Waraka kwa Maaskofu -Wakatoliki

Waraka kwa Maaskofu -Wakatoliki

Daudi Shoka

New Member
Joined
May 13, 2018
Posts
1
Reaction score
5
Waraka kwa Maaskofu -Wakatoliki
Wapendwa Maaskofu, miezi michache iliyopita kuliotokea hali ya kutofautiana kati ya viongozi wa kanisa Katoliki na serikali; vile vile kati yenu ninyi viongozi wa kanisa wenyewe kwa wenyewe kutokana na chapisho la Waraka ujulikanao kwa jina la “ujumbe wa Kwaresma” utolewao na kanisa Katoliki nchini Tanzania kila mwaka. Waraka huo wa mwaka huu ulikuwa na ujumbe uliikosoa serikali hasa katika suala ya kuminya demokrasia. Hali kadhalika kwa upande mwingine baadhi ya viongozi wa Kanisa kama Kardinali Pengo alitofautiana na maaskofu wenzake kwa kile alichosema kuwa waraka ulichanganya siasa na dini.

Wapendwa Maaskofu, ni jambo lilodhahiri kuwa ujumbe wenu kupitia waraka ule ulikuwa sehemu ya utume wenu wa kinabii. Kwa mujibu wa utume huo mnapaswa kukemea pale inapobidi na ndivyo ilivyokuwa kwa nyakati mbalimbali. Mifano ipo mingi ambapo viongozi wa Kanisa na baadhi ya waamini wa kawaida wakikemea maovu hata yaliyotendwa na viongozi wa dola ndiyo maana watu kama kina Thomas More waliuawa kule Uingereza katika karne ya 16. Baadaye Thomas More alitangazwa na kanisa kuwa Mtakatifu kwa msimamo wake wa kusimamia ukweli aliouamini na uliokuwa katika misingi ya Injli. Lakini jambo la kukumbuka ni kuwa viongozi wa Kanisa wanaotaka kukemea wengine wanatakiwa wawe na mamlaka ya kimaadili (moral authority), ili waweze kutekeleza jukumu hilo.

Wapendwa Maaskofu, mtakumbuka kuwa katika mitandao ya kijamii, moja ya mambo ambayo serikali ya awamu ya tano inalaumiwa na watu wengi ni pamoja kuwa na upendeleo katika ajira, hasa nafasi nyeti serikalini kwenda kwa watu wa kanda ya Ziwa. Sina uhakika na jambo hili kwa sasa, lakini kama lipo lisiendelee kuwepo na kama halipo lisije likafanyika kabisa. Athari ya ubaguzi na upendeleo litaligawa taifa na kuleta madhara makubwa sana. Ubaguzi unaweza kuanza kwa kuangaliana kwa kanda, baadaye kabila, koo na kadhalika. Ukweli ni kuwa hakuna mwisho mzuri wa jambo kama hilo. Nimesema kama kweli upo upendeleo wa kikanda, kama taifa tunapaswa kulitafutia suluhisho kabla hatujapata madhara. Je, katika hili Kanisa letu/lenu lipo salama?

Wapendwa Maaskofu, ili kupata suluhisho la tatizo la upendeleo na ubaguzi ni jukumu lenu viongozi wa Kanisa kushiriki na ninyi mnao wajibu huo ambao mnapaswa kuutekeleza kwa umakini mkubwa sana. Pamoja na kuwatwisha ninyi viongozi jukumu hilo nina mashaka kama mtalimudu jambo hilo. Mashaka yangu yanatokana na ukweli kuwa viongozi wangu mnanaanza kukosa mamlaka ya kimaadili. Historia ya Kanisa Katoliki inatukumbusha kuwa huko nyuma pamoja na kufanya mambo mazuri lakini kuna nyakati kanisa lilifanya makosa makubwa sana. Mwaka 1663 viongozi wa Kanisa Katoliki walimweka kiti moto mwanasayansi aitwaye Galileo Galilei akanushe nadharia yake kwamba dunia inaizunguka jua. Mwanasayansi huyo alitii maagizo ya viongozi wake akaikana nadharia yake ingawaje wakati anatoka mlangoni alisema kuwa hata hivyo dunia ndiyo inayozunguka jua. Ni baada ya miaka 359, yaani mwaka 1992 kanisa liliomba msamaha na kukiri kuwa lilikosea kwa kungángánia kuwa jua linaizunguka dunia badala ya dunia kuizunguka jua.

