Wapinzani Tanzania Jifunzeni Demokrasia Kukosoana ni Kuambiana Ukweli Kwa Faida ya Chama Zaidi!!

- Lets say kwamba huyu mtoto alifuatiliwa na CCM, so unasema ni sawa Chadema kuwatishia wanaokosoa kwa sababu CCM imemtishia huyu mtoto?

Le Mutuz
Kama ni sawa, basi iwe sawa kwa vyama vyote. Kama si sawa, pia si sawa kwa vyama vyote. Kwa hiyo title ya thread yako ilitakiwa kuwa "Vyama vya siasa jifunzeni demokrasia ...." na sio "Wapinzani jifunzeni demokrasia ...."
 
Warioba awa mbogo
By Richard Makore
4th October 2013

headline_bullet.jpg
Amtaka kigogo wa CCM aseme kama ametumwa kuichafua tume
headline_bullet.jpg
Asisitiza amemsikia sana akiendesha kampeni ya kuchafua Tume



Jaji%20Warioba%281%29.jpeg

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, amegeuka mbogo na kumtaka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, kuacha kupiga kelele dhidi yake kwa kuwa hakumtuma kazi ya kukusanya maoni ya katiba mpya, bali alitumwa na serikali kwa niaba ya wananchi.

Jaji Warioba alitoa kauli hiyo jana kama karipio kwa Bulembo hilo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, na kusisitiza kwamba Bulembo amekuwa na ajenda ya siri dhidi yake (Warioba) na baadhi ya wajumbe wa Tume kwa kuwa amekuwa akiwazungumzia wao binafsi kila anaposisimama katika majukwaa ya kisiasa.

Alimtaka Bulembo kuthibitisha kuhusu kauli ambazo amekuwa akizitoa kwenye mikutano ya CCM katika mikoa ya Arusha, Tanga na Mbeya kuwa yeye (Warioba) amegeuka kuwa msemaji wa wananchi katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.

Jaji Warioba alitamtahadharisha Bulembo na kumtaka kuacha kupiga kelele pamoja na kumshambulia badala yake azungumzie masuala yanayohusu Rasimu ya Katiba na siyo kuwajadili wajumbe.

Aidha, Jaji Warioba alimtaka Bulembo kuthibitisha kama kauli ambazo alizitoa kwa nyakati tofauti katika mikoa hiyo ametumwa na CCM ama ni kauli zake binafsi.

Jaji Warioba alisisitiza kuwa siku zote Tume yake imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwataka wanasiasa akiwamo Bulembo kujadili Rasimu iliyotolewa badala ya Tume au wajumbe wake.

Kwa mujibu wa Jaji Warioba, hakutumwa na CCM kufanya kazi anayoifanya na kwamba kazi hiyo alipewa na serikali kwa mujibu wa sheria na kwamba ataendelea kuifanya bila kusikiliza maneno yanayosemwa dhidi yake.

Alikiri kuwa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na Bulembo kwa nyakati mbalimbali zimechangia mchakato wa Katiba kuwa mgumu hususani wakati wananchi walipokuwa wakitoa maoni kupitia mabaraza ya katiba mkoani Mbeya.

"Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa elimu kwa umma, na ni kazi ya wakati wote. Sasa kama Bulembo anaona kutoa elimu ni dhambi ni sawa," alisema Jaji Warioba ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais.

Kuhusu kukatishwa tamaa kutokana na kauli za wanasiasa hususani kutoka CCM ambao wamekuwa wakimuandama binafsi, Jaji Warioba alisema haogopi wala hatetereki kwa kuwa anafanya kazi aliyotumwa na wananchi.

Alisema CCM iliishawasilisha maoni yake walipopewa nafasi ya kufanya hivyo, na kwamba masuala mengine yanayojitokeza zikiwamo kauli za Bulembo baada ya hapo hajui zinatoka wapi.

Aliongeza kuwa Tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za wanasiasa mbalimbali na kuongeza kuwa pamoja na kauli hizo, inafarijika na kauli za kutia moyo wanazozipata kutoka kwa wananchi wa kawaida.

