Viongozi wa Vyama vya Siasa Waeleza Manufaa ya Falsafa ya Rais Samia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,475
2,927
Viongozi wa vyama vya siasa nchini wamesema falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ikitekelezwa itakuwa na manufaa kwa ustawi wa nchi.

Wamesema hayo zikiwa zimepita siku chache tangu Rais Samia akiombee Chama cha Wanasheria Tanganyika
(TLS) kimsaidie falsafa hiyo ya R4 inayomaanisha Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga upya.

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu alisema chama hicho ni miongoni mwa vyama vilivyoipokea kwa mikono miwili falsafa hiyo kikiamini Tanzania inahitaji kufungua ukurasa mpya kisiasa.

Ado alisema ACTWa-zalendo wanatambua kuwa baadhi y a masuala muhimu yaliyomo katika hizo R4 ni utashi wa kisiasa kuleta mageuzi ya msingi.
Alisema utashi huo huanza na kiongozi mwenyewe na serikali anayoiongoza na wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa.

Ado alisema TLS na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kwa kushirikiana na wanasiasa wanapaswa kufanya mabadiliko ya kisheria kuhakiki-sha mageuzi yanayofanyika yanalindwa na sheria na yanajengewa msingi wa kisheria.

Kwa mujibu wa Ado, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliwaandikia barua makatibu wakuu wa vyama vya siasa kueleza maeneo ambayo mchakato wake umeanza ikiwemo kuandikwa upya kwa sheria ya uchaguzi, kuandikwa upya kwa sheria ya vyama vya siasa na kufanyia maboresho sheria ya gharama za uchaguzi.

Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Doyo Hassan Doyo alisema falsafa hiyo ya Rais Samia ya R4 ni muhimu
kwa kuwa inaangazia masuala mbalimbali.

Alisema TLS kupitia falsafa hiyo, imsaidie Rais katika kumaliza kesi kwa haraka kwa kuwasaidia Watanzania ambao hawana uwezo wa kifedha na uelewa wa masuala ya kisheria.

"TLS imsaidie Rais Samia kuhakikisha haki za watu zinapatikana kwa kutumia chama chao, wawatawanye wanasheria sehemu mbalimbali kwenda kufanya tafiti za kesi ambazo zimekwama na kuangalia wananchi wenye malalamiko ambayo hayafanyiwi kazi," alisema.

Kwamujibu wa Doyo, kama TLS watafanya hayo maana yake Taifa litakuwa linakwenda kwenye R4 ambako kuna kujenga upya, hivyo lazima kuwe na uwiano wa maisha yaliyokusudiwa na si maridhiano ya Kisiasa tu.

"Kwa hiyo TLS kama inahitaii kumsaidia Rais katika R4 zake basi watengeneze mtandao ambao utakwenda kusaidia watu katika haki zao za msingi sehemu za chini kabisa," alisema

Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi (Bara), Joseph Selasin alisema TLS ina jukumu la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi ikiwamo kuhusu R4 za Rais Samia.​
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom