Waraka kwa Maaskofu -Wakatoliki

Waraka kwa Maaskofu -Wakatoliki

Utapambana na wachaga na hutashinda maana Mungu yupo nasi
 
Mtoa mada unasikitisha sana.

Ni wazi kwamba unataka kuaminisha watu kwamba maaskofu Wakatoliki waliotoa barua ya kuonyesha mambo ya hovyo katika nchi hii wamefanya hivyo kwa sababu ni Wachaga. Halafu ukasema ni maaskofu watano tu walioandika huo waraka na wote ni Wachaga isipokuwa mmoja.

Nasema tena, wewe mtoa mada unasikitisha sana, tena sana !.

1. Maaskofu wa Kikatoliki hawateuani wao wenyewe, wanateuliwa na Pope kule Vatican. Kwa hivyo unachotaka kuwaaminisha watu kwamba maaskofu Wakatoliki ni wengi kwa sababu ni Wachaga waliojiteua ni ujinga, tena linaonyesha wewe una ukabila wa hali ya juu.

2. Ukatoliki ulianzia Kilimanjaro ziadi ya miaka 120 iliyopita. Kwa hivyo, lazima utegemee idadi ya mapadri Wakatoliki ambao ndio wanateuliwa kuwa maaskofu ni wengi kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania. Kwa maneno mengine, wingi wa maaskofu Wakatoliki ambao ni Wachaga unatokana na wingi wa mapadri Wachaga.

3. Umesema kwamba ni maaskofu wachache tu walioandika ule waraka. Kama unathubutu kusema jambo kama hilo unajionyesha wazi kwamba hata namna yako ya kufikiri ina kasoro. Unajua wazi kwamba kila askofu aliyetajwa katika ule waraka aliweka sahihi yake kwenye huo waraka. Unataka kutuambia kwamba askofu ambaye ni mtu msomi (wengi wana PhD) atakubali kutia sahihi yake kwenye waraka ambao hakubaliani nao? Unashangaza sana, sana

Ukitaka kuelewa vizuri lazima usome vizuri ili na wewe ueleweke. Naomba unifahamishe, Papa anapowatuea kule Vatican anawajuaje? Waraka wao unaosema walitia sahihi Kardinali Pengo aliukana pamoja na jina lake kuwemo, unawezaje kusema waliusaini? Au wewe unaishi dunia nyingine? Hata kama mtoa mada anapotosha mambo, hiyo haimaanishi na wewe uwe gumbaru asiyeelewa kinachojadiliwa.
 
Sawa!! Huu ni waraka wa waraka wa maaskofu wa katoliki ambao kwa mtazamo wako ulikuwa na chembechembe za uchadema na uchagga!! Umeelezea makosa yao ya miaka 359 iliyopita! Ila umeshindwa kuona kuwa content za waraka wao zinaelezea matukio halisi yaliyotokea ndani ya kipindi cha chini ya miaka mitatu tu iliyopita! Tukio halisi hutazamwa kiuhalisia bila kujali nani anayelitazama! Halihitaji sense of comparability! Kwa mfano chadema waliwahi kusema kuwa ndani ya ccm kuna mafisadi,ccm wakasema hapana! Baadaye ccm wakakiri kuwa kweli kuna ufisadi na wapo tayari kuushughulikia! Hapo main context ni Ufisadi(kitu kibaya) maana kwa hoja yako ya moral authority tukiichukulia serious itatubidi tuwatimue kazi majaji na mahakimu wengi mno kwa kutumia hilo rungu la moral authority!! Bado haujapima moral authority ya maaskofu wa kkkt? Fanya hivyo! Ukimaliza hayo nawewe ujipime moral authority yako juu ya wengine!
Kwa kama hii ndio CCM ya sasa basi taifa limekwisha kabisa.
Kila wanaloambiwa kwa nia njema kabisa wao wanalijibu kwa kejeli na kutafuta visa vya kupambana na wakosoaji.
Nilishangaa na wabunge wa CCM wanaulizwa ilipo Tr 1.5 ya walipa kodi wa Tanzania wao wanapiga vikembe na kusema Chadema nayo imefanya ufisadi.
Sasa leo wanaandikiwa waraka ulioko wazi na unaopambanua matatizo ya nchi yanayohusu haki za kibinadamu zilizobaimishwa na katiba lakini zinakiukwa kwa kutumia virisho na nguvu ya dola. Wakati huo huo watu wanapotea na maiti kuokotwa baharini . Badala ya kujitoleza na kujibu kuwa serikali kwa nini inakiuka katiba na kiwafunga watu wanaofanya shughuli zao kikatiba kabisa wanajitokeza watu wa ajabu ajabu na kuwatetea watu wasiojulikana badala ya kuibana serikali iwakamate wauaji na watekaji na kuukomesha huo uhalifu kwa maneno naatendo.

