Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.
Pole sana msomi Lissu kwa kuumwa. Lakini sasa kwa taarifa za jana ni kuwa unapata nafuu na Mungu Mwenyezi awe nawe urejee.
Hata hivyo huku ulipotuacha ni umeshindwa vibaya. Wale uliosema watatushitaki na kuwalipa mabilioni sasa wao ndio wanatulipa sisi mabilioni.
Kile ulichosema kuwa ni makosa yetu ya mikataba na ulofa, wamekubali kuwa ni makosa yao na wako tayari kwa marekebisho ya "terms" vipengele vipya kwenye mikataba.
Hata zile kesi ndogondogo tulizokuwa nao katika mahakama "tribunal" mbalimbali sasa nazo wamekubali iundwe kamati ya kuzimaliza kwa mazungumzo.
Lakini kubwa kuliko yote msomi Lissu ni kuwa wamekubali mgao wa 50/50 wa faida na Tz kuwa na wawakilishi kwenye bodi ya wakurugenzi na mengine mengi yenye kutia moyo. Sijui, lakin nadhan habari hizi sio njema sana kwako.
Msomi Lissu, siku nyingine ukiambiwa wako watu wana akili kuliko wewe uwe mwepesi tu kuelewa. Ukiambiwa wako watu wanaona maili 50 zaidi yako uelewe haraka.
Hatukatai, unaweza kuwa mzungumzaji mzuri lakin sio mwenye upeo. Upeo hupimwa kwa matokeo ya matendo. Na kwa matokeo haya twaweza tu kupima nani mwenye upeo kati ya wale uliowaita wa hovyo na wewe. Pia twaweza kujua wa hovyo ni nani sasa.
Nilikushangaa sana uliposema huoni kosa la Acacia. Watu wamedanganya uzito wa madini, wamedanganya sampuli walizobeba na ushahidi upo, msomi unasema huoni kosa !!!? , Looh.
Unajua vyema kuwa hawa jamaa wangekuwa upande salama kama ulivyopiga chapuo wasingefikia makubaliano kama haya. Wangeenda kwenye tribunal za kimataifa kama ulivyowasaidia kupendekeza na wangeshinda na tungelipa mabilioni kama ulivyokuwa umetabiri.
Ulikera sana hapa :
Makontena yakazuiwa, ukasema kimkataba ni yao na yamezuiwa kimakosa.
Ripoti ya kwanza ikasomwa,ukasema ripoti hiyo ni takataka"rubbish".
Ripoti ya pili ikasomwa, ukasema hamna jipya.
Akaja bosi wa Acacia Prof. John.L.Thompton akasema watalipa, ukasema hajasema kama watatulipa na hawawezi kutulipa.
Ulidhihirisha uadui na nia ovu na ndio maana ni halali leo kusema JAPO UNAUMWA LAKINI UMESHINDWA. Haikujulikana ulitaka nini hasa.
Msomi, hawa watu hawakuwa wasafi na hili kila Mtanzania aliliona isipokuwa wewe. Kwa matokeo haya sasa twaweza kujua nani ana maamuzi ya KUKURUPUKA na kuzungumza hovyo.
Tunakutakia afya njema lakini upunguze kidogo kuropoka msomi. Watu wako makini kuliko unavyofikiria.