Wapinzani, Lissu wazidi kumbana JK

Wapinzani, Lissu wazidi kumbana JK

Awafukuze kazi waliomwambia...! Akina Wasira,Lukuvi,Chikawe na wote waliomwambia ndiyo wanayumbisha Nchi hii... Jk fukuza kazi hao wachumia tumbo!
 
Kuna claims tofauti zinazotishia ustawi wa mchakato huu wa katiba
1. Vyama vya upinzani pamoja na taasisi mbalimbali zinalalamika kuwa rasimu iliyopitishwa bungeni haikutenda haki

2. Tume ya katiba wanalalamika kuwa wanasiasa wanaingilia mchakato wa katiba

3. Chama cha Mapinduzi kinalalamika kuwa Mwenyekiti wa tume ya katiba anahodhi suala zima la kutoa maoni

4. Wazanzibari wanalalamika kuwa hawakushirikishwa vya kutosha katika kuandaa mswada


USHAURI
Kwa kuwa raisi ndiye aliyeridhia kuanzishwa kwa machakato wa kuandika katiba mpya, basi aubebe mgogoro huu kwa uzito unaotosha, aufuatilie kwa karibu na asitegemee sana mambo ya kuambiwa

Kwa kutambua kuwa washauri wake waandamizi (mawaziri Wasira, Lukuvi, Simba, Chikawe, viongozi wa bunge) ni sehemu ya mgogoro huu, basi raisi afikirie kutafuta timu mpya ya kumshauri na ku-handle nayo hili suala. Akutane na pande zote, tume, wapinzani, CCM (yes, CCM hasa Bulembo), Wazanzibar na taasisi nyingine, wakae watatue hii shida mapema...
 
Jamhuri Ya Muungano Wa Kulalaika,rais anatoa hotuba ya kumlalamikia TL,na TL anamlalamikia Rais,Bulembo anamlalamikia Jaji Warioba,Jaji Warioba analalamika tume yeke inaingiliwa,Chadema,Cuf na Nccr Mageuzi wanailalamikia Ccm na Ccm inawalalamikia wapinzani na Tanzania Daima wanailalamikia chama tawala huku Uhuru na Habari leo Wanawalalamikia wapinzani,wachangiaji humu wanalalamikiana yaani kila mmoja anamlalamikia mwenzake!Nawahakikishieni tutapata Katiba yenye malalamiko kibao,ambayo haitamsaidia Mtanzania halisi wakijijini.Viongozi,Wanasiasa,Wasomi,Wanahakati,Wananchi na wadau wengine tuache kulalamika!Tupambane kwa nguvu ya hoja za sio hoja za nguvu!

We mwenyewe hujatoa hoja zaidi yakulalamika...! Nani asiyopaswa kulalamika??

Mi naona serikali ilyoshika dola haipaswi kulalamika zaidi yakutekeleza yale yanayolalamikiwa.
 
“Huyu huyu rais ndie aliwaambia wafanyakazi wakati wa mgomo wao kuwa akili za kuambiwa na viongozi wao wachanganye na za kwao, kwanini katika mambo aliyoambiwa na wasaidizi wake hakujiridhisha kwanza?”

Kweli hapa ni mahali pazuri..mkuki kwa nguruwe...ha ha ha aha ha
 
Moja ya sifa kubwa ya kiongozi ni kujua namna ya kuhandle situation inapokuwa tight
Na katika hili sina shaka na JK atalimaliza salama tu
 
Watanzania wenzangu,nachukua fursa hii kuwatakia heri na fanaka katika maisha yetu ya kila siku hasa ukizingatia usalama wa nchi zetu ndani ya kanda ya Afrika Mashariki ni tete kutokana na hali ya usalama kuzidi kudorora na kugeuzwa ya kisiasa zaidi bila kuonyesha umakini katika idara zetu,matokeo yake ni majibu mepesi yatokanayo na maswali magumu.Tumeona ukiukwaji wa haki za binadamu za watu fulani kunyang'anya haki za wengi za kuishi kwa makusudi na kukosa majibu ya msingi juu ya udhibiti wa usalama wa nchi na watu wake.

Tarehe 4/10/2013,Rais wa JMT alihutubia taifa kama ilivyo ada ya kila mwisho wa mwezi kuongea na Watanzania kwa njia ya hutuba zake ambazo ni mwendelezo wa utaratibu aliojiwekea aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Ndugu Benjamini W Mkapa.Katika hotuba hiyo,mheshimiwa Rais aliongea mambo matatu manne hivi lakini kubwa kuliko yote ni juu ya rasimu ya katiba ambayo usipotumika umakini wa hali ya juu nchi ina kwenda kutumbukia kati janga kubwa la vita vya wenye kwa wenyewe(civil war)

Katika hali ya kustaajabisha rais ana kiri kuambiwa kila kitu bila kufanya tafiti toka vyanzo vyake.Kulikuwa na haja gani ya kuwa na kurugenzi ya habari ikiwa chombo hicho ama kwa makusudi kinatumika vibaya kumpotosha rais kiai cha rais kumshambulia hadharani mbunge aliyetoa hoja tena ndani ya bunge juu ya kutoshirikishwa kwa wadau mbalimbali katika mchakato huo.Ikumbukwe kuwa kila mara rais wetu amekuwa akisistiza kuwa ukiambiwa jambo changanya na akili zako,sasa swali linakuja kwake katika kuambiwa huko alijaribu kuchanganya na akili zake ili kuweza kujibu hoja iliyotolewa kuliko kufanya ikulu sehemu ya mipasho.

