Waraka kwa wanaume wote

Waraka kwa wanaume wote

theriogenology

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
8,748
Reaction score
15,731
Leo waraka wetu wa kiumeni unaenda vyuoni pamoja na maofisini kusambaza mbegu ya Upendo na kuamsha vitu muhimu kwenye ubongo na vifua vya wanaume wenzetu Tanzania Bara na visiwani.

Usimsomeshe girfriend wako,badala yake kama una pesa za mchezo basi wape msaada watu wamchao Mwenyezi- Mungu.mtendee wema mcha Mungu nawe utatuzwa na mtu huyo na hakika Mungu mkubwa atabariki kazi ya mikono yako.

Mchezea nyoka akiumwa hahurumiwi na mtu yeyote ! usikubali kubeba mzigo upitao nguvu zako girfriend hasomeshwi badala yake mke ndio husomeshwa kuna tofauti kubwa sana kati ya mke na girlfriend.

Miezi tisa tumboni kwenye tumbo la mama yako ,malezi bora na faraja ya maneno na vitendo toka kwa mama yako iweje usomeshe girlfriend wakati mama yako alikupikia na kukufulia nguo ,hana kitenge wala gari ya kutembelea kutoka kwako na wewe unalipia girfriend chuo?

Mwanaume uliopo chuo usimhonge pesa ya mkopo girlfriend wako,sababu siku ya kulipa mkopo yeye hatochangia hata shilingi moja-Change today for the better tomorrow.Penzi la pesa huwa na mwisho mbaya na siku zote muathirika huwa ni mwanaume.wekeza pesa DSE na sio kusomesha Girfriend.

Tumia utashi wako wewe uliopo chuoni ,girfriend wako anatumia Iphone 7+ wewe unatumia Bontel ,na bado unamnunulia chakula,airtime pamoja na gharama za outing na wote ni wanafunzi na hakuna aliyeajiriwa huoni hilo ni tatizo kwako?

Girfriend anayeomba kuanzia pesa ya kusuka,airtime,beer,anayekutegemea outing hatoi pesa ya drinks or meals na yeye anapokea mkopo huyo ni liability na sio asset kwako...Amka na jifunze kutafakari juu ya moyo wako ,ubongo wako na future yako.

Girfriend anayeomba pesa anaitwa -Demu na msichana mwenye mapenzi ya dhati na kinywa thabiti asiyeomba pesa na mwenye mawazo chanya msikivu na adabu ana sifa za kuwa mke na jina lake ni Mchumba wa haki kiumeni na kikeni.

Ustioe pesa kwa ajili ya Penzi kaka mkubwa onyesha utashi wako ,maarifa yako ,elimu yako na utundu na ubunifu wako ila kumuiba mwanamke bila kutumia tendo la uwizi.We came into the world like brother and brother; And now let’s go hand in hand, not one before another.[HASHTAG]#MensTalk[/HASHTAG]

C & P from CraftsMan-Benjamini James
 
Sawa, asante kwa waraka ila umekosea kidogo, mwanamke matunzo, usipomtunza wewe kuna wenzio watakutunzia alafu utabaki kusifia tu na kumegewa bila huruma..
Poor assessment na dharau kwa mwanamke
Unaemdeleza mfumo dume na unyonge kwa wanawake
 
Sawa, asante kwa waraka ila umekosea kidogo, mwanamke matunzo, usipomtunza wewe kuna wenzio watakutunzia alafu utabaki kusifia tu na kumegewa bila huruma..
Anayestahili matunzo ya mwanaume ni mke na si mwanamke tu!kuna tofauti kati ya mke na mwanamke ujue!
 
Hahaha zamanii niliwahi kusikia "wanawake wakiwezeshwa wanaweza" hivi hawajaweza tu nao waanze kuwezesha wanaume?! Au wajiwezeshe sasa, bado mnawawezesha mpaka lini?!
 
Tuko pamoja mkuu..
Dem hasomeshwi kama unampenda sana mpe mimba kwanza ndio umsomeshe ili akikukimbia baadae basi mwanao atakusaidia kupunguza deni akiwa analelewa
 
Sawa, asante kwa waraka ila umekosea kidogo, mwanamke matunzo, usipomtunza wewe kuna wenzio watakutunzia alafu utabaki kusifia tu na kumegewa bila huruma..
Kwann hamuwezi kuridhika?..yani mmeweka mentality mpk mwanaume akutunze ndio utulie nae
 
Sawa, asante kwa waraka ila umekosea kidogo, mwanamke matunzo, usipomtunza wewe kuna wenzio watakutunzia alafu utabaki kusifia tu na kumegewa bila huruma..
Kwahiyo unaelezeaje hao wanawake wanapokuwa watoto wakiishi kwa wazazi wao, kwamba wao ndio wagharamikiwe zaidi kuliko wale wa kiume au?, hilo ulilolisema ni mapokeo tu wanayoyaamini watu wengi humu Tz, kama vipi kawatunze tu hao madem kwan unaenda kuwaoa?, pia kumbuka kuwa wapo watunzaji wengi tu wanawatunza kwa hali na mali ila still wanachapiwa, tatizo liko ktk akili ya mwanamke, ni either atakuwa na mindset ya kiDemu au mindset ya kiUchumba.
mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, hajatajwa mwanaume yeyote hapo [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] , kwa hapo tuseme mwanamke moumbavu hujiharibia future yake mwenyewe kwa mikono yake kabisa
 
Alafu mwanamke ukiwa nae sana seriaz sana hufiki nae mbali
 
Sawa, asante kwa waraka ila umekosea kidogo, mwanamke matunzo, usipomtunza wewe kuna wenzio watakutunzia alafu utabaki kusifia tu na kumegewa bila huruma..
Wicked beliefs, hata umtunze vipi mwanamke kama hana uaminifu ni kazi bure tu. Endelea kukazana kutunza wanawake wenzio wanakula bure kabisa [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
waoaji siku hz ni wachache mno
 
Mbona ombaomba huwa mnawapa nakuondoka? Ukisomesha ni swahabu maana unajivika majukumu ya mzazi mapema,...kusomesha gharama yake haizidi 5mil had anamaliza chuo sioni kosa hapo, mbona watu tunahonga Harrier ya 28mil Kwa penzi la hawala? Watu tunahonga cheo kikuubwa kabisa hata cha uwaziri ambacho unaweza kuliangamiza taifa Kwa papuchi lakini hatulalamiki tukipigwa chini? Hakuna mbinu mbadala ya kupata demu yeyote mkali bila kuhonga, ukisubiri upendwe hutapata demu roho inapenda! MUGABE MWENYEWE ALITAKA KUHONGA NCHI NZIMA...toa roho inapenda
 
sioni tatizo. "Likupatalo ilikuwa halikukosi, likukosalo ilikuwa lisikupate!"
 
Back
Top Bottom