Swali hili naamini mtoa mada hawezi kujibu na ndio msingi wa hoja yake ya "ukabila" kanisani. Anazunguka bure na kutoa mifano mingi isiyokuwa na uhusiano na alicho nacho nafsini. Huyu mtu na wengine kama yeye ndio "wakabila" wakubwa na hivyo ni wa kupuuzwa kwani mchango wao hauna tija kwa taifa wala kwa kanisa.
Chanzo cha mtu huyu mwenye moyo wa ukabila uliomzidi na kumpagawisha niwasaidie tu kumwelewa na kuwaelewesha ni uteuzi uliofanywa hivi karibuni wa Fr. Dr. Beatus Urassa (mtawa) kwa Papa Francisco kumteua kuwa askofu mpya wa sumbawanga ambapo mhashamu askofu Damian Kyaruzi anamaliza mda wake (anastaafu).
Kwa vile mtoa mada ni "mkabila" tena aliyeiva kwelikweli yeye angetaka askofu mteule wa sumbawanga awe "mfipa" wa palepale na si kutoka nje. Na kuonesha wazi kuwa huyu mtu si mkabila tu bali pia ana chuki binafsi na baadhi ya makabila ametaja mwenyewe orodha ya mababa maaskofu toka kabila la wachaga na wengine amewateua yeye mwenyewe na kuwapa vyeo wasivyokuwa navyo (mf. kumuita Padri Deogratius Matika askofu), hii ndio tabia ya nongwa ya chuki, haifichiki.
Nimkumbushe mwandishi kuwa amechelewa sana na yuko nyuma ya wakati, haya anayoandika humu yanamdharirisha na kumfunua uchi wake mbele ya walimwengu tena mchana kweupe, au ulitaka uteuliwe wewe kuwa askofu wa sumbawanga, Mwanza, kahama, Kigoma na kwingineko?
Kanisa katoliki lilikwisha ondoka zamani huko uliko wewe na unakotaka kwenda, angalia maaskofu wote ktk Baraza na useme wangapi ni wazawa wa majimbo yao, Mimi ni muumini mlei wa jimbo katoliki shinyanga, askofu wetu mhashamu Liberatus Sangu (mfipa) na anatuongoza vzr sana mashallah...nenda DSM, mtwara, songea, bunda, musoma, karagwe, tabora na kwingineko kwingi tu maaskofu wao ni Watanzania sio lazima wa makabila yao bali kanisa moja, takatifu, katoliki, LA mitume. Na hata majimbo yanayoongozwa na wazawa, sio sifa ya uzawa iliyowafanya wateuliwa na Kanisa bali sifa stahiki za cheo hicho.
Kanisa la Tanzania linaadhimisha miaka 150 ya ukatoliki Tanganyika na miaka 155 ukatoliki visiwani Zanzibar mwaka huu 2018, itakuwa ajabu kanisa kongwe namna hii kuchukua mawazo ya kitoto na kishamba kama haya ya huyu mtoa mada hii akijijengea kichaka cha "moral authority" na kufichama ndani yake kumbe kasahau "kufunga zipu"
Namaliza: injili imeonya kuwa "dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu" ndiyo dhambi pekee isiyokuwa na msamaha mbinguni na duniani, kazi za utume ni kazi za Roho Mtakatifu mgawaji wa vipaji na mpangaji wa kazi za wokovu wa waamini (rejea liturujia ya daraja takatifu) kadiri ya imani katoliki. Kujaribu kukosoa, kuhoji au kukataa teuzi za watumishi wa Mungu ktk nafasi yoyote ile ni kuingilia kazi za Mungu Roho Mtakatifu aliye sawa na Mungu Baba na Mwana, ni kukufuru kusiko sameheka.
Kama mleta mada ni "mkatoliki" kweli, nimsihi afanye mambo mawili, ama arudie mafundisho na kuelewa vyema imani yake au atulie anyamae na kuachana na hii biashara yake ya udaku kwani kinyume na hapo aweza ishia kubaya. Mungu mkarimu atusaidie sote, amina.