Wapinzani tusilaumiane, tufanye kazi pasipo kukoma, jitihada zetu ndizo zitaleta heshima kwa Tanzania ya kesho

Mar 3, 2018
75
799
WAPINZANI TUSILAUMIANE,TUFANYE KAZI PASIPO KUKOMA,JITIHADA ZETU NDIZO ZITALETA
HESHIMA KWA TANZANIA YA KESHO.

Salaam ndugu Watanzania,poleni na majukumu ya kutafuta mkate wa kila siku!
Leo pia naomba niwapongeze Waheshimiwa Wabunge nje ya Bunge ambao wamepata usajiri rasmi jumapili! Hongera sana Ndugu zangu Yonas Masiaya Laizer pamoja na Dada Asia Msangi kwa kutimiza wajibu wenu.

Naomba nitoe machache kwa UPINZANI,CCM NA SERIKALI kuhusu hali inavyoendelea;

1; UPINZANI.
Naomba kutoa pongezi kwa chama na wanachama chini ya uongozi wa mwenyekiti FREEMAN MBOWE kwa kuendelea kushiriki chaguzi ndogo hizi ambazo zinaendelea. Licha ya matokeo ambayo ambayo tunatangaziwa kwamba tumepata. Ni kweli kwamba unaposikia eti Kama Monduli tumepata kura elfu 3 na kidogo huku chama dola kikijitangaza kwamba kimepata kura elf 65 wakati sio sahihi,unaweza kuwaza yote mabaya dhidi ya Nchi yako kwasababu ni uchokozi wa hali ya juu sana.

Ni kweli inaumiza sana kupokwa haki yako,lakini kuchelewa kuamua baya kutokana na hasira za unyanyasaji huu ndio uhai wetu na kuimarika zaidi.

Naomba tuendelee kushiriki chaguzi hizi kwasababu zifuatazo;

1.Kushiriki chaguzi hizi,tunaifanya CCM ionekane kwa watu kwamba haina uwezo tena wa kutumia Sera,falsafa na itikadi kuwashawishi WANANCHI ili waichague. Baadala yake vitisho,kuteka na kuua ndio njia zinazotumiwa na chama hiki kongwe chenye wazee wasio na wosia wala hekima za kuongoza chama hiki.

2. Kushiriki chaguzi hizi inatusaidia kuivua nguo serikali na kusaidia WANANCHI kuona ni jinsi gani serikali inatumia nguvu ya vyombo vya ulinzi kama Polisi, usalama wa Taifa na kuchukua jeshi la WANANCHI( JWTZ) na kuwavisha nguo za jeshi la polisi ili tu kukabiliana na maamuzi ya WANANCHI kwenye sanduku la kura. Hii inamanisha kwamba kama tusingeshiriki,CCM ingeshinda kirahisi bila hata kujua ushiriki wa Polisi,usalama na wanajeshi katika chaguzi hizi.

3. Ushiriki wa chaguzi hizi hutusaidia kujenga chama na kuona uhalisia wa uwepo wa chama chetu. Kwa mfano Kule Buyungu , Monduli na Ukonga ambapo CCM ilitangazwa kuwa imeshinda, WANANCHI wengi wana huzuni kubwa saana na matokeo hayo. Ki uhalisia walitakiwa kuwa na furaha sasa unajiuliza inawezekanaje mtu atangazwe ameshinda kwa 95% lakini huzuni ya watu 5% inafunika furaha ya watu 95%? Hali hii inaonyesha dhahiri kwamba matokeo yamepikwa. Badala ya WANANCHI kufurahi,jeshi la polisi ndilo linafurahi na kushangilia ( Ukonga) pamoja na wateule wa Rais. Hii inaongeza hasira kwa WANANCHI na chuki dhidi ya serikali jambo ambalo kwetu ni mtaji mkubwa saana.

4. Kushiriki chaguzi hizi inatusaidia kupata uwanja wa kusema baada ya mikutano ya kisiasa kupigwa marufuku kihuni na walioshika madaraka pasipo kibali na shauri la Mungu.

Hivyo nawashauri tuendelee kushiriki,TUSILAUMIANE,wala tusituhumiane kwamba kuna mtu kati yetu hatimizi majukumu yake,wala msionyeshe dalili za kuanza kusema yule au huyu hafai kwa nafasi ile au hii.

Hakuna mtu awezae kupambana na mtawala ambae ameamua kutoheshimu sheria na taratibu zinazomfanya atambulike kama mtawala,ukaidi dhidi ya sheria zilizomhalalisha awe mtawala ndio utakua chanzo cha anguko la utawala wake.

