Waraka kwako

Speaker

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
6,324
Reaction score
2,244
Ndugu yangu, kila kukicha kwenye mbuga za wanyama za Serengeti,
Nyumbu anapoamka tu anafahamu kwamba ni lazima aweze kukimbia zaidi
ya Simba mwenye mbio kuliko wote la sivyo atakamatwa na kufanywa
kitoweo.

Vilevile, kila kukicha humo humo Serengeti,
Simba anapoamka tu anafahamu kwamba ni lazima aweze kukimbia zaidi
ya Nyumbu mwenye mbio hafifu kuliko wote la sivyo atakosa msosi na
atakufa kwa njaa.

Kwahiyo, haijalishi kama wewe ni Simba au ni Nyumbu, kukicha tu
lazima uanze kukimbia!

Kumbuka kwamba;
kila kitu kinawezekana ukiweza kuamini kwa kumtegemea MUNGU.

Uwe na week njema,anza kukimbilia ndoto zako na hakikisha ume zikamata.

 
Nice one!
'
Nimeipenda hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…