Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,908
Wapinzani nchi hii ni wengi lakini wapambanaji miongoni mwao ni wache kitu ambacho ni hatari kwa upinzani unaokusudia kushika dola.
Kwa mfano,kuna wabunge wa upinzani tangu Bunge la November liishe hawajasikika popote wakati kuna mengi tu ya kuyasemea,kuhoji na kukosoa.Hali hii haipaswi kuendelea kama kwelo tunataka kushika dola na zaidi kama tunaka wananchi waelewe madhaifu ya hii serikali.
Baadhi tutawasikia katika Bunge linaloanza mwezi huu mwishoni na likiisha hutawasikia tena mpaka Bunge la April!
Miongoni mwa mambo yaliyopaswa kuhojiwa na wapinzani ni pamoja na haya
1.Wanafunzi kukosa mikopo
2.Wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kusitishwa ufadhili wa masomo na serikali
3.Hatima ya zoezi la uhakiki wa watumishi(litaishi lini)
4.Swala la kulipa stahiki/madai ya watumishi
5.Uwepo wa taarifa kuwa waliositishiwa ajira miezi 6 iliyopita kupisha uhakiki ajira zao zimefutwa na watatakiwa kuomba upya
6.Sababu za TRA kutotangaza mapato ya Novembe na December kama walivyokuwa wakifanya kwa miezi ya nyuma(hii taarifa ya makusanyo ya miezi 6 waliyotoa leo hata wasingetoa kulikuwa hakuna wa kuhoji zaidi ya sisi huku mitandaoni)
7.Ni lini serikali itaanza kutoa ajira na sio tu kutoa matamko ya kuajiri bila kutoa timeframe ya utekelezaji.
8.Mahakama ya Mafisadi kukosa watuhumiwa (jambo la ajabu kabisa hili).
Hayo ni baadhi ya mambo miongoni mwa mengine mengi ambayo wapinzani walipaswa kuyahoji kama alivyofanya Waziri Kivuli wa Afya pale alipotoa tamko kuhoji/kuongelea swala la upungufu wa madawa mwaka jani mwezi wa 9 au wa 10 kama sikosei.
Wapinzani ambao wamekuwa active/ wapambanaji kwa sasa na wanasaidi serikali kujirekebisha/kujitafakari ni Lema,Lissu,Zitto na Kafulila lakini wengine wanaendesha soft politics tu na wengine ni kama wako likizo!
Niwambie tu hata hili swala la chakula mngekaa kimya kama mlivyokaa kimya kuhusu haya mambo mengine,leo sidhani kama mngesikia serikali inajipanga kuanza kusambaza chakula maana walishaonyesha nia ya kutofanya hivyo lakini kelele za Zitto na uamuzi wa CHADEMA kutaka kugawa chakula ndio bila shaka utakuwa umeishitua serikali.
Nina haikia hata haya matatizo mengine hayashuhulikiwa kwasababu yamekosa msukumo kutoka kwa wanasiasa na watu wengine wenye kuheshimika katika jamii.
Kumbukeni hata baada ya Lissu kukomaa kuhusu hoja ya kusitisha mikutano ya kisiasa mpaka 2020,ndio angalau likaja tamko tata kuwa mtaruhusiwa kufanya mikutano kwenye maeneo miochaguliwa tu na si vinginevyo.
Hivi sasa kampeni za udiwani zinaendelea lakini anaetumia mikutano hiyo kuongelea maswala mazito ya kitaifa amekuwa ni Zitto tu wengine hata hamsikiki.
Endeleeni hivyo hivyo mtaona matokeo yake japo jamaa kila siku anaharibu.