29,188,347 ndiyo idadi ya wapiga kura ktk daftari kwa uchaguzi wa Tanzania 2020.
Idadi ya waTanzania walioenda kupiga kura kufuatana na matokeo anayotangaza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi toka majimbo machache matokeo yake yaliyosomwa inaonesha ni asilimia ndogo wamejitokeza yaani kiasi cha asilimia 50 ndiyo wamekwenda kupiga kura.
Hamasa ilikuwa kubwa pande za wanaolinda kubaki madarakani kwa miaka mitano mingine na wakati pia hamasa ilikuwa kubwa kwa wale waliotaka kuingia mitano mwanzo kama serikali Mpya kupitia upinzani.
Nini kimepelekea waliojitokeza kuwa 50% ya wapiga kura 29,188,347 huku wengine hawakwenda kupiga kura ? Wapiga kura zaidi milioni 10 kutopiga kura hii inaashiria nini?