Wapinzani wata 'seize the moment'?

Wapinzani wata 'seize the moment'?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,675
Shida moja kubwa ya upinzani Tanzania ni kutojua kipi wanataka kwanza.

Kwa mtu mwenye akili kitu cha kwanza kabisa Kwa wapinzani ni Tume huru ya uchaguzi...na wala sio serikali tatu.

Tume huru ndo itawapa nafasi ya kuongoza na kubadili chochote wanachotaka..lakini Kwa wanaokumbuka Ule mchakato wa Katiba Mpya... wapinzani walitoka na kususa Kwa kipengele kimoja Tu cha serikali tatu. Hawakutaka hata kujadili kipengele cha Tume huru ya uchaguzi.....ambacho ndo muhimu kuliko vyote.

Binafsi naamini chini ya Samia kunaweza tokea 'New opportunity' ya kufanya marekebisho ya katiba au hata Katiba Mpya.

Kihistoria Viongozi wanaotoka Pwani na Visiwani huwa wanaacha Uhuru wa kisiasa. Na hata mawazo mapya ya Katiba Mpya hupewa nafasi ..... swali kuu hapa wapinzani wataweza kutumia nafasi na kukumbuka kipi cha muhimu zaidi kwao?

Au itajirudia Yale yale?
 
Opportunity ya katiba mpya chini ya Mh Rais madame Samia Hassan Suluhu, siyo suala la kuupuzwa. Naunga mkono hoja hii!
 
CCM hawawezi kukubali tume huru hata siku moja,na siku ya kukubali ndiyo itakuwa mwanzo wa mwisho was CCM.

Halafu tume huru ni niini?ukiwauliza wapinzani watakuambia mwenyekiti na makamishna wasiteuliwe na rais wakati watendaji wa tume na wakurugenzi ndiyo mainjinia wa kuiba kura au kuvuruga uchaguzi.

Pia Kitengo kinaingilia sana uchaguzi,wakoloni waliunda kitengo ili kilinde maslahi ya ukoloni,Sasa hivi kitengo kinailinda CCM isidondoke.
Pia vyombo vingine havitendi haki mfano TBC walikuwa wanatangaza mikutano ya JPM wengine walikuwa hawatangazi,walitangaza ya upinzani ya DSM pekee na walikuwa Wana kata kata matangazo.

Polisi vile vile inafikia hatua polisi anamwambia Mbowe hatashinda ubunge!

Kwahiyo tume huru pekee haitoshi na wala haina faida kinachotakiwa ni mfumo mzima ubadilike.
 
Hivi The Boss wewe ni mgeni nchi hii?

Unakosea Sana na unawakosea Sana wapinzani unaposema hawajui lipi wanataka Kwanza?

Wapinzani wanafanya kazi kubwa Sana,hata hiyo ajenda ya Katiba mpya wait ndio waanzilishi,wao ndio walishinikiza mara tu baada ya uchaguzi wa 2010 pale Dk Slaa alipolalamika kuibiwa ushindi na Kikwete.

Shinikizo lao kubwa lilikua Ni kutaka katiba mpya,walipiga Presha Hadi Kikwete akaongia hofu,akaruhusu mchakato was katiba, katiba ikaandikwa.

CCM wakashituka wakaona katiba mpya itawaondoa madarakani,Mkapa akamtisha Kikwete,wakavuruga utaratibu was bunge la katiba,wapinzani wakakasirika wakaona wanachezewa karata tatu wakasusa.

Unamkumbuka Samweli sita,na mahafidhina wengine ndani ya CCM wakaanza maneno ya vitisho oo Mara nitaingia msituni oo Mara nini,Mara warioba kapigwa ,Kila kitu kikavurugika.

Unawaonea bure wapinzani.

CCM hawana dhamira ya dhati juu ya Katiba.

Ok kwa Nini swala la katiba like Ni kuibembeleza CCam ama kuilazimimisha kwa vitisho?

Kwani was tu ndio hawaoni umuhimu wa katiba mpya?

Halafu Nani aliyekuambia swala la katiba mpya Ni la wapinzani tu? na sio la Kila mtanzania? Hata wanaCCM wenyewe?
Kwa Nini unawalaumu wapinzani tu?
Kwa Nini usiwalaumu
Wanasheria
Wafanyakazi
Wafanyabiashara
Wakulima
Vijana
Wazee
Wanajeshi
Mapolisi
Wabungewote
Viongozi was dini
Wanamichezo
Kwa ujumla wananchi wote?
Wapinzani wanakutana na vikwazo vingi Sana ikiwa na kupigwa risasi mabomu na vifungo.
Mtu mmoja tu Tanzania mwenye nguvu alisema yeye Katiba sio kipaumbele chake.Huyo Ni mwenyekiti wa chama tawala na Amiri jeshi was majeshi yoooote ya nchi hii.Mtamfanya Nini.
"Ingieni barabarani basi kama Kama mna ubavu",hayo ndio majigambo ya mtu huyo mmoja.
Kwa kumalizia ajenda ya Katiba na tume huru Ni ya wapinzani,lakini Nani ataruhusu?
Unamjua Jiwe wewe?
Tunawaonea bure wapinzani kazi wanayofanya Ni ya hatari Sana.
 
