mukulupapaa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 2,930
- 1,734
siyo mkazi wa dar lakini ntachangia
Moja ya gonjwa mtambuka linalokusumbua ni malengelenge! Hivyo nenda ukapime ili uanze kutumia ARV!Huyu meya mbona anatapatapa sana?
Kama ni mpumba ni mpumbavu tu hawezi akaficha hata sekunde. Ujinga unaweza kwenda likizo lakini upumbavu hauishi. Kuna watu wanazaliwa wapumbavu!Hebu jaribu kuficha upumbavu wako japo mara moja kwa wiki.
hata mimi pia nitachangia..siyo mkazi wa dar lakini ntachangia
Mkuu chakushangaza lumumba wanaleta siasa kwenye mambo ya muhimuWazo zuri, ndugu yangu uliyeleta post hii. Mimi siyo mkazi wa Dar/ Kinondoni lakini nipo tayari kuchangia. Tukiukosa mradi huu, wazungu watatudharau sana. Matakataka haya ya Dar halafu tunaukataa ukombozi huu. Please Major fungua hiyo/hizo accounts, tuarifu tutachanga. Waambie wahisani wetu, Wajerumani ili watupe muda kidogo tupige harambee tutapata tu hiyo pesa. Nawaomba Watanzania wote wenye mapenzi mema, tuchange. Angalia, Dar ndiyo sebule ya Tanzania.
ni sawa na ngoziKama ni mpumba ni ******** tu hawezi akaficha hata sekunde. Ujinga unaweza kwenda likizo lakini upumbavu hauishi. Kuna watu wanazaliwa wapumbavu!
Hata Mimi.Mie sio mkazi wa Kinondoni lakini ntachangia
tafadhali mkuu,usiseme viongozi wetu..maana ya kiongozi ni kuwaonyesha njia anaowaongoza,sasa hivi hao wamesha jibatiza kwa moto kuwa wao ni waheshimiwa watukufu..Ukiisoma taarifa ya mstahiki meya wa Kinondoni haki ya Mungu lazima upandwe na hasira! Hivi viongozi wetu wana akili timamu kweli? Unakuta mtu linasimama kwenye jukwaa eti linaomba liombewe huku nyuma matendo yake hayaendani na muumini wa dini yoyote inayomwamini Mungu! Huu unafiki wa viongozi wetu hautatufikisha popote! Nampongeza aliyetoa hilo wazo la kuwashirikisha wananchi uchangia hiyo pesa ya kodi wanayoitaka ili wafurahi. Ila kwa jinsi yalivyo mataahira hayatasita kuzuia huo mchango kutoka kwa wananchi! Nashindwa kuelewa hivi Rais naye anashabikia ujinga huu unaofanywa na wasaidizi wake? Ningekuwa mimi huyo Katibu wa wizara ya fedha aliyeandika hiyo barua ningekuwa nimeshamtumbua, maana ni ******** kati ya wapambavu wote!! Mtumishi wa umma unatumiakaje kwa maslahi ya chama cha mataahira?
achana nao,maana hata ktk safari ya wana wa Mungu kuelekea nchi ya ahadi walikuwepo watu kama hao.Mkuu chakushangaza lumumba wanaleta siasa kwenye mambo ya muhimu
Mstahiki meya,
Pole sana kwa Hujuma zinazoendelea juu yako na Mameya wenzako ambao wako chini ya mwamvuli wa UKAWA.
Binafsi nimeshuhudia namna ambavyo umekua ukijitoa (kucompromise na serikali),hata kama ni kwa kujiumiza nafsi yako, au maamuzi na Itikadi za chama chako, kwako maendeleo ya wananchi wa kinondoni bila kujali vyama vyao ndio imekua kipaumbele chako.
Nakumbuka ulivyoamua kushiriki mbio za Mwenge, naujua vizuri msimamo wako juu ya hili, lakini ulifunika kombe mwanaharamu apite.
