Waraka kwa Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Waraka kwa Waziri wa Tamisemi, Seleman Jaffo dhidi ya Mkurugenzi wa jiji Arusha,Dk Maulid Madeni na afisa habari wa jiji, Adriana Mariki

Mh.Waziri wa Tamisemi sisi ni baadhi ya Watumishi wa halmashauri ya jiji la Arusha ambao tumeona tukuandikie waraka huu kwa maslahi ya halmashauri yetu.

Hapa jiji la Arusha kumekuwa na tabia chafu na mwenendo wa mahusiano yasiyoridhisha kazini baina ya mkurugenzi wetu wa jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni na afisa habari wa jiji, Adriana Mariki.

Tangu kuwasili kwa afisa habari huyu hali ya hewa imechafuka hapa ofisini kwetu kwani Hawa watu wawili wamekuwa katika mahusiano ya karibu yanayotia Shaka kiasi kwamba ukaribu wao umepelekea kuharibu mwenendo wa kazi mbalimbali zinazofanyika hapa katika halmashauri yetu.

Kwanza afisa habari huyu amekuwa akipeleka majungu na kuwachongea fitina Watumishi mbalimbali waliopo hapa jijini Arusha kiasi kwamba mkurugenzi naye amejikuta akichukua hatua kwa kusikiliza majungu anayofikishiwa na kisha kuyachukulia hatua.

Afisa habari huyu amekuwa akikesha ofisini kwa mkurugenzi muda wa kazi hata kama kuna foleni ya watu mbalimbali wanaofika ofisini kuonana na mkurugenzi ukijaribu kuangalia ni kipi wanachokifanya ofisini hakuna bali Kuna muda utawakuta wanakunywa chai ofisini wakiwa wawili na kujifungia ndani kwa komeo kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Afisa habari huyu amekuwa na tabia ya kuzunguka na mkurugenzi Dk Madeni kwenye gari lake mara kwa mara hata kama kuna ziara utakuta hakuna mtumishi yoyote anayepanda gari la mkurugenzi zaidi ya huyu Adriana jambo Hili limekuwa likitushangaza kwani kwa muda mrefu tumefanya kazi na wakurugenzi mbalimbali lakini hatujawahi kuona kitendo Kama hiki kichafu.

Sisi kama watumishi hatupingi wawili hawa kuwa kwenye mahusiano maana wao ni binadamu lakini vitendo wanavyovifanya mahali pa kazi ni kinyume kabisa na maadili ya utumishi wa umma.

Afisa habari huyu amekuwa na tabia ya kuzuia watu mbalimbali wanaofika kuonana na mkurugenzi ingawa sio mtumishi wa ofisi ya mkurugenzi (secretary) sasa jukumu la kuhakikisha nani amuone mkurugenzi na nani asimuone limekuwa likisimamiwa na yeye kinyume na utaratibu.

Lakini kama haitoshi afisa habari huyu amekuwa akionekana na mkurugenzi kwenye sehemu mbalimbali za burudani na hoteli mbalimbali nyakati za usiku jambo ambalo tumekuwa tukijiuliza je ni mahusiano gani haya ya kuambatana nyakati baada ya kazi?


Afisa habari huyu amekuwa akiingilia hata ofisi ya mhasibu na kushinikiza malipo mbalimbali kinyume na utaratibu ,jambo ambalo limetufanya sisi wafanyakazi kutoa kilio chetu Tamisemi ili wizara itusaidie na ikumbukwe kuwa afisa habari huyu alishawahi kuitwa na Takukuru na kuhojiwa juu ya malipo. mbalimbali yasiopitia kwenye utaratibu .

Aidha amekuwa akiingilia maamuzi mbalimbali yanayofanywa na vikao vinavyofanyika hapa ndani ya halmashauri jambo ambalo limempelekea mgongano wa maamuzi yanayofanywa na wakuu wa idara na kupelekea kuzorotesha utendaji wa shughuli mbalimbali za halmashauri yetu.

Wito wetu kwa serikali kwanza tungependa serikali ifanye uchunguzi wa ajira ya mtumishi huyu kwa kuwa taaluma yake ya awali inayotambulika ni masuala ya mawasiliano (IT) lakini cha ajabu tunashangaa amepewa nafasi ya masuala ya habari ambayo tunajua hajasomea na pia nafasi yake ya ajira haikuwahi kutangazwa mahali popote.

Jambo la pili tungependa serikali ifuatilie kwa ukaribu mienendo ya watu hawa wawili mkurugenzi Dk Madeni na huyu afisa habari kwa kuwa mahusiano yao yanapelekea kudhorotesha utendaji hapa jiji la Arusha na kupelekea watumishi kukata tamaa ya kufanya kazi.

Mwisho sisi kama watumishi wa halmashauri ya jiji la Arusha tunapinga kwa nguvu zote vitendo vinavyofanywa na watumishi hawa kwa kuwa ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma lakini pia serikali inaweza kutumia vyombo vyake kufanyia uchunguzi hizi tuhuma kwa maslahi ya halmashauri yetu.


ni sisi Watumishi wa halmashauri ya jiji la Arusha.
IMG-20200331-WA0090.jpeg
IMG_20200402_155627_357.JPG


Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Mbona kama na nyie mnafanya majungu.

Kwani hakuna njia rasmi za nyie kufikisha hayo malalamiko yenu sehemu sahihi?

Fuateni sheria na utaratibu katika hili. Waziri anafanya kazi kwa Mambo rasmi, siyo malalamiko ya mitandaoni.
 
Hivi mtumishi wa umma ambaye amekula kiapo cha maadili anaweza kutumia mitandao ya kijamii kulalamikia mumishi mwenzie badala ya kupeleka taarifa kam hiyo katika ngazi husika. Kuna GSO, RAS na wengineo. Pengineni majungu!
 
Mbona kama na nyie mnafanya majungu.

Kwani hakuna njia rasmi za nyie kufikisha hayo malalamiko yenu sehemu sahihi?

Fuateni sheria na utaratibu katika hili. Waziri anafanya kazi kwa Mambo rasmi, siyo malalamiko ya mitandaoni.
Wao wanafuata taratibu? Kama wanafuata taratibu hawataandikwa!!!!
 
Back
Top Bottom