Wapiganaji wavamia bunge

Wapiganaji wavamia bunge

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,575
Reaction score
53,613
Watu waliokuwa wamejihami walivamia majengo ya bunge nchini Libya Jumanne jioni na kulazimisha wabunge kusitisha shughuli ya kumteua waziri mkuu mpya.
Maafisa wanasema kuwa wabunge waliondoka bunge punde waliposikia milio ya risasi.
[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]

Hatua ya kupigia kura waziri mkuu mpya imetokana na kujizulu kwa aliyekuwa waziri mkuu Abdullah al-Thinni, aliyeondoka mamlakani mapema mwezi huu baada ya yeye pamoja na familia yake kulengwa na wapiganaji.
Libya imekuwa ikikumbwa na mgogoro tangu harakati za kumuondoa mamlakani hayati Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Awali ripoti zilisema kuwa watu kadhaa walijeruhiwa katika mashambulizi siku ya Jumanne.
Haijulikani nani aliyehusika na shambulizi hilo.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli,Rana Jawad anasema kuwa bunge la Libya limewahi kuvamiwa na watu waliojihami katika kipindi cha mwaka mmoja unusu iliopita.
Wabunge wamekuwa wakitofautiana kuhusu kuteuliwa kwa waziri mkuu wakati shambulizi la Jumanne lilipotokea.
Tayari walikuwa wamefanya duru ya kwanza ya kura na kuwateua wagombea wawili kati ya saba.
Lakini duru ya pili ilipoanza ndipo watu hao waliposhambulia bunge na kulazimisha wabunge kuahirisha shughuli hiyo ambayo sasa itafanyika tarehe 4 mwezi Mei.

Wapiganaji wavamia bunge Libya - BBC Swahili - Habari
 
Libya, Iraki,Misiri hazitakaa zirud normal kamwe, USA yuko pemben anachekelea
 
Misiri sijui ni nchi gani hii? Nimetafuta kweli kwenye ramani ya dunia sijaiona
 
Back
Top Bottom