Hazikutumika taratibu na sheria za CHADEMA kumuweka Magufuli madarakani,ila zilitumika taratibu na sheria za nchi kumuweka madarakani,hivyo basi WANANCHI ndio wataamua anguko la utawala huu. Kitu pekee ambacho kama chama ni kuendelea kuelimisha WANANCHI namna wanavyoweza kuuangusha utawala huu pale ambapo tunapopata nafasi ya kusema hasa kupitia uchaguzi unaoendelea na zaidi kupitia mitandao ya kijamii na pengine itatubidi kufanya kazi usiku na mchana,mguu kwa mguu na nyumba kwa nyumba ili kupunguza kiwango cha uvumilivu cha Watanzania hawa. Bahati nzuri tunayo nafasi nzuri ya kuungwa mkono na WANANCHI kwani CCM na serikali inasema maendeleo ambayo hayaonekani kwa WANANCHI walio wengi ukiacha wateule wa Rais ambao wamegeuka Matajiri na Mungu watu. Japo kuna utekelezaji wa miradi mikubwa lakini niwambie tu kwamba hiyo haina madhara chanya kwa Watanzania walio wengi na zaidi ya yote inatekelezwa kwa hela za kukopa kopa ovyo.

Vijana wa UPINZANI acheni kuwakumbuka akina Slaa wakati huu,hao wameamua kuungana na maadui zetu.

Nawambieni mpaka muda huu hao hawana uwezo tena wa kufikiri vema kwa upande wetu.
Mazingira ya Tanzania ya sasa yanatengeneza yenye viongozi na wanaharakati wapya kabisa kutokana na hali ilivyo kwasasa. Tuendako inawezekana kabisa tukawa na viongozi imara kuliko wakati wowote ule. The environment determine the language to use!!!
Tuendelee kuibua uovu wa serikali hii bila kuchoka.

2.CCM.
CCM naomba niwambie kwamba hakuna kipindi ambacho mna hali ngumu kama sasa hivi,hapa nawambia wale CCM wenye akili.

Inawezekana wanaccm wengi hawajui wanatangazwaje lakini niwambie kwamba kupitia kura hua hamshindi,mnaogopa sana siku hizi maamuzi ya WANANCHI.

Nakumbuka pale Buyungu Mimi ambae hata sijai ndani ya ndoo ya lita 10 nikiwa pekee yangu halimashauri tena usiku wa saa kumi,mlihitaji FFU wa Katavi,Tabora na Kigoma yote ili tu atangazwe mtu wenu. Hii ni aibu kubwa saana. Hata viumbe vidogo vidogo mnaviogopa.

Hii njia ya kutumia polisi mmeifanya pia hata Ukonga kwa Binti Asia Msangi ambae nae ni kama Mimi tu. Kwa mwanzoni mnaweza kuifurahia hii njia ya kutumia polisi lakini nawambieni kwamba,polisi wa Tanzania hawakuzaliwa Kongo wala Kenya,kwa hiyo hawa polisi mnaotumia kupiga na kuua,wanapiga na kuua ndugu,jamaa na marafiki zao maana nao ni Watanzania.

Polisi aliyezaliwa Mara ataenda kupiga na kuua Baba,mama,Dada,rafiki na jamaa wa Polisi wa Mtwara,Dar,Singida na Arusha na polisi aliyezaliwa Dar mnambemba kwenda kupiga na kuua Baba,mama,Dada,shangazi,rafiki,na jamaa wa polisi aliyezaliwa Kigoma,Tabora,Shinyanga,Mara na Mwanza. Siku polisi hawa wakijua na kuona hawa ndugu zao wametwangika vilivyo wataanza kuwagomea na hao ndio watawatoa madarakani kwa kushirikiana na WANANCHI.

Sasa hivi mna nafasi ya kuendelea kutupiga,kutujeruhi na kutuua kwasababu hamjatugusa karibia wote japo yowe zinazotokana na vipigo tunavyopewa zinaanza kusambaa taratibu.

Ni vizuri Rais akajua kuwa wanaomlinda Leo Ikulu,ndio watakaoungana na WANANCHI kumtoa Ikulu (kumbuka Ghana miaka ya 70's Kwame Nkurumah alichofanyiwa na hatimae kupinduliwa)

2. CCM haina uwezo tena wa kuwashawishi wapiga kura wala miaka ambayo mmeongoza nchi hii sio ushahidi tena wa kujivunia na kutumia mafanikio yaliyopatikana miaka ya nyuma,kuomba kuaminiwa tena. Hamna uwezo tena wa kujitathmini kwa maana mnajidanganya. Hapa mnaanguka hakika,na anguko lenu haliko mbali. Limekaribia.

