Waraka wa January Makamba kwa Ruge; "Ruge, naomba nisikilize kidogo. "

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742

Na January Makamba
Ndugu yangu Ruge, najua ndio umewasili huko upande wa pili na si ajabu una mambo mengi na bado unasalimiana na jamaa zetu wengi waliotangulia.
Lakini naomba uchukue muda wako kidogo kunisikiliza. Nimeumia sana na nimelia peke yangu kwamba umetuacha namna hii. Sawa, umeitwa kwa wakati wako na sisi hatuna kauli kwenye suala la wakati wa kuitwa lakini nilitegemea, na sikuwa na shaka kabisa, kwamba tutakamilisha yale mawazo yako mengi mazuri uliyoniambia. Sikuwa na shaka kwasababu nilishuhudia pale Hospitali ya Kairuki kabla hujaenda India, ulivyorudi kutoka India, na siku nimekuona Afrika Kusini, ulivyokuwa unapigana kupona — hadi madaktari wa Afrika Kusini wakakupa jina “Ruge, The Fighter”. Jina sahihi kabisa lililotafsiri harakati za maisha yako.

Unajua nini? Nilikuwa nangoja urudi Dar nikwambie nilichogundua mara ya mwisho nilivyokuona hospitali. Lakini ngoja tu nikwambie kabla sijaja huko uliko. Ile kiu kubwa ya kupona niliyoiona kwenye macho yako haikuwa kwa ajili yako wewe, bali kwa ajili ya kutoiangusha familia yako nzima iliyosimamisha kila kitu kukuuguza na Watanzania wote waliokuwa wanakuombea. Ulipigana kupona, sio kwa ajili yako, bali kwa ajili yetu. Hukuamka kitandani lakini hukushindwa mapambano kwasababu umeamkia ndani ya mioyo ya Watanzania. Huku tuliko karibu watu wote tunakumbuka ulivyotugusa. Jamaa yangu, tunakuomboleza wakati huu, halafu tutabaki tunafurahia nuru yako katika maisha ya wengi kwa urefu wa uhai wetu. Umekimbia mbio njema, umemaliza safari yako vyema.

Majonzi yangu ni kwamba umeondoka kabla sijalipa kwa ukamilifu deni langu kwako. Deni la upendo na urafiki wa kweli. Ulinipa heshima kubwa ya kuwa msiri wako — kwa kuniamini na kunielezea wasiwasi wako, ndoto zako, matumaini yako, harakati zako, mipango yako. Ulinipa heshima ya kunipa fursa ya kubishana nawe kuhusu mawazo na fikra zako.

Majonzi yangu ni kwamba kuna vitu fulani vikubwa na vizuri tulivipanga — mimi na marafiki na wadogo zako, kwa ajili yako, kwa staili yako — mapema mwezi Machi, ambavyo naamini vingekupa tabasamu. Kama unaweza, hapo ulipolala, tupe ishara tufanyeje.

Nafarijika kidogo kwamba nilipata nafasi ya kukukumbatia kwa mara ya mwisho. Sikujua kwamba tunaagana. Ulinishika mkono kwa nguvu, hukutaka kuuachia, na ulitabasamu niliposema nakungoja Dar tukae pale THT, kama kawaida yetu, kujadili mawazo na mipango yako mingi.

Ingawa umeshawasili huko upande wa pili, familia yako na watu wengi watauaga mwili wako kwa heshima kubwa. Utajengewa kaburi. Nadhani litawekwa marumaru. Lakini tukitaka kukusalimia tena hatutakutafuta kaburini kwako. Tutakutafuta kwenye nyoyo za watu uliowagusa na kuwasaidia. Na ni wengi kweli. Kumbukumbu yako itabaki kwenye nyoyo zao na kwenye mafanikio yao. Watoto wako hawapo peke yao. Watalia sana, lakini ni kwa muda tu; kwasababu watafunikwa kwa upendo wetu sote na watafarijika, na watakuwa na fahari, kwa jinsi unavyosemwa na unavyokumbukwa.

Ndugu yangu, nisikuchoshe. Mengine tutaongea tutakapokutana tena kwasababu kwa hakika sisi sote, mmoja mmoja na kwa wakati wetu, kwa kadri ya mipango ya yeye aliyetuumba, tutakufuata huko. Miaka yote nimekujua, sijawahi kukuona umepumzika. Pumzika kwa amani kwa sasa — na milele.

