Waraka wangu kwa Madaktari!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wangu kwa Madaktari!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dark City, Jan 29, 2012.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ndugu Madaktari wote na wale wenye mapenzi mema,


  Nimepata habari za kusikitisha kwamba PM amekwanda kukutana nanyi bila mawasiliano ya karibu na viongozi wenu na kukuta hamko ukumbini. Kama kawaida ya watawala wetu (ambao kiukweli walitakiwa kuwa viongozi), ametoa maagizo yake. Kwamba lazima mrudi kazini kesho Jumatatu na ambaye hatarudi kazini amejifukuziisha. Pia inasemekana amepiga marufuku mikutano yote ya madaktari.

  Huu ni uthibitisho mwingine wa matumizi ya nguvu kupita kiasi kama ambavyo serikali imezoea kufanya huko nyuma. Nawaomba mpime uzito wa maagizo ya PM kwa kulinganisha na madai yenu. Natambua kuwa katika hali kama hii, ni rahisi watu kuanza kufikiria kitakachowakuta kesho au kesho kutwa baada ya kufukuzwa kazi. Ila naomba mtambue kuwa dokta habanwi kufanya kazi ya serikali. Kwa hiyo mnaweza kutumia ujuzi wenu mahali pengine lakini mkiwa watu wenye hadhi na heshima inayolingana na taaluma yenui

  Ila kama mtaona kuwa bila kufanya kazi serikalini hakuna maisha tena, basi nawashauri mrudi kazini kesho asubuhi na mapema. Hata hivyo kama hilo litatokea, basi mjue kuwa huo ndio utakuwa mgomo wenu wa mwisho kabisa labda baada ya kizazi chenu kuisha.

  Mungu awabariki madaktari wetu na awape uvumilivu na busara/hekima ili mpiganie hatima yenu wenyewe na generations zote za madaktari wa nchi hii.

  God bless you all,

  Dark City,
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  nadhani kesho watafuta kada ya udaktari tanzania.mamia ya madaktari wako safarini kwenda dar kwenye kikao endelevu..
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ushauri mzuri sana naungana nawe kwa yote isipokuwa kuwashauri kesho asubuhi wawahi kazini, kama ulivyosema hii itakuwa mwisho wa migomo yao na dharau kubwa kwa taaluma yao, nadhani hakuna haja ya kuogopa, endeleeni na mikutano yenu wawatumie FFU. Shime madaktari msijidhalilidhe kwa vitisho vya huyu aliyepinda.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kweli kabisa,

  Ndiyo maana nina hamau ya kuiona Thisi time tomrrow!!

  DC!!
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ndugu wapendwa madaktari,poleni sana kwa msukosuko unaoendelea.

  nawapongeza kwa kufikisha ujumbe wenu kwa watanzania na watawala.


  Nina ushauri kwenu jiono hii,sikiliza.

  Nakuombeni mrudi kazini,mimi nauona mgomo wenu kama ni ombi kwa baba na hakika amekusikieni hata kama hamjaonana mkaongea (mmepishana)

  Tafakarini madhara/matokeo ya keshokutwa kwa familia zenu.kwa kweli itakuwa ni kiama kwenu.

  Acheni kugombana na mzazi wenu,kwa kuwa mlishaonana na mawaziri nina imani madai yenu yameshamfikia waziri mkuu.

  Wahudumieni watoto wenu,mama zenu,wajomba zenu na hasa dada zenu ambao ni wajawazito na sasa wameyaweka maisha yao mikononi mwenu kama ndio wakombozi pekee.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka wakati wa utawala wa Mwinyi kuna wanafunzi pale UD waliwahi kufanya madudu wakafukuzwa wote.