Halafu usitegemee kabisa Samia atabadili chochote juu ya kilio Cha katiba mpya ama tume huru.

Kwa sababu vitu hivi ni sumu Kali kwa CCM, ni kitanzi.

Alishindwa Kikwete kuleta katiba mpya amabayo ndani yake Kuna tume huru,hakuna mwanaCCM mwingine atakaa alete.

Kila Rais Kutokea CCm huwa anaogopa kukabidhi nchi kwa wapinzani,Yuko radhi kuua maelfu ya watu ilimradi asikabidhi nchi kwa wapinzani.

Nadhani uliona mwenyewe uchaguzi wa 2015 na 2020.
 
Hamna lolote ndugu.
Kikwete alikua Ana nia ya kuleta katiba mpya,CCM walimuonya na kumtisha.
Samia Nani ndugu.?
Akileta za kuleta atakolimbwa.
CCM sio watu aisee.waone hivyohivyo tu mchana,usiku Ni viumbe wengine na hatari Kabisa .
Muache Chura kwenye karai ajifanye kutulia sisi tunachochea kuni Maji yakianza kuchemka mwenyewe atajirusha nje
 
Opportunity ya katiba mpya chini ya Mh Rais madame Samia Hassan Suluhu, siyo suala la kuupuzwa. Naunga mkono hoja hii!
Samia Suluhu alikuwa Makamu Mwenyekiti wa bunge la Katiba chini ya Samuel Sitta , ni miongoni mwa waliohujumu mchakato ule waziwazi ( ninao ushahidi ) , sijui imekuaje akaaminika sasa ?

Katiba Mpya haiwezi kuletwa na mwanaccm yeyote yule kwa sababu zozote zile , tuendelee kupambana ili kuhakikisha Katiba inapatikana watake wasitake .
 
Misimamo ya hayati Magufuli(Tutaonana baadaye) haiwezi kubadilika. Wale waliofaidika nayo hawawezi kubali na mbaya ni kuwa waliofaidika nayo ni wenye nguvu sana, CCM.
 
Shida moja kubwa ya upinzani Tanzania ni kutojua kipi wanataka kwanza...
Ccm tuna sauti kubwa bungeni, hakuna kambi rasmi ya upinzani bungeni, yaani unategemea hoja mfu kama hiyo itapita? ??? Thubutu.
By the way katiba ya sasa ni bora kuliko katiba zote Africa na baadhi ya nchi za ulaya.

Tungekuwa na katiba isiyokidhi sasa hivi tungekuwa tunahangaika kumpata mkuu wa nchi. Lakini kwa katiba hii mnayoilaumu ndiyo imeruwezesha kuwa na rais ndani ya saa 72 tangu kufariki kwa Jemedali Magufuli.

Ndani ya siku 21 tunatarajia kuwa na makamu wa Rais.Hatuwezi kubadili katiba sababu ya uchaguzi tu.ibara inayohusu uchaguzi iko sawa na ndiyo iliyowapa ushindi 38% ya ushindi 2015.Safari hii mliyataka wenyewe mmeadhibiwa kwa makosa yenu
 
Atawashangaza mama yule. Mtajua Hamjui yajayo sio mepesi
Wewe elewa tu kwamba kuanzia mwezi ujao full neema pesa itaanza kuonekana mitaani...kwasasa fedha iliyotambaa ni ya mazishi tu...Mambo ya katiba mpya , kuendeleza miesijiara au mistegolaz watajijua wao wenyewe,sisi tunataka mzunguko wa pesa kitaa tu basi.
 
Ccm tuna sauti kubwa bungeni, hakuna kambi rasmi ya upinzani bungeni, yaani unategemea hoja mfu kama hiyo itapita? ??? Thubutu.
By the way katiba ya sasa ni bora kuliko katiba zote Africa na baadhi ya nchi za ulaya.Tungekuwa na katiba isiyokidhi sasa hivi tungekuwa tunahangaika kumpata mkuu wa nchi. Lakini kwa katiba hii mnayoilaumu ndiyo imeruwezesha kuwa na rais ndani ya saa 72 tangu kufariki kwa Jemedali Magufuli. Ndani ya siku 21 tunatarajia kuwa na makamu wa Rais.Hatuwezi kubadili katiba sababu ya uchaguzi tu.ibara inayohusu uchaguzi iko sawa na ndiyo iliyowapa ushindi 38% ya ushindi 2015.Safari hii mliyataka wenyewe mmeadhibiwa kwa makosa yenu
Hivi kweli huwa mnayaamini haya mnayoyaandika?

Katiba ya Tz ni katiba bora kuliko zote Africa. Seriously....Either you have no idea what you are talking about au umeamua kudanganya wazi wazi.

We have one of the worst constitution. Hakuna anything redeeming about it. Katiba ambayo inayonyima haki za RAIA na kuruhusu utawala wakiimla siyo katiba ya kuifurahia hata kidogo.
 
Back
Top Bottom