Ndimi, rafiki yako,
January Makamba
27 Februari 2019
 
Ukweli ni kwamba kila kazi na fursa zake, palipo na fursa hapakosi changamoto na kila mtu na mazuri yake na mapungufu yake.

Ruge Mutahaba anaweza kuwa ametajwa kwenye masakata mengi ya ubaya dhidi ya wasanii, akibebeshwa lawama kuliko mtu mwingine yeyote kwenye tasnia ya muziki Tanzania.

THT, Tanzania House of Talent, ni kituo kilichoanzishwa mwishoni mwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji, lakini wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe kwenye sekta ya sanaa hapa nchini.

Mwaka 2005, baada ya Rais Jakaya Kikwete kufurahishwa na ushiriki wa wasanii kwenye kampeni za uchaguzi mkuu, aliwaahidi THT kuwajengea studio kubwa ya kisasa ili iweze kuwasaidia vijana wengi zaidi.

Baada ya serikali kutimiza ahadi yake na studio kukabidhiwa kwa THT, aliyekuwa Mkurugenzi mwanzilishi Ruge Mutahaba alianza kulalamikiwa na wasanii wenzake kuwa amejimilikisha studio hiyo kwa manufaa yake na rafiki zake, na ameifanya studio hiyo kama mali ya kampuni ya CMG inayomiliki vituo vya Clouds FM na Clouds TV, na kuwa anawabagua, kuwanyonya na kuwadhulumu wasanii wengine.

Baadhi ya wasanii ambao hawakukubaliana na Ruge ni Lady JD, Joseph Mbilinyi SUGU, Dudu Baya, Q Chief, Joseph Haule na wengine, walianzisha umoja wa kupinga unyonyaji huo uliopewa jina la Anti Virus.

Sugu na Ruge waliingia kwenye ugomvi baada ya Sugu kumtuhumu Ruge kujimilikisha Project ya Malaria iliyofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia THT.

Lady JD aliwahi kumtuhumu Ruge na Kusaga kuwa ndio wanaonyonya jasho la wasanii, hadi kufikishana mahakamani kiasi kwamba waliapizana kutozikana, ugomvi uliopelekea Clouds kutopiga nyimbo za Lady JD na yeye kukimbilia EATV.

Q Chief naye alikwaruzana na Ruge kwa tuhuma za Ruge akishirikiana na BASATA kuzuia kibali cha mwimbaji wa Nigeria Davido.

Si hao tu, Ruge ameshawahi kukwaruzana na kundi zima la WCB linaloongozwa na Diamond Plutnamuz, ilifikia hatua wasanii walio chini ya WCB nyimbo zao kutopigwa na Clouds FM wala Clouds TV na hata kutoalikwa kwenye matamasha ya Fiesta yaliyokuwa yanaandaliwa na CMG. Leo WCB wameanzisha tamasha lao linalojulikana kama WASAFI Festival na TV yao ya Wasafi TV.

Karibu tujadili.

THT inaweza kuwa chanzo na sababu kubwa ya Ruge kutofautiana na Wasanii wengi - JamiiForums
 
Kweli Tanzania tunayo safari , kwahiyo ataisoma hiyo habari yako ?

Hii inachora Picha ya ombwe la kitu cha kusema. Mtu akiwa hana jambo la maana la kusema mbele ya watu, matokeo ni kama haya. Sijaona Substance zaidi ya sentensi moja kufuatiwa na sentensi nyingine tu!

Hivi watanzania na Waafrika tunapenda sana kuongea kuliko kutafakari? Tunapenda sana kuongea kuliko kutenda? Tunawashwa sana kuongea kiasi kwamba tunasahau kuchuja cha kuongea? Hivi ni lazima kila mtu aongee juu ya Msiba Wa Ruge?

Hii kuropokaropoka, inatufunua kama Taifa kwamba ni watu ambao Mara zote hatuna agenda! Tu kama majani katika miti tunadansi kulingana na upepo unavyovuma. Tungalikuwa na agenda tusingalikuwa kila mtu anaamka na kusemasema tu lolote ilimradi watu wasikie Fulani naye kaongea. Kwa hiyo,huyu Makamba alilenga kuujulisha umma wa watanzania kwamba alienda kumsalimia Ruge hospitalini Afrika Kusini?

