Wapinzani wamemu-indorse JK? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapinzani wamemu-indorse JK?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlalahoi, Mar 1, 2010.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,067
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Wakati tumebakiwa na takriban miezi 6 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais na wabunge,vyama vya upinzani vimeendelea kuwa kimya kuhusu wagombea wao katika nafasi ya urais huku baadhi ya viongozi na wanachama wake wakiwa bize zaidi kuonyesha dhamira zao kuhusu majimbo ya ubunge watakayogombea.Japo natambua taratibu za kidemokrasia katika vyama hivyo zinavypaswa kufanya kazi katika kupata mgombea urais,napatwa na wasiwasi kwamba muda uliobaki unaonekana ni mchache sana kwa yeyote atakayeteuliwa na vyama hivyo kupambana kifanisi na mgombea wa chama tawala ambaye,unless kutokee miujiza,atakuwa rais wa sasa Jakaya Kikwete.

  Waingereza wana msemo poor planning produces poor performance.Pamoja na kuheshimu taratibu zinazotawala vyama vya upinzani,ni dhahiri kwamba kusuasua kwao kuonyesha angalau dhamira ya kusimamisha mgombea urais kwenye uchaguzi ujao ni mithili ya kumu-endorse mgombea wa CCM hata kama hawajatamka hivyo.Licha ya "home advantage" ya kuwa chama kilichopo madarakani,CCM inajivunia utajiri wa resources katika kumnadi mgombea wake kwa wapiga kura.

  Wakati element of surprise inaweza kuwa na ufanisi kwenye mapambano ya kivita,sidhani kama mkakati wa aina hiyo unaweza kuwanufaisha wapinzani katika mazingira ya siasa za Afrika,na hususan Tanzania.Ni muhimu kukumbuka nafasi ya haiba ya mgombea katika siasa zetu,hata kama hilo ni miongoni mwa mapungufu yetu.Kufahamika kwa wenye dhamira ya kugombea urais kunawasaidia sana wapiga kura linapokuja suala kama "sasa kama sio JK,ni nani basi?"Wengi tumekuwa mahiri katika kuonyesha kuwa JK ameshindwa kazi.Lakini tunajikuta njia panda linapokuja suala la kutaja kwa hakika nani anayeweza kufanya vizuri zaidi yake.Sanasana tunaishia kubashiri majina flani flani.Na hatupaswi kulaumiwa kwa hilo kwa vile hadi sasa wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wanaonekana kama "wanakwepa umande" kutangaza dhamira yao ya kumrithi JK.

  Tunaweza kuendelea kuilaumu CCM na kuonyesha kila baya ililofanya.Lakini pasipo kuwapo chaguo mbadala,lawama hizo zitaendelea kubaki sehemu tu ya wasifu mbovu wa chama hicho tawala.At the end of the day,kitaibuka kidedea na sie tutabaki kujilaumu.

  Hii ni failure ya waziwazi ya vyama vya upinzani.Vinafahamu fika kwamba wakati CCM ina mtandao mkubwa (licha ya ule binafsi ulomwingiza JK madarakani),vyenyewe vinalazimika kutegemea kura za wana-CCM walio disaffected na mwenendo wa chama hicho tawala,sambamba na kura za Watanzania wanaotaka maendeleo regardless ya chama gani kitakachowaongoza kufikia maendeleo hayo.Mtaji wa wanachama kwa vyama vya upinzani ni hafifu sana.Na hata kama recruitment drive ya kupata wanachama wengi ingekuwa na mafanikio,chaguzi nyingi duniani zimeonyesha kuwa uchaguzi wa rais ni suala la wananchi (regardless of their political affiliation) zaidi kuliko wanachama.

  Kwanini basi akina Dkt Slaa wasijifunze namna Obama alivyoweza,against all odds,kuweka historia ya kuwa mweusi wa kwanza kushinda urais wa Marekani?Na katika hilo,wanaweza pia kujifunza namna Wamarekani waliopotezwa matumaini na conservative politics (including baadhi ya wafuasi wa Republican Party) walivyokuwa mtaji muhimu kwa ushindi wa chama cha Democratic?Slaa na wana upinzani wenzake wanatambua wazi kuwa Watanzania wengi wamechoshwa kuona nchi yao ikiendelea kuwa chuo cha mafunzo ya ufisadi au "shamba la bibi".Wanafahamu pia kuwa kuna idadi kubwa tu ya wana-CCM wanaoweza kumsapoti mgombea atakayewapa matumaini ya kweli ya kuwaletea "uhuru wa pili baada ya ule wa mwaka 1961".Kadhalika,wanambua kuwa kazi ya kuiondoa madarakani CCM inahitaji zaidi ya kampeni za majukwaani,and for that matter,kunahitajika muda wa kutosha wa kumnadi mgombea wanayetaka atoe upinzani thabiti dhidi ya CCM.

  Swali linabaki: kwanini wameendelea kuwa kimya kana kwamba uchaguzi ujao ni wa wabunge pekee kwa vile "wameshakubali matokeo kwamba mgombea wa CCM lazima atashinda,piga ua"?
   
 2. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2010
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wapinzani gani ambao wewe unazungumzia? CHADEMA na CUF wote wameshatangaza kuwa wanasimamisha wagombea Urais. Tarehe zao za kuchukua na kurudisha fomu bado, vipi uanze kuwahukumu?

  Asha
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Ndugu yangu Mlalahoi kwani tofauti ni nini hasa? acha kupasua kichwa bro!

  Respect.


  FMEs!
   
 4. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,067
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Asha,nadhani umesoma vizuri post yangu na kuielewa.Tatizo sio kutangaza dhamira ya kugombea kwa vile wapigakura hawapigii kura dhamira,na wala sio tatizo sio tarehe ya kuchukua fomu kwa vile,kwanza si kila mchukua fomu atarudisha,na pili,voters hawapigii kura tarehe ya kuchukua na kurudisha fomu.Atakayepigiwa kura ni mwana-Chadema au Cuf,au mwanaupinzani mwingine, atakayepitishwa na chama chake kuchuana na mgombea wa CCM.

  Na hudhani kwamba kwa vyama hivyo kushindwa kutangaza angalau tarehe za kuchukua na kurejesha fomu za kugombea urais,LESS THAN 7 MONTHS kabla ya uchaguzi mkuu,ni sehemu ya mapungufu nayozungumzia?

  By the way,Asha,kuvikumbusha vyama vya upinzani umuhimu wa mikakati katika ushindi kwenye chaguzi sio kuvihukumu.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...