Waraka kwa Yahya wa StarTV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka kwa Yahya wa StarTV

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uswe, Apr 7, 2012.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hello Yahya, leo nilichangia kidogo katika kipindi chako ulichokua unatizama namna vyombo vya habari vilireport uchaguzi wa arumeru.

  sina shida sana na namna vyombo vya habari vinareport campaigns, ingawa kuna namna nyingi mnaweza kuboresha, mfano kuwa mnatuonesha kwa kulinganisha sifa za hao wagombea, kama walishawahi kuwa viongozi huko nyuma basi vitu walivovisimamia, kama walikua wabunge hoja gani walizisukuma, kama walikua ni watu wa kudai nyongeza zo posho tu basi msifiche tuwekeeni hivi vitu hadharani.

  Mchango wangu mkubwa ni namna mnacover ile siku ya uchaguzi, kama nilivochangia asubuhi, itakua nzuri kama mtakua na system ambayo kadiri mnavyopokea matokeo kutoka katika vituo basi yenyewe itakua inatupa jumla ya kura kwa kila mgombea na inatuambia ni vituo vingapi tayari mmepata matokeo yake na vituo vingapi bado, hii kitu mnakuwa mnaiweka katika screen inaupdate na inaonekana kadiri matokeo yanavyopokelewa (i hapo unaelewa najojaribu kusema, tizama namna tv za kenya zilifanya wakati wa kura ya katiba au cnn na msnbc ambavyo huwa wanafanya, hii itasaidia vitu viwili vifuatavyo

  1. wadau wenu tutapata muelekeo wa matokeo mapema kabisa, hivo kuinyima tume 'haki' ya kutuchakachua

  2. itapunguza mivutano na vurugu kwa sababu kila kitu kiko wazi, kama ni kuchakachua basi itakua maeneo mengine lakini sio katika ujumlishaji.
   
 2. rweyy

  rweyy Senior Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  ni kweli ila inatakiwa tbc waanze na hilo je inawezekana?
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kwa nini unafikiri tbc ndio wanapashwa kuanza?
   
 4. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Tumbuiza Baraza la Ccm kwanza(1)
   
 5. Makete Kwetu

  Makete Kwetu JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  makuunga sana mkono kwa ushauri huo star tv....sidhani kama ni technologia ngumu sana kiasi kituo makin kama star tv iwasinde koz mmesha fanya mambo makubwa zaii ya hili dogo....
   
 6. U

  Uswe JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  na pia starTV ndio walioonyesha uthubutu katika kureport campaign na badae uchaguzi kwa uhuru, kama wakiboresha kidogo tu maeneo hayo tunayowashauri, believe you me, jamaa watakua wamepiga bao sana lakini pia historia itwarikodi kama watu waliochangia kukuza democrasia na pia kuleta maendeleo kwa nchi.
   
 7. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  TBC nayo ni chombo cha habari? Startv wanafanya vyema!
   
 8. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hapa labda tusubiri t.v ya jf ndio itaweza haya unayoshauri.
   
 9. k

  kamanda wa anga Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  star tv atleast mmepunguza uccm japo nina wasiwasi na watu mnaowaalika wengi hawajui kujenga hoja.
   
 10. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...haya ni mawazo mazuri sana na kama Star mtayafanyia kazi...jambo moja ambalo na mimi ngependa niongeze ni kuwashauri kwamba..."jitahidini kuwa wepesi"...haipendezi tukio linatokea hapa hapa Mwanza mchana taharifa mnatuletea kesho yake kwenye taharifa ya habari ya saa mbili usiku,ebu kuweni wa kwanza kutupa habari...tofauti na haya mapungufu machache mnajitahidi sana na kazi yenu imeboreka na inapendeza hongereni sana...
   
 11. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Star TV mkiaacha uccm daima mtafika mbali sana na hii itawabeba hata nyinyi watangazaji kimasilahi. Nawapongeza kwa kupunguza uccm na kusema ukweli mim huwa siangalii tbccm only I use to luku star
   
 12. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Yeah! Hawapo makini katika kuchagua sample zao. Alafu yule PAULO MABUGA anausisiem sana, simpendi. Kitu kingine anachoboa ni kuingilia mazunguzo ya mtu kabla hata hajamalisha kuzunguzia hoja yake!
   
 13. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu Uswe pamoja na wadau wengine,

  Kwanza kabisa kwa niaba ya menejimenti ya Star TV nichukuefursa hii kuwashukuru sana kwa kuelekeza fikarazenu kama sehemu ya kuwezesha utoaji wetu wahuduma kulenga hitajio halisi la mlaji katika soko la Media.

  Mawazo haya ni ya thamani na mimi kama sehemu ya watumishiwa Star TV katika mstari wa utendaji nayachukulia kamanyongeza kubwa katika mipango yetu na matazamio tuliyojiwekea.

  Uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki ulikuwa jaribio zuri laelimu katika matumizi ya teknolojia mpya tunayoendelea kujifunza katikakuwasilisha taarifa kwa takwimu kwa kutumia usanifu wa kisasa zaidi.Tutakapofanikisha kumudu matumizi ya teknolojia hiyo kwa kiwangokinachostahili, haya mliyopendekeza wanaJF yatakuwa ndani ya uwezo wetu: Nisuala la wakati.

  ANGALIZO: Haya ni kauli rasmi ya menejimenti ya Star TV, nidokezo binafsi kati yangu na wanaJF kama mojawa watendaji walau kuwapa picha kidogo katika mawazo yenu mazuri.

