Waraka wangu kwa Wabunge CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wangu kwa Wabunge CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jun 17, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Waraka wangu kwa Wabunge CHADEMAIkiwa leo ni Ijumaa ya 17 Juni 2011 tayari siku 9 za bunge la Bajeti zimekwishaondoka huku dhahiri kambi ya wabunge wa CDM haijakaa imara katika kutetea hoja zao ambazo zinaipa changamoto serikali kwa kuondokana na vitendo dhalimu na ufisadi unaonyong'onyeza ustawi wa Taifa.

  Nimefuatilia kwa ukaribu mijadala yote tangu kuanza kwa Mkutano wa Nne wa Bunge na mijadala ya Bajeti kwa kuanzia na ule wa kupitisha rasimu ya mpango wa Maendeleo 2011/12 – 2015/16, hoja nyingi za kambi ya CDM zimekumbana na mgogoro wa kanuni za Bunge na nyingi kupuuzwa na waendeshaji wa Vikao vya Bunge na Nyingine kupewa maelekezo kuwa zipitie kwa katibu wa Bunge kwanza ajiridhishe kabla ya kupewa Baraka za kujadiliwa Bungeni.

  Sikujua ni fungu gani alilolitumia Mh.George Simbachawene hapo jana kukataa kusikiliza hoja binafsi ya Mh. John Mnyika, kwani hata alipotajiwa fungu la kanuni za Bunge kuwa kuna hoja ambazo zinaweza kuwasilishwa bila hata taarifa ya Maandishi alikataa hoja hiyo na kumwambia Mh Myika, '' kama kiti kimekosea kuna utaratibu unaopaswa kuutumia kuwasilisha malalamiko yako na si kwa kubishana na kiti na kwa mantiki hii naendelea kusisitiza kuwa sikubaliani na kuwasilishwa hoja yako kabla katibu wa Bunge hajajiridhisha''.

  Ukweli ni kwamba hoja hii iliwasilishwa na kupangwa katika kazi za Bunge za jana na ndio maana ilitambulishwa hata aliposimama Mnyika ni kwa ridhaa na kuitwa na Mwenyekiti, licha ya kuwa ghafla alimtaka kukaa kwa madai kuwa hajajiridhisha na uamuzi huo wa kuwasilishwa hoja jambo ambalo lilimchukua muda kutafakari na kisha kutoa uamuzi huo ambao sina shaka utakuwa uliharibu siku nzima ya Mnyika na mipango ya kambi ya upinzani.

  Haya yote yanatokea lakini bado zile silaha za kambi ya CDM ambazo zinapewa matumaini makubwa kwa kutetea na kusimamia hoja zimekuwa zikikabwa koo na waendesha mijadala kwa hoja za kukinzana na vifungu na kanuni za kutoa hoja au miongozo Bungeni.

  Sijui ni kwa kiasi gani kambi ya wabunge wa CDM wanakutana huko Dodoma na kupanga hoja zao kabla ya kusimama bungeni lakini pia kuchagua mwakilishi atakayesimamia hoja hiyo kwa mashiko na weledi wa hali ya juu, tumeshuhudia akina Mh.Regia, Leticia na Esther Matiko mara kadhaa hoja zao zikiwa kama zina mlengo wa eneo moja la kukuza CV katika jamii, jambo ambalo kambi ya CDM inapaswa kuliepuka na kujiapanga kwa kuendeleza imani yao kwa umma na kuutumikia kwa ufanisi mkubwa.

  Kukinzana kwa Hoja na michango ya Wabunge wa CDM na kanuni za Bunge ni jambo ambalo wanapaswa kulitafutia Tiba ya haraka ili kuendelea kuimarisha hoja za upinzani na kuepuka fadhaha ambayo inajaribu kujengwa kwa sasa kama ni watu wasiokuwa na ufahamu na mambo na taratibu za Bunge licha ya kusheheni wasomi wa Tasnia mbalimbali.

  Kipindi hiki ambacho hakika Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Mnadhimu mkuu kama biinadamu kifikara wanaonekana kusongwa na utitiri wa sintofahamu zinazotokana na kuandamwa sana na vyombo vya dola ni vema player makers wengine wakaunda umoja na kujipanga kwa dhati na kuratibu mipango ya upcoming players wengine ili kuimarisha shughuli na harakati za kambi ya Upinzani Bungeni.

  Naiona hatari ya kufanikiwa kwa agenda ya Chama tawala kudhoofisha kambi ya upinzani kwa kasi kwa kushirikiana na vibaraka wao ambao wamekuwa wakiuliza maswali mengine ya set up yasiyokuwa na mashiko ili mradi tu kambi ya CDM ionekane si chochote si lolote.

  Mfano mzuri ni swali la Mh.Habibu Nyaa Mbunge wa Mkanayageni CUF aliloliiuliza jana kwa Waziri Mkuu ambaye alitema majibu ambayo kwa akili ya kawaida kabisa lilifanyiwa kazi siku kadhaa zilizopita na kumpa nafasi kumeza na kutema vipengele ambavyo wakati mwingine alionekana kabisa kujigonga kuvitema kutokana na kukariri vitu vingi katika umri mkubwa.