Kama kweli tu watu tunaotumia AKILI badala ya HISIA, mbona sijasikia hata mmoja akitoka na wazo la kuunda hata RUGE TRUST FUND yenye mission ya kuhamasisha watanzania kuchukua tahadhari juu ya visababishi vya ugonjwa wa FIGO. Asasi ambayo itajikita kwa kusaidiana na asasi zingine za kitafiti Tanzania au duniani katika kutafuta ufumbuzi wa tiba ya kudumu ya ugonjwa wa Figo. Hakuna anafikiria juu ya hilo na sababu iko wazi: tunafikiria Mungu ndiye anatuletea magonjwa ili tufe. Mungu aliumba mema tu na Mabaya (EVIL) ni matokeo ya sisi kushindwa kuwajibika katika uelekeo chanya. Ni matokeo ya kutumia AKILI, UHURU na UTASHI kivingine.
 
Pengine wanaweza kumuenzi kwa namna hiyo, tusubiri tuone mkuu.
 
Kutegemeana na imani ya mtu...

Mimi imani yangu inasema kifo kikishawatenganisha watu,uwezekano wa watu hao kuonana na kuombana msamaha,n.k haupo isipokuwa siku wa Ufufuo tu pale Yesu Kristo atakapokuja (na hata hapo itakuwa nadra kujadili mambo ya ulimwenguni yaliyokwishapita,maana kila mtu atakuwa busy akifurahi au akihuzunika kadri anapotafakari "Umilele wake" - eternal life in heaven or eternal condemnation in hell).

Nafasi pekee ya kuombana misamaha,kupongezana,kushauriana,n.k NI LEO tukiwa hai.Na wengi huijutia sana hii fursa iitwayo LEO UKIWA HAI.Ndugu yako anakufa ndo unaanza kujuta kwanini hukumfanyia hivi au vile...

Nitoe nyongo:Nionavyo (japo Mimi si mmoja wa Holy beings in heaven),wanaCCM wengi moto utawahusu.Wengi wenu ni wanafiki,Serikali ya Chama chenu inawatendea mabaya Watanzania kuliko hata Shetani anavyoweza kutenda,na bado mnashangilia au kunyamazia uonevu huo.Endeleeni..

Tukutane mbele ya Kiti cha enzi cha Hukumu ya Mungu.Mwenyezi Mungu akitoa hukumu ya haki.
 
Hii inachora Picha ya ombwe la kitu cha kusema. Mtu akiwa hana jambo la maana la kusema mbele ya watu, matokeo ni kama haya. Sijaona Substance zaidi ya sentensi moja kufuatiwa na sentensi nyingine tu!

Hivi watanzania na Waafrika tunapenda sana kuongea kuliko kutafakari? Tunapenda sana kuongea kuliko kutenda? Tunawashwa sana kuongea kiasi kwamba tunasahau kuchuja cha kuongea? Hivi ni lazima kila mtu aongee juu ya Msiba Wa Ruge?

Hii kuropokaropoka, inatufunua kama Taifa kwamba ni watu ambao Mara zote hatuna agenda! Tu kama majani katika miti tunadansi kulingana na upepo unavyovuma. Tungalikuwa na agenda tusingalikuwa kila mtu anaamka na kusemasema tu lolote ilimradi watu wasikie Fulani naye kaongea. Kwa hiyo,huyu Makamba alilenga kuujulisha umma wa watanzania kwamba alienda kumsalimia Ruge hospitalini Afrika Kusini?

Kama kweli tu watu tunaotumia AKILI badala ya HISIA, mbona sijasikia hata mmoja akitoka na wazo la kuunda hata RUGE TRUST FUND yenye mission ya kuhamasisha watanzania kuchukua tahadhari juu ya visababishi vya ugonjwa wa FIGO. Asasi ambayo itajikita kwa kusaidiana na asasi zingine za kitafiti Tanzania au duniani katika kutafuta ufumbuzi wa tiba ya kudumu ya ugonjwa wa Figo. Hakuna anafikiria juu ya hilo na sababu iko wazi: tunafikiria Mungu ndiye anatuletea magonjwa ili tufe. Mungu aliumba mema tu na Mabaya (EVIL) ni matokeo ya sisi kushindwa kuwajibika katika uelekeo chanya. Ni matokeo ya kutumia AKILI, UHURU na UTASHI kivingine.
Watanzania {nafikiri na wewe ukiwa mmojawapo} kama kwenye andiko lako unavyotutanabsisha kama wasema hovyo pasi na ufikiri wa kina,