  WAY FORWARD: Thread hii nitaifikisha kamaagenda katika kikao cha menejimenti ya Star TV tuweze kuweka hadidu za rejea.

  Niendelee kuwashukuru sanakwa Utayari wenu na niwatakie Pasaka njema

  Max, Robbot na Wanafamilia wote wa JF
   
 14. U

  Uswe JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asante Yahya, Pamoja tujenge nchi yetu, nakutakia mafanikio katika kazi hii ya kujenga taifa!
   
 15. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mimi nataka message yangu ifike kwa ndugu Anton Dialo Mmiliki wa Chombo hiki na baadhi ya waandishi na watangazaji...

  Niseme tu watanzania tunampongeza kwa kazi zake anazofanya na kumshauri kuwa kama anataka kufanya biashara tunaomba asichanganye Siasa na biashara zake...

  Mfano Clouds FM, ITV na TBC hawa hawajaelewa watanzania wanahitaji nini.. Maana kuna waandishi na watangazaji wanakuwa upande wa chama tawala hiki kitu watu walishajua na kitakachofuata ni watazamaji na wasikilizaji wanapungua na Raia wanakosa imani wa waandishi wako wa habari na hatimaye wanakuwa na wasi wasi wakiwa kazini..

  Mfano na uhakika kuna waandishi wa TBC au Clouds FM hawawezi kwenda kwenye mikutano ya wapinzani au vijana wa nchi hii kwani ni most wanted wanabaki kupiga porojo tu studio kwa sababu ya unazi wao kwa CCM.

  Chonde chonde Dialo maana Kanda ya Ziwa lote liko CDM na wewe nenda na wakati angalia wateja wako wanahitaji nini..

  Usipende biashara yako ife pamoja na CCM maana kuna vyombo vingine vya habari vitaondoka na CCM 2015 wasipoangalia...

  Chonde chonde Waandishi msije kuwa most wanted mtashindwa kufanya kazi zenu ipasavyo kwani mtakuwa mnaibi habari badala ya kuwa karibu na wananchi na kupata habari..
   
 16. J

  JASOTA Member

  #16
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka hao star tbc hawana lolote,,mie nlikua mdau wao sana katika page yao ya tuongee asubuhi on fb,nkagundua napoteza mda kwa chombo chenye misimamo yake ya kisiasa,,ebu fikiria ni mara ngapi star tbc wamewahi kucover ipasavyo habari za mwnaume cdm??
  Huko ni mbali ebu piga picha siku ccm waliposhinda igunga,,,walitangaza the same tukio kila baada ya masaa 3,,what about arumeru???hata matokeo hawakujiunga kutoa na kesho yake kwenye magazeti wakawa wanasema ''habari nyingi katika kurasa za mbele zinafanana hivyo tuangalie habari za kimataifa"
  kweeli kwa mwendo huo tutafika???tazama juzi lema alivyong'olewa ubunge harusha,,walisoma kila gazeti bila kujali kama zinajirudia...nasema huku ni kutojitambua kwa waandishi wa star tbc,,,,hamjitambui mmepewa semina ilolalia upande mmoja ....amkeni msiwe kama masako wa radio two...siku hizi mavipindi yake yamembakia mwenyewe bila watazamaji,,,,
  nawasihi wa tz tuvisusie hivyo vyombo vya habari na mbadala wake tuzame kwenye magazeti na radio za kizalendo,,,,,,,viva cdm,,,haleluya chadema,,,mwokozi kafufuka...
   
 17. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  wadau hamuoni haja ikapelekwa hoja bungeni kwamba tbc ibadilishwe jina na iitwe tbccm? maana imechukua jina la taifa letu na inafnya mambo ya ccm tu, inadhalilisha jina letu la tanzania.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sina shaka kwamba maoni ya wadau hapa yatafanyiwa kazi ipasavyo. Kwa sisi wa kanda ya ziwa startv ndio tegemeo kubwa kwa ajili ya habari za kitaifa na kimataifa.
  Pamoja na uccm wa mmiliki wa startv bw. Diallo lakini tunadhani anaweza kuiacha startv ifanye kazi kitaaluma na kibiashara na hatimaye kukidhi mahitaji ya jamii.
  Mambo ya itikadi za kisiasa tuyaweke pembeni tunapohudumia wanajamii.
   
 19. m

  mangwela Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inapendeza sana wadau mnapo toa maoni yenu kuhusu vyombo vya habari hapa nchi. Mie ni mmoja kati ya wadau kuhusu mambo ya habari ila kuna kitu ambacho watanzania tunapaswa tukifahamu kuhusu vyombo vyetu vya habari navyo ni:
  1. ushawishi wa wamiliki wa vyombo hivyo ni wa hovyo kabisa
  2. waandishi wenyewe wa habari wengi wao si wasomi ki-vile na hata kama wamesoma basi hawaendani na mabadiliko ya kijamii kuweza kujua jamii inahitaji nini na kwa wakati gani - inawapasa wasome vitabu na watazame wenzao wanafanya nini kwenye vyombo vyao vya habari.
  3. Inapofika wakati wa kuripoti masuala ya kisiasa achana na unazi wako na kama inakuwa nguma basi acha mwandishi mwingine aripoti ili uepuke kudhalilisha fani ya habari nchini.
   
 20. C

  CHIEF MVUNGI Senior Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amponda Masako atatkua afuatilii vipindi vyke kiukweli jamaa yuko against ccm bwana
   
Loading...