"Nilisema mwishoni mwa mwezi uliopita, wanasiasa wamekuwa wakitoa matamshi yaliyoifanya kazi ya Tume kuwa ngumu katika mikutano ya mabaraza ya katiba," alisema na kuongeza:

"Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia rasimu," alisema
Warioba alisema siku zote Tume yake imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida, lakini alisisitiza kuwa ni vyema wananchi na wanasiasa wakajadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa badala ya watu au Tume.

"Nadhani wangezungumzia Rasimu wangetusaidia sana, badala ya kuzungumzia Tume na watu," aliongeza.
Juzi CCM iliendeleza kauli zake zinazoonyesha kumuingilia na kumshambulia vikali Jaji Warioba na kumtaka aache kuwasemea Watanzania juu ya aina ya Katiba wanayoitaka.

Matamshi ya kumshambulia Jaji Warioba yalitolewa mkoani Tanga na Bulembo, wakati akihutubia moja ya mikutano ya hadhara ya wanachama wa chama hicho.

Bulembo alinukuliwa katika vyombo vya habari akisema kuwa siyo sahihi kwa Jaji Warioba kuwa msemaji wa Watanzania kuhusiana na mambo wanayoyataka yaingizwe ndani ya katiba.

"Jaji Warioba ni mmoja kati ya Watanzania mamilioni na kwa hali hiyo hawezi kubeba mawazo ya Watanzania wengine, ni vizuri akasimamia Rasimu, badala ya kuwa msemaji wa wananchi," alisema Bulembo ambaye pia ni Mjumbe wa kamati Kuu (CC) ya CCM.

Kauli hiyo ya Bulembo imetolewa wakati kukiwa na msuguano kati ya CCM na serikali yake kwa upande mmoja, na vyama vitatu vya upinzani vyenye wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Jaji Warioba akizungumza na waandishi wa habari, aliwakemea baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa kuiingilia mchakato wa kupata Katiba mpya unaoendelea.

Alisema baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa kuendesha Mabaraza ya Katiba, ni kwa baadhi ya vyama vya siasa kuingilia uhuru wa wajumbe katika kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba, wakiwafundisha nini cha kusema.

Jaji Warioba aliwasihi viongozi wa vyama vya siasa kuwaachia wananchi, cha kusema kwani, katiba inayotafutwa ni ya wananchi, na si ya vyama au kundi fulani

Bulembo alipotafutwa jana kufafanua kama kauli hizo ni zake binafsi au ametumwa na CCM,hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita bila majibu.
Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms),pia hakujibu hadi tunakwenda mitamboni




SOURCE: NIPASHE
 
- Ila sijaona huyo mtoto alipoitwa mhaini, msaliti, pandikizi au mamluki au wewe umeona hiyo mkuu? sijaona aliposimamishwa chama kwa siku 14 akisubiri kujieleza ili asifukuzwe chama au?


Le Mutuz

Sasa wewe umeamua kubishana sasa huyo mtoto kuhoji tayari afisa usalama wameanza kumfuatilia democracy ipo wapi hapo? Kwani we huoni kuwa ccm ni mzigo.
 
Kama ni sawa, basi iwe sawa kwa vyama vyote. Kama si sawa, pia si sawa kwa vyama vyote. Kwa hiyo title ya thread yako ilitakiwa kuwa "Vyama vya siasa jifunzeni demokrasia ...." na sio "Wapinzani jifunzeni demokrasia ...."

- Una maana huyo mtoto ni mbunge au naibu katibu mkuu wa CCM?

Le Mutuz
 
Sasa wewe umeamua kubishana sasa huyo mtoto kuhoji tayari afisa usalama wameanza kumfuatilia democracy ipo wapi hapo? Kwani we huoni kuwa ccm ni mzigo.

- Kumbe yule mtoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM? Nafahamu Sheria za Uasalama wa Taifa ni kwamba kuna mambo ukiyafanya kwa Kiongozi mkuu wa Taifa, wanatakiwa kukufuatilia kukujua kama una nia na madhumuni tofauti na yale uliyoyaonyesha ila sikujua huyu mtoto mdogo ndiye sababu ya Chadema, kumpiga Mwenyekiti Arusha na kumnynga'anya Laptop, kuwasimamisha Zitto na Kitila, kumbe walikuwa wanaiiga CCM kwa sababu ya huyu mtoto? ha1 ha! ha!

