Waraka: Serikali yatangaza kima cha chini mishahara ya kisekta

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
Serikali imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyumbani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.

Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha.

Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000.

“Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo.

Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi.

Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000.

Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini kitaanzia Sh150,000.

Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni Sh130,000.

Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa na kampuni ndogo za huduma za nishati. Kampuni ndogo za ulinzi zitatakiwa kulipa Sh100,000.

Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini, uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000.

Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000.

TGTS A.1 (223,000 HADI 296,000),
TGTS A.2 ( 225,400 HADI 296,000)
TGTS B.1 (277,000 HADI 344,000)
TGTS C.1 (370,000 HADI 432,500)
TGTS D.1 (532,000 HADI 589,000)
TGTS E.1 (720,000 HADI 769,00O)
TGTS F.1 (980,000 HADI 1,003,000)
TGTS G.1 (1,232,000 HADI 1,232,500)
TGTS H.1 ( 1,618,000 HADI 1,734,000)
TGTS I.1 (2,254,000 HADI 2,415,000)

Kwa wengine, mnaweza kupata mshahara wako kwa kuangalia asilimia zilizoongezeka katika mishahara hiyo. Pia mishahara huwa na Incremental ya kila mwaka kulingana na madaraja.

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyumbani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.

Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha.

Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000.

“Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo.

Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi.

Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000.

Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini kitaanzia Sh150,000.

Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni Sh130,000.

Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa na kampuni ndogo za huduma za nishati. Kampuni ndogo za ulinzi zitatakiwa kulipa Sh100,000.

Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini, uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000.

Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000.

Wafanyakazi katika kampuni za uuzaji wa magari watatakiwa kulipwa Sh300,000 na madalali wa bima watalipwa Sh200,000. Kampuni za wachimbaji wadogo wa madini zitalazimika kulipa mshahara usiopungua Sh200,000 kwa wafanyakazi wake.

Mishahara ya chini kwa wafanyakazi wa shule za awali, msingi na sekondari za binafsi ni Sh140,000 huku wafanyakazi wa viwandani wakipaswa kulipwa Sh100,000.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Kazi imesema sekta ambazo hazijaorodheshwa, wafanyakazi wake watatakiwa kulipwa kuanzia Sh100,000.

CHANZO: MWANANCHI
 
Leo asubuhi nimeanza kupata machungu ya kukatwa kodi ya line ya cm, nilikuwa na shida sana ya kuwasiliana ili kutatua matatizo yanayonikabili na ndugu zangu pia. Nimeweka Tsh. 1000 ghafla nilipopiga nikaambiwa sina salio nimeshangazwa sana na kitendo hiki na kuumizwa sana maana nilikuwa na hiyo hiyo 1000, baada ya kukumbuka kumbe CCM walishachukua chao.

Ndugu zangu nimeamua kurusha uzi huu kwa kutafakari mengi sana, kwani nimejaribu kutafakari LUNDO la kodi ninazokatwa na impact ya moja kwa moja ama isiyo moja kwa moja katika maisha yangu binafsi na familia yangu kwa mapana yake. Ndugu zangu miongoni mwa kodi ninazokatwa bila kuona mafanikio yake ni:-

  1. PAYE
  2. VAT KATIKA MANUNUZI YOTE MADUKANI
  3. LINE YA SIMU
  4. VOCHA
  5. HANDSET
  6. MPESA NA AIRTEL MONEY
  7. KODI YA ARDHI
  8. KODI YA MAKAZI
  9. KODI YA VIWANJA
  10. KODI YA VIBANDA VYANGU VYA BIASHARA
  11. KODI YA MAZAO
  12. KODI YA GARI, MOTOR VEHICLE
  13. kODI YA FIRE
  14. NK, NK, NK, NK

Ndugu zangu wakati huo nina mlundikano mkubwa wa kodi hizi bado ninalipa umeme kwa serikali hiyo hiyo inayonikamua kila siku kodi, bado ninalipia maji, nyumba, ada na vingenevyo vingi sana na sioni mazingira yoyote yale yanayorahisisha maisha yangu.

Ndugu zangu ndiyo maana kwa uchungu mkubwa sana ninaoendelea kuupata chini ya serikali hii inayoongozwa na ccmn nimejikuta nashangaa sana kuona eti bado kuna Watanzania masikini kama mimi bado wanajiita ni wana ccm ndani ya mateso haya makubwa tunayoyapata.

Ndugu zangu ninapoandika thread hii ninaona uchungu unanizidi ngoja niishie hapa na niwatakie kila la kheri Wana ccm waendelee ku enjoy MAISHA chini ya serikali yao.

Naomba kuwasilisha machungu yangu na ku declare kwamba ninaichukia sana ccm na sitakaa nishawishike na yeyote yule aliyeko ccm wala mfumo wake.
 
Nani anaweza kuishi Dar kwa kima cha chini huku alipe pango,maji,umeme na basic needs zake bila wizi na maharamia wengine??!! Ngumu kutokomeza rushwa!!
 
Mkuu pole sana hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania, ni maumivu kila upande hata hatujia tukimbilie wapi kodi karibia mia alafu maendeleo duni hakuna dawa hopsitalini, maji ya shida mpaka tununue yani elimu ndo hoi watoto wanakaa chini hakuna usawa kabisa chini ya hii serikali ya ccm
 
.....
Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000......

CHANZO: MWANANCHI
yay!! mshahara wangu utaongezeka, ntaacha kushinda milo 2 per day
 
Yaani mkandarasi analipwa laki tatu na kitu baada ya kusoma miaka minne?
 
Hata mim nashangaa...niko chuo na kwa huu msoto huwez nishaur nifanye kaz kwa laki3 hata cku moja...huwez jua wenda ni wa diploma!!!
 
