Waraka Wa Jaji Warioba kwa Wassira

Waraka Wa Jaji Warioba kwa Wassira

frema120

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Posts
5,098
Reaction score
1,341
Jana nilipata kusikia kuwa jaji warioba kaandika waraka mzito kwa mh. wassira juu ya anachokifanya sasa kupotosha rasmi ya katiba na mambo mengi juu ya ubaya wa wasira na misimamo yake sasa.

Na kikubwa kuelezea alivyomfanya kukimbia/kufukuzwa CCM na kuelekea NCCR. pls mwenye nao hatuweke hapa tusome.


Dar. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ameandika waraka kumjibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira kwa kauli yake kuwa ndiye aliyemkimbiza CCM kwenda upinzani mwaka 1995.

Katika waraka wa maandishi alioutuma kwa gazeti hili, Jaji Warioba alisema maelezo ya Wasira dhidi yake katika mahojiano maalumu na gazeti hili hayakuwa sahihi na hivyo akamtaka ajifunze kusema ukweli kwa kuwa mambo anayosema yanaweza kumrudia baadaye.

Waraka wenyewe

Tarehe 22 Septemba 2014, Gazeti la Mwananchi lilitoa taarifa ya mahojiano kati yake na Mheshimiwa Steven Wasira. Katika mahojiano hayo, Mheshimiwa Wasira alisema mimi ndiye niliyemkimbiza CCM.

Tangu mchakato wa Katiba Mpya kuanza nilikuwa napata taarifa kwamba Mheshimiwa Wasira alikuwa amenifanya mtaji wake katika kutetea msimamo wake. Wakati mmoja kuna kiongozi mwenzake aliniuliza kama nina ugomvi binafsi na Mheshimiwa Wasira kwa sababu kila akipata nafasi kwenye vikao vyao ananishambulia. Wakati wa mabaraza ya Katiba nilipata taarifa za aina hiyo. Nilichofanya ni kuwaarifu viongozi wake wa CCM.

Mengi aliyosema Mheshimiwa Wasira siyo ya kweli. Napenda nitoe ufafanuzi kwa machache yafuatayo:-

Niligombea mara mbili na Mheshimiwa Wasira. Baada ya Uchaguzi wa 1990 ambao nilishinda kwa kura nyingi sana, uchaguzi huo ilitenguliwa kwa sababu nilifanya kampeni kwa kutumia gari la Waziri Mkuu.

Uchaguzi ulirudiwa mwaka 1992. Niliunda timu ya kampeni, Mheshimiwa Wasira akiwa kiongozi. Aliniomba atangulie jimboni kuandaa mazingira. Alipofika huko akaanza kampeni dhidi yangu na kutangaza kwamba anagombea. Wakati huo kura za maoni zilikuwa zinapigwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya. Wajumbe walikuwa kama 600. Nilipata kura 400 na Mheshimiwa Wasira alipata kura chache akiwa mtu wa tatu au nne. Baada ya matokeo akatangaza anajitoa kwenye mchakato na jina lake lisipelekwe NEC. Alikataliwa kwa sababu kufuatana na kanuni, muda wa mtu kujitoa ulikuwa umepita.

Mwaka 1995, kura za maoni zilikuwa zinapigwa kwenye kata. Tulianza na Kata ya Sarama ambayo iko upande wa mashariki, siku ya tatu tulifika Nyamuswa ambacho ndicho kijiji ninachotoka. Nyamuswa ilikuwa kituo cha tano kati ya vituo 12.

Baada ya hapo tulielekea magharibi ya jimbo anakotoka Mheshimiwa Wasira. Baada ya kura kupigwa katika Kata ya Guta, Mheshimiwa Wasira alijitoa kwa sababu aliona hawezi kunishinda hata kama angepata kura zote za kata mbili zilizobaki. Siyo kweli kwamba Nyamuswa ilikuwa ya mwisho kupiga kura na siyo kweli wananchi wa kata nzima walipiga kura. Kumbukumbu zote zinaweza kupatikana wilayani na makao makuu ya CCM.

Mheshimiwa Wasira anasema kwamba nilikuwa Jaji na kesi iliyopelekwa mahakamani ni kama kesi ya tumbili kupelekwa kwa nyani, kwa maana kwamba majaji walinipendelea. Kumbukumbu za kesi hiyo zipo. Wakati huo sikuwa jaji. Isitoshe huko nyuma uchaguzi nilioshinda 1992 ulitenguliwa. Kwa nini wakati huo sikupendelewa? Kumbukumbu za kesi zinaeleza kwa nini Mheshimiwa Wasira alifungiwa kugombea kwa kipindi.