Wapendwa Maaskofu, kuna mambo mengine mengi ndani ya Kanisa yenye ushahidi unaoonesha kuwa pale ambapo viongozi nao wameshiriki katika maovu, ama kwa kukaa kimya au kushirki kimatendo, viongozi wamepata ugumu katika kukemea maovu katika jamii. Kwa kuchukua mifano michache tu ya hivi karibuni, mwaka 1994 wakati yanatokea mauaji ya kimbali kule Rwanda, baadhi ya watu waliuawa wakiwa wamejihifadhi kanisani. Je, viongozi wa Kanisa hawakuwa na mchango katika kufanikisha mauaji? Je, viongozi walikuwa wapi kushindwa kukemea hilo? Kule Nigeria mwaka 2012 aliteuliwa Padre Peter Okpaleke, kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Ahiara lakini waamini na mapadre wa jimbo hilo walimkataa askofu mteule. Moja ya malalamiko ya waamini wa jimbo hilo ambalo linasemakana kuwa na mapdre zaidi ya 500, ni kuwa anakosekanaje padre mmoja anayefaa kuwa askofu miongoni mwa mapadre 500? Hata hivyo kulikuwa na hisia kuwa kuna upendeleo uliokuwa nyuma ya uteuzi ule, hasa shutuma nyingi zikielekezwa kwa Cardinal Arinze ambako anatoka katika eneo moja na Askofu Peter Okpaleke. Hatimaye huyo askofu alijiuzulu mwaka 2018 baada ya kukataliwa na kutambua mwenyewe kuwa mazingira ya kazi huenda yangekuwa magumu.
Wapendwa Maaskofu, kama shutuma za baadhi ya Watanzania wanaokinyooshea kidole serikali ya awamu tano kwamba inafanya upendeleo na ubaguzi kwa kutoa ajira nyeti kwa watu wa kanda ya ziwa ni kweli, je, maaskofu wetu mna uwezo wa kulitolea waraka jambo hilo? Nina mashaka kama mtaweza kwani wakati waraka wenu ulipoanza kujadiliwa maaskofu mlishutumiwa kuwa mlibeba ajenda ya upinzani hususani Chadema. Na kwa mbali ukitazama shutuma dhidi yenu ilikuwa kwamba ajenda mliyoibeba ilikuwa ya Kanda ya Kaskazini (hasa Kilimanjaro) kwani maaskofu waliotajwa kuwa waandaaji wa waraka wengi wanu mlikuwa na asili ya mkoa Kilimanjaro. Waliotajwa kuandaa waraka ni Askofu Mkuu wa Dodoma – Beatus Kinyaiya (mchaga), Askofu Mkuu wa Mwanza – Thaddeus Ruwaichi (mchaga) na Askofu wa Zanzibar – Augustino Shao (mchaga) na mmoja tu ambaye si mchaga katika kundi hilo la walioandaa waraka ni Askofu Severine Niwemugizi – wa Rulenge Ngara. Kwa kuangalia orodha hiyo utagundua kuwa, wakati wa kupinga ukanda na ukabila ninyi viongozi wetu hamtaweza kutuokoa. Hata ukiangalia orodha yenu katika baraza la maaskofu wa Tanzania utaona kuwa karibu moja ya tatu () ya maaskofu wote Tanzania wana asili ya Kilimanajaro. Tazama orodha ifuatayo yenye Maaskofu Wachaga: (i) Askofu mkuu Thaddeus Ruwaich Mwanza (ii) Askofu mkuu Beatus Kinyaiya –Dodoma (iii) Askofu mkuu Isack Masawe – Arusha (iv) Askofu Augustine Shao - Zanzibar (v) Askofu Ludovick Minde – Kahama (vi) Askofu Rogath Kimario - Same (vii) Askofu Joseph Mlola - Kigoma (viii) Askofu Msaidizi (Arusha) - Prosper Lyimo (ix) Askofu mteule Beatus Urassa – Sumbawanga (x) Msimamizi wa Jimbo Padre Deogratias Matika (Askofu mtarajiwa wa Jimbo la Moshi). Hali kadhalika katika mashirika ya kitawa yanayofanya kazi Tanzania viongozi wao wengi ni watu wenye asili ya Kilimanjaro. Mfano mashrika ya (i) Precious Blood (ii) Holy Ghost, (iii) OSS/ ALCP (iv) Mitume wa Yesu (v) Capuchin (vi) Jesuit nk.
