BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Posted Date::10/27/2007
Wapinzani waeleza kilichomkosesha Mkapa tuzo ya uongozi Afrika
Na Kizitto Noya
Mwananchi
VYAMA vya CUF, TLP na Chadema, vimeeleza sababu ya rais Mstaafu Benjamin Mkapa kushindwa kupata tuzo ya rais bora barani Afrika kuwa ni kukithiri kwa vitendo vya rushwa, ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu katika kipindi cha utawala wake.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti viongozi wa vyama hivyo walisema vitu hivyo vitatu ndivyo vilivyofanya rais Mkapa ashindwe kupata tuzo hiyo na badala yake ikachukuliwa na rais Mstaafu wa Msumbiji Joaqim Chissano.
Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa Chama Cha Wananchi (CUF) Salim Bimani alisema kuwa mauaji ya MwembeChai mwaka 1998, Bulyankulu mwaka 1999 na mauaji ya Zanzibar ya Januari 26 na 27 mwaka 2001, ni baadhi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyomtia doa rais Mkapa katika utawala wake.
Alisema pamoja na mambo mengine Mkapa amehusika kuvunja haki za binadamu kwa kushindwa kutekeleza ahadi yake ya kuwalipa fidia waathirika wa mauaji ya Zanzibar baada ya Tume ya Hashim Mbita iliyoundwa kuchunguza mauaji hayo kuwasilisha mapendekezo yake serikalini.
"Hili ni doa kwani baada ya Tume hiyo kumaliza kazi ilipendekeza kuwa Serikali iwalipe fidia waathirika wa mauaji ya Zanzibar na rais (Mkapa) alikubali lakini hakutekeleza," alisema Bimani.
Alisema Mkapa pia alishindwa kujenga demokrasia ya mfumo wa vyama vingi kwa kusikiliza ushauri wa wapinzani tofauti na rais Chissano ambaye alimshirikisha mpinzani wake wa Chama cha RENAMO katika kutatua mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Kwa mujibu wa Bimani doa jingine lililoifanya Tanzania ikose tuzo hiyo ni kushindwa kwa serikali ya awamu ya tatu kumaliza mgogoro wa kisiasa Zanzibar tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.
Alisema tofauti na Msumbiji ambako rais Chissano alitumia mfumo wa vyama vingi kukuza demokrasia, Mkapa alitumia mfumo huo kuleta vurugu ambapo kwa mara ya kwanza nchi ilitengeneza wakimbizi 45 mwaka 2001 baada ya mauaji ya Zanzibar.
"Hakuna mtu anaweza kusahau kwamba wakati wa Mkapa ndio kwa mara ya kwanza Tanzania ilianza kutengeneza wakimbizi. Mkapa alishindwa kulinda amani na utulivu alivyorithi kutoka kwa watangulizi wake, Mwalimu Julius Nyerere na Ali Hassan Mwinyi," alisema.
Kwa mujibu wa Bimani, Rais Chissano wa Msumbiji amestahili kupata nishani hiyo kwani aliweza kuitoa nchi ya Msumbiji katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuileta katika demokrasia ya kweli.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe alisema Mkapa hakustahili kupata tuzo hiyo kwa kuwa alitumia nafasi yake kama rais kuzorotesha upinzani.
Alisema katika kipindi chake, upinzani ulizorota kwa kiasi kikubwa kutokana na rais Mkapa kuudhibiti kwa nguvu ya dola hata katika mambo ambaye upinzani ulifanya kwa manufaa ya taifa.
"Alitumia nguvu kuzuia maandamano ya Zanzibar na kusababisha vifo na wakimbizi. Pia alishindwa kudumisha uhuru wa vyama vya upinzani kuikosoa serikali,"alisema Kabwe.
Alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiongozwa na rais Mstaafu Benjamini Mkapa pia kiliuzoofisha upinzani kwa kununua wagombea badala ya kuujengea uwezo wa kudumu ili utoe changamoto za kiutendaji kwa serikali yake.
Kwa mujibu wa Kabwe Mkapa na Chissano walitofautiana kwa mambo mengi hasa katika dhamira ya kweli ya kujenga nchi mambo ambayo wadhamini wa shindano la kumpata rais bora Afrika walilizingatia.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema alisema kuwa serikali ya awamu ya tatu chini ya rais Benjamini Mkapa ilipalilia rushwa na ufisadi kwa kutoa madaraka kwa watu wasiokuwa waadilifu na kuwalinda.
Alisema tatizo hilo pamoja na tuhuma za hivi karibuni kwamba Mkapa alifanya Ikulu sehemu ya biashara, ni doa ambalo sio tu limechangia katika yeye kushindwa kuteuliwa kupata nishati ya rais Bora bali pia kustahili kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
"Unapozungumzia ufisadi unamtaja Mkapa kwa sababu ndiye aliyewateua mafisadi na kuwabeba katika utawala wake" alisema Mrema.
Alisema Tanzania haikuwa na sababu ya kuikosa tuzo hiyo kwani historia yake imejengwa katika misingi ya uadilifu lakini uongozi wa rais Mkapa umeibadilisha historia hiyo.
Kwa mujibu wa Mrema kitendo cha Tanzania kukosa tuzo hiyo ni changamoto kwa utawala wa awamu ya nne chini ya rais Jakaya Kikwete ambaye sasa anatakiwa kufanya kazi ya ziada kurudisha heshima ya nchi machoni pa Jumuiya za Kimataifa.
"Kikwete anapaswa kusikitika kwa Tanzania kukosa tuzo hiyo na kufanya jitahada za makusudi kurejesha heshima ya taifa machoni pa Jumuiya za Kimataifa" alisema.