Mheshimiwa Wasira ni kiongozi wa Taifa kwa kipindi kirefu. Ni mbunge wangu na namtambua hivyo. Tunaweza kuwa na mtazamo tofauti katika baadhi ya mambo lakini hiyo si sababu ya kusema mambo yasiyo ya kweli kwa nia ya kujijenga kisiasa.

Yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM. Yeye ni Waziri mwandamizi. Yeye anafikiria kugombea urais. Ni vizuri basi akajifunza kusema kweli (ambayo ni ahadi mojawapo ya WanaCCM). Akumbuke anayosema yanaweza kumrudia mbele ya safari.

J.S. Warioba

Chanzo: Mwananchi
 
huo waraka akiandika Warioba nitaona uzee umemfika kiwango cha juu sasa na ni utoto.
 
Nilikuwa najiuliza kwanini Makamba na Wassira ni watu wa karibu? Sasa nimepata jibu, hawa wote wako tayari kukupakazia lolote ailimuradi ana survive ktk siasa maslahi....JK akamtosa Makqmba kwa shinikizo la wenye CCM ila huyu amemganda kama ruba.....lakini ni suala la wasaa tu naye ataondoka naye ktk siasa za nchi hii, nashangaa Bulaya leo kuitwa msagaji eti kwa sababu anatishia ustawi wa Wasssira pale Bunda! Makamba , Wasira, Makinda waliwatumia Kombani na Mkulo huku Aziz Aboud aki finance operesheni tokomeza Ngasongwa 2007...2008...2010. Nikikumbuka hawa watu walivyomfanyia visa Alhaj Ngasongwa siamini mpaka leo kama kweli hii ndio Tanzania! Dhambi kubwa ni influence yake ktk kumminya Aboud Morogoro 2000 na 2005 pale alipowabeba wazawa Mazola na Dkt Mzeru.....ktk ubunge, Polyster na vitu kama hivyo. Wasira alimuhofia sana Ngasongwa huku akimuita anajifanya Msomi sana huyu jamaa. Wassira ni janga ambalo limeachwa litamalaki kwa miaka 10 ya JK. Kuna mtu alihoji kwanini Jakaya anayumbishwa na watu wawili wa Mara? kila mmoja ana mapungufu yake but Wassira is the worst thing happened to Jakaya na hana pa kujitenga naye.
 
Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Sinde Warioba ameandika waraka kumjibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira kwa akauli yake kuwa ndiye aliyemkimbiza CCM kwenda upinzani mwaka 1995. Jaji Warioba amemtaka Wasira ajifunze kusema ukweli kwakuwa mambo anayoyasema yanaweza kumrudia baadaye.

Kimsingi,waraka wa Jaji Warioba unamuasa Wasira kuacha kutumia Jaji Warioba kama mtaji wake katika kutetea msimamo wake juu ya Rasimu ya Katiba mpya."Yeye anafikiria kugombea urais.Ni vizuri basi akajifunza kusema ukweli (ambayo ni ahadi mojawapo ya wanaCCM)"inasema sehemu ya waraka huo.

Chanzo: Mwananchi
 
Weka waraka hapa. Habari isiyo na nyama inakuwa ni mifupa.
 
Siku zote Msemakweli ni ADUI wa ccm!Warioba kawa adui no 1 wa ccm
 
Asante mkuu, umebarikiwa ktk kutukana watu, mchunguze vizuri huyo unayemuabudu utajua kama una haki ya kutukana watu eti ------,! Lipi jema kukueleza ukweli au kumpakazia Bint wa watu eti Msagaji! Kisa nini hasaa? Ubunge au ? Tz haitaji rais anayewatusi wananchi wake kisa anampinga tena kwa hoja safi na za kujipima. Tunakumbuka alichosema Mwalimu 1995 Bunda, kuwa kati ya hawa wawili Joseph Warioba ni bora sana lakini kwa ulevi wa gongo mkalishwa rushwa mkamdondosha Joseph.

