mipango ya kambi ya upinzani.
Haya yote yanatokea lakini bado zile silaha za kambi ya CDM ambazo zinapewa matumaini makubwa kwa kutetea na kusimamia hoja zimekuwa zikikabwa koo na waendesha mijadala kwa hoja za kukinzana na vifungu na kanuni za kutoa hoja au miongozo Bungeni.
Sijui ni kwa kiasi gani kambi ya wabunge wa CDM wanakutana huko Dodoma na kupanga hoja zao kabla ya kusimama bungeni lakini pia kuchagua mwakilishi atakayesimamia hoja hiyo kwa mashiko na weledi wa hali ya juu, tumeshuhudia akina Mh.Regia, Leticia na Esther Matiko mara kadhaa hoja zao zikiwa kama zina mlengo wa eneo moja la kukuza CV katika jamii, jambo ambalo kambi ya CDM inapaswa kuliepuka na kujiapanga kwa kuendeleza imani yao kwa umma na kuutumikia kwa ufanisi mkubwa.
Kukinzana kwa Hoja na michango ya Wabunge wa CDM na kanuni za Bunge ni jambo ambalo wanapaswa kulitafutia Tiba ya haraka ili kuendelea kuimarisha hoja za upinzani na kuepuka fadhaha ambayo inajaribu kujengwa kwa sasa kama ni watu wasiokuwa na ufahamu na mambo na taratibu za Bunge licha ya kusheheni wasomi wa Tasnia mbalimbali.
Kipindi hiki ambacho hakika Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Mnadhimu mkuu kama biinadamu kifikara wanaonekana kusongwa na utitiri wa sintofahamu zinazotokana na kuandamwa sana na vyombo vya dola ni vema player makers wengine wakaunda umoja na kujipanga kwa dhati na kuratibu mipango ya upcoming players wengine ili kuimarisha shughuli na harakati za kambi ya Upinzani Bungeni.
Naiona hatari ya kufanikiwa kwa agenda ya Chama tawala kudhoofisha kambi ya upinzani kwa kasi kwa kushirikiana na vibaraka wao ambao wamekuwa wakiuliza maswali mengine ya set up yasiyokuwa na mashiko ili mradi tu kambi ya CDM ionekane si chochote si lolote.
Mfano mzuri ni swali la Mh.Habibu Nyaa Mbunge wa Mkanayageni CUF aliloliiuliza jana kwa Waziri Mkuu ambaye alitema majibu ambayo kwa akili ya kawaida kabisa lilifanyiwa kazi siku kadhaa zilizopita na kumpa nafasi kumeza na kutema vipengele ambavyo wakati mwingine alionekana kabisa kujigonga kuvitema kutokana na kukariri vitu vingi katika umri mkubwa.
Inawezekana kabisa mipango ipo katika kambi ya Wabunge wa CDM na labda tuvute subira kuona mabadiliko, lakini kwa mwenendo wa siku hizi 9 za awali nasukumwa kuandika waraka huu tukihitaji kuona kasi yenu na udadisi mkubwa wa mambo yenye maslahi ya Taifa kwa pamoja.
Daima hakuna awali mbovu…Aluta Kontinua
Nawasilisha