nina uhakika 100% siku hii ya 3 toka kutangazwa kifo cha Ruge hatharani mtu aje na wazo la "RUGE TRUST FUND" wewe hapo kuna uwezekano mkubwa wa kumuita mtu huyo katili, anatumia msiba kujitajirisha, ndio aliemuua marehemu, hata hatujampumzisha tayari taasisi za donations zimeanza, na kauli nyingi za kebehi na dharau japo nyingine zaweza kua na mashiko.

Anza wewe kutafakari kauli zako kabla ya kuzitoa na ujifunze kutoa boriti katika jicho lako kabla ya kuhoji kibanzi katika jicho la jirani yako.

"RUGE TRUST FUND"
 
Watanzania {nafikiri na wewe ukiwa mmojawapo} kama kwenye andiko lako unavyotutanabsisha kama wasema hovyo pasi na ufikiri wa kina,

Nakushukuru kwa kunitaka niikague nafsi yangu kwanza. Niliposema hayo sikumaanisha kwamba Mimi nimekamilika kifikra. Hata hivyo, hiyo haifinyi nafasi yangu ya kuonyesha kwamba watanzania tuna udhaifu Wa kutumia nafasi,wakati na mazingira.

Sio nadra kushangaa kwamba Wakati Wa kuzungumza kihuzuni sisi ndio tunaweka matumbuizo ya Ndombolo na Bongoflevo. Wakati wa kuandaa mashamba na kulima sisi tunakuwa na hoja za kuhifadhi mazao maghalani.

Tunao watu wengi sana maarufu wamefariki hapa Tanzania na wengine Kwa matatizo sawa na Yale yanayowasumbua watanzania wengine maelfu lakini baada ya salamu za rambirambi na mazishi ya watu hao, mambo yakakomea hapo! Kuzaliwa ama kufariki dunia Kwa mtu siku zote kunaambatana funzo. Je,leo tuna matokeo yoyote chanya ambayo tunaweza kusema asili yake ni mafunzo tokana na Msiba Wa mtu fulani maarufu, zaidi ya Miwani Nyeusi ambayo nina imani baadhi ya watu wanaotegemea kuhudhuria huo Msiba wameshakaza mawazo kwenda kuzinunua.
 
RIP Boss Ruge...lkn mh Makamba mbona hamkua upande wake kipindi Bashite anavamia clouds mlikaa kimya hata kumtetea hamna mkamwacha Nape peke yake uliogopa nn? Ukikutana nae uko umwombe msamaha
Nape alikuwa upande wake kilichomtokea ni kutenguliwa uwaziri. Makamba hakuwa tayari kuitwa mbunge, uwaziri mtamu jamani
 
January pamoja na elimu yake anamwandikia mtu aliyekufa ??

Kweli Tanzania tunayo safari , kwahiyo ataisoma hiyo habari yako ??

Kama kiongozi ana uelewa wa hivi , je mkulima wa nyamongo ??
Kuna waziri mwingine pia ameweka picha halafu kaandika
Hii picha Ruge tulipiga mwaka 2018 sasa sijui wanawasilianaje na wafu hawa watu au ndio shirki zenyewe hizi
Ngoja #mshana jn aje huku

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
January pamoja na elimu yake anamwandikia mtu aliyekufa ??

Kweli Tanzania tunayo safari , kwahiyo ataisoma hiyo habari yako ??

Kama kiongozi ana uelewa wa hivi , je mkulima wa nyamongo ??

Hapana..inasaidia sana kupunguza machungu..mir niliwah pitia uchungu sana dk akanishauri niandike barua kwa marehem..!yupo sawa
 
January, dead people tell no tales and hear no tales. Umeandika vitu vizuri sana lakini ni majuto yako ya kushindwa kumfanyia alipokuwa hai au kutuonyesha sisi sasa na hapa kwama alikuwa rafiki yako. Ushauri: stay close to Ruges family in these difficult times and give them something nice to say about you now and always.
 
Back
Top Bottom