Kitu pekee mnachoweza kufanya kwasasa ni kuanza kuwaza kutenganisha uenyekiti wa CCM na nafasi ya Urais. Hili linatokana na ukweli kwamba Rais akiwa wa ovyo,ama akipata kashfa mbaya kama huyu tulie nae hata chama pia kinapata sifa mbaya. Ofisi yenu ya uenezi haiongozwi tena na Polepole ila IPO Chini ya Kamanda Sirro na Wasaidizi wake ambao ni wakuu wa Mikoa na Wilaya. Mmeisha kabisa,mmepoteza sifa ya kuwa chama cha siasa. Chama chenu kina idara ya ulinzi na usalama kinachomiliki Bunduki na mapanga,jambo ambalo ni kinyume kabisa!
Nina uhakika kama ingekuwa halali vyama vya siasa vingekuwa na Uhuru wa kufanya diplomasia ya vifaa vya kivita na nchi Rafiki,basi na Mimi sina shaka ningekuwa Nina AK47 Mkononi maana nina watamani kinyama na pengine tungekua na jeshi imara sana kuliko la kwenu.

Sasa mnabebwa na polisi na Green guard wenu kuna wakati mnawapa uhalali wa kujeruhi, kupora fomu za wagombea wa UPINZANI,na wakati mwingine kutucharanga mapanga na hatimae kutuua kwasababu tu ya nguvu ya hoja zetu.

Kumbukeni kwamba baadhi ya wanaccm ni ndugu zetu kwahiyo ipo siku wataogopa kutekeleza maagizo ya kutuua. Binafsi nipo salama mpaka sasa kwasababu baadhi ya wauaji wenu wanavujisha siri na kutuokoa . Japo vijana wenu mnawasafirisha kuwatoa mkoa mmoja kwenda mwingine ili wamwage damu lakini kama ilivyo kwa polisi nao watachoka pia kuua ndugu zao.

Kwasababu ya hofu mlioipandikiza kwa wanachama wenu hata kile kidogo mlichofanikiwa kufanya,hakiwezi kutetewa mtandaoni na vijana wenu maana mnawalea kuwa vijana wenye akili za kushikiwa ( zidumu fikra za mwenyekiti).
Hata akitokea kijana wenu akiwatetea basi atajichanganya na hapo ndipo atakutana na vijana jeuri wenye akili timamu wenye Uhuru wa fikra zao. Ndio maana hata spika anataka wabunge wa CCM wajibu hoja mitandaoni wakati hawawezi maana mlishawaharibu mfumo wa kufikiri vizuri( mmefanya kosa la uumbaji wa Mungu)

3. Kuhonga vyeo UPINZANI hii njia walitumia wakoloni lakini haikufanikiwa.
Miaka ya ukoloni Tanganyika( Tanzania sasa) Mwl Julius Nyerere alihongwa cheo na kuwa mjumbe wa chombo cha kutunga sheria (LEGCO) ili akose muda wa kutembelea na kuunganisha vyama vya ushirika. Mawazo yake katika baraza lile yalikua hayaheshimiwi kwasababu hakuwekwa ili alete mawazo yake,aliwekwa ili ale na atulie lakini aliamua kujiuzulu.

Haikutosha mwaka 60 Julius Nyerere aliteuliwa Kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika ili atulie ale na anywe asiwe na muda wa kuiongoza TANU lakini Februali 1961 aliamua kujiuzulu ili apate muda wa Kutosha wa kuiongoza TANU ili tupate Uhuru. Aliamua kumpendekeza Rashid Mfaume Kawawa awe Waziri Mkuu. Ni wazi kwamba Kama Nyerere angekuwa na akili kama ya Kafulila,Katambi,Machari ,Kalanga,Molel na Waitara nawambieni mpaka muda huu tungekuwa tunamlimia Mwingeleza tena safari hii tungelimia meno.