Najua ambavyo uzinduzi wa Program ya Jeshi la Polisi pale Biafra, mgeni rasmi akiwa Rais ulivyohujumiwa na bado ukapigwa madongo huku hata wewe haupo, haikukufanya urudi nyuma kuwatumikia watu wako. Spidi ndio kwanza naona imeongezeka
Mstahiki Meya,
Nimesoma maelezo yako mara baada ya ziara ya Rais Kinondoni, nimepatwa na simanzi sana. Hasa hasa hujuma ya mradi wa kuzoa takataka na kuanzisha kiwanda cha mbolea, ambao ni msaada kutoka Ujerumani.Hili si la kufumbia macho kabisa.
Nimekutana na wadau kadhaa, wa vyama na Itikadi tofauti, kama wakazi wa kinondoni, tumedhamiria kuuokoa mradi huo, ilimradi utuhakikishie kwamba kodi wanayoitaka serikali ya TZS 900m ikipatikana, waliotuahidi msaada, wako tayari kurudi.
Tumepiga hesabu ya wakazi 90,000 pekee wa Kinondoni watakaokuwa tayari kuchangia TZS 10,000 tutakua tayari tumepata TZS 900m. Lakini tunadhamiria kupokea hata kiasi kidogo kama 500 au hata mwenye kikubwa zaidi ya 100,000.
Tunaomba uanzishe account maalum za Tigopesa, Mpesa, Aitelmoney, Halotel money kwa Jina la Meya na tulete kampeni ya kukusanya pesa hizo ngazi ya Kata, Mtaa, Nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu.
Kama Serikali haitaki kutupa maendeleo acha tupambane kwa nguvu zetu tuwaonyeshe udhaifu walio nao.
Nitakuwa mstari wa mbele, kama utaridhia wazo hili kuhakikisha tukafanikiwa na mradi uanze mara moja.
NAKUTAKIA UTUMISHI ULIOTUKUKA KWA WANANCHI WAKO, MUNGU YUKO NAWE SIKU ZOTE NA DAIMA HAKI HUSIMAMA KWENYE UKWELI
Sam Ntakamulenga
Mkazi wa Kinondoni,
Mtumishi wa watu wa Urambo Mashariki
heri waitafutio haki kwa mateso,maana wataipata tu.Hili ni wazo jipya. Ujasiri wa kufa msalabani kwa ajili ya wengine
Wanatumia makalio kufikiri,ubongo kupangilia mipasho,mikono kuonyeshea wapinzani wao vidole kwa kuwatisha,miguu kwa kuchochea maovu na kuyakimbilia maovu....I like this idea!
Mimi siishi Kinondoni wala DSM. Niko zangu Shinyanga. Lakini niko tayari kuchangia chochote nitakachokuwa nacho.
Tafadhali Meya wa Kinondoni, thibitisha kama hao wafadhili hawajaghairi kutoa msaada huo wenye manufaa makubwa sana kwa wananchi maskini wa Kinondoni, sisi tuchangishane kidogo ku rescue huo mradi.
Kwa kweli na kama ni kweli hili limefanywa na serikali hii, watanzania tutaonekana wajinga sana kama baadhi ya wananchi wa Ujerumani wameamua kutusaidia ktk mradi ambao hata sio wa kibiashara, tunawaambia walipe kodi!!
Hivi tunajua hizo fedha za mradi huo ambazo ni zaidi ya 3bn wamezipataje ili kutusaidia? Inawezekana kabisa kwa upendo wao wamejichangisha na kuamua kutusaidia sisi!!
Na kwa nini kama serikali inajiona inaweza isitoe hizo bilioni tatu kwa ajili mradi huo?
Ni kwa nini tunaingiza siasa ktk mambo ya maendeleo na viongozi wetu wakituimbia wimbo wa "siasa ni mpaka 2020, sasa ni wakati wa kuwaletea watu maendeleo" huku wakifanya kinyume chake??
Ki ukweli siwasomi kabisa hawa viongozi wetu!!
What is 900milions ktk mradi wenye thamani ya zaidi ya 3.4bn unaosadiwa na mtu mwingine? Tunatumia akili kweli ktk kuamua au......???
