Waraka wa Wazi kwa Mh Magufuli

Waraka wa Wazi kwa Mh Magufuli

Dazzle

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
214
Reaction score
56
Kwanza nianze kwa kukupongeza kwa kuchaguliwa kuongoza chama cha mapinduzi kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu wa octoba.

Sina shaka na utendaji wako wa kazi na wala sina shaka na uadilifu wako. Nalisema hili kutoka moyoni maana hata kama nikinyamaza kazi zako ulizofanya zitaongea.

Ninaandika waraka huu kwako mh nikitambua ukubwa wa jukumu lililoko mbele yako. Jukumu hili ni kubwa hasa kutokana na nchi yetu kuwa katika kipindi kigumu ambacho wananchi wengi wanaishi ktk umaskini wa kutupa,dhuluma kwa wanyoge, rushwa na maradhi.

Kuteuliwa kwako kuna maana kuwa wewe Mh Magufuli una uwezo wa kubeba mzigo huu. Waraka wangu utajikita katika mambo makuu yafuatayo

Kwanza unamuhitaji Mungu kuliko vipindi vingine vyovyote ktk maisha yako ili akupe hekima kama mfalme Sulemani ya kuweza kuongoza na kuamua kwa haki. Akupe ujasiri kama mfalme Daud ambaye aliweza kukabiliana na goliati ktk kushughulikia wala rushwa na waonevu ktk jamii yetu ya watanzania.

Jiepushe na mambo ya kishirikina maana viongozi wengi wa leo wanaamini kuwa hirizi inaweza kuongoza. Watawala wengi waliotumia njia hii mwisho wao umekuwa mbaya. Mtangulize Mungu katika kila jambo utakalolifanya.

Mungu anapenda mtu anayesimama ktk haki. Simama ktk haki. Anayestahili haki apewe haki na anayestahili huku apewe sawa sawa na matendo yake. Watawala wengi wameminya haki za watu wakawapa wasiostahili. Maumivu na majozi ya watu hawa yamesababisha laana ktk nchi yetu.

Jambo la tatu siasa si uadui. Jihadhari na siasa za chuki. Wako watakaokushauri kupanga au kutumia mbinu ovu kwa washindani wako nakushauri hawa waepuke.Usiingie ikulu na mikono yenye damu maana hii itakuwa ni laana kwako na kwa nchi. Kazi zako na upendo wa dhati walionao kwako watanzania unatosha kukupa uongozi wa nchi hii.

Mwisho nautambua unyenyekevu wako.nafasi uliyopewa isikupe kiburi ukaacha tabia yako ya unyenyekevu ulionao. Bibilia inasema Mungu huwapinga wenye kiburi na kuwapa wanyenyekevu neema. Nakusihi utakapofanikiwa kuongoza nchi hii yakumbuke sana haya na yawe sehemu ya dira ya uongozi wako.

Nakutakia afya njema ktk mbio hizi za kugombea urais wa kuongoza nchi hii.
 
Back
Top Bottom