Hata Ghana pia Kwame Nkurumah alihongwa uwaziri mkuu vilevile miaka ya 56 ili atulie ale wakoloni waendelee lakini akajiuzulu ili awakomboe wana wa Acra na Ghana yote na akafanikiwa. CCM imeiga mfumo wa kikoloni walioshindwa wao wakidhani wataweza.
"Huwezi kuwanunua wanaopinga mawazo yako wote kwa maana idadi yao inazidi kuongezeka kadri ya matendo yako yanavyoathiri watu,watakaokubali kununuliwa hakuzuii wanaokupinga kuongezeka kama ambavyo vifo havizuii watu kuzaliwa na kuongezeka" njia pekee ya kupunguza wanaopinga fikra zako ni kuwa na fikra zinazotokana na ushirikishwaji wa pande inayokupinga vinginevyo tarajia kuanguka tu.( soma kitabu cha Kaduma " Enzi kwa Mwalimu Nyerere" utakutana na haya)

3.SERIKALI.
Baadhi ya WANANCHI wenzetu ambao wameunda serikali kwa ajiri ya Watanzania wote siku hizi wanafanya maamuzi kumfurahisha Rais. Wameacha maadili ya kazi zao,wako tayari kufanya maamuzi yatakayoathiri maisha ya wengi ili wao waishi maisha salama na yenye anasa. Wengine wanapandishwa vyeo baada ya kufanya maamuzi ya kijinga na kipuuzi kabisa,afanyaye ujinga na upuuzi safari hii ni shujaa kwa awamu hii.

Mfano,Ushahidi wa Rushwa ya Mnyeti kwa madiwani wa Arumeru umemfanya awe Mkuu wa Mkoa Manyara,Makonda na vyeti pamoja na maamuzi ya ovyo ya kudhalilisha viongozi,hata mahakimu na majaji nao baadhi yao wanatamani wapande vyeo Kwa kuhukumu viongozi wa UPINZANI.
Mkuu wa wilaya wa sehemu yoyote nchi hii anaonekana amefanya kazi akifanikiwa kumlaza mpinzani rumande na sio kupambana na majambazi au kuinua kilimo. Boss anafurahi kusikia kama baadhi ya wanachama wa upinzani wamevunjwa miguu,hapo utapata promotion.

Tume ya uchaguzi inaonekana imetenda haki kama ikitangaza CCM kwamba imeshinda,Mkurugenzi akifanikisha hili basi yeye ahesabu kupandishwa cheo ( Yule wa Kakonko sasa yupo manispaa ya Temeke) kutoka halmashauri ya kwanza kwa umaskini mpaka jiji la kwanza kwa maendeleo ni promotion kubwa sana.

Haya mambo yatakuwa na mwisho kama WANANCHI ambao kwasasa hawana uwezo wa kuikosoa serikali yao watafika kiwango cha mwisho kwa uvumilivu.

Hili halitakuwa rahisi kama WANANCHI wataendelea kuwa na kiwango kikubwa cha uvumilivu juu ya haya yanayoendelea,jukumu tulilo nalo ni kuendelea kuwaelimisha WANANCHI ikiwa ni pamoja na kuendelea kushiriki uchaguzi maana ndio uwanja uliobaki wa kukutana na WANANCHI wa aina zote. Wasiojua kusoma kuandika,wamama na watoto ambao hawawezi kupata taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii. Chonde chonde tutafika maana naona kasi ya dikteta kujimaliza mwenyewe imekaribia!!
Tusipukutishe majani nasi tukabadilika mwonekano na tabia,kwa kufanya hivyo hatutaishi milele,nasi tunatakiwa kuwa na mizizi mirefu tufuate maji chini ya ardhi ili tupambane na kiangazi kisha tudumu katika imani.

Elia F Michael.
Mbunge nje ya Bunge.
Diwani Gwarama.
Mwenyekiti wa Madiwani Kanda ya Magharibi.
18/Septemba /2018
Babati-Manyara Tanzania.
 
Write your reply...Mungu akubari sana. kaka yangu sana......endelea hivyo hivyo roho wa shetan asije akakuingia ukawa kama kina yuda(katambi,kitila,slaa,machali,waitara,Kalangi,mtungirehi wa kyerwa nk....)
 
Nimesoma nimeelimika,kijana yuko vizuri,flow of ideas ni mara mia ya maprof wa makenikia.Mungu aendelee kukupa maarifa zaidi usikengeuke,CCM na secretariat yake hawataki kuwaona vijana kama nyie.wapo tayar kuwanunua kwa mapesa na hata kuwaangamiza!
May our great lord bless you.Amen!
 
CHADEMA , mna bahati ya kuwa na vijana wenye akili sana. Nakuomba mwenyekiti Mbowe uwe karibu na huyu kijana . Huyu atakuwa hazina kubwa sana kwa badae. Sijawahi kuona kijana katika umri wako akawa na mawazo mazuri namna hii kuliko hata wazee wenye vyeo vikubwa hapa nchini. Hongera sana mdogo wangu ELIA , Wewe unafanana na wale vijana maarufu wa kwenye bibilia hawa ni Daudi, Yusuph, Isaya , Yeremia na wengine wengi. Nakuombea kwa Mungu uzidi kukua katika maarifa na hekima hii ambayo Mungu amekujalia.
 