Mwambieni asipoteze muda hafai kwa mboga wala kiungo chochote. CCM ina hazina kubwa huyu hakuwahi kuwa mmoja wao na hatakuwapo....,

Sasa kama wewe shabiiki uko hivyo tutarajie nini mkipewa tena fursa? Kuwa mstaarabu

Umeendika nn sasa Mkuu mbona watu mnaendeshwa na chuki??? Kwanza mi ni CDM ila sitaki siasa zenu za majitaka
 
Jamani waraka upo na Mwananchi wamejikongoja kuuweka hadharani.....huu ndio msimu wa kuufahamu ukweli. Nyerere ndie aliyemkimbiza Wasira na si Warioba kama kumbukumbu zetu ziko sawa....1995, ni sawa na Slaa alivyokimbizwa na Mwinyi 1995 pale alipomtaka Qorro ....fact hizi si za kubezwa, Slaa alipinga NEC akagomewa ikabidi atumie haki yake nje ya CCM na akasimamia haki hiyo. Wassira hakufanya hivyo na kibaya zaidi alitumia rushwa ktk kupata ushindi wake....akabainika mahakamani pia. Sasa kuendelea kutudanganya eti alionewa ilihali alikosea mwenyewe, asiyesikia la mkuu huvunjika mguu, kama wengi hamuamini huu waraka utamuumiza Wassira mbele ya safari. Akubali tu amepewa second chance kimagumashi imetosha....kung'ang'ania tena 2015 ni kusaka unhealthy downfall. Ukiiba bila kuonwa...bila kuhisiwa...basi shukuru kuwa umekula na vipofu imetosha. Funika kombe.....
siyo kutukana watu
 
Warioba hana ukweli wowote ni MTU anaependa popularity

Ni umaarufu upi autake zaidi alionao? Tunaweka wazi matendo mabaya ya watu wanaotaka tuamini ni wapenda amani na Tanzania ilihali ni watu wafitini, wasio wakweli na ni hatari sana kwa nchi yetu....Huyu ndie mshauri wa Rais tutegemee nini ? JK amefanya uislamu wake kwa kuwanusuru watu kama hawa ili wazeeke kwa heshima japo kidogo lakini wanamuangusha...hilo si tatizo lake kama ni deni la fadhira 1995 campaign amezilipa huyu Mkuu hana deni, deni liko kwao kina Wassira kuonyesha uaminifu kiutendaji uliotukuka kwa umma na siyo fitina na ulafi wa madaaraka na mali anaouonyesha! Kwanini tusimkemee yeye na ninyi wachumia tumbo wake? Muogopeni Mungu kwa kutenda haki na kuwa wakweli.
 
Ni kweli watu wanajifanya wapambe na kutukana watu hapa mtandaoni! siyo wote tuko imara ktk lugha kengeufu kama hizo.
 
Huyu Mzee Warioba anazeeka vibaya anapenda kutumia MIC kama mswaki wa kusukutua meno, mtu akipiga chafya tu akataja jina lake tayari ameisha wakusanya Wandishi wa Habari.

Arudi Nyamuswa akapumzike, awaombe radhi waikizu kwani amekuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa muda mrefu lakini hata kisima hakuchimba.
 
huo waraka akiandika Warioba nitaona uzee umemfika kiwango cha juu sasa na ni utoto.

kwa akili yako ya lumumba unaweza kujilinganisha ki elimu au ufahamu zaidi ya jaji warioba?
 
Wasira hajatueleza kuhusu ile BILIONI 1 aliyompatia mwanae.AJIBU KWANZA ILO.

wasira hafai mahakama kuu iliyoketi musoma ilimkuta na hatia ya kutoa rushwa. Hafaiiiii

Anayekutumia amekuharibu ubongo wako, sasa unawaza kama yeye, pole.
Kamwambie Wassira hana kashfa hata moja, hayo yote mnajitahidi kutunga kumchafua Rais wa Watanzania mtarajiwa.
 
Huyu Mzee Warioba anazeeka vibaya anapenda kutumia MIC kama mswaki wa kusukutua meno, mtu akipiga chafya tu akataja jina lake tayari ameisha wakusanya Wandishi wa Habari.

Arudi Nyamuswa akapumzike, awaombe radhi waikizu kwani amekuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa muda mrefu lakini hata kisima hakuchimba.

Huyu wasira ametufanyia nini hapa bunda?maji tunaenda zaidi ya km 3,wacha kucheza ngoma husiyo ijua sisi ndio tunaojua ubaya wa hao watu wawili.
 
Back
Top Bottom