Amina, Mungu ni mwema.Pole sana Mungu akufute machozi yako. Mama zake wamejua kutulinda sana na wengi wanefichia siri waume zao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Amina, Mungu ni mwema.Pole sana Mungu akufute machozi yako. Mama zake wamejua kutulinda sana na wengi wanefichia siri waume zao.
Kiukweli Mungu ni muaminifu sana. Yote tunashukuruPole sana Wiser, Mungu amemgifafhi mahali salama na siki ys meisho tutaonana naye huko mbinguni kwa Baba.
Wanaume wengi hata humu utawasikia wakijimwambafy kuishi maisha mazuri kila pombe njema, kuhonga wanswake huku kwenye familia zao hata kilo ya nyama hakuna.
Hii simulizi imenikumbusha mambo mengi.
Mama yangu alifariki kwa cancer ya ziwa ambayo ilipelekea cancer kusambaa mpaka kwenye ini. Niseme nini Mimi?
Baba yangu hakuwa mtu wa kujali hata kidogo, japokuwa taarifa nyingi mama alikuwa anamwambia baba, baba anamjibu jeuri na kuona ana jifanyisha kuumwa. Mama yangu aliumwa sanaa mnooo, nikiwa kidato cha nne mpaka uvumi ukatokea shuleni mama yangu amefariki.
Ila ilikuwa uongo! Niliongea na mama yangu siku mbili mbele na kujua ni mzima.
Nilivyomaliza sikufanya vzuri sana darasani kwasababu muda mwingi niliutumia kulia na kusali bila mafanikio.
Nikiwa nyumbani baada ya kumaliza form four niliona dharau na majibu ya baba wazi wazi bila chenga, mama alikuwa na miradi mingi sana ya kuingiza pesa nasema ni ya mama kwasababu baba alikuwa hafanyi kazi wakati huo na alikuwa akichukua mayai na kuuza huku hela akizinywea pombe na wanawake.
Mama alichoka sana, miradi yote ikayumba na kuisha akiwa amebakiwa na ng'ombe wa maziwa wawili tu pamoja na kazi yake akipata mshahara kiduchu kwasababu ya kuchukua mkopo wa kumalizia nyumba ambayo hakuwahi kuishi.
Niseme nini Mimi? Maisha ya mama yangu yamenifundisha mambo mengi sana mno! Yamenifundisha mengi sana! Mnooo.
Mama aliumwa sana nikiwa kidato cha tano na kabla hajafariki nilifanikiwa kumuona ,mama alikuwa amechoka sana zaidi ya kawaida.. Mama alikuwa amelala kitandani utasema hakuna mtu! Mama alikuwa anaumwa mno.
Nilirudi shule baada ya siku mbili mama yangu alifariki.
Mungu mpumzishe pema.
Ni mengi ila baba alichangia sana kwa kiasi kikubwa mpaka mama anafariki hajawahi oa ni miaka zaidi ya 13. Nalia Mimi nalia sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaume wasio na vipato walevi hutesa Sana wanawake bila huruma na vile jamii imejijengea eti kuvumilia ndoa wengi wanakufaa siku si zao
Sent using Jamii Forums mobile app