Kuwaandikia waraka Maasko kwa sababu ya kuitetea serikali ni ujinga mtupu kwa kuwa maaskofu wa Katoliki hawawajibuki kusimamia na kulinda haki za wanzania wote. Wao ni taasisi tu ya kundi moja na dhehebu moja tu la latoliki.
Serikali ya CCM inajisahau kuwa ni ya watanzania wote na ndiye inayowakilisha watanzania kimataifa. Ndiyo inayosimamia dola. Ndiyo iliyoapa kulinda katiba ya nchi. Ndiyo inayoshika funguo za hazina. Ndiyo inayoteua mabalozi wa kuiwakilisha tanzania dunia nzima. Ndiyo inayopanga nani apate na nani akose. Ndiyo inayosajili madhehebu yote ya dini. Ndiyo inayoagiza zana zote za kivita na kijeshi kwa ajili ya ulinzi wa nchi.
Lakini maaskofu ni kwa ajili yaadhebu yao tu. Na kwa nchi hii ni mjinga tu atashangaa ni kwa nini maaskofu wanaweza kutoka sehemu moja kwa sababu sio kila mkoa au ukanda una waumini wa dini au dhehebu hilo. Kuna wilaya mzima hazina waumini hata mia tano wa dhehebu au dini fulani.
Mfano Pemba ni vigumu na haiwezekani kumpata askofu mzawa. Na maeneo mengi tu.

Sasa kulinganisha Chama au dhehebu la dini au maaskofu na mamlaka ya serikali na utendaji wake ni upuuzi na uelewa mdogo sana wa mambo wa vijana wa kileo ndani ya chama kikubwa kama CCM.
Uteuzi wa serikali ukiwa na ukanda,udini,ukabila ni hatari sana.
Utauzi wa serikali ni matumizi ya kodi za watu wote.
Na watanzania wote wako chini ya serikali inayotawala . Hivyo ina mamlaka ya kumteua hata mpinzani alimradi awe mtanzania na kuondoa minong'ono ya ukanda ,ukabila na udini.
Kwenye dini ya katoliki kwa mfano ni wazi kuwa huwezi kumpata Askofu mpemba kutokana na kuwa pemba 100% ni waislam. Lakini serikali haiwezi kujitetea kuwa imekosa mpemba mwenye sifa za uteuzi wanaouhitaji. Hii ni kwa sababu pemba ni sehemu ya Jamhuri na iko chini ya serikali ya chama tawala na uchaguzi unapopita ni kazi ya serikali iliyoshinda na chama chake kuwatendea haki sawa kikatiba wananchi wote bila kujali vyama,vyao ,dini zao na makabila na kanda zao.

Ukiona serikali inalalamikiwa na watu na makundi mbalimbali ya kijamii kuhusu uvunjifu wa katiba basi ujue kuna ukweli japo hata kidogo. Hivyo ni wajibu wa serikali kujirekebisha na kujisahihisha na kufuata katiba na sio kugombana na wale walio ikosoa kwa kuwa wanakosoa watu waliowachagua kwa kura na wanalipwa kwa kazi hiyo ya utawala na uongozi.
 
Sahihi kabisa mkuu!
 
Nakuunga mkono kwa asilimia kubwa. Naamini mleta mada anatokea Mkoa wa Rukwa na tatizo lake ni kutoona mfipa mwenzake akipewa daraja la Uaskofu. Labda nimuulize; Ni Padri gani Mfipa alistahili kuwa Askofu?
Sina uhakika kama yupo lakini sina uhakika kama hayupo. Lakini dhana kwamba wanaofaa wanatoka huko unakodhani wanastahili kutokea, basi kuna tatizo lingine linakuja hapo. Hao wa Kilimanjaro wanasomea wapi ambako hao wa Sumbawanga hawakuweza kwenda kusoma, au hawana akili ya kumudu masomo?
Kuweka sawa rekodi, kuna maaskofu wawili wenye asili ya mkoa wa Rukwa; Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo la Shinyanga.

