Wapinzani wa Babu wa Samunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapinzani wa Babu wa Samunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lekanjobe Kubinika, Feb 10, 2012.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kutoka Yahoofriends

  [TABLE]
  [TR]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Haya ni matokeo ya Tiba ya Babu Ambi

  MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ (pichani), anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza Mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.

  [​IMG]...nyumba yake mpya.

  Wanaharakati wameeleza kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo wanamfungulia Babu Ambi, mojawapo ni kumfilisi mali zote alizochuma endapo atakutwa na hatia ya ulaghai, wakati wa kutangaza maono aliyopewa na Mungu kuhusu tiba ya kikombe. Wanadai kuwa Babu Ambi, mkazi wa Kijiji cha Samunge, Loliondo, alitumia matatizo ya Watanzania ya kuugua maradhi sugu ili kujinufaisha, hivyo akatengeneza ulaghai wa tiba ya kikombe kwa maelezo kwamba ni ufunuo aliopewa na Mungu. Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up). Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.  [​IMG]...sola anayotumia nyumbani kwake.
  Wakati Babu alizoea kukanyaga vumbi kwenye nyumba yake ya awali ya udongo, yenye chumba kimoja cha kulala, hivi sasa anatembea juu ya sakafu iliyotandikwa vigae (tiles) kila eneo. Nyumba ya Babu, pia ina kila kitu ambacho hustahili kuwemo kwenye nyumba ya kisasa yenye hadhi ya mtu mwenye fedha, vile vile ina umeme wa mionzi ya jua na maji ya uhakika. Mali zote hizo, wanaharakati wanataka zifilisiwe kwa sababu zimepatikana kwa njia ya udanganyifu. Muungano wa Vyama vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (Tanopha) ni wanaharakati wa kwanza kutoa tamko la kumburuza mahakamani. Tanopha wanasema, miongoni mwao, walitumia kikombe cha Babu Ambi lakini hakuna hata mmoja aliyepona. Wanasema, kila walipokwenda kupima ili waone matokeo ya tiba ya kikombe, majibu yalikuwa ni yaleyale kwamba hakuna mabadiliko.  [​IMG]...Babu akiwa amepozi nyumbani kwake.
  “Hatuwezi kupoteza muda na fedha zetu kwa kwenda kunywa dawa ambayo haitibu, hii ni kuwarubuni wananchi, wengi wameuza mali zao, wengine kutumia akiba ya fedha walizokuwanazo kwenda Loliondo wakijua wangepona lakini cha kushangaza ni kwamba baadhi yetu wanakufa. “Wengine wako mahututi baada ya kupewa kikombe, tulikuwa na matumaini ya kupona hadi tuliacha kutumia vidonge vya kurefusha maisha vya ARV, hatuna mengi zaidi ila tunaomba umtafute mwenyekiti wetu akueleza zaidi,” alisema mmoja wa wanachama wa Tanopha. Mwenyekiti wa Tanopha, Julius Kaaya, aliliambia Uwazi kwa njia ya simu kuwa taasisi yake ilipeleka watu 14 kunywa dawa Loliondo lakini hakuna hata mmoja aliyepona. “Nakumbuka kwamba kipindi tunaenda huko Loliondo Machi 19, mwaka huu, tulifanya mkutano na waandishi wa habari, tulifika Samunge Machi 22, ambapo Machi 24 walikunywa dawa hiyo kila mmoja akiwa na matumaini ya kupona. “Baada ya siku 20 tangu wanywe dawa hiyo walienda hospitali kuangalia kama wamepona, daktari aliwaambia hakuna hata mmoja aliyepona, siku 90 baadaye majibu yakawa yaleyale,“ alisema Kaaya. MCHUNGAJI MTIKILA Naye Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikila kwa upande wake amesema kwamba dawa hiyo haitibu na analishughulikia suala hilo ili kumfikisha mahakamani pamoja na mawaziri, wabunge na viongozi wa juu waliokunywa kikombe.


  [​IMG]..mjengo wake mpya.
  “Mawaziri hao wamewahamasisha wananchi kwenda Loliondo kunywa dawa, lazima tuwashitaki pamoja na viongozi wa dini waliopiga debe,” alisema Mtikila. Viongozi wa dini waliohamasisha ni Askofu Thomas Laizer na Martine Shayo. Baadhi ya Mawaziri waliopata kikombe ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli. Wengine ni wabunge Augustino Mrema, Edward Lowassa na wakuu wa mikoa Yohana Balele na Abbas Kandoro. TAMKO LA WIZARA Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda, alisema hivi karibuni kuwa kikombe cha Babu siyo tiba na kwamba wote waliokwenda Loliondo, walipoteza muda. Kauli ya waziri, ilifuatia ripoti ya uchunguzi wa madaktari bingwa kwamba kikombe cha Babu wa Loliondo, hakitibu. WABUNGE NAO Katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 10, baadhi ya wabunge walitaka Babu wa Loliondo achukuliwe hatua kwa sababu dawa yake haitibu. Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, alikwenda mbali zaidi kwa kutaka mawaziri waliokwenda Loliondo, wahojiwe na waseme kama wamepona, kwani wao kwa kiwango kikubwa walihusika kupotosha umma.