Le Mutuz
 
- Una maana huyo mtoto ni mbunge au naibu katibu mkuu wa CCM?

Le Mutuz
Kwani kukubali kukosolewa ni lazima kuwe kunatokana na mawazo ya viongozi wa chama? Ukikataa kukosolewa na mifumo iliyo nje ya siasa, hilo unaona ni sawa tu? That's why nilisema tatizo linaelekea lipo kwako
 
- Labda ujiulize mwenyewe maana ni wewe uliyeyaleta hayo na nje sana ya hii mada

Le Mutuz

Mkuu umejenga hoja kwa kushauri wapinzani tu kujifunza kuambiana ukweli kama CCM ndio mfano bora sasa issue ya Kolimba si ndio ingekuwa good point of reference?

BTW ukaamua kumtaja Wangwe ku dissolve issue ya Kolimba! Nikakubali hoja yako lakini nikataka ufafanue tena dhana ya msingi uliyojenga kwenye mada yako kwa reference ya Kolimba na Wangwe alafu unaruka havihusiani tena?

Mzee wa sauti ya umeme vipi tena?
 
Prof Kapuya vipi? Njelu kasaka, babako na G** walifanywaje? shibuda alipotangaza kugomea urais mlimfanyaje? kura za maruhani zilikuwa za nini? Samwel Sitta ilikuwaje mkamtemesha u-speaker? Kolimba, babu Kambona, Imran Kombe, Nyerere, Wangwe, Sokoine, Mwangosi, mliwafanya nini? Kibanda na Dr Ulimboka waliwakosea nini?
 
Hawa vijana waliozaliwa kwenye familia za mboga 7 halafu kibaya zaidi ni jasho letu makabwela huwaga najiuliza ni laana zutu au manake utamkuta mtu huku anakuambia sijui ana phd sijui master zote kazikokoto uk lakini topic zake anazotoa ukizisoma ni uzoba mtupu jamani dhulma mbaya haijalishi babako ndio alikula rushwa au nduguyo laana itawazunguka tu ndo maana huwa mnaweweseka hata mnavyotoa topic zenu
 
- Kumbe yule mtoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM? Nafahamu Sheria za Uasalama wa Taifa ni kwamba kuna mambo ukiyafanya kwa Kiongozi mkuu wa Taifa, wanatakiwa kukufuatilia kukujua kama una nia na madhumuni tofauti na yale uliyoyaonyesha ila sikujua huyu mtoto mdogo ndiye sababu ya Chadema, kumpiga Mwenyekiti Arusha na kumnynga'anya Laptop, kuwasimamisha Zitto na Kitila, kumbe walikuwa wanaiiga CCM kwa sababu ya huyu mtoto? ha1 ha! ha!

Le Mutuz

Ntapoteza nguvu nkiendelea kujadiliana na wewe jamaa kweli nimeamini ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi.Amina.
 
- Katika Demokrasia Siasa ina rules zake na mikakati yake ambayo kuicheza sio kuvunja Sheria wala Katiba kuanzia za chama mpaka Jamhuri, Shibuda aligombea CCM akashindwa akaingia kwenu na it has nothing to do na kicha cha hii mada kwamba badilikeni mjifunze maana ya Demokrasia, nashangaa leo wewe kukosa maneno mengi ya kujibu vipi?

Le Mutuz

We ni mfano wa kutoigwa maishani.
 
Kwani kukubali kukosolewa ni lazima kuwe kunatokana na mawazo ya viongozi wa chama? Ukikataa kukosolewa na mifumo iliyo nje ya siasa, hilo unaona ni sawa tu? That's why nilisema tatizo linaelekea lipo kwako

- Nimezungumzima vyama vya siasa sio vya mpira!!

Le Mutuz
 
Mkuu umejenga hoja kwa kushauri wapinzani tu kujifunza kuambiana ukweli kama CCM ndio mfano bora sasa issue ya Kolimba si ndio ingekuwa good point of reference?

