Wapinzani wafanye nini ili kuing'oa CCM?

Umeona huyu jamaa anavyojitoa ufahamu makusudi !! Eti aliitwa fisadi sababu ya kuvunja mkataba wa City water Na Dawasa!! Utakuta hawa ndio strategists wa huo upinzani.
 
Mkuu nia ya vyama vingi ni nzuri tu, lakini kama unavyoijua Afrika tuna asili ya ubinafsi sana. Hili haliwahusu CCM na Chadema tu,angalia karibu nchi nyingi za Africa vyama tawala na vya upinzani vingi vinagombania Ikulu sio kwasababu vina uchungu na wananchi, ni kwasababu vinapigania maslahi yao tu. Kenya iliondolewa KANU watu wakadhani ndo unafuu wa maisha utakuwepo, ila ikawa kinyume chake. Ufisadi ukaongezeka mara tano. Inaongoza kwa kuwa na SLAMS nyingi Africa.(google biggest slams in Africa), ukiacha Kenya nipe mfano wa nchi za Africa ambapo vyama tawala viliangushwa, vikaingia vipya kukawa na mabadiliko makubwa??, vyama vingi vya upinzani vina hasira ya kuingia madarakani nao wale(ZAMU YETU). Basi, hivi unaamini kabisa kabisa mtu kama Lowassa akizungukwa na masela wake akina Rostam Azizi, Kalamagi na genge lao la wanyang'anyi lilikuwa na machungu ya kuwaletea watanzania maendeleo??., hebu acheni utani bwana.
 
Hapa ndio wapinzani mliopokosea.Lowasa aliitwa Fisadi kwa kuwa na maslahi binafsi dhidi ya kampuni ya kufua Umeme ya Richmond.
Wakati List of Shame inatangazwa Richmond ilikuwa bado kutokea!

Leta uzushi mwingine!!
 
Yaani mnaota kuing'oa CCM!!? Hamtaweza sasa hivi inaimarika sana. Mawazo ya kitoto hayo.
 
Broo Hivi unategemea ccm na nccr na kina dovutwa wakupe ushauri gani?? Kuna mambo matatu ya kufanya kwa sasa japo yapo mengi ila haya ndo tuanze nayo
1) tumekosa katiba mpya basi mwenyekiti wa NEC asiteuliwe na mwenyekiti WA ccm
2)kwa Tanzania cjaona umuhimu WA kuwa na vya vya siasa vingi kwa sasa tuna vyama 20+ ambavyo vingine tunaonaga kwenye karatasi za kupigia kura..so futa angalau vibaki vitatu Tu.
3) kura zote zihesabiwe na kutangaziwa kituoni na NEC watangaze matokeo ya kila kituo hata kama tuna vituo milioni..kwani kazi Yao ndo hiyo...tukifanikiwa hivi nahisi hata kelele za wizi WA kura zitapungua
 
Hoja za kichovu hizi! Eti watanzania kwa ujumla wanahitaji maendeleo, basi! Hizi ndizo blah blah mlizolishwa na kutaka kupumbaza watu. Kuna uhusiano mkubwa wa maendeleo ya nchi na sera za chama kinachoongoza nchi kwa wakati husika. Ni mtu mjinga pekee atakayeendelea kung'ang'ana na Lowasa kwa hoja ya ufisadi ilihali mambo yote yaliishawekwa wazi kwamba hiyo ilikuwa ni vita ya madaraka ndani ya CCM.

Kwanini usijiulize swali dogo tu. Hivi Lowasa ana kinga gani kiasi kwamba kama alihusika na huo ufisadi asifikishwe kortni tangu mwaka 2008? Tena kwa siasa hizi za chuki, leo Lowasa angekuwa uraiani? Na kama hoja ni ufisadi, hawa akina Chenge, Ngeleja, Karamagi; na the like ambao wamejazana CCM mnawazungumziaje? Hakuna mtu mwenye mawaa atakayeondoka CCM kwenda upinzani, hifadhi ya mafisadi iko CCM,
 
Si wanajitoa ufahamu, eti huo kwao sio ufisadi kwa kuwa unafanywa na malaika wao!!
 
Hongera kumbe wewe ndio msimamizi mkuu, wa kujua kila kinachofanyika!!
 
Tutashinda endapo CcM wataacha kutuibia kura
 
Andika maneno machache lakini yenye point. Hapo umeandika maneno mengi lakini pointless
 
Tatizo tunadanganyana. Watakaoitoa ccm madarakani sio wapinzani. Ni watanzania.

Watanzania wakiamua hakuna atakayeweza kuzuia. Kwa sasa watanzania hawajawa tayari kuitoa ccm maana kizazi kilichounda TANU bado kipo. Kikishapita kazi itakua rahisi sana. Kikubwa ni kuwa na subira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…