  [​IMG]...Babu Ambi akiwa amepozi, pembeni ni bafu la kisasa analotumia kwa sasa.
  UTETEZI WA BABU Kwa upande wa Babu Ambi, ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa dawa yake imeponyesha wengi. “Kama hawajapona siyo makosa yetu. Tuliwaambia kabla kuwa katika tiba hii kigezo cha kwanza ni kuwa na imani na hapa tuna uthibitisho wa kutosha wa watu walioponywa na maajabu ya dawa hii wakiwemo wagonjwa wenye Ukimwi,” alisema Babu Ambi na kuongeza kuwa anapigwa vita na wengi kwa sababu ya wivu. Kuhusu utajiri wake, alisema kuwa yeye hana mamilioni ya fedha kama inavyodaiwa ila akakiri kumiliki nyumba ya kisasa pamoja na magari mawili ambayo amesema yanamsaidia kubeba dawa pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Loliondo. KUHUSU KIKOMBE Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa KKKT Arusha, Thomas Laizer, zaidi ya watu milioni tatu wameshatibiwa Loliondo. Kila mgonjwa alikuwa analipa shilingi 500, hivyo kwa hesabu ya watu milioni tatu, maana yake kikombe kimeshaingiza zaidi ya shilingi bilioni 1.5.
  Mjinga ni nani......


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,027
  Trophy Points: 280
  Nyumba ya kawaida sana hiyo.....:juggle:
   
 3. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Thanks for useful Post

  Hii kali hizo sheria za kutaifisha mali imeanza kutekelezwa lini? basi na waliokunywa nao wataifishwe aanziwe EL
   
 4. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  duh bongo tambalale unapiga bingo kisha unatulia
   
 5. Gwandalized

  Gwandalized JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  aisi alijipanga kweli kweli kutoka alipokuwa mpaka hapo,hongera babu
   
 6. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Bahati ya mtu usiilalie mlango wazi. Kama una wivu jinyonge tu, PERIOD!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  DAh kweli sitasahau safari ya samunge, ilikuwa adventure moja kali sana! Wasonjo, lake Magadi, Mlima Oldonyo lengai ni vitu ambavyo nilikuwa navisikia tu lkn babu akaniwezesha kuviona
   
 8. N

  Nguto JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,654
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  Kumbe umetoa habari hii kwenye gazeti la "UWAZI". Sio la udaku hilo?? Nina shemeji yangu alienda akapata dawa hiyo mpaka leo anadunda mzima!! Kikubwa ni kuwa na imani na Mungu. Mbona babu alishasema!!!
   
 9. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Maisha ni pamoja na kuwa mbunifu ili kupambana nayo,
  Mwacheni Babu Ambilikile, alichanga karata zake vyema.
   
 10. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Babu alieleza wazi kabisa mgawanyo wa mapato katika kila 500. Sehemu kubwa ilikuwa sio ya kwake. Magari hayo nakumbuka mtu mmoja alimpelekea Pick up ili isaidie kusomba dawa ili awafikie wateja wake, tena alitoa kama shukrani baada ya kupona. Madaktari wanaojitia walifanya utafiti walikuwa biased kwa sababu ripoti yao haijawa published kupitia njia za kisayansi. Who evaluated the report any way, did it go through any peer evaluation reputable organ? Walitumia lugha ya mitaani badala ya sayansi hata wao mioyo yao inawasuta kuupotosha umma kwa kutumia fani tukuka. Walionyesha kuwa na nia ya kukandia na wakampelekea aliyewapa per diem ili afurahie kutoa tamko hasi alilopendelea kusema.

  Tumezoea kuamini sana madawa ya wazungu ambayo nayo yanatokana kwa kiasi kikubwa na miti ya kwetu hapahapa. Badala ya kutafiti zaidi wenyewe walibugia per diem kuhalalisha uharamia wao. Huo nao ni ufisadi, walipaswa kushitakiwa kwa kukitumia MAT kama chombo cha kujinufaisha wao. Binafsi nimewaona wengi waliokunywa kikombe cha babu wamekuwa fit sana kama wamefuata masharti ya babu. Wengine niliowauliza wanasema magonjwa yamerudi kwa sababu ya uzembe wao kutotii masharti na kujisahau (Wanakiri kabisa). Sasa siwezi kutumia niliokutana nao japo ni wengi, kuita matokeo hayo kwamba ni ya kisayansi, kwa sababu hayana ladha ya kisayansi. Information is scientific only if it comes up through scientifically accepted guidelines.

