Mtu haachi asili yake.Lakini kaandika akiwa Dar es salaam, kazi kwelikweli.
Mimi nitajikomba na kumuombea raisi wangu kuliko hao wengine, raisi ana mzigo mkubwa sana juu ya taifa hilo kuliko hao wanaotawala watu wa imani moja.Kujikomba kwa aina hii unatutia aibu.
Hujui kuwa mapadre licha ya kuendesha ibada kila siku, hasa jumapili , wako exposed?
Na haiingii akilini mwako kuwa wamezika watu wengi sana waliokufa kwa corona?
Muwage na akili basi hata kama mnajikomba!
Usichojua ni kwamba nchi hii sio ya kidini lazima utambue kuwa hata washirikina ni sehemu ya taifa. Kwa hiyo raisi hawezi kutawala nchi kivatican au kizungu.Context ya arguments zako na muelekeo ni ule tunaona wazi kusupport washirikina.
Tatizo mheshimiwa Mimi sijaliona hilo kanisa kubeba sura ya Yesu wanayemuhubiri. Inawezekana hata hayo maneno mene mene yanalihusu hata hilo kanisa. Hivi hujatambua kwamba hivi sasa duniani hata fasheni ya vijana kujiunga na usista na upadri inaondoka kwa sababu ya matendo ya hao watu? Kwa tabia zao watu wanaanza kusita kuwafanya watoto zao kuwa mapadri au masista.Huo ni uamuzi wako mkuu.
Ila sote tunamuombea Rais wa madaraka makubwa nchini, ayatende mema daima na kuutukuza Ukuu wa Mungu, Ukweli daima.
Na tunafanya hivyo kila jumapili.
Tukiona maandishi " mene mene tekel upharsin " ukutani, kama mapadre wanavyoonyesha ukweli, tujirudi nyuma na kutafakari.
Na wewe umechukua hatua gani? Umewahi siku za ibada kuomba walau dakika 5 utoe tahadhari na kukumbusha kujikinga kwa waumini wenzako? Unamnyooshea kidolekNa Mimi alichonishangaza Doctor huyu ni kuelekeza lawama kwa serikali na wakati huohuo kuwa kipofu wa wajibu wake na wa kanisa!
Kanisa lilishatoa waraka wa maelekezo kwa wakleri na walei juu ya umuhimu na namna ya kujikinga na korona! Mimi ni mkatoliki ninayehudhuria misa kila jumapili lakini makanisa tofauti kulingana na ratiba yangu, hivyo tangazo hilo nililisikia makanisa tofauti niliyohudhuria.
Kinacho nisikitisha ni kwamba makanisa mengi ya RC hayana mpango kabisa wa kutkeleza waraka huo. Waumini wanarundikana kanisani na kwenye shughuli nyingine za kanisa bila tahadhari yeyote. Hakuna cha barakoa (labda upende mwenyewe), hakuna cha kunawa mikono na waumini wanajazana kwenye bench bila kuacha nafasi.
Viongozi wapo, Dr Kitima yupo, tena Katibu wa TEC, mwenyekiti wa Baraza la maaskofu yupo, maaskofu wapo, mapadre wapo! Kinachonishangaza Dr ana guts gani za kunyoshea vidole wengine( japo kiujanja) wakati mwenyewe ameshindwa kuchukua hatua kwenye himaya yake ambayo ana mamlaka nayo?
Kwa kweli hana moral authority ya kukosoa. Asidondokee kwenye siasa za Jamaa zetu ambao wana kosoa wakati wenyewe hawachukui hatua za kujikinga. Hao iko wazi wanatafuta political mileage.
Usihamishe magoli, swala hapa ni ukweli.Tatizo mheshimiwa Mimi sijaliona hilo kanisa kubeba sura ya Yesu wanayemuhubiri. Inawezekana hata hayo maneno mene mene yanalihusu hata hilo kanisa. Hivi hujatambua kwamba hivi sasa duniani hata fasheni ya vijana kujiunga na usista na upadri inaondoka kwa sababu ya matendo ya hao watu? Kwa tabia zao watu wanaanza kusita kuwafanya watoto zao kuwa mapadri au masista.