  Inawezekana kabisa mipango ipo katika kambi ya Wabunge wa CDM na labda tuvute subira kuona mabadiliko, lakini kwa mwenendo wa siku hizi 9 za awali nasukumwa kuandika waraka huu tukihitaji kuona kasi yenu na udadisi mkubwa wa mambo yenye maslahi ya Taifa kwa pamoja.

  Daima hakuna awali mbovu…Aluta Kontinua

  Nawasilisha
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbe na wewe kichwa chako kinawaka moto kama changu ...!
  Safi sana.
  Nakungongea thnks ya maneno<<<THANKS>>>
   
 3. h

  hoyce JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hivi ninyi mlitegemea hoja za Chadema zipite bungeni, kwenda wapu? Ajabu! Wanachofanya chadema ni siasa zenye nia ya kuonesha mapungufu katika sheria, kanuni, na mipango na utendaji wa CCM na serikali yake, lengo ni kuelimisha wananchi na kuwaonesha kwa CCM imeshindwa kutawala/kuongoza na mbadala wake ni Chadema. Ukiwapima kwa hili kwa hizi siku 9 wamefanikiwa sana. Usitegemee hata siku moja, mfano Mkulo aachane na bajeti yake achukue ya Zitto, au spika ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu CCM apitishe kiulaini hoja ya Mnyika ya kuimaliza serikali ya Magamba; au mbunge wa CCM au wa CUF asimame aseme wanachofanya Chadema ndiyo sahii.
   
 4. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hata wasipozikubali hoja kwa uwazi lakini ukweli unabaki palepale na utawachoma mioyoni kama mkuki watasutwa na dhamila zao Mungu washa moto wa majuto katika nafsi za wanaopindisha ukweli kwa masilahi yao bila kujali umma
   
 5. Joyum

  Joyum Senior Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wengi wa sisiem wapo so defensive na ndo walichotumwa hata kama hoja ni mbovu kiasi gani. na teknik yao ya kuingilia marakwamara wakati wabunge wa upinzani wanapoongea naona imepangwa vizuri sana. Kwa kweli CDM wanatakiwa wajipange mana interuption ni kubwa na bajet itapita kwa kulazimisha na haitabdilika na wala hakutakua na tija.
   
 6. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu Hoyce Hatujaelewana bado hebu soma taratibu thread ubaini mashiko yako wapi na nini hasa ambacho tunakitahimini kwa wapiganaji wetu mjengoni. Hakuna kufanikiwa unakokuona otherwise kama hufuatilii Bunge.
  Kuna mchezo mchafu unaendelea huko hebu chukua muda walau asubuhi hii utazame kinachoendelea Mjengoni.
   
 7. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Teacher We need changes na katika zama hizi za Ukomavu na upana wa Demokrasia na uhuru wa maoni, uwanja wa siasa lazima uwe unatoa mazingira ya usawa kwa wapiganaji wote ili mwisho wa siku sauti ya mnyonge iweze kupenya.

  Hatuhitaji ukweli uwaume tu na ubaki kama ulivyo, tunahitaji majemedari wasimame imara kusimamia mabadilko na inawezekana kwa mipango mipya na iliyosimama hasa kuvunja ukuta huu unaojengwa sasa kwa interruptions na kudhihakiana kusiko na misingi.
   
 8. j

  justo james Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa ukweli sasa hivi CDM wakiongea lolote lile haliungwi mkono kwa namna yoyote ile, so kilichobaki ni kitu kimoja tu, mwenye akili aelewe na kufahamu nia ya CDM then tutakutana kwenye uchaguzi 2015
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  SERIKALI YAO,
  BUNGE LAO,
  SPIKA WAO,
  MAHAKAMA ZAO,
  RAIS WAO,
  POLICE WAO,
  USALAMA WA TAIFA WAO,
  TUME YA UCHAGUZI YAO,
  TAKUKURU YAO,


  Sasa wewe kwa akili zako unategemea haki gani hapo? hata hili suala la posho nina uhakika 99% halitavuka - cha msingi CHADEMA wasirudi nyuma na kizuri zaidi wananchi wameanza kuelewa taratibu haki zao za msingi kupitia mikutano ya hadhara - kuna siku watazidia kwa nguvu.

  Peleka hoja bungeni, unajua kabisa itabezwa, baada ya bunge rudi kwa wananchi waeleleze kwa lugha nyepesi nini makusudio ya hoja yako na nini kimetokea bungeni - fanya aandamano na mikutano ya hadhara bila kuchoka - HIYO NDIYO NJIA PEKEE YA KUDAI HAKI YA WATANZANIA WAKO.

   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  ushauri mzuri sana
   
 11. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wao wana pesa na dola sisi tuna mungu na nguvu ya uma.
  kitaeleweka tu.
   
 12. s

  sawabho JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Waache kukurupuka na kufanya mambo kwa pipa kabla ya kufanya uchambuzi makini na kujiridhisha wao wenywe na washauri wao.
   