Aisiiii KAMANDA Hakika umepikwa kisiasa umekwiva hongera kwa chama chini ya mbowe Hakika hii Chadema nizaidi ya shule KAMANDA mbowe ongoza jahazi achana na mishoga ya lumumba
 
Nimerudia hii makala mara mbili., it's amazing! Nna mashaka kama watesi wa umma wataelewa, kama wahenga walivyosema: Sikio la kufa halisikii dawa
 
WAPINZANI TUSILAUMIANE,TUFANYE KAZI PASIPO KUKOMA,JITIHADA ZETU NDIZO ZITALETA
HESHIMA KWA TANZANIA YA KESHO.

Salaam ndugu Watanzania,poleni na majukumu ya kutafuta mkate wa kila siku!
Leo pia naomba niwapongeze Waheshimiwa Wabunge nje ya Bunge ambao wamepata usajiri rasmi jumapili! Hongera sana Ndugu zangu Yonas Masiaya Laizer pamoja na Dada Asia Msangi kwa kutimiza wajibu wenu.

Naomba nitoe machache kwa UPINZANI,CCM NA SERIKALI kuhusu hali inavyoendelea;

1; UPINZANI.
Naomba kutoa pongezi kwa chama na wanachama chini ya uongozi wa mwenyekiti FREEMAN MBOWE kwa kuendelea kushiriki chaguzi ndogo hizi ambazo zinaendelea. Licha ya matokeo ambayo ambayo tunatangaziwa kwamba tumepata. Ni kweli kwamba unaposikia eti Kama Monduli tumepata kura elfu 3 na kidogo huku chama dola kikijitangaza kwamba kimepata kura elf 65 wakati sio sahihi,unaweza kuwaza yote mabaya dhidi ya Nchi yako kwasababu ni uchokozi wa hali ya juu sana.

Ni kweli inaumiza sana kupokwa haki yako,lakini kuchelewa kuamua baya kutokana na hasira za unyanyasaji huu ndio uhai wetu na kuimarika zaidi.

Naomba tuendelee kushiriki chaguzi hizi kwasababu zifuatazo;

1.Kushiriki chaguzi hizi,tunaifanya CCM ionekane kwa watu kwamba haina uwezo tena wa kutumia Sera,falsafa na itikadi kuwashawishi WANANCHI ili waichague. Baadala yake vitisho,kuteka na kuua ndio njia zinazotumiwa na chama hiki kongwe chenye wazee wasio na wosia wala hekima za kuongoza chama hiki.

2. Kushiriki chaguzi hizi inatusaidia kuivua nguo serikali na kusaidia WANANCHI kuona ni jinsi gani serikali inatumia nguvu ya vyombo vya ulinzi kama Polisi, usalama wa Taifa na kuchukua jeshi la WANANCHI( JWTZ) na kuwavisha nguo za jeshi la polisi ili tu kukabiliana na maamuzi ya WANANCHI kwenye sanduku la kura. Hii inamanisha kwamba kama tusingeshiriki,CCM ingeshinda kirahisi bila hata kujua ushiriki wa Polisi,usalama na wanajeshi katika chaguzi hizi.

3. Ushiriki wa chaguzi hizi hutusaidia kujenga chama na kuona uhalisia wa uwepo wa chama chetu. Kwa mfano Kule Buyungu , Monduli na Ukonga ambapo CCM ilitangazwa kuwa imeshinda, WANANCHI wengi wana huzuni kubwa saana na matokeo hayo. Ki uhalisia walitakiwa kuwa na furaha sasa unajiuliza inawezekanaje mtu atangazwe ameshinda kwa 95% lakini huzuni ya watu 5% inafunika furaha ya watu 95%? Hali hii inaonyesha dhahiri kwamba matokeo yamepikwa. Badala ya WANANCHI kufurahi,jeshi la polisi ndilo linafurahi na kushangilia ( Ukonga) pamoja na wateule wa Rais. Hii inaongeza hasira kwa WANANCHI na chuki dhidi ya serikali jambo ambalo kwetu ni mtaji mkubwa saana.

4. Kushiriki chaguzi hizi inatusaidia kupata uwanja wa kusema baada ya mikutano ya kisiasa kupigwa marufuku kihuni na walioshika madaraka pasipo kibali na shauri la Mungu.

