Dr Atom
Member
- Oct 21, 2016
- 37
- 43
Nawasalimu kwa jina la demokrasia, japo hamjaionja hata robo. Naona macho yenu yamegubikwa na hasira na mioyo imejawa na manung'uniko, ni hali ya kawaida na itakwisha. 'usiache mbachao kwa msala upitao'.
Niliwahi kusema 'tujipange upya', kwa sasa haitawezekana tena kwani njia iliyobaki ni kuichafua [HASHTAG]#Amani[/HASHTAG] kitu ambacho ni sawa na kutema lawalawa kwa njugu za kuonjeshwa.
Tutumie hekima na busara katika kujenga taifa tunalo lihitaji. Najua ni kundi kubwa lenye matamanio ya jamii mpya ila matamanio hayo yamezimwa na kundi la watu wachache waliojipanga kwa mfumo dhabiti.
Waswahili husema 'funika kombe MWANAHARAMU apite'. Basi tuwe wavumilivu kwa sasa na tusikubali taifa liingie katika machafuko yasiyokuwa na tija. Najua tunasukumwa sana na hisia kwa sasa ila kwa jina la uvumilivu tukubali kuzishinda hisia japo dhuluma na rafu imetendeka. Tusikubali vikundi vya watu wachache kuharibu ndoto na furaha yetu.
Muhimu ni kujipanga upya, kwani kosa tulilifanya wenyewe kwa kushindwa kutengeneza na kutetea KATIBA bora. Ombi langu tutumie hekima na busara na tupigane kufa na kupona kuilinda kwanza Amani kisha mengine yatafuata.
Mwisho, tukumbuke UCHU WA MADARAKA NDIYO CHANZO CHA MIGOGORO AFRIKA.