BTW ukaamua kumtaja Wangwe ku dissolve issue ya Kolimba! Nikakubali hoja yako lakini nikataka ufafanue tena dhana ya msingi uliyojenga kwenye mada yako kwa reference ya Kolimba na Wangwe alafu unaruka havihusiani tena?

Mzee wa sauti ya umeme vipi tena?

- Wangwe alikufa akidai Demokrasia akasimamishwa uongozi na uanachama, Kolimba alidai Demokrasia akapewa kamati ya kuchunguza matatizo ya CCM akafariki tizama tofauti zao, ingawa sio the topic nimekujibu tu lakini please lets get back to the topic!!

Le Mutuz
 
.

- Huu ni wakati wa Vyama vyote vya Upinzani nchini kukaa chini na kujitafakari nini kimewasibu mpaka kufikia kukataa kukosolewa kila wakati viongozi baadhi ya Viongozi wa vyama hivyo wakijaribu kukosoa basi inakuwa shida na balaa kila mahali. Mrema alipokosolewa NCCR kikaishia kubaki kivuli mpaka leo, CUF ilipokosolewa na kina Rashid ikawa kizaaa zaa kila mahali, sasa wenzetu Chadema nao yale yale, tena wao wameeenda mbali zaidi mpaka kuita wakosoaji ni Mamluki, Wahaini, Mapandikizi, Wasaliti jamani mbona CCM Mbunge sasa anataka Waziri Mkuu aondolewe kwa uwajibikaji na hatujasikia haya ya kuitana majina ya ajabu ajabu? Jamani Wapinzani Tanzania jifunzeni uvumilivu wa kisiasa na kama hamuwezi basi siasa sio fani yenu si mrudi tu mnako-fit vizuri kuliko kunga'nga'nia siasa. I mean wewe umechagliwa kwa mujibu wa katiba halaafu unaanza kuhangaika kila kona kutaka kupindisha katiba ile ile iliyokupa nafasi ya kuongoza ili usitoke kwenye uongozi, sasa mkipewa Taifa itakuwaje? Viongozi wakubwa wa Taifa wa chama cha siasa mnapofikia kulumbana mbele ya jamii kuhusu ukweli na uongoa wa katiba yenu wenyewe mlioitunga wenyewe mnatutisha wengine kwenye jamii, kwamba mkishika dola itakuwaje na katiba ya jamhuri ambayo hamkuitunga? si itakuwa vurugu kila siku kugombania ukweli na uongo wa katiba, badilikeni jamani Demokrasia mnayoidai kwa wengine muanze nayo wenyewe ili muwe mfano kwa jamii, kwenye hili la kukataa kukososlewa mmejitia doa kubwa sana ambalo litawachukua muda mrefu sana kujisafisha mbele ya jamii.

- Kwenye hili la kujikosoa mnahitaji kujifunza kutoka kwa CCM, kwamba kukosoana sio Uhaini, Usaliti, Upandikizi, wala Mamluki ila ni Demokrasia ya kweli. (Soma gazeti la Jambo Leo leo Ukurasa wa 10)

Le Mutuz

True Mr. big fat belly, that why your step mom did not get UWT-CCM chairperson position and your Dad too lost his MP sit. When will you grow up? 52yrs old and you still talking pumba? You need Jesus
 
.