Hivyo nawashauri tuendelee kushiriki,TUSILAUMIANE,wala tusituhumiane kwamba kuna mtu kati yetu hatimizi majukumu yake,wala msionyeshe dalili za kuanza kusema yule au huyu hafai kwa nafasi ile au hii.

Hakuna mtu awezae kupambana na mtawala ambae ameamua kutoheshimu sheria na taratibu zinazomfanya atambulike kama mtawala,ukaidi dhidi ya sheria zilizomhalalisha awe mtawala ndio utakua chanzo cha anguko la utawala wake.

Hazikutumika taratibu na sheria za CHADEMA kumuweka Magufuli madarakani,ila zilitumika taratibu na sheria za nchi kumuweka madarakani,hivyo basi WANANCHI ndio wataamua anguko la utawala huu. Kitu pekee ambacho kama chama ni kuendelea kuelimisha WANANCHI namna wanavyoweza kuuangusha utawala huu pale ambapo tunapopata nafasi ya kusema hasa kupitia uchaguzi unaoendelea na zaidi kupitia mitandao ya kijamii na pengine itatubidi kufanya kazi usiku na mchana,mguu kwa mguu na nyumba kwa nyumba ili kupunguza kiwango cha uvumilivu cha Watanzania hawa. Bahati nzuri tunayo nafasi nzuri ya kuungwa mkono na WANANCHI kwani CCM na serikali inasema maendeleo ambayo hayaonekani kwa WANANCHI walio wengi ukiacha wateule wa Rais ambao wamegeuka Matajiri na Mungu watu. Japo kuna utekelezaji wa miradi mikubwa lakini niwambie tu kwamba hiyo haina madhara chanya kwa Watanzania walio wengi na zaidi ya yote inatekelezwa kwa hela za kukopa kopa ovyo.

Vijana wa UPINZANI acheni kuwakumbuka akina Slaa wakati huu,hao wameamua kuungana na maadui zetu.

Nawambieni mpaka muda huu hao hawana uwezo tena wa kufikiri vema kwa upande wetu.
Mazingira ya Tanzania ya sasa yanatengeneza yenye viongozi na wanaharakati wapya kabisa kutokana na hali ilivyo kwasasa. Tuendako inawezekana kabisa tukawa na viongozi imara kuliko wakati wowote ule. The environment determine the language to use!!!
Tuendelee kuibua uovu wa serikali hii bila kuchoka.

2.CCM.
CCM naomba niwambie kwamba hakuna kipindi ambacho mna hali ngumu kama sasa hivi,hapa nawambia wale CCM wenye akili.

Inawezekana wanaccm wengi hawajui wanatangazwaje lakini niwambie kwamba kupitia kura hua hamshindi,mnaogopa sana siku hizi maamuzi ya WANANCHI.

Nakumbuka pale Buyungu Mimi ambae hata sijai ndani ya ndoo ya lita 10 nikiwa pekee yangu halimashauri tena usiku wa saa kumi,mlihitaji FFU wa Katavi,Tabora na Kigoma yote ili tu atangazwe mtu wenu. Hii ni aibu kubwa saana. Hata viumbe vidogo vidogo mnaviogopa.

Hii njia ya kutumia polisi mmeifanya pia hata Ukonga kwa Binti Asia Msangi ambae nae ni kama Mimi tu. Kwa mwanzoni mnaweza kuifurahia hii njia ya kutumia polisi lakini nawambieni kwamba,polisi wa Tanzania hawakuzaliwa Kongo wala Kenya,kwa hiyo hawa polisi mnaotumia kupiga na kuua,wanapiga na kuua ndugu,jamaa na marafiki zao maana nao ni Watanzania.

Polisi aliyezaliwa Mara ataenda kupiga na kuua Baba,mama,Dada,rafiki na jamaa wa Polisi wa Mtwara,Dar,Singida na Arusha na polisi aliyezaliwa Dar mnambemba kwenda kupiga na kuua Baba,mama,Dada,shangazi,rafiki,na jamaa wa polisi aliyezaliwa Kigoma,Tabora,Shinyanga,Mara na Mwanza. Siku polisi hawa wakijua na kuona hawa ndugu zao wametwangika vilivyo wataanza kuwagomea na hao ndio watawatoa madarakani kwa kushirikiana na WANANCHI.

Sasa hivi mna nafasi ya kuendelea kutupiga,kutujeruhi na kutuua kwasababu hamjatugusa karibia wote japo yowe zinazotokana na vipigo tunavyopewa zinaanza kusambaa taratibu.

Ni vizuri Rais akajua kuwa wanaomlinda Leo Ikulu,ndio watakaoungana na WANANCHI kumtoa Ikulu (kumbuka Ghana miaka ya 70's Kwame Nkurumah alichofanyiwa na hatimae kupinduliwa)

2. CCM haina uwezo tena wa kuwashawishi wapiga kura wala miaka ambayo mmeongoza nchi hii sio ushahidi tena wa kujivunia na kutumia mafanikio yaliyopatikana miaka ya nyuma,kuomba kuaminiwa tena. Hamna uwezo tena wa kujitathmini kwa maana mnajidanganya. Hapa mnaanguka hakika,na anguko lenu haliko mbali. Limekaribia.

Kitu pekee mnachoweza kufanya kwasasa ni kuanza kuwaza kutenganisha uenyekiti wa CCM na nafasi ya Urais. Hili linatokana na ukweli kwamba Rais akiwa wa ovyo,ama akipata kashfa mbaya kama huyu tulie nae hata chama pia kinapata sifa mbaya. Ofisi yenu ya uenezi haiongozwi tena na Polepole ila IPO Chini ya Kamanda Sirro na Wasaidizi wake ambao ni wakuu wa Mikoa na Wilaya. Mmeisha kabisa,mmepoteza sifa ya kuwa chama cha siasa. Chama chenu kina idara ya ulinzi na usalama kinachomiliki Bunduki na mapanga,jambo ambalo ni kinyume kabisa!
Nina uhakika kama ingekuwa halali vyama vya siasa vingekuwa na Uhuru wa kufanya diplomasia ya vifaa vya kivita na nchi Rafiki,basi na Mimi sina shaka ningekuwa Nina AK47 Mkononi maana nina watamani kinyama na pengine tungekua na jeshi imara sana kuliko la kwenu.

Sasa mnabebwa na polisi na Green guard wenu kuna wakati mnawapa uhalali wa kujeruhi, kupora fomu za wagombea wa UPINZANI,na wakati mwingine kutucharanga mapanga na hatimae kutuua kwasababu tu ya nguvu ya hoja zetu.

Kumbukeni kwamba baadhi ya wanaccm ni ndugu zetu kwahiyo ipo siku wataogopa kutekeleza maagizo ya kutuua. Binafsi nipo salama mpaka sasa kwasababu baadhi ya wauaji wenu wanavujisha siri na kutuokoa . Japo vijana wenu mnawasafirisha kuwatoa mkoa mmoja kwenda mwingine ili wamwage damu lakini kama ilivyo kwa polisi nao watachoka pia kuua ndugu zao.

Kwasababu ya hofu mlioipandikiza kwa wanachama wenu hata kile kidogo mlichofanikiwa kufanya,hakiwezi kutetewa mtandaoni na vijana wenu maana mnawalea kuwa vijana wenye akili za kushikiwa ( zidumu fikra za mwenyekiti).
Hata akitokea kijana wenu akiwatetea basi atajichanganya na hapo ndipo atakutana na vijana jeuri wenye akili timamu wenye Uhuru wa fikra zao. Ndio maana hata spika anataka wabunge wa CCM wajibu hoja mitandaoni wakati hawawezi maana mlishawaharibu mfumo wa kufikiri vizuri( mmefanya kosa la uumbaji wa Mungu)

3. Kuhonga vyeo UPINZANI hii njia walitumia wakoloni lakini haikufanikiwa.
Miaka ya ukoloni Tanganyika( Tanzania sasa) Mwl Julius Nyerere alihongwa cheo na kuwa mjumbe wa chombo cha kutunga sheria (LEGCO) ili akose muda wa kutembelea na kuunganisha vyama vya ushirika. Mawazo yake katika baraza lile yalikua hayaheshimiwi kwasababu hakuwekwa ili alete mawazo yake,aliwekwa ili ale na atulie lakini aliamua kujiuzulu.

Haikutosha mwaka 60 Julius Nyerere aliteuliwa Kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika ili atulie ale na anywe asiwe na muda wa kuiongoza TANU lakini Februali 1961 aliamua kujiuzulu ili apate muda wa Kutosha wa kuiongoza TANU ili tupate Uhuru. Aliamua kumpendekeza Rashid Mfaume Kawawa awe Waziri Mkuu. Ni wazi kwamba Kama Nyerere angekuwa na akili kama ya Kafulila,Katambi,Machari ,Kalanga,Molel na Waitara nawambieni mpaka muda huu tungekuwa tunamlimia Mwingeleza tena safari hii tungelimia meno.