Huyu mleta mada kinachomsumbua ni ukada na si ukanda, ila ameutumia ukanda kujaribu kudhoofisha maudhui ya Waraka wa Maaskofu, mambo ambayo hayanana uhusiano kabisa
 
Unafikiri hata biashara nyingi walizonazo wachagga wamepedelewa na Nani?
 
Waraka kwa Maaskofu -Wakatoliki
Wapendwa Maaskofu, miezi michache iliyopita kuliotokea hali ya kutofautiana kati ya viongozi wa kanisa Katoliki na serikali; vile vile kati yenu ninyi viongozi wa kanisa wenyewe kwa wenyewe kutokana na chapisho la Waraka ujulikanao kwa jina la “ujumbe wa Kwaresma” utolewao na kanisa Katoliki nchini Tanzania kila mwaka. Waraka huo wa mwaka huu ulikuwa na ujumbe uliikosoa serikali hasa katika suala ya kuminya demokrasia. Hali kadhalika kwa upande mwingine baadhi ya viongozi wa Kanisa kama Kardinali Pengo alitofautiana na maaskofu wenzake kwa kile alichosema kuwa waraka ulichanganya siasa na dini.

Wapendwa Maaskofu, ni jambo lilodhahiri kuwa ujumbe wenu kupitia waraka ule ulikuwa sehemu ya utume wenu wa kinabii. Kwa mujibu wa utume huo mnapaswa kukemea pale inapobidi na ndivyo ilivyokuwa kwa nyakati mbalimbali. Mifano ipo mingi ambapo viongozi wa Kanisa na baadhi ya waamini wa kawaida wakikemea maovu hata yaliyotendwa na viongozi wa dola ndiyo maana watu kama kina Thomas More waliuawa kule Uingereza katika karne ya 16. Baadaye Thomas More alitangazwa na kanisa kuwa Mtakatifu kwa msimamo wake wa kusimamia ukweli aliouamini na uliokuwa katika misingi ya Injli. Lakini jambo la kukumbuka ni kuwa viongozi wa Kanisa wanaotaka kukemea wengine wanatakiwa wawe na mamlaka ya kimaadili (moral authority), ili waweze kutekeleza jukumu hilo.

Wapendwa Maaskofu, mtakumbuka kuwa katika mitandao ya kijamii, moja ya mambo ambayo serikali ya awamu ya tano inalaumiwa na watu wengi ni pamoja kuwa na upendeleo katika ajira, hasa nafasi nyeti serikalini kwenda kwa watu wa kanda ya Ziwa. Sina uhakika na jambo hili kwa sasa, lakini kama lipo lisiendelee kuwepo na kama halipo lisije likafanyika kabisa. Athari ya ubaguzi na upendeleo litaligawa taifa na kuleta madhara makubwa sana. Ubaguzi unaweza kuanza kwa kuangaliana kwa kanda, baadaye kabila, koo na kadhalika. Ukweli ni kuwa hakuna mwisho mzuri wa jambo kama hilo. Nimesema kama kweli upo upendeleo wa kikanda, kama taifa tunapaswa kulitafutia suluhisho kabla hatujapata madhara. Je, katika hili Kanisa letu/lenu lipo salama?

Wapendwa Maaskofu, ili kupata suluhisho la tatizo la upendeleo na ubaguzi ni jukumu lenu viongozi wa Kanisa kushiriki na ninyi mnao wajibu huo ambao mnapaswa kuutekeleza kwa umakini mkubwa sana. Pamoja na kuwatwisha ninyi viongozi jukumu hilo nina mashaka kama mtalimudu jambo hilo. Mashaka yangu yanatokana na ukweli kuwa viongozi wangu mnanaanza kukosa mamlaka ya kimaadili. Historia ya Kanisa Katoliki inatukumbusha kuwa huko nyuma pamoja na kufanya mambo mazuri lakini kuna nyakati kanisa lilifanya makosa makubwa sana. Mwaka 1663 viongozi wa Kanisa Katoliki walimweka kiti moto mwanasayansi aitwaye Galileo Galilei akanushe nadharia yake kwamba dunia inaizunguka jua. Mwanasayansi huyo alitii maagizo ya viongozi wake akaikana nadharia yake ingawaje wakati anatoka mlangoni alisema kuwa hata hivyo dunia ndiyo inayozunguka jua. Ni baada ya miaka 359, yaani mwaka 1992 kanisa liliomba msamaha na kukiri kuwa lilikosea kwa kungángánia kuwa jua linaizunguka dunia badala ya dunia kuizunguka jua.

