Wapinzani acheni kulialia! Tafteni katiba mpya kwa namna yoyote ile

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Suala la kulialia kwamba CCM inatumia rasirimali za umma kujinufaisha au inatumia mgumu uliopo kuendelea kutawala.

Msiishie kupiga kelele tu, tumieni kila namna kuitafuta katiba mpya kwa namna yeyote ile mtafanikiwa na hayo mengine yatafikia mwisho tu.Hii ndio itakua solution ya yote hayo.
 
Anza wewe kuelezea way forward, kwa kuwa wapinzani wametumia juhudi zote kuidai Katiba mpya, lakini kama kawaida yao wabunge wa CCM ambao ndiyo wengi bungeni, lakini kama kawaida yao, wenyewe huwa wanaweka mbele maslahi ya Chama chao mbele kuliko maslahi ya Taifa.

Na hicho ndicho kilichosababisha Rasimu ya Tume ya Warioba ambayo ndiyo iliyokuwa na maoni ya wananchi, kutupwa kwenye 'dust bin' na wabunge wa CCM wa Bunge Maalum la Katiba, baada ya wabunge wa upinzani kuamua kutoka bungeni baada ya kuona kuwa yale maoni mengi yaliyokuwemo kwenye Rasimu ya Warioba, ambayo yalikuwa yana maslahi mapana kwa Taifa letu kunyofolewa, na badala yake wabunge hao wa CCM kumpa jukumu mzee wa vijisenti, kuandika upya Katiba mpya ya nchi.

Sasa katika mazingira hayo ambayo wabunge wa CCM wanataka Katiba ambayo inaziweka Tume za uchaguzi 'mbovu' ambazo jukumu lake ni kuendelea kuiweka madarakani CCM hadi mwisho wa dunia, inakuwa ni jukumu ambalo ni sawa na next to impossible kupata Katiba mpya ambayo itakuwa kwa ajili ya maskahi mapana ya nchi na siyo kwa ajili ya maslahi ya chama chochote cha siasa.
 
WAkati mwingine hoja itolewe angalau ioneshwe kuwa imefikiriwa; kama anatoka Ikulu kwenda Segerea inabidi apande ndege au huko asiende na askari?
 
Mchakato ukianza mnajichetua na kususa kama mademu ili mbembelezwe.

Hiyo katiba mnayoitaka yenye maoni mnayoyataka nyinyi tu kuipata mpaka mshike dola au muwe na wajumbe wengi kwenye vyombo vya uwakilishi.

Magufuli kashinda bila kuahidi katiba mpya,unadhani ataacha mambo aliyoyaahidi arukie katiba mpya? Labda
kama atatekeleza ahadi zote kwanza of which ni ndoto.

Mambo yenyewe yanayopiganiwa ni ya kisiasa zaidi kuliko welfares za wasio wanasiasa.

Idadi ya serikali za muungano zinamsaidia nini mkulima wa Ubaruku?

Futeni posho zenu za makalio zielekezwe kwenye mambo ya maendeleo tujue kweli mnapigania ustawi wa wanyonge.
 
Katiba mpya si kwaajili ya Wapinzani pekee.... Katiba mpya ni kwa manufaa yetu sote.

Ni ujinga kufikiri jukumu la kudai Katiba Mpya ni la Upinzani pekee... Ni jukumu letu sote.
 
Suala la kulialia kwamba CCM inatumia rasirimali za umma kujinufaisha au inatumia mgumu uliopo kuendelea kutawala.

Msiishie kupiga kelele tu, tumieni kila namna kuitafuta katiba mpya kwa namna yeyote ile mtafanikiwa na hayo mengine yatafikia mwisho tu.Hii ndio itakua solution ya yote hayo.
Tanzania hakuna vyama vya upinzani bali kuna vyama vya hovyohovyo
 
kichekesho wale waliokuwa wanapinga katiba sasa ndio wanaidai kwa sababu tu upande walioko hawanufaiki nayo, tusije tukatengeneza katiba ya wanasiasa na wote tunajua katiba mpya ilivurugika kutokana na bunge la katiba kujaza wanasiasa
 
WAkati mwingine hoja itolewe angalau ioneshwe kuwa imefikiriwa; kama anatoka Ikulu kwenda Segerea inabidi apande ndege au huko asiende na askari?

Nashindwa kupata uhusiano kati ya ulichokiandika na mada husika, unaweza kunielezea ulichomaanisha?
 
Katiba mpya si kwaajili ya Wapinzani pekee.... Katiba mpya ni kwa manufaa yetu sote.

Ni ujinga kufikiri jukumu la kudai Katiba Mpya ni la Upinzani pekee... Ni jukumu letu sote.
Hakika wewe na mjinga sana! Nioneshe ni wapi CCM walikua na mpango wa katiba mpya?
 
Nashindwa kupata uhusiano kati ya ulichokiandika na mada husika, unaweza kunielezea ulichomaanisha?
Hili lizee hua silielewi sijui hata limeandika nini hapo! Lipotezee tu mkuu ni libeba mabox huko nje.
 
Tanzania hakuna vyama vya upinzani bali kuna vyama vya hovyohovyo
Kwa tamaa zenu za madaraka mtaendelea kuviona vya hovyo hovyo mpaka mtakapotolewa! Na mtaondoka tu mpende msipende.
 
Hakika wewe na mjinga sana! Nioneshe ni wapi CCM walikua na mpango wa katiba mpya?

Nina wasiwasi yai lililokuzaa lilikuwa yai Viza....

Hii nchi si ya CCM wala Ukawa... Hii nchi ni yetu sote.
 
Suala la kulialia kwamba CCM inatumia rasirimali za umma kujinufaisha au inatumia mgumu uliopo kuendelea kutawala.

Msiishie kupiga kelele tu, tumieni kila namna kuitafuta katiba mpya kwa namna yeyote ile mtafanikiwa na hayo mengine yatafikia mwisho tu.Hii ndio itakua solution ya yote hayo.
Watanzania wengi wana mawazo kama yako i.e. kazi ya kuleta mabadiliko yoyote positive katika nchi ni ya serikali au upinzani! You are very wrong dears! Mabadiliko yataletwa na SISI WANANCHI. Kwahiyo unapofikiri kazi ya kuleta katiba mpya ni ya upinzani tu umekosea kabisa. Upinzani unaweza kuwa kama uongozi wenye ramani kakini mimi na wewe na yule na wale ndio tunatakiwa tudai katiba
 
Mchakato ukianza mnajichetua na kususa kama mademu ili mbembelezwe.

Hiyo katiba mnayoitaka yenye maoni mnayoyataka nyinyi tu kuipata mpaka mshike dola au muwe na wajumbe wengi kwenye vyombo vya uwakilishi.

Magufuli kashinda bila kuahidi katiba mpya,unadhani ataacha mambo aliyoyaahidi arukie katiba mpya? Labda
kama atatekeleza ahadi zote kwanza of which ni ndoto.

Mambo yenyewe yanayopiganiwa ni ya kisiasa zaidi kuliko welfares za wasio wanasiasa.

Idadi ya serikali za muungano zinamsaidia nini mkulima wa Ubaruku?

Futeni posho zenu za makalio zielekezwe kwenye mambo ya maendeleo tujue kweli mnapigania ustawi wa wanyonge.
Aaaaah aaaaah Salamu kwa Wanaubaruku hapo 5 lodge
 
Back
Top Bottom