Lakini pia nimestushwa na kauli ya rais kuwa wapinzani wasingetoka ili wapewe haki yao ya kuchangia hoja zao wanazoona zinafaa ilihali KUB mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe alibezwa,kupuuzwa na kudhalilishwa kwa kutolewa nje kwa kuwa tu alitaka kuchangia hoja.Haingii akilini kwa akili ya haraka haraka kusema kuwa kulikuwa na nia ya dhati ya naibu spika wa Bunge kutenda haki ilhali alionyesha ushabiki wa kivyama ndani ya bunge.

Pia nimkumbushe mh. Rais kuwa kilichojadiliwa na wabunge wa CCM mara baada ya kutoka wabunge wa upinzani na kubaki wabunge wawili wa TLP na UDP na CCM ni bunge kupoteza haki yake na hadhi yake ya kibunge kwa kiti cha Spika kuruhusu ukumbi huo kuwa sehemu ya kuwananga wapinzani bila kujali kuwa hoja iliyo mbele ya Bunge ni nzito inayotaka hekima na busara ya hali ya juu kwa kuwa tu ikfanyiwa uupuzi inaweza kuligawa taifa na kuliangamiza.

Pamoja na hayo yote na tume ya Jaji Warioba kushambuliwa mara kwa mara na wanachama na viongozi wa CCM waliokosa weredi na kutanguliza maslahi ya vyama mbele na kufikia mawaziri na baadhi ya wabunge kumtishia Rais kwa kuonekana msaliti ndani ya chama chake,nachukua fursa hii kumpongeza kwa busara aliyoina ina stahili kufanywa katika kufikia malengo ya kuijenga Tanzania tuitakayo.

Mwisho,nachukua fursa hii kuwaasa Watanzania wenzangu kuwa ni bora tutumike katika kujenga maslahi ya taifa zima kwa kusimamia katiba ambayo angalau itatoa suluhisho la kansa na ulevi wa madaraka miongoni mwa viongozi wetu kuliko kuwa wapambe wa watu wachache wenye kutumia kila rasiliamli waliyonayo na ya taifa kujitengenezea usalama wa kuendelea kufisidi mali za umma.
 
Tanzania Daima ni gazeti la udaku

Halifai hata kwa kufungia maandazi.

Gazeti kama hili hupatikana kwenye vyoo vya vilabu vya mataputapu
Hivi mtu mzima mwenye akili timamu anaweza kuandika hiki?
 
Source: Gazeti lisilokuwa la Udaku (Uhuru)
UHURU limejiweka wazi ni la chama,lkn Tanzania daima munaveshwa limu,kama la chama kumbe la familia,ushauri wa bure muanzishe la CDM wenzenu CUF wanalo FAHAMU.HIKI CHAMA KIMEKAA KIFAMILIAFAMILIA TU.
 
UHURU limejiweka wazi ni la chama,lkn Tanzania daima munaveshwa limu,kama la chama kumbe la familia,ushauri wa bure muanzishe la CDM wenzenu CUF wanalo FAHAMU.HIKI CHAMA KIMEKAA KIFAMILIAFAMILIA TU.

Ndiyo maana tunakipenda,maana ukiwa CHADEMA unakuwa MWANAFAMILIA,a'm too proud to be part of CHADEMA'S family.
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...

Hongera kwa mawazo yako, angalau Tanzania Daima ni gazeti, ila uhuru na mzalendo hayafai hata kwa kufungia kitu, ni zaidi ya used n' dumped tissue paper
 
NIMEAMBIWA.........Mh.hana muda wa kusoma,kufuatilia na kujiridhisha kabla hajasimama mbele ya camera,shame.......ikitokea waliomwambia wamempotosha atasimamia wapi?.........kumbe alivyokuwa anasema TUKIAMBIWA TUCHANGANYE NA ZETU hakujua ipo siku na yeye ataambiwa.
 
Teh teh, rais wa kuambiwa kila kitu na washauri wabovu, kikwete ameweka washauri wa hovyo, ambao muda wote ni kudanganywa kwa kwenda mbele!
 
ila hii hotuba imejaa maneno ya kuambiwa? Hotuba imeonyesha kupooza mambo kama sio kuogopa "kuanzia issue ya wahamiaji haramu na katiba mpya" - yaani Rais wangu amekuwa kama katishiwa sijui! kapigwa mkwara
JK kamgeuka nani?

JK ametoa hotuba nzuri zaidi kuliko zote zilizowahi kutolewa na Ikulu ya Magogoni tangu nchi ipate Uhuru.
 
Back
Top Bottom