Wapendwa Maaskofu, kuna mambo mengine mengi ndani ya Kanisa yenye ushahidi unaoonesha kuwa pale ambapo viongozi nao wameshiriki katika maovu, ama kwa kukaa kimya au kushirki kimatendo, viongozi wamepata ugumu katika kukemea maovu katika jamii. Kwa kuchukua mifano michache tu ya hivi karibuni, mwaka 1994 wakati yanatokea mauaji ya kimbali kule Rwanda, baadhi ya watu waliuawa wakiwa wamejihifadhi kanisani. Je, viongozi wa Kanisa hawakuwa na mchango katika kufanikisha mauaji? Je, viongozi walikuwa wapi kushindwa kukemea hilo? Kule Nigeria mwaka 2012 aliteuliwa Padre Peter Okpaleke, kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Ahiara lakini waamini na mapadre wa jimbo hilo walimkataa askofu mteule. Moja ya malalamiko ya waamini wa jimbo hilo ambalo linasemakana kuwa na mapdre zaidi ya 500, ni kuwa anakosekanaje padre mmoja anayefaa kuwa askofu miongoni mwa mapadre 500? Hata hivyo kulikuwa na hisia kuwa kuna upendeleo uliokuwa nyuma ya uteuzi ule, hasa shutuma nyingi zikielekezwa kwa Cardinal Arinze ambako anatoka katika eneo moja na Askofu Peter Okpaleke. Hatimaye huyo askofu alijiuzulu mwaka 2018 baada ya kukataliwa na kutambua mwenyewe kuwa mazingira ya kazi huenda yangekuwa magumu.
Wapendwa Maaskofu, kama shutuma za baadhi ya Watanzania wanaokinyooshea kidole serikali ya awamu tano kwamba inafanya upendeleo na ubaguzi kwa kutoa ajira nyeti kwa watu wa kanda ya ziwa ni kweli, je, maaskofu wetu mna uwezo wa kulitolea waraka jambo hilo? Nina mashaka kama mtaweza kwani wakati waraka wenu ulipoanza kujadiliwa maaskofu mlishutumiwa kuwa mlibeba ajenda ya upinzani hususani Chadema. Na kwa mbali ukitazama shutuma dhidi yenu ilikuwa kwamba ajenda mliyoibeba ilikuwa ya Kanda ya Kaskazini (hasa Kilimanjaro) kwani maaskofu waliotajwa kuwa waandaaji wa waraka wengi wanu mlikuwa na asili ya mkoa Kilimanjaro. Waliotajwa kuandaa waraka ni Askofu Mkuu wa Dodoma – Beatus Kinyaiya (mchaga), Askofu Mkuu wa Mwanza – Thaddeus Ruwaichi (mchaga) na Askofu wa Zanzibar – Augustino Shao (mchaga) na mmoja tu ambaye si mchaga katika kundi hilo la walioandaa waraka ni Askofu Severine Niwemugizi – wa Rulenge Ngara. Kwa kuangalia orodha hiyo utagundua kuwa, wakati wa kupinga ukanda na ukabila ninyi viongozi wetu hamtaweza kutuokoa. Hata ukiangalia orodha yenu katika baraza la maaskofu wa Tanzania utaona kuwa karibu moja ya tatu () ya maaskofu wote Tanzania wana asili ya Kilimanajaro. Tazama orodha ifuatayo yenye Maaskofu Wachaga: (i) Askofu mkuu Thaddeus Ruwaich Mwanza (ii) Askofu mkuu Beatus Kinyaiya –Dodoma (iii) Askofu mkuu Isack Masawe – Arusha (iv) Askofu Augustine Shao - Zanzibar (v) Askofu Ludovick Minde – Kahama (vi) Askofu Rogath Kimario - Same (vii) Askofu Joseph Mlola - Kigoma (viii) Askofu Msaidizi (Arusha) - Prosper Lyimo (ix) Askofu mteule Beatus Urassa – Sumbawanga (x) Msimamizi wa Jimbo Padre Deogratias Matika (Askofu mtarajiwa wa Jimbo la Moshi). Hali kadhalika katika mashirika ya kitawa yanayofanya kazi Tanzania viongozi wao wengi ni watu wenye asili ya Kilimanjaro. Mfano mashrika ya (i) Precious Blood (ii) Holy Ghost, (iii) OSS/ ALCP (iv) Mitume wa Yesu (v) Capuchin (vi) Jesuit nk.
