The Prophet
JF-Expert Member
- Mar 17, 2011
- 682
- 94
Vijana tunakiamini chama cha demokrasia na maendeleo,kwa namna kinavyosimama na kuibua na kuhoji mambo muhimu sana katika jamii yetu.
Hata wazazi wetu wanaamini chadema ndio kimbilio letu, licha ya wao kutuonya kuhusu kujitokeza mbele sana kwenye harakati za siasa, wakihofia usalama wetu.
Ila sasa viongozi wetu mnapoonekana kuvutana kwa ajiri ya tamaa za madaraka na ruzuku, ni aibu sana na ipo siku vijana wengi watafuatilia kiundani mambo ya chama chetu na ikiwa watabaini ukweli ulio tofauti na hisia zao, basi wataingia msituni kwani hawataamini mabadiliko kupitia chama cha siasa.
Ikiwa CHADEMA hakitabadilika kimtazamo, kisera na ki-organisation, hakuna mafanikio, nawaomba sana Mbowe, Slaa na Zitto kubalini kukaa na kushauriana.
I dnt understant wht the deal with uwenyekiti, tafadhali sana vijana vyuoni sasa wameanza kuhoji undani wa ugomvi wa Mbowe na Zitto kila wanapo onana.
Na ni kwa nini wanaonekana kutosikilizana hata kwa jambo la maana, tunajitahidi kujibu maswali magumu sana kutoka kwa vijana wasiojua CHADEMA, ila tunafanikiwa kuwatuliza na kuwapa moyo, ila wakati mwingine unajibu mtu na unaona haimwingii akilini.
Please msituumize kabisaaa.
Hoja kama hii badala ya kufanyiwa tafakuri na viongozi wa CHADEMA na kutoa majibu muafaka na yenye upeo basi utaambiwa umetumwa au una spin!!
Hizo ni propaganda za CCM tu.Achana na magazeti uchwara yanayoripoti hizo habari za uongo..Chadema ni kanyaga twende.Mbowe angekuwa na ugomvi na Zitto angemteua kuwa Naibu Katibu mkuu? Au angemteua kuwa Naibu Kiongozi wa upinzani bungeni?? Je, angemteua kuwa waziri kivuli wa Fedha?? Achana na propaganda broo...Zitto Slaa na Mbowe kanyaga twende..Sasa hivi wote wako njiani kuelekea Mbeya kuongoza maandamano lkesho..
Mbowe angekuwa na ugomvi na Zitto angemteua kuwa Naibu Katibu mkuu? Au angemteua kuwa Naibu Kiongozi wa upinzani bungeni?? Je, angemteua kuwa waziri kivuli wa Fedha?? Achana na propaganda broo
tatizo ni kwamba zitto anapenda kuingilia mambo ya mwenzake mbowe. mbowe akicheza dili zake yy anaingilia kwa mfano mbowe yy baada ya kuona magari yamekosa wateja anataka kuwauzia chama zitto anaingilia, mbowe akamwambia zitto na wewe kama unataka nawewe tuuzie hammer lako ili mwisho wa wiki slaa baada ya kuchoka na kazi za kukisafishia chama njia ya ikulu atumie, zitto akakataa sasa hapo ndio mwanzo wa ugonvi wao.
Nachukia sana watu wasiopenda kukosolewa hata kama ukweli unaonekana dhahiri.Vijana wa ccm wanajulikana mapema humu ndani kutokana na uwezo wao mdogo wa kujenga hoja mimi nakwambia tunatumia kauli hii:Its your choice either to join us or to be against us' anguko kuu la chama tawala Tanzania ni 2015 shime wananchi njoni tulikate kichwa joka hili linalomeza maendeleo yetu
Ni kweli mkuu, hawa watu wawili wanatuchanganya sana. Endapo wakiendelea tutawafukuza wote wawili, ili wakatafute vyama vya kurumbania sio chadema. Mbowe na Zitto tutawafukuza chamani, uwezo huo tunao.
wewe ben ni mgombea uwenyekiti ee sio....haya kaa chonjo na utetezi wako wa upofu huo, na heche huyo ajaaaa.