Wapinzani Burundi wamkataa Mkapa

Wapinzani Burundi wamkataa Mkapa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,896
_92908661_38c07ddf-4f9b-4c1b-b9db-44baa28937d5.jpg


Wanasiasa wa upinzani nchini Burundi walio uhamishoni wamepinga jitihada za aliyekuwa Rais wa Tanzania za kutatua mzozo ulio nchini humo.

Hii inajiri baada ya William Mkapa kuwaambia waandishi wa habari kuwa si jambo zuri kuendelea kutilia shaka uhalali wa Rais Pierre Nkurunzia.

Nchi ya Burundi ilitumbukia kwenye mzozo baada ya bwana Nkurunziza kutangaza kuwa angewania muhula wa tatu.

Mamia ya watu wameuawa na maelfu kukimbia nchi kulipozuka ghasia.

Bwana Mkapa alipewa jukumu la kusaidia kutatua mzozo huo, na amesema kuwa makubaliano yatafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni wanatafutwa na serikali kwa kupanga maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunziza hatua ambazo serikali inazitaja kuwa za kihalifu.

Wengine walilaumiwa kwa kushiriki kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli mwezi Mei.


Chanzo: BBC Swahili
 
Ndo huyu aliyetuambia SISI NI malofa na wapumbavu
 
aibu sana nadhani ndio kiongozi wa kwanza watz kukataliwa abroad!!hatukuwai kuonekana wa hovyo tunasifika kwa ustahimilivu na busara
 
Mkapa kasababisha maafa makubwa sana Zanzibar nasikia anaitwa Lodilofa aisee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkapa naye kama msuluhishi alichemka, msuluhishi unatakiwa unakuwa na ka unafiki flan hivi, kakuongea kitu hata kama hukiamini, ili uwavute pande zote. Ni kama refa huwezi kuwa na upande unapo chezesha mechi
 
Huyu mzee akirudia tena kauli yake kwamba wanaompiga Nkurunzinza ni wapumbavu, anaweza patwa na lolote kule maana yale majamaa mtutu nje-nje.
 
Back
Top Bottom