Waraka wa January Makamba kwa Ruge; "Ruge, naomba nisikilize kidogo. "

karibu..kuna magazine fulan linaitwa readers digest niliwah soma humo pia..!inaheal a lot..huyo mdada yy aliandika barua kbs kwa mumewe alokuwa amefariki akaiweka chn ya mti..unaweza hisi uchawi ila inasaidia mno nafsi kutulia
Kweli kabisa naamini hilo inasaidia in a way
Kuna wakati unakuwambuka wapendwa waliotangulia na unaanza kuongea nao peke yako
Lakini tunaumia kimoyo moyo

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
January pamoja na elimu yake anamwandikia mtu aliyekufa ??

Kweli Tanzania tunayo safari , kwahiyo ataisoma hiyo habari yako ??

Kama kiongozi ana uelewa wa hivi , je mkulima wa nyamongo ??
Hayo anatuandikia sisi tulio hai, kaka jiongeze kidogo. Hii ndio fasihi andishi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii inachora Picha ya ombwe la kitu cha kusema. Mtu akiwa hana jambo la maana la kusema mbele ya watu, matokeo ni kama haya. Sijaona Substance zaidi ya sentensi moja kufuatiwa na sentensi nyingine tu!

Hivi watanzania na Waafrika tunapenda sana kuongea kuliko kutafakari? Tunapenda sana kuongea kuliko kutenda? Tunawashwa sana kuongea kiasi kwamba tunasahau kuchuja cha kuongea? Hivi ni lazima kila mtu aongee juu ya Msiba Wa Ruge?

Hii kuropokaropoka, inatufunua kama Taifa kwamba ni watu ambao Mara zote hatuna agenda! Tu kama majani katika miti tunadansi kulingana na upepo unavyovuma. Tungalikuwa na agenda tusingalikuwa kila mtu anaamka na kusemasema tu lolote ilimradi watu wasikie Fulani naye kaongea. Kwa hiyo,huyu Makamba alilenga kuujulisha umma wa watanzania kwamba alienda kumsalimia Ruge hospitalini Afrika Kusini?

Kama kweli tu watu tunaotumia AKILI badala ya HISIA, mbona sijasikia hata mmoja akitoka na wazo la kuunda hata RUGE TRUST FUND yenye mission ya kuhamasisha watanzania kuchukua tahadhari juu ya visababishi vya ugonjwa wa FIGO. Asasi ambayo itajikita kwa kusaidiana na asasi zingine za kitafiti Tanzania au duniani katika kutafuta ufumbuzi wa tiba ya kudumu ya ugonjwa wa Figo. Hakuna anafikiria juu ya hilo na sababu iko wazi: tunafikiria Mungu ndiye anatuletea magonjwa ili tufe. Mungu aliumba mema tu na Mabaya (EVIL) ni matokeo ya sisi kushindwa kuwajibika katika uelekeo chanya. Ni matokeo ya kutumia AKILI, UHURU na UTASHI kivingine.
Mmhhhh!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na January Makamba
Ndugu yangu Ruge, najua ndio umewasili huko upande wa pili na si ajabu una mambo mengi na bado unasalimiana na jamaa zetu wengi waliotangulia.
Lakini naomba uchukue muda wako kidogo kunisikiliza. Nimeumia sana na nimelia peke yangu kwamba umetuacha namna hii. Sawa, umeitwa kwa wakati wako na sisi hatuna kauli kwenye suala la wakati wa kuitwa lakini nilitegemea, na sikuwa na shaka kabisa, kwamba tutakamilisha yale mawazo yako mengi mazuri uliyoniambia. Sikuwa na shaka kwasababu nilishuhudia pale Hospitali ya Kairuki kabla hujaenda India, ulivyorudi kutoka India, na siku nimekuona Afrika Kusini, ulivyokuwa unapigana kupona — hadi madaktari wa Afrika Kusini wakakupa jina “Ruge, The Fighter”. Jina sahihi kabisa lililotafsiri harakati za maisha yako.

