Kufanya maandamano ni kukosa maarifa, nidhamu na uvumilivu

Nov 6, 2016
53
146
MAANDAMANO HAYANA TIJA KATIKA SIASA ZA SASA - (SIASA KAZI NA MAARIFA)

Na Comrade Ally Maftah

Moja kati ya jambo ambalo halitaungwa mkono na vijana wa kileo ni suala la kuandamana.

Kuandamana ni kukosa maadili, ufahamu, utambuzi, wa mambo katika hali ya siasa za sasa za ushindani wa hoja, na katika ulimwengu wa mitandao, katika ulimwengu wa ukweli na uwazi.

Kijana huna haja ya kuandamana, fursa za kupaza sauti yako ipo kubwa sana kwa kutumia mitandao ya kijamii, redio na TV, panga hoja zako vizuri ziwasilishe kwenye vyombo husika kuliko kujihusisha kwenye misongamano isiyo na lazima, kuna magonjwa ya mlipuko mtaambukizana, kuna majasho ya watu wenye mikosi, kuna kuvunjika miguu kutokana na presha za kukimbia kimbia barabarani

Wenzako wanaokuhimiza uandamane wakivunjika miguu wanaenda kutibiwa nje ya nchi, na wana watabibu wao, wanakuja kwenye hizo vurugu wakiwa wameshiba.

Acha kuandamana jitume kwenye kazi, tenda haki, ukigombea utashinda Tume yetu ya Uchaguzi ipo huru sana, Dr Samia anatulinda wote pasipo kujali itikadi za vyama vyetu

Comrade Ally Maftah
Mjumbe Mkutano Mkuu Mkoa CCM & Wazazi - Dar es Salaam

IMG-20240114-WA0050.jpg
 
Ni mpumbavu peke yake atayeamini upumbavu kama huu. Tanzania tumejazwa ujinga mkubwa sana na kuamini kuwa chochote kinachofanywa na MTU mwenye madaraka ni Sahihi ila ni dhambi kitu hicho hicho kikifanywa na MTU tofauti

Wale wanaondamana kumpongeza Samia kila siku sijawahi kuona bandiko lolote likikemea UJUHA ule ila linapokuja suala la mambo ya msingi kila mbuzi inajifanya inajua kuandika.
 
Acha kuandamana jitume kwenye kazi, tenda haki, ukigombea utashinda Tume yetu ya Uchaguzi ipo huru sana, Dr Samia anatulinda wote pasipo kujali itikadi za vyama vyetu
Upumbavu kama huu then unategemea nchi ipige hatua? Tanzania ni nchi ya ajabu mnoooo!
 
Tuwekee namba yako ya simu utumiwe hela... Sisi wanaccm wenzako tunakupongeza Sana Kwa mada yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom