Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Mstahiki meya,
Pole sana kwa Hujuma zinazoendelea juu yako na Mameya wenzako ambao wako chini ya mwamvuli wa UKAWA.
Binafsi nimeshuhudia namna ambavyo umekua ukijitoa (kucompromise na serikali),hata kama ni kwa kujiumiza nafsi yako, au maamuzi na Itikadi za chama chako, kwako maendeleo ya wananchi wa kinondoni bila kujali vyama vyao ndio imekua kipaumbele chako.
Nakumbuka ulivyoamua kushiriki mbio za Mwenge, naujua vizuri msimamo wako juu ya hili, lakini ulifunika kombe mwanaharamu apite.
Najua ambavyo uzinduzi wa Program ya Jeshi la Polisi pale Biafra, mgeni rasmi akiwa Rais ulivyohujumiwa na bado ukapigwa madongo huku hata wewe haupo, haikukufanya urudi nyuma kuwatumikia watu wako. Spidi ndio kwanza naona imeongezeka
Mstahiki Meya,
Nimesoma maelezo yako mara baada ya ziara ya Rais Kinondoni, nimepatwa na simanzi sana. Hasa hasa hujuma ya mradi wa kuzoa takataka na kuanzisha kiwanda cha mbolea, ambao ni msaada kutoka Ujerumani.Hili si la kufumbia macho kabisa.
Nimekutana na wadau kadhaa, wa vyama na Itikadi tofauti, kama wakazi wa kinondoni, tumedhamiria kuuokoa mradi huo, ilimradi utuhakikishie kwamba kodi wanayoitaka serikali ya TZS 900m ikipatikana, waliotuahidi msaada, wako tayari kurudi.
Tumepiga hesabu ya wakazi 90,000 pekee wa Kinondoni watakaokuwa tayari kuchangia TZS 10,000 tutakua tayari tumepata TZS 900m. Lakini tunadhamiria kupokea hata kiasi kidogo kama 500 au hata mwenye kikubwa zaidi ya 100,000.
Tunaomba uanzishe account maalum za Tigopesa, Mpesa, Aitelmoney, Halotel money kwa Jina la Meya na tulete kampeni ya kukusanya pesa hizo ngazi ya Kata, Mtaa, Nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu.
Kama Serikali haitaki kutupa maendeleo acha tupambane kwa nguvu zetu tuwaonyeshe udhaifu walio nao.
Nitakuwa mstari wa mbele, kama utaridhia wazo hili kuhakikisha tukafanikiwa na mradi uanze mara moja.
NAKUTAKIA UTUMISHI ULIOTUKUKA KWA WANANCHI WAKO, MUNGU YUKO NAWE SIKU ZOTE NA DAIMA HAKI HUSIMAMA KWENYE UKWELI
Sam Ntakamulenga
Mkazi wa Kinondoni,
Mtumishi wa watu wa Urambo Mashariki