Wapendwa Maaskofu, wengi wenu katika miaka ya 1960 hadi 1970 mlikuwa mnateuliwa katika maeneo yenu kama Sumbawanga, Mbulu, Kigoma, Mwanza, Shinyinga, Tabora nakadhalika. Inakuwaje wakati huo uinjilishaji ukiwa bado siyo wa kina waliweza kupatikana maaskofu katika maeneo yao, lakini leo Askofu anatokea Moshi anaenda Kigoma, Mwanza, Kahama, Sumbawanga? Lakini kinyume chake hakuna anayetoka Kigoma kuelekea Moshi. Hata Yesu alipoanzisha Kanisa aliwateua mitume wake pale Uyahudi siyo Moshi, ndipo baadaye kila mahali Injili ilipofika walipatikana Mitume katika maeneo yao. Ili kuwapotosha na kuwalaghai watu, mtaniambia kuwa karibu majimbo yote Tanzania yana maaskofu wanaotoka maeneo tofauti na maeneo yao ya asili. Umoja wa Kanisa tangu mwanzo ulikuwa katika imani na si katika hili la hadaa na ulaghai wa uteuzi wa maaskofu kutoka Kilimanjaro. Kama mnateua maaskofu kutoka Kilimanjaro kwenda Sumbawanga, kuna sababu gani kwenu ninyi kuwakataa Wahindi na Wazungu wanaofanya kazi za Kimisiaonari hapa Tanzania kuwa maaskofu kama ninyi? Dhambi ya ubaguzi na upendeleo haitawaacha salama. Mkiukataa uweli wangu leo, watakuja watakaogundua hata baada ya miaka 359 kama wenzenu walivyoukubali ukweli kuwa dunia ndiyo inayozunguka jua na siyo kinyume chake. Ni afadhali mkaziba ufa kuliko kujenga ukuta, na majuto ni mjukuu. Mwenye masikio ya kusikia na asikie na mwenye macho ya kuona aone. Mkaiishi Injili kama mlivyoipokea na kuihubiri na siyo vinginevyo.
Wapendwa maaskofu, maangamizo ya umoja wa kitaifa yatakuja kama tutayapuuzia mambo ambayo yanaonekana lakini tunajifanya hatuyaoni. Siku hiyo ya kuangamia kwa taifa kutakuja bila kubagua na ninyi ndio mtakaoulizwa kuwa mlinya nini katika kuzuia hili? Mimi nimenawa mikono kwa sababu nimewaambia. Msishawishike kuwa wajibu wenu unaishia katika kutoa Kipaimara na Upadre. Katika hili tunataka mshiriki kukemea ubaguzi na ukanda mkianzia kwenu wenyewe ili kuliepusha taifa letu kupata madhara yatakayofikia hata walio kondoo wenu na hata wasio kondoo wenu.
Wapendwa maaskofu, bila shaka wengi mtasema maaskofu wa Kanisa katoliki wanapatikana kwa utaratibu maalum na kwamba haya ninawaambia hayawahusu na pia kwamba waraka wangu huu unapandikiza ukabila. Waraka wangu hauleti ukabila bali unawaambia kuwa ukabila mmeupanda na sasa umeota, ila kataeni kuupalilia ili usije ukaiva. Nawaambia kuwa mtaukata ukweli na mtaniambia niukane ukweli wangu, lakini nawaambia ipo siku mtakubaliana na mimi kama ambavyo mlikubaliana na Galileo na mkaukubali ukweli wake baada ya miaka 359. Mimi siyo nabii lakini baada ya miaka kadhaa mtaamini kuwa Wanyarwanda hawakuanza chuki mwaka 1994, bali wapo waliopandikiza chuki, kuipalilia na kuiivisha na wakavuna matunda yake mwaka 1994 huku viongozi wa kanisa wakiwa wameshiriki katika hayo. Vivyo hivyo Kanisa Katoliki lina historia yake nzuri na chafu vile vile, mkubali tu mmefanya makosa na mnaendelea kuyafanya, basi tubuni na mrejee katika misingi ya haki na ukweli; na ukweli utawaweka huru. Kama taifa litafika mahali pabaya isiwe kwa mchango wenu, mnawe mikono yenu kama alivyofanya Pilato wakati wa kuuawa kwa Yesu.
Waraka wenu tuliupokea nanyi muupokee wa kwangu.