- Huu ni wakati wa Vyama vyote vya Upinzani nchini kukaa chini na kujitafakari nini kimewasibu mpaka kufikia kukataa kukosolewa [ Kukataa kukosolewa ni nini?] kila wakati viongozi baadhi ya Viongozi wa vyama hivyo wakijaribu kukosoa basi inakuwa shida na balaa kila mahali [ ni nini mantiki na maudhui ya kukosoa uongozi? [Je, katiba ya chama husika inasemaje kuhusu muktadha wa kukosoana?]. Mrema alipokosolewa NCCR kikaishia kubaki kivuli mpaka leo [ni nini dhumuni la Mh Mrema kwenda upinzani?], CUF ilipokosolewa na kina Rashid ikawa kizaaa zaa kila mahali, sasa wenzetu Chadema nao yale yale, tena wao wameeenda mbali zaidi mpaka kuita wakosoaji ni Mamluki, Wahaini, Mapandikizi, Wasaliti [Wajua sababu hasa za Chadema kuwaita wakosoaji wake wa ndani majina haya? Je, wajua kuwa Ikulu ya Mh Kikwete pia hutumia lugha hii kwa muktadha tofauti na huu unaotuaminisha hapa?] jamani mbona CCM Mbunge sasa anataka Waziri Mkuu aondolewe kwa uwajibikaji [Unao uhakika kuwa Waziri Mkuu anaondolewa ama ni kipaji kipya cha utabiri kama ilivyokuwa kwa al maarufu Sheikh Yahya Hussein?] Jamani Wapinzani Tanzania jifunzeni uvumilivu wa kisiasa na kama hamuwezi basi siasa sio fani yenu si mrudi tu mnako-fit vizuri kuliko kunga'nga'nia siasa [Kwani siasa ni nini le Mutuz?]. I mean wewe umechagliwa kwa mujibu wa katiba halaafu unaanza kuhangaika kila kona kutaka kupindisha katiba ile ile iliyokupa nafasi ya kuongoza ili usitoke kwenye uongozi, sasa mkipewa Taifa itakuwaje? [ Unamaanisha nini hapa Le Mutuz?] Viongozi wakubwa wa Taifa wa chama cha siasa mnapofikia kulumbana mbele ya jamii kuhusu ukweli na uongoa wa katiba yenu wenyewe mlioitunga wenyewe mnatutisha wengine kwenye jamii, kwamba mkishika dola itakuwaje na katiba ya jamhuri ambayo hamkuitunga? [Mbona ni kama unaelewa msingi wa msuguano ndani ya chadema halafu kwa makusudi unapotosha ukweli? Je, Wakazi wa Dar es Salaam tupo salama kiasi gani kwa kuwa na kiongozi wa CCM wa calibre yako? btw, nini vipaumbele kumi vya CCM katika kuboresha maisha ya wakazi wa Dar es Salaam?] si itakuwa vurugu kila siku kugombania ukweli na uongo wa katiba, badilikeni jamani Demokrasia mnayoidai kwa wengine muanze nayo wenyewe ili muwe mfano kwa jamii, kwenye hili la kukataa kukososlewa mmejitia doa kubwa sana ambalo litawachukua muda mrefu sana kujisafisha mbele ya jamii [ Unamaanisha CCM imepea kwa demokrasia? Unaweza akufafanua japo kidogo kuhusu demokrasia ndani ya CCM ipo kwa kiwango gani? ama unatukumbusha lile neno la Katibu Mkuu Makamba kuwa zimefika zama za kuwa na Spika wa Bunge Mwanamke bila kujali kuwa mwanamama huyo anazo sifa stahiki kuongoza na kusimamia chombo nyeti kama Bunge la Jamhuri, hii ndio demokrasia unayoizungumzia ati imeota mizizi ndani ya Chama Cha Mapinduzi kinachoogopa Mapinduzi?]

- Kwenye hili la kujikosoa mnahitaji kujifunza kutoka kwa CCM, kwamba kukosoana sio Uhaini, Usaliti, Upandikizi, wala Mamluki ila ni Demokrasia ya kweli [ Le Mutuz, kwa nini hujifunzi vigezo vinavyotamka haya makosa? hujui mwongozo ni katiba ya institution husika? unataka Chadema watoe hukumu sawa bin sawia kwa makosa yanayokinzana na katiba yao kwa kufuata yanayotokea CCM? Sasa tofauti ya CCM na Chadema itakuwa ni nini?]. (Soma gazeti la Jambo Leo leo Ukurasa wa 10)

Le Mutuz

Le Mutuz, kama huna la maana la kuchangia sio lazima uanzishe uzi ambao hujui mantiki, maudhui na muktadha wa unachoongelea.

Ficha ujinga wako
 
Kwani vyama vinakataa kukosolewa ama vinasema ufate vikao na katiba kulalamika?


CDM haijamwajibisha ZK kwasababu ya kukosoa nje ya vikao tu bali pia kwasababu amehusika waziwazi kukihujumu chama chake na watanzania wanaokitumainia chama hicho
 
Back
Top Bottom