Unajua nini? Nilikuwa nangoja urudi Dar nikwambie nilichogundua mara ya mwisho nilivyokuona hospitali. Lakini ngoja tu nikwambie kabla sijaja huko uliko. Ile kiu kubwa ya kupona niliyoiona kwenye macho yako haikuwa kwa ajili yako wewe, bali kwa ajili ya kutoiangusha familia yako nzima iliyosimamisha kila kitu kukuuguza na Watanzania wote waliokuwa wanakuombea. Ulipigana kupona, sio kwa ajili yako, bali kwa ajili yetu. Hukuamka kitandani lakini hukushindwa mapambano kwasababu umeamkia ndani ya mioyo ya Watanzania. Huku tuliko karibu watu wote tunakumbuka ulivyotugusa. Jamaa yangu, tunakuomboleza wakati huu, halafu tutabaki tunafurahia nuru yako katika maisha ya wengi kwa urefu wa uhai wetu. Umekimbia mbio njema, umemaliza safari yako vyema.

Majonzi yangu ni kwamba umeondoka kabla sijalipa kwa ukamilifu deni langu kwako. Deni la upendo na urafiki wa kweli. Ulinipa heshima kubwa ya kuwa msiri wako — kwa kuniamini na kunielezea wasiwasi wako, ndoto zako, matumaini yako, harakati zako, mipango yako. Ulinipa heshima ya kunipa fursa ya kubishana nawe kuhusu mawazo na fikra zako.

Majonzi yangu ni kwamba kuna vitu fulani vikubwa na vizuri tulivipanga — mimi na marafiki na wadogo zako, kwa ajili yako, kwa staili yako — mapema mwezi Machi, ambavyo naamini vingekupa tabasamu. Kama unaweza, hapo ulipolala, tupe ishara tufanyeje.

Nafarijika kidogo kwamba nilipata nafasi ya kukukumbatia kwa mara ya mwisho. Sikujua kwamba tunaagana. Ulinishika mkono kwa nguvu, hukutaka kuuachia, na ulitabasamu niliposema nakungoja Dar tukae pale THT, kama kawaida yetu, kujadili mawazo na mipango yako mingi.

Ingawa umeshawasili huko upande wa pili, familia yako na watu wengi watauaga mwili wako kwa heshima kubwa. Utajengewa kaburi. Nadhani litawekwa marumaru. Lakini tukitaka kukusalimia tena hatutakutafuta kaburini kwako. Tutakutafuta kwenye nyoyo za watu uliowagusa na kuwasaidia. Na ni wengi kweli. Kumbukumbu yako itabaki kwenye nyoyo zao na kwenye mafanikio yao. Watoto wako hawapo peke yao. Watalia sana, lakini ni kwa muda tu; kwasababu watafunikwa kwa upendo wetu sote na watafarijika, na watakuwa na fahari, kwa jinsi unavyosemwa na unavyokumbukwa.

Ndugu yangu, nisikuchoshe. Mengine tutaongea tutakapokutana tena kwasababu kwa hakika sisi sote, mmoja mmoja na kwa wakati wetu, kwa kadri ya mipango ya yeye aliyetuumba, tutakufuata huko. Miaka yote nimekujua, sijawahi kukuona umepumzika. Pumzika kwa amani kwa sasa — na milele.

Ndimi, rafiki yako,
January Makamba
27 Februari 2019
Isivyo bahat jambo la kuonana ni halipo tena,
Na hata hiyo siku ya malipo kila mmoja atashughulishwa na lake
Na huyo anaeliliwa laa shaka hana tena ila Maangamivu,
 
Umemuombolezea sana Ruge homeboy wangu January,na mimi niseme R.I.P shemeji yangu na ndugu yangu Ruge.Lakini hebu seriously tu reflect back a bit.Kwa nini maombolezo yote haya?Sina wivu,but exactly,why all this.Kuna jambo gani nyuma ya pazia?To me frankly kifo cha Ruge ni kifo kama vifo vingine!But why all this fuss.Is he more human than other people?
 
Back
Top Bottom