MZALENDO,
MPENDA TANZANIA
 
Ngoja nitulie niusome. Hapa kuna mambo mazito sana.
 
Sawa!! Huu ni waraka wa waraka wa maaskofu wa katoliki ambao kwa mtazamo wako ulikuwa na chembechembe za uchadema na uchagga!! Umeelezea makosa yao ya miaka 359 iliyopita! Ila umeshindwa kuona kuwa content za waraka wao zinaelezea matukio halisi yaliyotokea ndani ya kipindi cha chini ya miaka mitatu tu iliyopita! Tukio halisi hutazamwa kiuhalisia bila kujali nani anayelitazama! Halihitaji sense of comparability! Kwa mfano chadema waliwahi kusema kuwa ndani ya ccm kuna mafisadi,ccm wakasema hapana! Baadaye ccm wakakiri kuwa kweli kuna ufisadi na wapo tayari kuushughulikia! Hapo main context ni Ufisadi(kitu kibaya) maana kwa hoja yako ya moral authority tukiichukulia serious itatubidi tuwatimue kazi majaji na mahakimu wengi mno kwa kutumia hilo rungu la moral authority!! Bado haujapima moral authority ya maaskofu wa kkkt? Fanya hivyo! Ukimaliza hayo nawewe ujipime moral authority yako juu ya wengine!
 
...Hata ukiangalia orodha yenu katika baraza la maaskofu wa Tanzania utaona kuwa karibu moja ya tatu () ya maaskofu wote Tanzania wana asili ya Kilimanajaro. ....Kama mnateua maaskofu kutoka Kilimanjaro kwenda Sumbawanga, kuna sababu gani kwenu ninyi kuwakataa Wahindi na Wazungu wanaofanya kazi za Kimisiaonari hapa Tanzania kuwa maaskofu kama ninyi?
Maaskofu wa Kikatoliki hawateuani, hoja yako imekufa hapo. Hakuna mjadala mpya tena
 
Sawa!! Huu ni waraka wa waraka wa maaskofu wa katoliki ambao kwa mtazamo wako ulikuwa na chembechembe za uchadema na uchagga!! Umeelezea makosa yao ya miaka 359 iliyopita! Ila umeshindwa kuona kuwa content za waraka wao zinaelezea matukio halisi yaliyotokea ndani ya kipindi cha chini ya miaka mitatu tu iliyopita! Tukio halisi hutazamwa kiuhalisia bila kujali nani anayelitazama! Halihitaji sense of comparability! Kwa mfano chadema waliwahi kusema kuwa ndani ya ccm kuna mafisadi,ccm wakasema hapana! Baadaye ccm wakakiri kuwa kweli kuna ufisadi na wapo tayari kuushughulikia! Hapo main context ni Ufisadi(kitu kibaya) maana kwa hoja yako ya moral authority tukiichukulia serious itatubidi tuwatimue kazi majaji na mahakimu wengi mno kwa kutumia hilo rungu la moral authority!! Bado haujapima moral authority ya maaskofu wa kkkt? Fanya hivyo! Ukimaliza hayo nawewe ujipime moral authority yako juu ya wengine!