Leo asubuhi nimeanza kupata machungu ya kukatwa kodi ya line ya cm, nilikuwa na shida sana ya kuwasiliana ili kutatua matatizo yanayonikabili na ndugu zangu pia. Nimeweka Tsh. 1000 ghafla nilipopiga nikaambiwa sina salio nimeshangazwa sana na kitendo hiki na kuumizwa sana maana nilikuwa na hiyo hiyo 1000, baada ya kukumbuka kumbe CCM walishachukua chao.

Ndugu zangu nimeamua kurusha uzi huu kwa kutafakari mengi sana, kwani nimejaribu kutafakari LUNDO la kodi ninazokatwa na impact ya moja kwa moja ama isiyo moja kwa moja katika maisha yangu binafsi na familia yangu kwa mapana yake. Ndugu zangu miongoni mwa kodi ninazokatwa bila kuona mafanikio yake ni:-

  1. PAYE
  2. VAT KATIKA MANUNUZI YOTE MADUKANI
  3. LINE YA SIMU
  4. VOCHA
  5. HANDSET
  6. MPESA NA AIRTEL MONEY
  7. KODI YA ARDHI
  8. KODI YA MAKAZI
  9. KODI YA VIWANJA
  10. KODI YA VIBANDA VYANGU VYA BIASHARA
  11. KODI YA MAZAO
  12. KODI YA GARI, MOTOR VEHICLE
  13. kODI YA FIRE
  14. NK, NK, NK, NK

Ndugu zangu wakati huo nina mlundikano mkubwa wa kodi hizi bado ninalipa umeme kwa serikali hiyo hiyo inayonikamua kila siku kodi, bado ninalipia maji, nyumba, ada na vingenevyo vingi sana na sioni mazingira yoyote yale yanayorahisisha maisha yangu.

Ndugu zangu ndiyo maana kwa uchungu mkubwa sana ninaoendelea kuupata chini ya serikali hii inayoongozwa na ccmn nimejikuta nashangaa sana kuona eti bado kuna Watanzania masikini kama mimi bado wanajiita ni wana ccm ndani ya mateso haya makubwa tunayoyapata.

Ndugu zangu ninapoandika thread hii ninaona uchungu unanizidi ngoja niishie hapa na niwatakie kila la kheri Wana ccm waendelee ku enjoy MAISHA chini ya serikali yao.

Naomba kuwasilisha machungu yangu na ku declare kwamba ninaichukia sana ccm na sitakaa nishawishike na yeyote yule aliyeko ccm wala mfumo wake.

mkuu pole sn kwa machungu hayo uliyonayo!!je unadhan chama kingine kisichokua ccm kikichukua dola hizo kodi ulizozitaja hatutolipa????
 
Hata mim nashangaa...niko chuo na kwa huu msoto huwez nishaur nifanye kaz kwa laki3 hata cku moja...huwez jua wenda ni wa diploma!!!

jaman hamjaelewa hapa,mkandarasi ni mtu mwenye kampuni ya ujenzi na wala sio injinia au mwandisi mwenye degree ya miaka minne ya engineering!!

Hivyo,mtu yeyeto mwenye kampuni ya ujenzi(mkandarasi) anatakiwa awalipe wafanya kazi wake kima cha chini sh 325,000 yaan wale walinzi,wafagiaji,office attendants ,ps na wengineo wanaostahili kupokea kima cha chini ndio watapata kiasi hiki cha pesa ndani ya kampuni za ukandarasi!!

Nawasilisha!!
 
Yaani mkandarasi analipwa laki tatu na kitu baada ya kusoma miaka minne?

Hata mim nashangaa...niko chuo na kwa huu msoto huwez nishaur nifanye kaz kwa laki3 hata cku moja...huwez jua wenda ni wa diploma!!!

hapana ww hujaelewa hapa,mkandarasi ni mtu mwenye kampuni ya ujenzi na wala sio injinia au mwandisi mwenye degree ya miaka minne ya engineering!!

Hivyo,mtu yeyeto mwenye kampuni ya ujenzi(mkandarasi) anatakiwa awalipe wafanya kazi wake kima cha chini sh 325,000 yaan wale walinzi,wafagiaji,office attendants ,ps na wengineo wanaostahili kupokea kima cha chini ndio watapata kiasi hiki cha pesa ndani ya kampuni za ukandarasi!!

Nawasilisha!!
 
Goooooooood morning Teeeaacherrrrrrrrrrrrrrraaaah ha ha ha haaaaaaaaa teh
Yani leo nimecheka mpaka nikavunja meza yangu kwa teke sebuleni......
 
mkuu pole sn kwa machungu hayo uliyonayo!!je unadhan chama kingine kisichokua ccm kikichukua dola hizo kodi ulizozitaja hatutolipa????
Naamini haya majibu yako yanatokana na hayo malipo yenu kutoka lumumba kugharimia kujibu maswali ya jamii forum kutokatwa kodi.issue siyo kukatwa kodi,kinachoongelewa ni kulipa kodi nyingi ambazo hatuoni zinakoenda.Tumekuwa tukiambiwa kuwa kodi zinagharimia miradi ya maendeleo,hapo hapo kwenye bajeti ya serikali tameambiwa deni la taifa limeongezeka.Kwa mtu yeyote asiyelipa kodi hawezi kuelewa wanachosema walipa kodi,especially waajiliwa ambao pamoja na kulipa kodi lundo bado hawana TIN number,kodi zao zinahesabika zimetolewa na mwajili wao.Mshirazy ni vema kunyamaza utaonekana una hekima.
 
Makubwa haya nani atasimamia watu wapate haki zao?
Mashaka kidogo.
 
Back
Top Bottom