Wapendwa Maaskofu, wengi wenu katika miaka ya 1960 hadi 1970 mlikuwa mnateuliwa katika maeneo yenu kama Sumbawanga, Mbulu, Kigoma, Mwanza, Shinyinga, Tabora nakadhalika. Inakuwaje wakati huo uinjilishaji ukiwa bado siyo wa kina waliweza kupatikana maaskofu katika maeneo yao, lakini leo Askofu anatokea Moshi anaenda Kigoma, Mwanza, Kahama, Sumbawanga? Lakini kinyume chake hakuna anayetoka Kigoma kuelekea Moshi. Hata Yesu alipoanzisha Kanisa aliwateua mitume wake pale Uyahudi siyo Moshi, ndipo baadaye kila mahali Injili ilipofika walipatikana Mitume katika maeneo yao. Ili kuwapotosha na kuwalaghai watu, mtaniambia kuwa karibu majimbo yote Tanzania yana maaskofu wanaotoka maeneo tofauti na maeneo yao ya asili. Umoja wa Kanisa tangu mwanzo ulikuwa katika imani na si katika hili la hadaa na ulaghai wa uteuzi wa maaskofu kutoka Kilimanjaro. Kama mnateua maaskofu kutoka Kilimanjaro kwenda Sumbawanga, kuna sababu gani kwenu ninyi kuwakataa Wahindi na Wazungu wanaofanya kazi za Kimisiaonari hapa Tanzania kuwa maaskofu kama ninyi? Dhambi ya ubaguzi na upendeleo haitawaacha salama. Mkiukataa uweli wangu leo, watakuja watakaogundua hata baada ya miaka 359 kama wenzenu walivyoukubali ukweli kuwa dunia ndiyo inayozunguka jua na siyo kinyume chake. Ni afadhali mkaziba ufa kuliko kujenga ukuta, na majuto ni mjukuu. Mwenye masikio ya kusikia na asikie na mwenye macho ya kuona aone. Mkaiishi Injili kama mlivyoipokea na kuihubiri na siyo vinginevyo.
Wapendwa maaskofu, maangamizo ya umoja wa kitaifa yatakuja kama tutayapuuzia mambo ambayo yanaonekana lakini tunajifanya hatuyaoni. Siku hiyo ya kuangamia kwa taifa kutakuja bila kubagua na ninyi ndio mtakaoulizwa kuwa mlinya nini katika kuzuia hili? Mimi nimenawa mikono kwa sababu nimewaambia. Msishawishike kuwa wajibu wenu unaishia katika kutoa Kipaimara na Upadre. Katika hili tunataka mshiriki kukemea ubaguzi na ukanda mkianzia kwenu wenyewe ili kuliepusha taifa letu kupata madhara yatakayofikia hata walio kondoo wenu na hata wasio kondoo wenu.
Wapendwa maaskofu, bila shaka wengi mtasema maaskofu wa Kanisa katoliki wanapatikana kwa utaratibu maalum na kwamba haya ninawaambia hayawahusu na pia kwamba waraka wangu huu unapandikiza ukabila. Waraka wangu hauleti ukabila bali unawaambia kuwa ukabila mmeupanda na sasa umeota, ila kataeni kuupalilia ili usije ukaiva. Nawaambia kuwa mtaukata ukweli na mtaniambia niukane ukweli wangu, lakini nawaambia ipo siku mtakubaliana na mimi kama ambavyo mlikubaliana na Galileo na mkaukubali ukweli wake baada ya miaka 359. Mimi siyo nabii lakini baada ya miaka kadhaa mtaamini kuwa Wanyarwanda hawakuanza chuki mwaka 1994, bali wapo waliopandikiza chuki, kuipalilia na kuiivisha na wakavuna matunda yake mwaka 1994 huku viongozi wa kanisa wakiwa wameshiriki katika hayo. Vivyo hivyo Kanisa Katoliki lina historia yake nzuri na chafu vile vile, mkubali tu mmefanya makosa na mnaendelea kuyafanya, basi tubuni na mrejee katika misingi ya haki na ukweli; na ukweli utawaweka huru. Kama taifa litafika mahali pabaya isiwe kwa mchango wenu, mnawe mikono yenu kama alivyofanya Pilato wakati wa kuuawa kwa Yesu.
Waraka wenu tuliupokea nanyi muupokee wa kwangu.

MZALENDO,
MPENDA TANZANIA
Hivi bado uko hai? Unaonaje huo ukabila wa kanda ya kaskazini, kule mlimani?
 
Back
Top Bottom