Kwa nini wewe usimsaidie mwandishi kwenye hilo la Maaskofu wa KKKT? Mwandishi hakusema majaji watimuliewe ila wajisahihishe kama wana kasoro ambazo wao wenyewe wanataka kuwasahihisha wengine
 
usiwe mjinga wanateuana, usidhani Pope anawajua in person!!!!!
Unatakiwa ujibu kwa hoja, sio kwa matusi. Onyesha ni namna gani maaskofu wanahusika kumfanya Pope amteue padre kuwa askofu mwenzao. Tujifunze kujibu kwa hoja ili jukwaa liheshimike
 
Unatakiwa ujibu kwa hoja, sio kwa matusi. Onyesha ni namna gani maaskofu wanahusika kumfanya Pope amteue padre kuwa askofu mwenzao. Tujifunze kujibu kwa hoja ili jukwaa liheshimike

in systematic philosophy tunafundishwa kutojibu fallacy argument, mtoa mada ame commit a fallacy inaitwa "ignorantia elenchi" Pia kwa taarifa yako ujinga sio tusi ila upumbafu ndio!
 
Mbona sioni chanzo cha habari
Swali hili naamini mtoa mada hawezi kujibu na ndio msingi wa hoja yake ya "ukabila" kanisani. Anazunguka bure na kutoa mifano mingi isiyokuwa na uhusiano na alicho nacho nafsini. Huyu mtu na wengine kama yeye ndio "wakabila" wakubwa na hivyo ni wa kupuuzwa kwani mchango wao hauna tija kwa taifa wala kwa kanisa.

Chanzo cha mtu huyu mwenye moyo wa ukabila uliomzidi na kumpagawisha niwasaidie tu kumwelewa na kuwaelewesha ni uteuzi uliofanywa hivi karibuni wa Fr. Dr. Beatus Urassa (mtawa) kwa Papa Francisco kumteua kuwa askofu mpya wa sumbawanga ambapo mhashamu askofu Damian Kyaruzi anamaliza mda wake (anastaafu).

Kwa vile mtoa mada ni "mkabila" tena aliyeiva kwelikweli yeye angetaka askofu mteule wa sumbawanga awe "mfipa" wa palepale na si kutoka nje. Na kuonesha wazi kuwa huyu mtu si mkabila tu bali pia ana chuki binafsi na baadhi ya makabila ametaja mwenyewe orodha ya mababa maaskofu toka kabila la wachaga na wengine amewateua yeye mwenyewe na kuwapa vyeo wasivyokuwa navyo (mf. kumuita Padri Deogratius Matika askofu), hii ndio tabia ya nongwa ya chuki, haifichiki.

Nimkumbushe mwandishi kuwa amechelewa sana na yuko nyuma ya wakati, haya anayoandika humu yanamdharirisha na kumfunua uchi wake mbele ya walimwengu tena mchana kweupe, au ulitaka uteuliwe wewe kuwa askofu wa sumbawanga, Mwanza, kahama, Kigoma na kwingineko?

Kanisa katoliki lilikwisha ondoka zamani huko uliko wewe na unakotaka kwenda, angalia maaskofu wote ktk Baraza na useme wangapi ni wazawa wa majimbo yao, Mimi ni muumini mlei wa jimbo katoliki shinyanga, askofu wetu mhashamu Liberatus Sangu (mfipa) na anatuongoza vzr sana mashallah...nenda DSM, mtwara, songea, bunda, musoma, karagwe, tabora na kwingineko kwingi tu maaskofu wao ni Watanzania sio lazima wa makabila yao bali kanisa moja, takatifu, katoliki, LA mitume. Na hata majimbo yanayoongozwa na wazawa, sio sifa ya uzawa iliyowafanya wateuliwa na Kanisa bali sifa stahiki za cheo hicho.