 13. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mch. Msingwa muda si mrefu anahoji Utawala bora na Sheria anasema Serikali ya CCM inapiga watu inaua watu, imekuwa ikigandamiza na kukandamiza wananchi wa kutozingatia utawala wa Sheria
  Ghafla napigwa Utaratibu wa Kanuni na LUKUVI
  Utaratibu Lukuvi: Kwa utaratibuwa Kanuni za Bunge Mbunge yeyote hatakiwi kuzungumzia jambo lolote ambalo liko nje ya mjadala unaoendelea jambo ambalo Mh. Msigwa kalifanya, Nikiwa kama kiongozi wa Serikali napingana na madai ya Mh. Mbunge pia namtaka anithibitishie ni mahala gani serikali ya mapinduzi imefanya mambo haya. Atoe uthibitisho
  Jenista Mhagama: Anasema suala hilo halipo katika hoja ya Msingi ya Agenda ya Fedha na anamtaka Mh. Mchungaji Msigwa athibitishe au aondoe kauli yake
  Mh. Mchungaji Msigwa: Serikali imeua watu Arusha na Nyamongo na imepiga wanafunzi wa UDOM ambao ni majeruhi na kwa sasa wamelazwa Hospitali
  Mhagama: Unathibitisha
  Msigwa: Ndiyo
  Mhagama: Nileletee uthibitisho kwa maandishi na kama utashindwa sheria itachukua mkondo wake
  Msigwa: anaanza tena kwa kutoa ufafanuzi maandamano
  Mhagama: anasimama na kumtaka kurejea katika mjadala na vinginenvyo amwite mchangiaji mwingine
  Msingwa: anaendelea na Hoja na deni lakuwasilisha kwa maandishi madai ya kuwa serikali ya CCM imeua na kupiga watanzania

  Nani asiyejua haya yanatokea, wanakataa nini sasa, narejea katika waraka wangu kwa Wabunge wa CDM kuna jambo hapa la msingi sana linalopaswa kushughulikiwa haraka.
  Vita inaendelea katika ya Mhagama na Msigwa&#8230;Kazi ipo leo
  Hatimaye Msigwa anarejea katika Hoja.
   
 14. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mch. Msingwa muda si mrefu anahoji Utawala bora na Sheria anasema Serikali ya CCM inapiga watu inaua watu, imekuwa ikigandamiza na kukandamiza wananchi wa kutozingatia utawala wa Sheria

  Ghafla napigwa Utaratibu wa Kanuni na LUKUVI

  Utaratibu Lukuvi: Kwa utaratibuwa Kanuni za Bunge Mbunge yeyote hatakiwi kuzungumzia jambo lolote ambalo liko nje ya mjadala unaoendelea jambo ambalo Mh. Msigwa kalifanya, Nikiwa kama kiongozi wa Serikali napingana na madai ya Mh. Mbunge pia namtaka anithibitishie ni mahala gani serikali ya mapinduzi imefanya mambo haya. Atoe uthibitisho

  Jenista Mhagama: Anasema suala hilo halipo katika hoja ya Msingi ya Agenda ya Fedha na anamtaka Mh. Mchungaji Msigwa athibitishe au aondoe kauli yake

  Mh. Mchungaji Msigwa: Serikali imeua watu Arusha na Nyamongo na imepiga wanafunzi wa UDOM ambao ni majeruhi na kwa sasa wamelazwa Hospitali

  Mhagama: Unathibitisha

  Msigwa: Ndiyo

  Mhagama: Nileletee uthibitisho kwa maandishi na kama utashindwa sheria itachukua mkondo wake

  Msigwa: anaanza tena kwa kutoa ufafanuzi maandamano

  Mhagama: anasimama na kumtaka kurejea katika mjadala na vinginenvyo amwite mchangiaji mwingine

  Msingwa: anaendelea na Hoja na deni lakuwasilisha kwa maandishi madai ya kuwa serikali ya CCM imeua na kupiga watanzania

  Nani asiyejua haya yanatokea, wanakataa nini sasa, narejea katika waraka wangu kwa Wabunge wa CDM kuna jambo hapa la msingi sana linalopaswa kushughulikiwa haraka.

  Vita inaendelea katika ya Mhagama na MsigwaÂ…Kazi ipo leo

  Hatimaye Msigwa anarejea katika Hoja.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Huu ni waraka au taarifa? anyway, imekaa vizuri japo tulitaka utoe strategies kufanikisha hili zoezi la wenyeviti wa kamati
   
 16. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mie nimenzia hapo Mkuu, weka nyongeza lengo tunataka walau kuanzia wiki ijayo walu turejeshe uhai katika Jumba
   
 17. m

  mtimbaru Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  chadema- tufungue matawi ya chama mpaka vijijini ili tuweze kuikomboa nchi wananchi wengi hawajui haki zao kabisa
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
   
 19. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
   
 20. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hoja ya Mauaji ya Nyamongo na Arusha kwa Malngo wa Nyuma na imesikilizwa licha ya Technical Time Knock out but message sent BIG UP LISSU mbinu na maarifa sasa yanaonekana.

  Aluta Continua
   
Loading...