Hata Ghana pia Kwame Nkurumah alihongwa uwaziri mkuu vilevile miaka ya 56 ili atulie ale wakoloni waendelee lakini akajiuzulu ili awakomboe wana wa Acra na Ghana yote na akafanikiwa. CCM imeiga mfumo wa kikoloni walioshindwa wao wakidhani wataweza.
"Huwezi kuwanunua wanaopinga mawazo yako wote kwa maana idadi yao inazidi kuongezeka kadri ya matendo yako yanavyoathiri watu,watakaokubali kununuliwa hakuzuii wanaokupinga kuongezeka kama ambavyo vifo havizuii watu kuzaliwa na kuongezeka" njia pekee ya kupunguza wanaopinga fikra zako ni kuwa na fikra zinazotokana na ushirikishwaji wa pande inayokupinga vinginevyo tarajia kuanguka tu.( soma kitabu cha Kaduma " Enzi kwa Mwalimu Nyerere" utakutana na haya)

3.SERIKALI.
Baadhi ya WANANCHI wenzetu ambao wameunda serikali kwa ajiri ya Watanzania wote siku hizi wanafanya maamuzi kumfurahisha Rais. Wameacha maadili ya kazi zao,wako tayari kufanya maamuzi yatakayoathiri maisha ya wengi ili wao waishi maisha salama na yenye anasa. Wengine wanapandishwa vyeo baada ya kufanya maamuzi ya kijinga na kipuuzi kabisa,afanyaye ujinga na upuuzi safari hii ni shujaa kwa awamu hii.

Mfano,Ushahidi wa Rushwa ya Mnyeti kwa madiwani wa Arumeru umemfanya awe Mkuu wa Mkoa Manyara,Makonda na vyeti pamoja na maamuzi ya ovyo ya kudhalilisha viongozi,hata mahakimu na majaji nao baadhi yao wanatamani wapande vyeo Kwa kuhukumu viongozi wa UPINZANI.
Mkuu wa wilaya wa sehemu yoyote nchi hii anaonekana amefanya kazi akifanikiwa kumlaza mpinzani rumande na sio kupambana na majambazi au kuinua kilimo. Boss anafurahi kusikia kama baadhi ya wanachama wa upinzani wamevunjwa miguu,hapo utapata promotion.

Tume ya uchaguzi inaonekana imetenda haki kama ikitangaza CCM kwamba imeshinda,Mkurugenzi akifanikisha hili basi yeye ahesabu kupandishwa cheo ( Yule wa Kakonko sasa yupo manispaa ya Temeke) kutoka halmashauri ya kwanza kwa umaskini mpaka jiji la kwanza kwa maendeleo ni promotion kubwa sana.

Haya mambo yatakuwa na mwisho kama WANANCHI ambao kwasasa hawana uwezo wa kuikosoa serikali yao watafika kiwango cha mwisho kwa uvumilivu.

Hili halitakuwa rahisi kama WANANCHI wataendelea kuwa na kiwango kikubwa cha uvumilivu juu ya haya yanayoendelea,jukumu tulilo nalo ni kuendelea kuwaelimisha WANANCHI ikiwa ni pamoja na kuendelea kushiriki uchaguzi maana ndio uwanja uliobaki wa kukutana na WANANCHI wa aina zote. Wasiojua kusoma kuandika,wamama na watoto ambao hawawezi kupata taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii. Chonde chonde tutafika maana naona kasi ya dikteta kujimaliza mwenyewe imekaribia!!
Tusipukutishe majani nasi tukabadilika mwonekano na tabia,kwa kufanya hivyo hatutaishi milele,nasi tunatakiwa kuwa na mizizi mirefu tufuate maji chini ya ardhi ili tupambane na kiangazi kisha tudumu katika imani.

Elia F Michael.
Mbunge nje ya Bunge.
Diwani Gwarama.
Mwenyekiti wa Madiwani Kanda ya Magharibi.
18/Septemba /2018
Babati-Manyara Tanzania.
Safi sana.ila ww jamaa unakaunafiki kachinichini.
 
Inavutia,mazombie ya lumumba yapo na slowly yanakenua mimeno mithili ya simba mwenye njaaa.Mungu akubariki!!Mashetani FC yamefura mithili ya chui aliyekosa nyama ya binadamu.
 
Dah... Ukisoma kwa jicho la tatu...hili ni tusi na dhihaka kubwa kwa mwenyekiti...na wapinzani wachache waliobaki...tena wale wenye akili tu
 
Back
Top Bottom