Kanisa la Tanzania linaadhimisha miaka 150 ya ukatoliki Tanganyika na miaka 155 ukatoliki visiwani Zanzibar mwaka huu 2018, itakuwa ajabu kanisa kongwe namna hii kuchukua mawazo ya kitoto na kishamba kama haya ya huyu mtoa mada hii akijijengea kichaka cha "moral authority" na kufichama ndani yake kumbe kasahau "kufunga zipu"

Namaliza: injili imeonya kuwa "dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu" ndiyo dhambi pekee isiyokuwa na msamaha mbinguni na duniani, kazi za utume ni kazi za Roho Mtakatifu mgawaji wa vipaji na mpangaji wa kazi za wokovu wa waamini (rejea liturujia ya daraja takatifu) kadiri ya imani katoliki. Kujaribu kukosoa, kuhoji au kukataa teuzi za watumishi wa Mungu ktk nafasi yoyote ile ni kuingilia kazi za Mungu Roho Mtakatifu aliye sawa na Mungu Baba na Mwana, ni kukufuru kusiko sameheka.

Kama mleta mada ni "mkatoliki" kweli, nimsihi afanye mambo mawili, ama arudie mafundisho na kuelewa vyema imani yake au atulie anyamae na kuachana na hii biashara yake ya udaku kwani kinyume na hapo aweza ishia kubaya. Mungu mkarimu atusaidie sote, amina.
 
Ni kweli mleta mada ni mkabila, ila suala ambalo hulitambui ni kuwa mtu hatakuwa mkabila kwa sababu anaitwa hivyo. Na mtu hawezi kuitwa kwamba siyo mkabila kwa sababu hataitwa hivyo. Hata madikteta duniani kitu cha kwanza ambacho walikifanya ni kuhakikisha hakuna watu watakaowaita wao kuwa ni madikteta. Kama mleta mada ni mkabila ukweli utajulikana tu, na kama siyo hivyo basi hilo nalo litajulikana pia
 
Kwa vile mtoa mada ni "mkabila" tena aliyeiva kwelikweli yeye angetaka askofu mteule wa sumbawanga awe "mfipa" wa palepale na si kutoka nje. Na kuonesha wazi kuwa huyu mtu si mkabila tu bali pia ana chuki binafsi na baadhi ya makabila ametaja mwenyewe orodha ya mababa maaskofu toka kabila la wachaga na wengine amewateua yeye mwenyewe na kuwapa vyeo wasivyokuwa navyo (mf. kumuita Padri Deogratius Matika askofu), hii ndio tabia ya nongwa ya chuki, haifichiki

Basi mwache huyo mwandishi na chuki yake na wewe uepuke kuwa na chuki. Katika andishi hakuna mahali Matika alipotajwa kuwa askofu, ila "askofu mtarajiwa". Usitumie hoja dhaifu kujibu hoja dhaifu.
 
Ni kweli mleta mada ni mkabila, ila suala ambalo hulitambui ni kuwa mtu hatakuwa mkabila kwa sababu anaitwa hivyo. Na mtu hawezi kuitwa kwamba siyo mkabila kwa sababu hataitwa hivyo. Hata madikteta duniani kitu cha kwanza ambacho walikifanya ni kuhakikisha hakuna watu watakaowaita wao kuwa ni madikteta. Kama mleta mada ni mkabila ukweli utajulikana tu, na kama siyo hivyo basi hilo nalo litajulikana pia
Bali matendo yake na maneno yake ndiyo yatamweka kundi sahihi, kama mkabila tutamtambua kwa maneno na matendo yake kama tulivyomtambua mtoa mada.
 
Basi mwache huyo mwandishi na chuki yake na wewe uepuke kuwa na chuki. Katika andishi hakuna mahali Matika alipotajwa kuwa askofu, ila "askofu mtarajiwa". Usitumie hoja dhaifu kujibu hoja dhaifu.
Napokea rekebisho hilo mkuu na nakubaliana na wewe kabisa maana hata hiyo nafasi ya "askofu mtarajiwa" haipo ktk kanisa, hivyo mtoa mada aliiweka/aliipachika kutaka kuishibisha kiu yake na nia yake "ovu"
 
Back
Top Bottom