  Kama Babu kajenga nyumba kuna ubaya gani? Walitaka anywee pombe kama wao na kuhonga wanawake hadi iishe bila hekima? Amewaeleza kwamba ni suala la imani, nao walienda kumjaribu kama anatibu lakini imani haijaribiwi kihivyo. Laizer aliwaambia waende maabara kupima imani kwenye test tubes zao kama wanaweza. Nasema hivi, waliopona wamepona na hawapigi makelele. Wale wenye kwenda kumjaribu babu imekula kwao na sasa majuto ni mjukuu. Kwishney! Wapo wengi wanaotaka kwenda mbinguni, lakini wasipofuata masharti wataisikia mbingu redioni tu.
   
 11. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wajinga ndio waliwao.
   
 12. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mjinga mwenye tija ni yule anayejitambua kuwa ni mjinga. Mjinga anayekataa kutambua ujinga wake afanyweje kama upumbavu sio stahili yake? Maana mpumbavu anajua anachofanya kuwa ni cha hovyo, lakini kwa makusudi atafanya. Hao wapo wengi. Ujinga unaotokana na umasikini wa kifikra nao huua usipodhibitiwa haraka. Masikini anapoona mwenzake ananyenyuka atafanya kila mbinu kumrudisha mwenziwe kwenye umaskini badala ya kuomba ushauri wa naye kutoka humo. Tutamkumbuka Mwalimu JK kwa nasaha zake nyingi sana, lakini kaburi lake halisemi tena hata tujapoenda kutwa mara tatu kama vile daktari anavyoandika dawa. Kaaaazi kwelikweli!
   
 13. meeku

  meeku JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 571
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hilo bifu tu. Badala ya kutafuta maisha kivyao wanakimbilia kutafuta majibu ya ndotoni. Aliwaita?? mbona taassisi muhimbili watu hawaponi na wengine wanakufa lakini haijashtakiwa? Hao watu wanaakili za panzi.
   
 14. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]Mtume na Nabii Josephat Mwingira asaidia maendeleo mkoa wa Rukwa[/FONT]
  [FONT=&quot][​IMG][/FONT][FONT=&quot][/FONT]​
  [FONT=&quot]Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/FONT]
   
 15. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,782
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Mh...hawa wachungaji kazi kweli kweli....yani babu katoka shavu alafu katupia t-shirt ya ukweli......aya babu mchungaji mungu akubaliki
   
 16. L

  Losemo Senior Member

  #16
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ulikuwa ubunifu tu. Na wewe buni wa kwako
   
 17. 1

  19don JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  hongera babu sasa gombea udiwani wa samunge , kwa vigezo vifuatavywo
  1; umewaleta viongozi kalibia wote wa tanzania hapo samunge
  2; umesababisha watu wa samunge waone helcopita kila siku
  3; ulitengeneza foleni ya magari kwa zaidi ya km 30
  4; ulileta wajasilia mali kutoka hadi huku dar kuja kuuza maji na chakula
  5; ulisababisha red cross waje samunge
  6; hospital zilikosa wagonjwa kwani wote walikuwa kwako
  7; uliongeza idadi ya vifo hapo kijijini
  8;ulikuwa wa kwanza kumiliki simu ya mkononi ya bure
  9; ulisababisha kujengwa mnara wa simu
  10; ulitengezeza nauli ya kuja samunge ya ghali kuliko kupanda ndege
  11; uliitangaza samunge duniani
  hongera sana babu ambilikile na kalibu kwenye siasa
   
 18. S

  Shansila Senior Member

  #18
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwacheni babu ale matuda ya jasho lake.Wakati anaanza kutoa dawa alibainisha kigezo cha kupona kuwa ni IMANI.Sote tunajua imani ilivyo ngumu na pana,sasa babu angefanyaje?Unaenda kujaribu kama utapona!Hakika imani haiko hivyo,ukiamini amini,usipoamini usiamini,udiwe 50/50.ada ya kikombe ilikuwa sh 500 tu,gharama kubwa ilikuwa ktk nauli tu!Na suala la nauli c lake,je,wanaotaka kumshitaki wanataka kulipwa jerojero zao?Mwacheni babu jamani.
   
 19. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  tuacheni unafiki kuna watu watatu ninao wafahamu tangu wanywe kikombe mpaka leo kisukari chao hakijapanda tena na wameacha kutumia dawa za hospitalini
   
Loading...