Arrrrrrrgh......inaudhi sana aisee!!!????
Ukiisoma taarifa ya mstahiki meya wa Kinondoni haki ya Mungu lazima upandwe na hasira! Hivi viongozi wetu wana akili timamu kweli? Unakuta mtu linasimama kwenye jukwaa eti linaomba liombewe huku nyuma matendo yake hayaendani na muumini wa dini yoyote inayomwamini Mungu! Huu unafiki wa viongozi wetu hautatufikisha popote! Nampongeza aliyetoa hilo wazo la kuwashirikisha wananchi uchangia hiyo pesa ya kodi wanayoitaka ili wafurahi. Ila kwa jinsi yalivyo mataahira hayatasita kuzuia huo mchango kutoka kwa wananchi! Nashindwa kuelewa hivi Rais naye anashabikia ujinga huu unaofanywa na wasaidizi wake? Ningekuwa mimi huyo Katibu wa wizara ya fedha aliyeandika hiyo barua ningekuwa nimeshamtumbua, maana ni ******** kati ya wapambavu wote!! Mtumishi wa umma unatumiakaje kwa maslahi ya chama cha mataahira?
hizo ni figisu za walio juu,hawapendi maendeleo ya watz japo wanayahubiri kila siku kwenye majukwaa.Mkuu mimi huwa nasema jamii yetu watanzania ni ya watu wapuuzi kabisa ambao hatukustahili kuwepo duniani. Huwa sielewi kabisa hizi roho mbaya tulizo nazo kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe. Viongozi wetu walio wengi ni tatizo kubwa. Hili sakata lililomkumba Meya wa kinondoni ni sawa na jamaa yangu mmoja anafanya kazi serkalini kapata aliongea na wafadhili kusaidia wanafunzi wanaohitaji interniship baada ya kumaliza masomo vyuoni. Mfadhili alikubali kuchukuwa wahitimu 30 -50 kwa mwaka kwenye NGOs zianazofanya kazi Tanzania. Huyu bwana alipowasilisha hili wazo kwa wakubwa wake wa kazi ambao ndo decision makers, walimuuliza wao watafaidika na kitu gani kwa kuwapeleka hao wahitimu? Hebu fikiria jinsi gani watanzania tulivyo na roho mbaya (roho za kishetani). Kwa sababu tu mtu hana anachopata kwa kumsaidia mtoto wa masikini aligoma katu katu hata kuwasiliana na hao wafadhili ili tu watoto wa masikini wasipate hizo nafasi za kufanya interniship. Jamii ya kitanzania nadhani tumelaaniwa.
YANI TUMELAANIWA VIBAYA SANA KWA KWELI.. KUNA WATU WANATIA UCHUNGU UNATAMANI UMTOE ROHO TU ASIWEPO.Mkuu mimi huwa nasema jamii yetu watanzania ni ya watu wapuuzi kabisa ambao hatukustahili kuwepo duniani. Huwa sielewi kabisa hizi roho mbaya tulizo nazo kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe. Viongozi wetu walio wengi ni tatizo kubwa. Hili sakata lililomkumba Meya wa kinondoni ni sawa na jamaa yangu mmoja anafanya kazi serkalini kapata aliongea na wafadhili kusaidia wanafunzi wanaohitaji interniship baada ya kumaliza masomo vyuoni. Mfadhili alikubali kuchukuwa wahitimu 30 -50 kwa mwaka kwenye NGOs zianazofanya kazi Tanzania. Huyu bwana alipowasilisha hili wazo kwa wakubwa wake wa kazi ambao ndo decision makers, walimuuliza wao watafaidika na kitu gani kwa kuwapeleka hao wahitimu? Hebu fikiria jinsi gani watanzania tulivyo na roho mbaya (roho za kishetani). Kwa sababu tu mtu hana anachopata kwa kumsaidia mtoto wa masikini aligoma katu katu hata kuwasiliana na hao wafadhili ili tu watoto wa masikini wasipate hizo nafasi za kufanya interniship. Jamii ya kitanzania nadhani tumelaaniwa.