  Upo wakati pia sikumbuki ilikuwa ni awamu ya nani pale mhimbili waliwahi kutimuliwa madaktari wote.sasa madaktari msipambane na dola.RUDINI KAZINI HUKU MKIENDELEA KUTUMIA DIPLOMASIA KUDAI HAKI ZENU.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  DC, kama kweli serikali inajali wananchi, tutajua kesho

  maana wao wakiugua wanaenda india, kwahiyo hata hospitals zetu zikiwa hazina madaktari wao hawaathiriki
   
 8. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Natamani kuiona hiyo kesho,tuone
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kumbukeni kitu kimoja kuwa success never comes without sacrifice. Madaktari inabidi mjitoe muhanga ili vizazi vijavyo vya madaktari vije vipate heshima wanayostahili madaktari wote duniani, msipojitoa muhanga mtakuwa wasaliti kwa vizazi vijavyo vya madaktari
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Huu ni uchochezi sasa... hebu tuwaache madaktari waamue wenyewe jamani... wakifukuzwa utawasaidia kupata hizo nafasi???
   
 11. T

  TUMY JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli mgomo huu ni wa madaktari wote hakuna maamuzi ya kuwafukuza kazi yatakayo chukua nafasi kesho, Pamoja na kwamba Serikali imekuwa ikitumia maguvu kwenye maamuzi yao mbalimbali kuna mifano mingi hapo. Ila Tatizo langu kwa Madaktari ni kwanini mmegoma kukutana na PM leo, suala la kwamba leo ni jumapili kama ndio sababu pekee binafsi siiungi mkono kwani hata Kitabu Kitakatifu Biblia kinasema huwezi kumwacha punda shimoni kisa tu ni siku ya sabato mlipaswa kwenda kukutana nae hata kama leo ni jumapili, unless otherwise pana sababu nyingine ya ninyi kutotokea ukumbini, malalamiko yenu ni ya msingi lakini suala la kutotokea ukumbini mimi siliungi mkono.
   
 12. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Serikali yenyewe imeshindwa kuziedesha Hospital wataweza kuajiri madokta wapya? kwa pesa gani walionao. Naungamkono Madaktari hakuna kurudi nyuma, mpaka kieleweke
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,212
  Trophy Points: 280
  Mkuu mie nakubaliana nawe. Sasa hivi madaktari wanahitaji kuwa na mshikamano wa hali ya juu ili kupambana na hii Serikali dhalimu. Natumai hiyo kesho wataendelea na mgomo na kutokubali vitisho vya kipumbavu toka Serikali dhalimu.
   
 14. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wananchi wengi wako nyuma ya madaktari,tunajua wanachopigania!inatakiwa wawe na msimamo wa dhati!
   
 15. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usilete vitu vya kusadikika na ambavyo hauna uhakika navyo!
   
 16. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wewe una taaluma gani?
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Watanzania wengi tuko kama wewe...tunataka watoto wazaliwe ila mama asitoke damu hata tone moja!!
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kweli mkuu,

  Kama wakiweza kuvuka masaa 24 ya kuanzia leo saa 6 usiku...watakuwa wamepiga hatua muhimu katika kuifanya taaluma ya udaktari urejeshewe heshima yake!!

  Babu DC
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nimewahi kushiriki katika migomo mingi tangia nipo A level hadi chuo. kuna migomo ambayo nilishiriki kikamilifu na kuna migomo ambayo nilishiriki kama sehemu ya jumuiya. Sasa huwa unafika wakati kama huu ambao linatolewa tamko kwamba kufikia kesho ingieni madarasani na kama mtu hataingia darasani basi amejifukuza. Hatua hii huwa ni kimbembe manake hapa ndipo wana mgomo hufarakana baada ya kufikiria wametoka wapi wanategemewa na nani na mipango yao ni ipi! Wengi hurudi nyuma.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,212
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa Mkuu wengine wana wake zao na watoto na hawana income nyingine hivyo hapa wanakuwa njia panda huku wakiwa hawajui wataendelea vipi kujikimu wao na familia zao katika kipindi hiki kigumu kwao. Kama wataamua kuendelea na mgomo basi tuanzishe michango kupitia hapa jamvini ili kuwasaidia hawa wenzetu katika hali ngumu zitakazowakabili siku za usoni.
   
Loading...